Kulinda utambulisho wako

Tungependa ujihisi salama unapotumia YouTube. Ndiyo maana tunakuhimiza utufahamishe iwapo video au maoni kwenye tovuti yanakiuka faragha au usalama wako.

Iwapo mtu alichapisha taarifa zako binafsi au alipakia video uliyomo bila wewe kujua (ikiwa ni pamoja na hali za faragha au nyeti), mwombe aliyepakia aondoe maudhui hayo. Iwapo hamtakubaliana na aliyepakia au iwapo hungependa kuwasiliana naye, unaweza kufuata Utaratibu wa Kuwasilisha Malalamiko kuhusu Faragha kuomba maudhui hayo yaondolewe kwa mujibu wa Mwongozo wetu wa Faragha

Ripoti maudhui yaliyotayarishwa kwa AI au maudhui mengine sanisi yanayofanana au yanayoendana na wewe: Ikiwa mtu fulani ametumia AI kubadilisha au kuunda maudhui yanayofanana nawe au yaliyo na sauti kama yako, unaweza kuomba yaondolewe. Ili yatimize vigezo vya kuondolewa, maudhui yanapaswa kuonyesha toleo la kweli lililobadilishwa au lililosanisiwa la hali ya kufanana na wewe. Tutazingatia vigezo mbalimbali wakati wa kutathmini malalamiko, kama vile:

  • Ikiwa maudhui hayo ni sanisi au yamebadilishwa
  • Ikiwa mtu huyo anaweza kutambuliwa kimahususi
  • Ikiwa maudhui ni halisi 
  • Ikiwa maudhui yanajumuisha mwigo wa kubeza, tashtiti au thamani nyingine ya maslahi ya umma.
  • Ikiwa maudhui yanamwangazia mtu maarufu au mashuhuri akijihusisha na tabia nyeti kama vile shughuli ya uhalifu, vurugu au akiidhinisha bidhaa au mgombea wa kisiasa

Ili uanze kuripoti, fuata Utaratibu wa Kuwasilisha Malalamiko kuhusu Faragha kwa maudhui sanisi au yaliyobadilishwa. Pata maelezo zaidi kuhusu lebo za maudhui sanisi na yaliyobadilishwa.

Utaratibu wa kuondoa maudhui

Mwongozo wetu wa Faragha unafafanua kwa kina utaratibu wetu wa kuwasilisha malalamiko kuhusu faragha. Pia, unafafanua vigezo tunavyozingatia wakati wa kutathmini madai ya faragha.

Ili tuzingatie kuondoa maudhui, ni lazima mtu awe anayetambulika kimahususi na ni lazima mtu huyo au mwakilishi wake wa kisheria awasilishe malalamiko. Iwapo ungependa kutumia Utaratibu wa Kuwasilisha Malalamiko kuhusu Faragha, hakikisha kuwa unatambulika kimahususi katika maudhui wakati unatumia utaratibu wa kuwasilisha malalamiko kuhusu faragha. Tunapotathmini iwapo mtu anatambulika kimahususi, tunazingatia mambo yafuatayo:

  • Picha au sauti
  • Jina kamili
  • Maelezo ya fedha
  • Maelezo ya mawasiliano
  • Maelezo mengine yanayoweza kumtambulisha mtu

Unaporipoti malalamiko kuhusu faragha, tunazingatia maslahi ya umma, ustahiki wa habari na idhini kama vigezo katika uamuzi wetu wa mwisho; na pia iwapo video hizo zinaonyesha mtu akifa au jeraha baya.

Ili kuheshimu faragha na kumbukumbu ya watumiaji walioaga dunia, tunazingatia maombi kutoka kwa wanafamilia wa karibu zaidi au wawakilishi wa kisheria baada ya kuthibitisha kuwa mhusika amefariki.

Vidokezo kuhusu jinsi ya kulinda faragha yako kwenye YouTube:

  • Tafakari kwa umakini kabla ya kuchapisha taarifa binafsi. Hujumuisha mifano kama vile mji ambako unaishi, shule ambako unasomea na anwani yako ya nyumbani.
  • Linda data ya akaunti yako na usishiriki nenosiri lako na wengine. Wafanyakazi wa YouTube hawatawahi kukuomba nenosiri lako. Usidanganywe na mtu atakayewasiliana nawe akijifanya kuwa mfanyakazi kutoka YouTube.
  • Pata ruhusa kwanza. Pata ruhusa kabla ya kurekodi watu wengine au kuchapisha taarifa zao binafsi.
  • Tembelea ukurasa wetu wa Mipangilio ya Faragha na Usalama ili upate orodha ya zana unazoweza kutumia kudhibiti maudhui na hali yako ya utumiaji kwenye tovuti.
  • Angalia desturi bora za kudumisha usalama wa Akaunti yako ya Google.
  • Usalama thabiti kwenye akaunti ya Google: Imarisha usalama wa akaunti zako kupitia Uthibitishaji wa Hatua Mbili.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9153444520206901014
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false