Maswali yanayoulizwa sana kuhusu hakimiliki

Katika video hii, tunajibu maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu hakimiliki:

Copyright Permissions - Copyright on YouTube

Maswali ya jumla kuhusu hakimiliki

Je, matumizi ya haki ni nini?

Matumizi ya haki ni kanuni ya kisheria inayosema kwamba unaweza kutumia tena nyenzo zinazolindwa kwa hakimiliki katika hali fulani bila ruhusa ya mwenye hakimiliki.

Nchini Marekani, ni mahakama tu ndiyo inaweza kuamua ni matumizi yapi yanafaa kuwa matumizi ya haki.

Mahakama zinategemea vigezo vinne ili kubaini matumizi ya haki kulingana na hali mahususi, ikiwa ni pamoja na:

  • Madhumuni na sifa ya matumizi
  • Asili ya kazi iliyo na hakimiliki
  • Kiasi na umuhimu wa kazi iliyo na hakimiliki iliyotumiwa
  • Athari kwenye soko tarajiwa au thamani ya kazi iliyo na hakimiliki

Pata maelezo zaidi katika makala ya Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu Matumizi ya haki.

Je, kazi iliyo wazi kutumiwa na umma ni nini?

Kazi hatimaye hupoteza ulinzi wake wa hakimiliki na huwa "wazi kutumiwa na umma" hali inayofanya kazi hizo ziweze kutumiwa na kila mtu, bila malipo. Kwa kawaida, inachukua miaka mingi kabla ya kazi kuwa wazi kutumiwa na umma.

Urefu wa kipindi cha ulinzi wa hakimiliki hutofautiana kulingana na vigezo kama vile:

  • Mahali na mwaka ambao kazi ilichapishwa
  • Iwapo mtu mwingine aliajiriwa ili kuandaa kazi hiyo

Baadhi ya kazi zilizotengenezwa na mashirika ya serikali ya Marekani huwa wazi kutumiwa na umma baada tu ya kuchapishwa. Kumbuka kwamba sheria zinazohusiana na kazi zilizo wazi kutumiwa na umma hutofautiana baina ya nchi.

Unawajibika kuthibitisha kuwa kazi ipo wazi kutumiwa na umma kabla ya kuipakia kwenye YouTube. Hakuna orodha rasmi ya kazi zilizo wazi kutumiwa na umma. Hata hivyo, kuna nyenzo muhimu mtandaoni zinazoweza kukusaidia. Kwa mfano, Cornell University inatoa mwongozo wa kazi ambazo huenda zipo wazi kutumiwa na umma. Kumbuka kwamba hakuna huluki yoyote, ikiwa ni pamoja na YouTube, inayoweza kukuhakikishia kuwa kazi zote zilizowekewa viungo hazina ulinzi wa hakimiliki.

Je, miigo ya kazi ni nini?

Unahitaji ruhusa ya mwenye hakimiliki ili utayarishe kazi zinazotokana na maudhui yake asili. Miigo ya kazi inaweza kujumuisha hadithi zinazoandikwa na mashabiki, matoleo ya mwendelezo, tafsiri, vijalizo, uwasilishaji wa maudhui katika mifumo mbalimbali na zaidi. Jaribu kupata ushauri wa kisheria kutoka kwa mtaalamu kabla ya kupakia video zinazotokana na wahusika, hadithi na vipengee vinginevyo vya nyenzo zinazolindwa kwa hakimiliki.

Je, ninaweza kupata wapi taarifa zaidi kuhusu hakimiliki nje ya Marekani?

Tovuti ya Your Europe ina viungo na maelezo muhimu kuhusu hakimiliki katika nchi au maeneo ya Umoja wa Ulaya.

Shirika la World Intellectual Property Organization (WIPO) lina orodha ya ofisi za kimataifa zinazohusika na hakimiliki na mali ya uvumbuzi unapoweza kupata maelezo kuhusu sheria za hakimiliki za eneo uliko.

Tovuti hapo juu zimetajwa kwa madhumuni ya elimu tu na hazijaidhinishwa na YouTube.

Maswali kuhusu kupakia maudhui kwenye YouTube

Ninawezaje kupata ruhusa ya kutumia maudhui ya mtu mwingine kwenye video yangu?

Iwapo unapanga kujumuisha nyenzo zinazolindwa kwa hakimiliki katika video yako, kwa kawaida utahitaji kwanza kuomba ruhusa. YouTube haiwezi kukupatia haki hizi na hatuwezi kukusaidia kupata wahusika muhususi wenye uwezo wa kukupatia haki hizo. Utahitaji kufanya utafiti na kushughulikia mchakato huu mwenyewe au kwa usaidizi wa mwanasheria.

Kwa mfano, YouTube haitaweza kukupatia haki ya kutumia maudhui yaliyopakiwa kwenye tovuti tayari. Endapo ungependa kutumia video ya YouTube ya mtu mwingine, tunakushauri uwasiliane naye moja kwa moja. Baadhi ya watayarishi huorodhesha njia unazoweza kuwasiliana nao katika chaneli yao.

Njia rahisi ya kupata muziki wa chinichini au madoido ya sauti kwa ajili ya video zako za YouTube ni kupitia kipengele cha YouTube cha Maktaba ya Sauti. Unaweza kutafuta muziki unaoweza kutumia bila malipo.

Ikiwa unafikiria kutumia muziki wa mtu mwingine kwenye video yako, pata maelezo zaidi kuhusu chaguo zako za kutumia muziki:

Machaguo ya kutumia muziki katika video zako

Ninawezaje kupata leseni ya kutumia maudhui ya wahusika wengine?

Kabla ya kupakia video kwenye YouTube, lazima upate haki za kutumia vipengele vyote katika video yako. Vipengele hivi vinajumuisha muziki wowote (hata kama unacheza kwa chinichini), klipu za video, picha na zaidi.

Kwanza, wasiliana moja kwa moja na wenye hakimiliki au wenye haki kisha mjadiliane kuhusu leseni inayofaa kwa matumizi yako.

Kisha, angalia leseni. Leseni huwa na ruhusa dhahiri za matumizi ya maudhui na mara nyingi hujumuisha mipaka ya jinsi maudhui yanavyoweza kutumiwa. Tafuta ushauri wa kisheria kwa makubaliano yoyote ya leseni ili ufahamu haki zilizotolewa na zile ambazo mmiliki amehifadhi.

Pia, unaweza kutumia maktaba ya YouTube ya muziki na madoido ya sauti, yanayoweza kutumiwa kwenye video bila malipo kulingana na masharti yaliyobainishwa.

Kumbuka: Ikiwa unaimba toleo lingine la wimbo ulioimbwa na mtu mwingine, hakikisha una ruhusa kutoka kwa wenye hakimiliki (yaani, mwandishi wa wimbo au mchapishaji wa muziki). Huenda ukahitaji leseni za ziada ili kutengeneza upya rekodi ya sauti halisi, ikiwa ni pamoja na wimbo katika video au kuonyesha maneno ya wimbo.

Kwa nini maudhui ambayo ninaruhusiwa kuyatumia yameondolewa au kuzuiwa?

Ikiwa una haki za kutumia nyenzo zinazolindwa kwa hakimiliki katika video yako, mtumie mwenye hakimiliki jina na URL ya video yako. Hatua hii inaweza kukusaidia kuzuia video kuondolewa au kuzuiwa kimakosa.

Endapo video yako iliondolewa kimakosa kupitia ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki, unaweza:

Iwapo video yako imezuiwa na dai la Content ID unalodhani si sahihi:

Hata hivyo, kabla hujapinga dai au kutuma arifa ya kukanusha, jiulize haya maswali machache:

  1. Je, wewe ni mwenye hakimiliki ya maudhui yaliyopo kwenye video yako?
  2. Je, una ruhusa ya kutumia maudhui yote ya wahusika wengine kwenye video yako kutoka kwa mwenye hakimiliki?
  3. Je, video yako inalindwa na kanuni ya matumizi ya haki, matumizi yasiyo ya biashara au hali nyingineyo inayofanana isiyofuata kanuni chini ya sheria husika ya hakimiliki?

Ikiwa mojawapo ya hali zilizo hapo juu zinatumika kwenye video yako, tunakushauri ufanye utafiti kuhusu mchakato wa kupinga dai unaofaa zaidi au uwasiliane na mwanasheria. Iwapo hakuna hali yoyote hapo juu inayoendana na video yako, huenda ukawa umekiuka sheria za hakimiliki.

Kwa nini maudhui niliyorekodi au kununua yameondolewa?

Kununua maudhui hakumaanishi kwamba unamiliki haki za kupakia maudhui hayo kwenye YouTube. Hata ukimtambua mwenye hakimiliki kwenye video au maelezo ya video, kuchapisha video zenye maudhui uliyonunua bado kunaweza kukiuka sheria ya hakimiliki.

Pia, kurekodi kitu hakumaanishi kwamba unamiliki haki zote za kupakia video hiyo kwenye YouTube. Iwapo video yako inajumuisha maudhui yaliyo na hakimiliki ya mtu mwingine, kama vile muziki ulio na hakimiliki unaocheza chinichini, bado utahitaji ruhusa kutoka kwa wamiliki sahihi wa haki.

Kwa nini YouTube imeruhusu video yangu kuondolewa na mlalamishi anayekiuka mchakato wa hakimiliki?
YouTube huchukua hatua ili kukabiliana na kesi za matumizi mabaya ya michakato yetu ya kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki. Japo hatuwezi kuzungumzia kesi mahususi au michakato yetu, tunafanya uchunguzi wa matumizi mabaya ya zana na michakato yetu ya hakimiliki. Pia, tuna sera ya kutoruhusu kabisa walalamishi tunaobaini kuwa wana matumizi mabaya ya zana na michakato ya hakimiliki. Matumizi mabaya ya mchakato wa hakimiliki (kwa maombi ya kuondoa video na arifa za kukanusha) yanaweza kusababisha akaunti kufungwa.
Kanusho: Maelezo yaliyo katika makala haya si ushauri wa kisheria. Tunayatoa tu kwa madhumuni ya kutoa taarifa. Ikiwa unatafuta ushauri wa kisheria, huenda ukahitaji kuwasiliana na mwanasheria.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
1622828721558372646
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false