Utaratibu wa Content ID

Baadhi ya wenye hakimiliki hutumia Content ID, mfumo wa kiotomatiki wa utambulisho wa maudhui ya YouTube, ili kutambua kwa urahisi na kudhibiti maudhui yao yanayolindwa kwa hakimiliki kwenye YouTube.

Je, mfumo wa Content ID hufanya nini?

Kwa kutumia hifadhidata ya faili za sauti na video zilizowasilishwa na wenye hakimiliki, Content ID hubainisha maudhui yanayolingana na yanayolindwa kwa hakimiliki. Video inapopakiwa kwenye YouTube, huchanganuliwa kiotomatiki na Content ID.

Ikiwa Content ID itapata video inayolingana, video inayopakiwa itapokea dai la Content ID. Kulingana na mipangilio ya Content ID ya mwenye hakimiliki, dai la Content ID husababisha mojawapo ya hatua zifuatazo:

  • Kuzuia video isitazamwe
  • Kuchuma mapato kwenye video kwa kuonyesha matangazo na wakati mwingine kugawana mapato na aliyepakia
  • Kufuatilia takwimu za watazamaji wa video

Kumbuka kuwa hatua yoyote kati ya hizi inaweza kutegemea eneo mahususi la kijiografia. Kwa mfano, video inaweza kuchumiwa mapato katika nchi au eneo moja na kuzuiwa au kufuatiliwa katika nchi au eneo tofauti.

Je, nani hutumia Content ID?

Content ID inapatikana kwa wenye hakimiliki wanaotimiza vigezo mahususi. Ili waidhinishwe, ni lazima wamiliki haki za kipekee za kiasi kikubwa cha maudhui halisi yanayopakiwa mara kwa mara kwenye YouTube.

YouTube huweka pia mwongozo dhahiri kuhusu jinsi Content ID inaweza kutumiwa. Matumizi na mizozo ya Content ID hufuatiliwa kila mara ili kuhakikisha kuwa mwongozo huu unafuatwa.

Wenye hakimiliki ambao mara kwa mara hutoa madai ya Content ID yaliyo na makosa wanaweza kuzimiwa ufikiaji wao wa Content ID na ushirika wao na YouTube ukasimamishwa.

Ikiwa wewe ni mwenye hakimiliki na unaamini kuwa maudhui yako yanatimiza vigezo vya Content ID, unaweza kujaza fomu hii ili utufahamishe zaidi kuhusu mahitaji yako ya udhibiti wa hakimiliki.

Mada zinazohusiana

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
5965956368164178409
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false