Maudhui yanayostahiki kwa Content ID

Vipengele vinavyofafanuliwa katika makala haya vinapatikana tu kwa washirika wanaotumia mifumo ya ulinganishaji wa Content ID katika YouTube.

Unapowasha maudhui kwa ajili ya ulinganishaji wa Content ID, YouTube huzalisha kiotomatiki madai dhidi ya maudhui mengine yaliyopakiwa na watumiaji wengine yanayolingana na (sehemu za) faili ya marejeleo unayotoa. Pata maelezo zaidi kuhusu misingi ya sera na madai.

Si maudhui yote yanafaa kwa ajili ya kudai kupitia Content ID. Usitumie mfumo kudai maudhui ambayo huna haki za kutosha kuyahusu. Una wajibu wa kuepuka matokeo yasiyo sahihi, kama vile madai yanayopelekea maudhui yaliyotambuliwa kwa njia isiyo sahihi au madai yanayokatiza matumizi yaliyoidhinishwa ya maudhui.

YouTube huchukua hatua ili kukabiliana na kesi za matumizi mabaya na hitilafu katika mfumo wa Content ID. Hii ni pamoja na kuzima faili mahususi za marejeleo au sehemu za faili za marejeleo na kuondoa madai yote yanayohusiana, kuhitaji mkague wenyewe aina fulani za marejeleo, kuzima Content ID au hata kusimamisha ushirika na YouTube.

Mwongozo wa Content ID

Tumia amri zifuatazo ili uepuke matatizo yoyote. Kumbuka kuwa mifano chini ya kila amri hutolewa kwa ajili ya kukufahamisha na hii si orodha kamilifu ya matatizo yanayoweza kutokea. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuepuka na kutatua madai yasiyo sahihi.

Haki za kipekee

Ni lazima uwe na haki za kipekee za maudhui yaliyo katika faili ya marejeleo kwa ajili ya maeneo ambako unadai umiliki.

Mifano ifuatayo hairuhusiwi kutumiwa katika au kama marejeleo:

  • Maudhui yaliyopewa leseni ya jumla kutoka kwa mhusika mwingine
  • Maudhui yaliyotolewa chini ya Creative Commons au leseni zisizolipishwa/huria kama hizo
  • Tungo, video au rekodi zilizo wazi kutumiwa na umma
  • Klipu kutoka vyanzo vingine zinazotumiwa kwa mujibu wa kanuni za matumizi ya haki
  • Video ya uchezaji wa video (na wengine tofauti na mchapishaji wa mchezo)
Maudhui ya marejeleo dhahiri

Ni lazima maudhui yote ya marejeleo yawe ya kipekee.

Mifano ifuatayo hairuhusiwi kutumiwa katika au kama marejeleo:

  • Rekodi za Karaoke, rekodi zilizoboreshwa, rekodi za sauti zinazofanana na maudhui fulani yaliyowekwa sauti nyingine (iliyotafsiriwa)
  • Madoido ya sauti, sauti zinazotumiwa chinichini ya maudhui mengine au rekodi za kucheza zikirudia bila kukoma
Marejeleo mahususi ya kila kipande cha mali ya uvumbuzi

Ni sharti utoe marejeleo mahususi kwa kila kipande cha mali ya uvumbuzi.

Mifano ifuatayo hairuhusiwi kutumiwa katika au kama marejeleo:

  • Mikusanyiko
  • Miseto Endelevu ya DJ
  • Michanganyiko
  • Orodha ya zinazovuma
  • Albamu kamili ya rekodi za sauti

Hata kama unamiliki kipekee maudhui yote katika aina hii ya mifano katika maeneo yote, ni sharti uyatenganishe katika vipengee, nyimbo na video mahususi.

Mwongozo wa Nyimbo Halisi za Mchezo wa Video

Nyimbo Halisi za Mchezo wa Video ni marejeleo yanayoruhusiwa pale tu ambapo yanamilikiwa na mchapishaji wa mchezo wa video.

Nyimbo Halisi za Mchezo wa Video ni rekodi za sauti zilizotungwa maalum kwa ajili ya matumizi katika mchezo wa video, kama vile wimbo halisi au muziki wa chinichini unaochezwa kwenye mchezo wa video. (Sera hii haitumiki kwenye muziki maarufu uliopewa leseni, ambao haukutungwa maalum kwa ajili ya mchezo.)

Marejeleo haya yanatumika tu yanapowasilishwa chini ya mmiliki wa maudhui ya mchapishaji wa mchezo wa video. Ikiwa wewe ni mchapishaji wa mchezo na una maswali, tafadhali wasiliana na msimamizi wako wa washirika.

Maudhui yanayouzwa au kupewa leseni kwa kiwango kinachofaa ili yajumuishwe kwenye kazi nyingine

Maudhui yanayouzwa au kupewa leseni kwa kiwango kinachofaa ili yajumuishwe kwenye kazi nyingine ni sharti yaelekezwe kwa ukaguzi.

Kwa mfano, ni sharti maudhui yanayolingana na aina zifuatazo za maudhui yaelekezwe kwa wakaguzi kabla ya kudaiwa:

  • Maktaba za muziki za uzalishaji unaosemekana kuwa "hauna mirabaha" uliopewa leseni kwa kawaida kwa ajili ya matumizi katika mchezo, filamu, televisheni au nyimbo nyingine.
Metadata ya kipengee ya maudhui ya marejeleo

Unapojaza metadata ya kipengee yako, weka maelezo mahususi uwezavyo. Ni sharti wanaopakia wapewe maelezo ya kutosha ili kuelewa ni maudhui gani yanadaiwa na nani anayemiliki maudhui hayo. Ni sharti vipengee vyote vijumuisha kichwa chenye maelezo (k.m., sio “Wimbo wa 4” au nambari ya ufuatiliaji wa ndani).

Vile vile, kwa kila aina ya kipengee ifuatayo, kiasi cha chini kinachohitajika cha metadata ya kipengee kinapaswa kuwekwa kama ifuatavyo:

  • Ikiwa kipengee ni rekodi ya sauti au video ya muziki, weka Jina, Msanii, na Studio ya Kurekodia
  • Ikiwa kipengee ni utungo wa muziki, weka Jina na Mwandishi
  • Ikiwa kipengee ni kipindi cha televisheni, weka Jina la Onyesho na Jina la Kipindi au Namba ya Kipindi
  • Ikiwa kipengee ni filamu, weka Jina na Waelekezi
  • Ikiwa kipengee ni tangazo la spoti, weka Majina ya Timu (majina ya washindani ikiwa ni mchezo wa mtu binafsi) na tarehe ya tukio

Tunakuhimiza pia kuweka metadata nyingine yoyote inayoweza kusaidia kubaini vipengee mahususi.

Maudhui ya marejeleo ya alama bainifu pekee

Ikiwa unafikia zana iliyopitwa na wakati inayokuruhusu kuweka alama bainifu za sauti na video kama marejeleo bila kuweka faili za maudhui husika, unapaswa kufahamu sera zifuatazo:
  1. Marejeleo ya alama bainifu pekee yatabadilishwa kiotomatiki na marejeleo ya faili ya maudhui yanayozingatia maudhui yanayofanana.  Ukiweka marejeleo ya alama bainifu pekee, nakala ya marejeleo ya faili ya maudhui itatengenezwa kwa niaba yako na kuhusishwa na akaunti yako kuhusu kipengee cha Content ID.
  2. Marejeleo ya alama bainifu pekee hayawezi kusasishwa kiotomatiki ili kutumia teknolojia mpya ya Ulinganishaji wa Content ID. Kwa hivyo, ikiwa wewe ni mtumiaji wa marejeleo ya alama bainifu pekee na hujasasisha marejeleo husika ya alama bainifu pekee miezi sita baada ya kupokea mfumo mpya wa jozi wa kuunda alama bainifu, marejeleo yaliyopitwa na wakati huenda yakazimwa kiotomatiki.

 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
739219949495100890
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false