Miundo ya Utangazaji kwenye YouTube

Tumerahisisha chaguo za miundo ya matangazo yanayoonyeshwa kabla au baada ya video yako kucheza ili kuongeza mapato ya mtayarishi. Tumeondoa chaguo za matangazo mahususi kwa matangazo yanayoonyeshwa kabla ya video kucheza au baada ya video kucheza, yanayoweza kurukwa na yasiyorukika. Sasa unapowasha matangazo kwenye video ndefu mpya, tunawaonyesha watazamaji wako matangazo yanayoonyeshwa kabla ya video kucheza au baada ya video kucheza, yanayoweza kurukwa na yasiyorukika panapofaa. Badiliko hili linafanya mbinu bora zinazopendekezwa za kuwasha miundo yote ya matangazo zifae kwa kila mtu. Chaguo zako za matangazo yanayochezwa katikati ya video hazijabadilika. Pia, tumehifadhi chaguo zako za matangazo katika video ndefu zilizopo, isipokuwa ukibadilisha mipangilio ya uchumaji wa mapato.
Ili kuboresha hali ya utazamaji na kuongeza utendaji wa miundo ya matangazo kwenye kompyuta ya mezani na vifaa vya mkononi, YouTube haitaonyesha tena matangazo yaliyowekelewa juu ya maudhui kuanzia tarehe 6 Aprili, 2023. Matangazo yaliyowekelewa juu ya maudhui ni ya muundo wa matangazo uliopitwa na wakati unaoonekana tu kwenye kompyuta ya mezani na tunatarajia athari ndogo tu kwa uchumaji wa mapato kwa Watayarishi wengi jinsi ushirikishaji unavyohamia kwenye miundo mingine ya matangazo.

Kuna aina kadhaa za matangazo ambayo yanaweza kuonekana wakati video zinacheza au pembeni ya video zako ikiwa umewasha kipengele cha uchumaji wa mapato kupitia video. Tunaweza kuonyesha miundo ya matangazo katika jedwali hapa chini kabla ya ("kabla"), wakati wa ("katikati") au baada ya ("baada") video kucheza.

Unapowasha matangazo kwenye video ndefu mpya, tunawaonyesha kiotomatiki watazamaji wako matangazo yanayoonyeshwa kabla ya video kucheza au baada ya video kucheza, yanayoweza kurukwa na yasiyorukika panapofaa. Unaweza pia kuwasha matangazo yanayochezwa katikati ya video kwa video zenye urefu wa zaidi ya dakika 8 na uamue ikiwa utaweka mapumziko ya matangazo mwenyewe au kiotomatiki. Pata maelezo zaidi kuhusu kudhibiti matangazo yanayochezwa katikati ya video.

Muundo wa tangazo la video Maelezo Mfumo Viwango
Matangazo ya video yanayoweza kurukwa

Matangazo ya video yanayoweza kurukwa huwawezesha watazamaji kuruka matangazo baada ya sekunde 5. Kompyuta, vifaa vya mkononi, televisheni na vifaa vya michezo ya video Hucheza katika kicheza video (unaweza kuliruka baada ya sekunde 5).

Matangazo ya video yasiyoweza kurukwa

Matangazo ya video yasiyowezesha kurukwa sharti yatazamwe kabla ya video kutazamwa. Kompyuta, vifaa vya mkononi, televisheni na vifaa vya michezo ya video

Hucheza katika kicheza video.

Urefu wa sekunde 15 au 20, kulingana na viwango vya eneo husika. Kwenye TV pekee, inaweza kuwa sekunde 30.

Matangazo ya bamba

Matangazo mafupi ya video yasiyoweza kurukwa yanayoweza kucheza kwa hadi sekunde 6, ambayo ni lazima yatazamwe kabla ya video kutazamwa. Matangazo kwenye bamba huwashwa wakati matangazo yanayoweza kurukwa au yasiyoweza kurukwa yamewashwa. Kompyuta, vifaa vya mkononi, televisheni na vifaa vya michezo ya video Hucheza kwa hadi sekunde 6 katika kicheza video.

Washa matangazo kwenye video nyingi

Ili uwashe matangazo kwenye video nyingi ambazo umeshapakia tayari:

  1. Nenda kwenye Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui .
  3. Teua kisanduku cha kijivu kilicho upande wa kushoto wa kijipicha cha video yoyote unayotaka kutumia kuchuma mapato.
  4. Bofya menyu kunjuzi ya Badilisha katika upau mweusi ulio juu ya orodha ya video kisha Uchumaji wa mapato.
  5. Bofya Washa katika menyu kunjuzi ya uchumaji wa mapato.
    • Ili ubadilishe mipangilio ya matangazo yanayochezwa katikati ya video kwa wingi: Bofya Badilisha kisha Mipangilio ya matangazo kisha Teua kisanduku karibu na “Weka matangazo wakati video inacheza (katikati ya video)” na uamue ikiwa unataka matangazo yanayochezwa kiotomatiki katikati ya video bila mapumziko ya matangazo au video zote.
  6. Bofya Sasisha video kisha Teua kisanduku kilicho karibu na “Ninaelewa matokeo ya kitendo hiki” kisha Sasisha video.

Matangazo ya Video Fupi za YouTube

Matangazo kwenye Video Fupi ni matangazo ya video au picha yanayoweza kuondelewa papo hapo kwa kutelezeshwa yanayoonekana kati ya Video Fupi kwenye Mipasho ya Video Fupi. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi matangazo yanavyofanya kazi kwenye Sera za uchumaji mapato kwenye Video Fupi za YouTube.

Mipangilio chaguomsingi ya tangazo linalochezwa katikati ya video

Pata maelezo kuhusu jinsi ya kubadilisha mipangilio chaguomsingi ya kituo chako ili uangazie mapumziko ya matangazo yanayochezwa katikati ya video katika vipakiwa vipya.

Matangazo nje ya kicheza video

Matangazo ya mipasho unayotazama ni matangazo yanayoonekana kwenye mipasho ya video zinazopendekezwa chini ya kichezaji kwenye kifaa cha mkononi na karibu na kichezaji kwenye kompyuta. Aina hizi za matangazo haziwezi kudhibitiwa ndani ya Studio ya YouTube.

Matangazo yanayofuatana

Pia, hujulikana kama podi za matangazo, matangazo mawili yanayofuatana ya video yanaweza kutokea unapowasha matangazo kwenye video yako ndefu (angalau urefu wa dakika 5). Podi za matangazo husaidia kupunguza matukio ya kukatizwa kwa watazamaji wa video ndefu na hivyo kuwapatia hali bora zaidi watazamaji.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9920184693639683557
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false