Kukata Rufaa dhidi ya onyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya au kuondolewa kwa video

Maudhui haya yanashughulikia jinsi ya kukata rufaa dhidi ya uondoaji na maonyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya. Iwapo video yako iliondolewa kwa sababu za hakimiliki, pata maelezo kuhusu chaguo ulizo nazo za maonyo ya hakimiliki.

Tunapoondoa maudhui yako kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya, huenda ukapokea onyo. Maonyo hutolewa maudhui kwenye YouTube yanaporipotiwa ili yakaguliwe, na wanajumuiya wa YouTube au teknolojia yetu mahiri ya utambuzi, na timu zetu za ukaguzi zikaamua kuwa maudhui hayo hayafuati Mwongozo wa Jumuiya yetu. Iwapo chaneli yako itapokea onyo, utapata barua pepe, arifa kwenye kifaa cha mkononi na kompyuta ya mezani, na arifa katika mipangilio ya chaneli yako wakati mwingine unapoingia katika akaunti ya YouTube.

Kabla ya kuanza, kagua sera inayohusiana na onyo. Pia, tunaorodhesha mifano ya maudhui yanayosababisha onyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya. Unaweza tu kukata rufaa kwa siku 90 baada ya kupokea tahadhari au onyo.

Programu ya Studio ya YouTube kwenye Android

  1. Fungua programu ya Studio ya YouTube .
  2. Kwenye Menyu ya chini, gusa Maudhui .
  3. Chagua video iliyo na kizuizi, kisha uguse kizuizi hicho.
  4. Gusa Kagua matatizo.
  5. Gusa dai husika.
  6. Weka sababu yako ya kukata rufaa kisha ubofye Tuma.

Ikiwa ni orodha au kijipicha:

Utapokea barua pepe iwapo orodha au kijipicha chako kiliondolewa kwa kukiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya. Iwapo unaamini kuwa maudhui hayakiuki Mwongozo wa Jumuiya na yaliondolewa kimakosa, tumia fomu iliyotolewa katika barua pepe kukata rufaa.

Kumbuka: Hatua ya kufuta video haitasuluhisha onyo. Ukifuta video yako, onyo litasalia kwenye chaneli yako na hutaweza kukata rufaa tena.

Iwapo ulipokea onyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya kwenye viungo katika maudhui yako, hakikisha kuwa unafahamu sera na mchakato wetu wa kukata rufaa kwa viungo katika maudhui yako.

Kukata Rufaa dhidi ya onyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya

Tunapoondoa maudhui yako kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya, huenda ukapokea onyo. Maonyo hutolewa maudhui kwenye YouTube yanaporipotiwa ili yakaguliwe, na wanajumuiya wa YouTube au teknolojia yetu mahiri ya utambuzi, na timu zetu za ukaguzi zikaamua kuwa maudhui hayo hayafuati Mwongozo wa Jumuiya yetu. Iwapo chaneli yako itapokea onyo, utapata barua pepe, arifa kwenye kifaa cha mkononi na kompyuta ya mezani, na arifa katika mipangilio ya chaneli yako wakati mwingine unapoingia katika akaunti ya YouTube.

Kabla ya kuanza, kagua sera inayohusiana na onyo. Pia, tunaorodhesha mifano ya maudhui yanayosababisha onyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya. Unaweza tu kukata rufaa kwa siku 90 baada ya kupokea tahadhari au onyo.

Kukata rufaa dhidi ya onyo 

  1. Nenda kwenye Dashibodi yako ya Studio ya YouTube.
  2. Chagua kadi ya ukiukaji wa Kituo.
  3. Chagua KATA RUFAA.
Kumbuka: Hatua ya kufuta video haitasuluhisha onyo. Ukifuta video yako, onyo litasalia kwenye chaneli yako na hutaweza kukata rufaa tena.

Iwapo ulipokea onyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya kwa sababu ya viungo vilivyo katika maudhui yako, hakikisha kuwa unafahamu sera na mchakato wetu wa kukata rufaa kuhusu viungo vilivyo katika maudhui yako.

Ikiwa ni orodha au kijipicha:
Utapokea barua pepe iwapo orodha au kijipicha chako kiliondolewa kwa kukiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya. Iwapo unaamini kuwa maudhui hayakiuki Mwongozo wa Jumuiya na yaliondolewa kimakosa, tumia fomu iliyotolewa katika barua pepe kukata rufaa.

Kumbuka: Video zinaweza kuondolewa kwa sababu nyingi. Iwapo unatatizika kukata rufaa dhidi ya uondoaji wa video, huenda iliondolewa kwa sababu nyingine mbali na ukiukaji wa Mwongozo wa Jumuiya. Unaweza kutatua uondoaji wa video kupitia makala haya ya Kituo cha Usaidizi

Ukishakata rufaa

Utapokea barua pepe kutoka YouTube inayokufahamisha matokeo ya ombi lako la kukata rufaa. Mojawapo kati ya yafuatayo litafanyika:

  • Tukibaini kuwa maudhui yako yalifuata Mwongozo wa Jumuiya yetu, tutayarejesha na kuondoa onyo kwenye chaneli yako. Iwapo utakata rufaa dhidi ya onyo na rufaa ikubaliwe, kosa litakalofuata litakuwa na tahadhari.
  • Tukibaini kuwa maudhui yako yalifuata Mwongozo wa Jumuiya yetu, lakini hayafai hadhira zote, tutaweka mipaka ya umri. Iwapo ni video, haitaonekana kwa watumiaji ambao hawajaingia kwenye akaunti, wana umri wa chini ya miaka 18 au wamewasha Hali Yenye Mipaka . Iwapo ni kijipicha maalum, kitaondolewa.
  • Tukibaini kuwa maudhui yako yalikiuka Mwongozo wa Jumuiya yetu, onyo litabaki na video haitarejeshwa kwenye tovuti. Hamna adhabu ya ziada kwa rufaa zilizokataliwa.

Unaweza kukata rufaa dhidi ya kila onyo mara moja tu.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
1817079341516928656
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false