Kuwasha au kuzima Hali yenye Mipaka kwenye YouTube

Hali Yenye Mipaka ni mipangilio isiyo ya lazima unayoweza kutumia kwenye YouTube. Kipengele hiki kinaweza kukusaidia kuchuja maudhui ambayo huenda yakawa ya watu wazima ambayo wewe au wengine wanaotumia vifaa vyako msingependa kuona. 

Kompyuta katika maktaba, vyuo vikuu na taasisi nyingine za umma zinaweza kuwa na Hali yenye Mipaka iliyowashwa na msimamizi wa mtandao.

Kumbuka: Kuwasha kipengele cha Hali yenye Mipaka si sawa na kuwekea video mipaka ya umri. Pata maelezo zaidi kuhusu maudhui yenye mipaka ya umri.

How to turn Restricted Mode on and off

Fuatilia chaneli ya Watazamaji ya YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.

Kuwasha au kuzima Hali yenye mipaka

  1. Ingia katika akaunti yako.
  2. Katika sehemu ya juu kulia, gusa picha yako ya wasifu .
  3. Katika sehemu ya chini, bofya Hali yenye mipaka.
  4. Katika kisanduku cha sehemu ya juu kulia kinachofunguka, ili uwashe au uzime Hali yenye mipaka, bofya Wezesha Hali yenye mipaka.

Tatua hitilafu za kuzima Hali yenye mipaka

Ikiwa umeweka jina la mtumiaji na nenosiri lako, na mipangilio ya Hali yenye mipaka inaendelea kuwaka, unaweza kuangalia mipangilio yako kwenye ukurasa wa vizuizi vya maudhui kwenye YouTube kwa maelezo zaidi. Zana itatathmini iwapo msimamizi aliweka vizuizi hivi, au iwapo vipo kwenye akaunti yako ya binafsi. Alama ya kuteua itaonyeshwa kando ya kizuizi husika. Ikiwa usaidizi zaidi unahitajika, zana itakuelekeza kwenye hatua inayofuata ya utatuzi.

Kumbuka: Baadhi ya watoa huduma za mtandao wa simu hutoa vichujio vya maudhui. Vichujio hivi huzuia aina ya maudhui ya wavuti unayoweza kufikia wakati kifaa chako kimeunganishwa kwenye mtandao wao wa simu. Angalia ukurasa wa vizuizi vya maudhui kwenye YouTube ili uone iwapo una vizuizi vyovyote katika kiwango cha mtandao au akaunti. Alama ya kuteua itaonyeshwa kando ya kizuizi husika, maandishi yaliyo hapa chini yataonyesha kiwango cha kizuizi. Ikiwa vizuizi vya DNS vimewashwa, na kiwango kimewekwa kuwa “wastani” au “kali," mipangilio ya kuchuja maudhui imewashwa. Jaribu kuwasiliana na mtoa huduma wa mtandao wako wa simu ili upate maelezo kuhusu jinsi ya kudhibiti au kuzima mipangilio hii.

Dhibiti Hali yenye mipaka kwa ajili ya familia yako

Ikiwa wewe ni mzazi unayetumia programu ya Family Link, unaweza kuwasha Hali yenye mipaka kwa ajili ya akaunti ya mtoto wako ikiwa hajatimiza masharti ya matumizi yanayosimamiwa kwenye YouTube. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuwasha Hali yenye mipaka katika Mipangilio ya programu ya Family Link.

Unapowasha Hali yenye mipaka katika programu ya Family Link, mtoto wako hawezi kubadilisha mipangilio ya Hali yenye mipaka kwenye kifaa chochote alikoingia katika akaunti.

Kumbuka: Huwezi kuweka mipangilio ya Hali yenye mipaka kwa ajili ya mtoto wako iwapo:

Pata maelezo zaidi kuhusu Hali yenye mipaka

  • Tunatumia ishara nyingi, kama vile jina la video, maelezo, metadata, Mwongozo wa Jumuiya maoni, na mipaka ya umri ili kubaini na kuchuja maudhui ambayo huenda yakawa ya watu wazima.
  • Hali yenye mipaka inapatikana katika kila lugha, lakini kutokana na tofauti za taratibu na kawaida za kitamaduni, ubora inaweza kutofautiana.
  • Wakati umewasha Hali Yenye Mipaka, huwezi kuona maoni kwenye video unazotazama.
  • Hali yenye mipaka hufanya kazi kwenye kiwango cha kivinjari au kifaa, kwa hivyo lazima iwashwe kwa kila kivinjari unachotumia. Ikiwa kivinjari au kifaa chako kinaruhusu kutumia zaidi ya wasifu mmoja, ni lazima uwashe hali hii kwa ajili ya kila wasifu.
  • Watayarishi: Pata maelezo kuhusu jinsi Hali yenye mipaka inavyoathiri maudhui yako.

Spika ya Programu ya Mratibu na Skrini Mahiri

  1. Fungua programu ya Google Home kwenye kifaa chako cha mkononi.
  2. Gusa Spika au Skrini Mahiri ambayo ungependa kurekebisha.
  3. Gusa Mipangilio.
  4. Gusa Arifa na nidhamu dijitali.
  5. Gusa Mipangilio ya YouTube.
  6. Kuna njia mbili unazoweza kutumia kudhibiti mipangilio ya Hali yenye Mipaka kwenye Skrini yako Mahiri:
    1. Unaweza kuwasha au kuzima Hali yenye Mipaka wewe mwenyewe, na
    2. Ikiwa wewe ni msimamizi wa kifaa, unaweza kuwasha au kuzima Hali yenye Mipaka kwa ajili ya watumiaji wengine wote.
Kumbuka: Hali yenye Mipaka huwekwa kwenye kifaa. Ikiwa maudhui hayachezi kwenye kifaa chako, angalia mipangilio yako ya Hali yenye Mipaka. 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
4765215709268281345
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false