Kuweka bidhaa zilizolipiwa ili zitangazwe katika maudhui, udhamini na maudhui yaliyoidhinishwa

Unaweza kujumuisha bidhaa zinazolipiwa ili zitangazwe katika maudhui, maudhui yaliyoidhinishwa, udhamini au maudhui mengine yanayohitaji ufumbuzi kwa watazamaji katika video zako. Unapaswa kutujulisha ikiwa utachagua kujumuisha yoyote kati ya hayo kwa kuchagua kisanduku cha matangazo yanayolipiwa katika maelezo ya video yako. 

Matangazo yote yanayolipiwa yanapaswa kufuata sera za Google Ads na Mwongozo wa Jumuiya wa YouTube. Wewe na chapa unazofanya nazo kazi mna jukumu la kuelewa na kutii wajibu wa kisheria na wa mahali ulipo yanayohusu ufumbuzi wa Matangazo Yanayolipiwa katika maudhui. Wajibu huu unajumuisha wakati, jinsi na hadhira mahususi inayostahili kupewa ufumbuzi.

Iwapo ungependa kutafuta video mahususi ambazo mtayarishi amebainisha kuwa zina matangazo yanayolipiwa, tumia kiungo hiki. Ikiwa unatumia kifaa cha mkononi, gusa na ushikilie kiungo ili unakili anwani ya wavuti, kisha ukibandike kwenye sehemu ya viungo muhimu ya kivinjari chako.
Sehemu ambazo hupaswi kujumuisha bidhaa zinazolipiwa ili zitangazwe katika maudhui, udhamini na maudhui yaliyoidhinishwa

Kufuata Sera za Google Ads kunamaanisha huwezi kujumuisha matangazo yanayolipiwa ya bidhaa na huduma zifuatazo kwenye maudhui yako:

  • Bidhaa au huduma zisizo halali
  • Huduma za ngono na ukahaba
  • Maudhui ya watu wazima
  • Mabibi harusi kupitia barua
  • Dawa za kujistarehesha
  • Dawa ambazo hazijaagizwa na daktari
  • Tovuti za kucheza kamari mtandaoni ambazo bado hazijakaguliwa na Google au YouTube
  • Huduma za kufanya udanganyifu kwenye mitihani au majaribio
  • Udukuzi, wizi wa data binafsi au vidadisi
  • Vilipuzi
  • Biashara za ulaghai au zinazopotosha

Sera hii hutumika kwa video, maelezo ya video, maoni, mitiririko mubashara, Video Fupi na bidhaa au vipengele vingine vyovyote kwenye YouTube. Hii ni orodha ambayo haijataja vipengele vyote. Usichapishe maudhui iwapo unafikiri kuwa huenda yatakiuka sera hii. 

Mifano

Ifuatayo ni baadhi ya mifano ya maudhui ambayo hayaruhusiwi kwenye YouTube.

  • Matangazo yanayolipiwa ya huduma za kuandika insha za kielimu
  • Matangazo yanayolipiwa ya tovuti inayouza pasipoti bandia au kutoa maagizo kuhusu kutengeneza hati rasmi bandia
  • Matangazo yanayolipiwa ya programu inayozalisha namba bandia za kadi za mikopo
  • Matangazo yanayolipiwa ya duka la dawa la mtandaoni linalouza dawa zinazodhibitiwa bila maagizo ya daktari

Kitakachofanyika iwapo maudhui yako yatakiuka sera hii

Iwapo maudhui yako yatakiuka sera hii, tutaondoa maudhui hayo na kukutumia barua pepe ili kukufahamisha. Iwapo hii ni mara yako ya kwanza kukiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya, utapewa tahadhari bila kupewa adhabu kwenye chaneli yako. Unaweza kushiriki katika mafunzo ya sera ili kuruhusu muda wa tahadhari uishe baada ya siku 90. Hata hivyo, ikiwa maudhui yako yatakiuka sera ile ile ndani ya kipindi cha siku 90, muda wa tahadhari hautaisha na chaneli yako itapewa onyo. Ikiwa utakiuka sera tofauti baada ya kukamilisha mafunzo, utapewa tahadhari nyingine. Huenda tukazuia watu wanaorudia kufanya makosa wasishiriki katika mafunzo ya sera siku zijazo.

Ukipata maonyo 3, chaneli yako itasimamishwa. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu Maonyo msingi kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya kwenye YouTube

Pia, tunaweza kuweka mipaka ya umri kwenye maudhui iwapo bidhaa au huduma inayotangazwa haifai watu wa rika zote.

Je, tunamaanisha nini tunapozungumzia bidhaa zinazolipiwa ili zitangazwe katika maudhui, maudhui yaliyoidhinishwa na udhamini?

Bidhaa zinazolipiwa ili zitangazwe katika maudhui ni vipande vya maudhui vinavyobuniwa kwa ajili ya mtu au kampuni nyingine kwa malipo. Maudhui kama haya pia ni yale ambapo chapa, ujumbe au bidhaa za wengine zinajumuishwa moja kwa moja katika maudhui.

Maudhui yaliyoidhinishwa ni maudhui yaliyobuniwa kwa ajili ya mtangazaji (au kwa ajili ya chapa binafsi ya mtayarishi iwapo uhusiano kati ya mtayarishi au chapa si dhahiri) yakiwa na ujumbe ambao watumiaji wana uwezekano wa kuamini kuwa unaangazia maoni ya mtayarishi wa maudhui.

Udhamini ni vipande vya maudhui ambavyo vimefadhiliwa kikamilifu au kwa sehemu na wengine. Kwa jumla, udhamini unatangaza chapa, ujumbe au bidhaa za wengine bila kujumuisha chapa, ujumbe au bidhaa moja kwa moja katika maudhui.

Kumbuka kuwa sheria zinazotumika kwako zinaweza kufafanua matangazo yanayolipiwa kwa njia tofauti. Watayarishi na chapa wana wajibu wa kufahamu na kufuata kikamilifu wajibu wa kisheria ili kufumbua matangazo yanayolipiwa katika maudhui yao kwa mujibu wa eneo waliko la mamlaka. Huenda wajibu wa kisheria ukajumuisha wakati na jinsi ya kufumbua na hadhira inayofumbuliwa.

Watayarishi na chapa wanapaswa pia kufahamu iwapo aina mahususi za matangazo yanayolipiwa zinaruhusiwa chini ya sheria za mahali walipo. Kwa mfano, nchini Uingereza na Umoja wa Ulaya, video fulani zinazobainishwa kuwa "vipindi vya watoto" chini ya Agizo la Huduma za Maudhui ya Sauti na Video zinaweza kupigwa marufuku zisijumuishe udhamini au bidhaa zinazolipiwa ili zitangazwe katika maudhui.
Je, ninahitaji kufahamisha YouTube iwapo video yangu ina bidhaa zinazolipiwa ili zitangazwe katika maudhui, maudhui yaliyoidhinishwa au uhusiano mwingine wa kibiashara?
Iwapo maudhui yako yana bidhaa zilizolipiwa ili zitangazwe katika maudhui, maudhui yaliyoidhinishwa au uhusiano mwingine wa kibiashara, unahitaji kufahamisha YouTube ili tuwezeshe ufumbuzi kwa watumiaji. Kumbuka kuwa huenda ukawa na wajibu zaidi kulingana na sheria katika eneo uliko la mamlaka. Iwapo hutafuata wajibu huo, tunaweza kuchukua hatua dhidi ya maudhui au akaunti yako. Ili ufahamishe YouTube:
  1. Kwenye kompyuta, ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye sehemu ya kushoto, chagua Maudhui.
  3. Bofya video ambayo ungependa kuhariri.
  4. Teua Chaguo zaidi
  5. Teua kisanduku kilicho karibu na “Video yangu ina matangazo yanayolipiwa kama vile utangazaji wa bidhaa, udhamini au maudhui yaliyoidhinishwa.”
  6. Chagua HIFADHI.

Nini kitafanyika iwapo nitateua kisanduku cha "Video yangu ina matangazo yanayolipiwa kama vile utangazaji wa bidhaa, udhamini au maudhui yaliyoidhinishwa"?
Ukiteua kisanduku cha "video ina matangazo yanayolipiwa" chini ya sehemu ya "Taarifa ya kubainisha maudhui" kwenye Mipangilio ya Kina, unasaidia kudumisha hali bora kwa mtazamaji.
Bado tutaonyesha matangazo kwenye video hizi. Unapotujulisha kuwa video inajumuisha matangazo yanayolipiwa, tunaweza kubadilisha tangazo linalokinzana na mshirika wa chapa yako kwa kuweka tangazo mbadala. Pia, ukitujulisha, tutaondoa video yako kwenye programu ya YouTube Kids kwa mujibu wa sera zetu zilizopo.
Je, bado YouTube itaonyesha matangazo kwenye video hizi?
Ndiyo, bado YouTube itaonyesha matangazo kwenye video hizi.
 
Wakati mwingine, tunaweza kubadilisha tangazo linalokinzana na tangazo la mshirika wa chapa yako kwa kuweka tangazo tofauti kwenye video zilizo na matangazo yanayolipiwa. Mabadiliko haya yanafanyika ili kulinda thamani tunayowapa watangazaji.
 
Kwa mfano, ukipakia video iliyo na mitajo ya chapa na matangazo ya bidhaa ya Kampuni A. Haitakuwa na maana kuuza nafasi ya tangazo katika video hiyo kwa Kampuni B.
Je, ninahitaji kumwambia mtu mwingine yeyote kuhusu uhusiano wowote wa kibashara uliopo kwenye video yangu?
Huenda ukahitaji kufanya hivyo. Maeneo tofauti ya mamlaka yana masharti kadhaa kwa watayarishi na chapa zinazohusishwa katika matangazo yanayolipiwa. 
 
Wakati maudhui yako yanajumuisha matangazo yanayolipiwa, baadhi ya maeneo ya mamlaka na washirika wa chapa wanahitaji uwaambie watazamaji kuhusu uhusiano wowote wa kibiashara ambao huenda ulishawishi maudhui yako. Ni wajibu wako kukagua na kutii sheria na kanuni kuhusu maudhui ya matangazo yanayolipiwa ambayo yanatumika kwako. 
Je, kuna kipengele kinachoweza kunisaidia kuwafahamisha watazamaji kuhusu Matangazo Yanayolipiwa katika video zangu?

Ndiyo. Wakati wowote unapoweka alama kuwa video yako ina matangazo yanayolipiwa, tunaonyesha watazamaji kiotomatiki ujumbe wa ufumbuzi kwa sekunde 10 mwanzoni mwa video. Ujumbe huu wa ufumbuzi utamfahamisha mtazamaji kuwa video ina matangazo yanayolipiwa na ina kiungo cha ukurasa huu unaoelimisha watumiaji kuhusu kulipia bidhaa ili zitangazwe katika maudhui, udhamini na maudhui yaliyoidhinishwa.

Kumbuka kuwa, maeneo tofauti ya mamlaka yana masharti kadhaa kwa watayarishi na chapa zinazojumuishwa katika tangazo linalolipiwa ambayo huenda yakahitaji uchukue hatua zaidi. Hakikisha umekagua na kufuata sheria zinazotumika. 

Je, hali hii inamaanisha kuwa ninaweza kujumuisha matangazo ya video (kabla ya video kucheza, katikati ya video na baada ya video kucheza) katika video zangu?
Hapana. sera za matangazo za YouTube hazikuruhusu kuweka au kupachika matangazo ya video yaliyobuniwa na kusambazwa na watangazaji au matangazo mengine ya kibiashara kwenye maudhui yako. 
 
Iwapo una mtangazaji ambaye angependa kuonyesha matangazo hasa kwenye maudhui yako, shirikiana na msimamizi wa washirika wako. Angalia maelezo zaidi kwenye sera zetu kuhusu udhamini uliopachikwa na wahusika wengine.
 
Sera hii haitumiki kwenye video zilizobuniwa na au kwa ajili ya chapa na kupakiwa kwenye chaneli ya YouTube ya chapa. 
Je, ninaweza kutumia kadi yenye maelezo kabla au baada ya video iliyo na jina la mtangazaji au chapa ya mdhamini na maelezo kuhusu bidhaa?
Ndiyo. Tunaruhusu kadi zenye maelezo na kadi za mwishoni zisizobadilika ambako kuna matangazo yanayolipiwa. Kadi hizi zenye maelezo na kadi za mwishoni zinaweza kujumuisha picha na mdhamini au nembo ya mtangazaji na chapa ya bidhaa.
  • Kadi zenye maelezo: Sekunde 5 au chache zaidi na zisizobadilika. Iwapo zimewekwa mwanzoni mwa video (sekunde 0:01), lazima kadi iambatanishwe na chapa iliyo na jina au nembo ya mtayarishi.
  • Kadi za mwishoni: Huwekwa ndani ya sekunde 30 za mwisho za video na lazima zisibadilike. 
Nyenzo zaidi
Kwa maelezo zaidi, tunapendekeza urejelee mara kwa mara nyenzo za kisheria za mahali ulipo, kama vile Tume ya Biashara ya Marekani (FTC), Mamlaka ya Viwango vya Utangazaji (ASA) nchini Uingereza, Ofisi Kuu ya Ushindani, Masuala ya Watumiaji na Kuzuia Ulaghai (DGCCRF) nchini Ufaransa, mamlaka za vyombo vya habari Medienanstalten nchini Ujerumani au Tume ya Kuhakikisha Haki kwenye Biashara nchini Korea (KFTC).
Maelezo yaliyotolewa kwenye makala haya ya Kituo cha Usaidizi si ushauri wa kisheria. Tunayatoa kwa madhumuni ya kutoa maelezo, kwa hivyo, ukipenda unaweza kuwasiliana na wawakilishi wako wa kisheria.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9835306445702996922
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false