Kuunganisha maudhui yako ya kibiashara na akaunti ya mtangazaji

Iwapo unashirikiana na mtangazaji kwenye kampeni ya maudhui yaliyo na chapa, mtangazaji anaweza kutuma ombi la kuunganisha maudhui yaliyo katika kampeni na akaunti yake ya Google Ads. Ukikubali maombi yao, watangazaji wanaweza kuangalia vipimo vya utendaji wa maudhui kwenye Google Ads. YouTube pia itamruhusu mtangazaji (na asasi zozote zilizounganishwa na akaunti ya Google Ads ya mtangazaji) alenge matangazo kwa watazamaji wa video ya YouTube, kama inavyoruhusiwa na mfumo wa Google Ads.

Kuunganisha maudhui yako ya kibiashara na akaunti ya mtangazaji wako kunaweza kukusaidia:

  • Kudhibiti ushirika na biashara
  • Kutuma vipimo halisi vya video
  • Kuongeza uwezekano wa watangazaji kutangaza maudhui yako

Maombi mengi ya kuunganisha yanatoka kwa watangazaji ambao umeshirikiana nao hapo awali, lakini unaweza kupata maombi kutoka kwa biashara ambazo hukuwahi kushirikiana nazo. Kukubali ombi la mtangazaji la kuunganisha, iwe umeshirikiana naye au la, ni uamuzi wako. Kila wakati, unapaswa kuchukua hatua zinazofaa zaidi chaneli yako.

Ukikubali ombi lake, kumbuka kuwa utahitaji kutoa haki za kutosha kwa mtangazaji ili aweze kutumia video yako katika utangazaji wake na kwamba YouTube haihusiki katika mkataba huo. Hakikisha kuwa unaelewa masharti ya makubaliano yoyote unayotia saini na mtangazaji.

Kukubali ombi la kuunganisha

Mtangazaji anapotaka kuunganisha maudhui yako na Akaunti yake ya Google Ads, tutakuarifu kupitia barua pepe na arifa kwenye YouTube na Studio ya YouTube. Unaweza kukagua na kujibu kwenye Studio ya YouTube, programu ya Studio ya YouTube ya vifaa vya mkononi na katika programu ya YouTube ya vifaa vya mkononi.

Ukichagua kiungo kwenye barua pepe yako, utaelekezwa moja kwa moja kwenye "Ombi la kuunganisha Chapa" ambapo unaweza kuunganisha video yako au kukataa ombi.

Unaweza pia kukagua na kujibu maombi kwenye Studio ya YouTube:

  1. Katika kompyuta, nenda kwenye Studio ya YouTube.
  2. Kwenye Menyu ya kushoto, bofya Maudhui .
  3. Tafuta video husika na karibu na kijipicha cha video, bofya Maelezo .
  4. Katika sehemu ya "Kuunganisha biashara", karibu na maelezo ya mtangazaji, bofya KAGUA OMBI LA KUUNGANISHA.
  5. Chagua iwapo ungependa kuunganisha video au kukataa ombi.

Kutenganisha maudhui yako

Wakati wowote, wewe au mtangazaji anaweza kutenganisha video iliyounganishwa. Ili utenganishe video na akaunti ya mtangazaji, nenda kwenye sehemu ya "Kuunganisha chapa" ya video yako kisha uchague TENGANISHA   karibu na maelezo ya mtangazaji.

Maswali Yanayoulizwa Sana

Je, maombi ya kuunganisha hudumu kwa muda gani?

Ingawa muda wa maombi ya kuunganisha hauishi baada ya kipindi fulani, mtangazaji anaweza kubatilisha ombi la kuunganisha linalosubiri kujibiwa. Unaweza pia kutenganisha video wakati wowote. Kutenganisha maudhui yako kutamwondolea mtangazaji:
  • Uwezo wa kufikia vipimo vya utendaji wa maudhui
  • Uwezo wa kulenga matangazo kwa watazamaji wa maudhui yaliyounganishwa
Vilevile, iwapo video iliyoombwa imefutwa au kuwekwa kuwa ya faragha, muda wa ombi la kuunganisha utaisha.

Iwapo mtangazaji tayari anatumia video zangu kwenye shughuli zake za utangazaji, je, ninahitaji kuunganisha maudhui yangu ya kibiashara na akaunti yake ya Google Ads?

Watangazaji hawatakiwi kuunganisha akaunti zao na maudhui yako ili waonyeshe matangazo, lakini tunapendekeza uunganishe maudhui yako ya kibiashara na akaunti zao. Kuunganisha hukusaidia kudhibiti ushirika wako wa biashara kwa urahisi zaidi na humwezesha mtangazaji kuangalia utendaji halisi wa video. Vilevile, unaweza kudhibiti ufikiaji wa maudhui ya chaneli yako kwa kuunganisha tu video husika.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
10215129350794382318
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false