Jinsi ya kulipwa kwenye YouTube

Je, ulijiunga na Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP) hivi majuzi? Je ungependa kufahamu kuhusu jinsi YouTube itakavyokulipa? Je, unajiuliza malipo yako ya kwanza yatafanywa lini? Unajaribu kufikiri iwapo utalipwa mwezi huu au mwezi ujao?

Unapaswa kufanya yafuatayo ili ulipwe:

  1. Thibitisha taarifa zako binafsi
  2. Tuma taarifa zako za kodi
  3. Chagua njia ya malipo
  4. Fikia kima cha malipo

Baada ya kukamilisha hatua zilizo hapo juu, utakuwa tayari kupokea malipo yako ya kwanza.

1. Kuthibitisha taarifa zako binafsi

Mapato yako yanapofikia kima cha chini cha kuthibitishwa, tutakuomba uthibitishe utambulisho na anwani yako. Tunafanya hivi ili kuthibitisha usahihi wa taarifa za akaunti yako na kukulinda dhidi ya ulaghai.

Kabla hujafikia kima cha chini cha kuthibitishwa, hakikisha kuwa jina na anwani ya malipo kwenye akaunti yako ya AdSense katika YouTube ni sahihi. Tutatumia taarifa hii kuthibitisha utambuisho na anwani yako.

Je, umekosea? Pata maelezo kuhusu jinsi ya kubadilisha jina au anwani yako ya malipo.

1. Thibitisha utambulisho wako

Baada ya mapato yako ya YouTube kufikia kima cha chini cha kuthibitishwa, tutakuomba uthibitishe utambulisho wako. Utahitaji kuthibitisha utambulisho wako ili uendelee kuchuma mapato na kulipwa.

2. Thibitisha anwani yako

Baada ya kuthibitisha utambulisho wako, tutakutumia barua iliyo na PIN kwenye anwani yako ya malipo. Weka PIN hii kwenye akaunti yako ya AdSense katika YouTube ili tuweze kuthibitisha anwani yako na kutuma malipo ya baadaye. Tutakutumia PIN kupitia posta ya kawaida na huenda ikachukua muda wa wiki 3 hadi 4 ili kufika.

Iwapo una akaunti tofauti ya malipo ya AdSense na ya AdSense katika YouTube, utathibitisha taarifa zako za malipo wakati mojawapo ya akaunti zako za malipo inafikia kima cha chini cha kuthibitishwa. Utatahitaji kuthibitisha taarifa zako mara moja pekee.

2. Kutuma taarifa zako za kodi

Ni lazima watayarishi wote wanaochuma mapato kwenye YouTube watume taarifa zao za kodi, bila kujali mahali walipo.

Google inatakiwa kukusanya taarifa za kodi kutoka kwa watayarishi walio katika Mpango wa Washirika wa YouTube. Iwapo makato yoyote ya kodi yanatumika, Google huzuia kodi kwenye mapato ya YouTube yanayotokana na watazamaji walio Marekani. Usipotutumia taarifa zako za kodi, huenda Google ikatakiwa kukata hadi asilimia 24 ya jumla ya mapato yako uliyochuma kote duniani.

Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutuma taarifa zako za kodi kwenda Google.

3. Kuchagua njia yako ya malipo

Mapato yako yanapofikia kima cha chini cha kuchagua njia ya malipo, unaweza kuchagua jinsi ambavyo ungependa kupokea pesa zako.

Anwani yako ya malipo hubaini chaguo utakazopata za njia za malipo. Chaguo zinazopatikana zinaweza kujumuisha Mfumo wa Malipo wa Kielektroniki (EFT), hawala ya fedha ya kielektroniki au cheki. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuweka mipangilio ya njia yako ya malipo.

Iwapo una akaunti tofauti ya malipo ya AdSense na ya AdSense katika YouTube, utahitaji kuchagua njia ya malipo kwa kila akaunti inapofikia kima cha malipo.

4. Kufikia kima cha malipo

Iwapo mapato yako ya YouTube yatafikia kima cha malipo kufikia mwisho wa mwezi, basi kipindi cha uchakataji wa malipo huanza. Baada ya kipindi cha uchakataji kuisha, malipo yako hukamilishwa na kutumwa kwenye akaunti yako ya AdSense katika YouTube. Ikiwa una chaneli moja pekee inayohusishwa na akaunti yako ya AdSense katika YouTube, unaweza pia kuangalia shughuli zako za malipo kwenye programu ya vifaa vya mkononi ya Studio ya YouTube. Tutakutumia malipo mradi hakuna malipo yaliyoahirishwa kwenye akaunti yako na unafuata:

Pata maelezo zaidi kuhusu ratiba za malipo.

Mfano
Kwa mfano, hebu tuchukulie kuwa kima cha malipo cha akaunti yako ni $100. Iwapo salio lako la sasa lilifikia $100 mwezi Januari na umekamilisha hatua zote zilizo hapo juu na huna malipo yoyote yaliyoahirishwa, basi tutakutumia malipo mwishoni mwa Februari.

Iwapo una akaunti tofauti ya malipo ya AdSense na ya AdSense katika YouTube, kila akaunti inahitaji kufikia kima cha malipo ili ulipwe.

Iwapo mapato yako ya YouTube hayafii kima cha malipo kufikia mwisho wa mwezi, mapato yako yatasogezwa mwezi unaofuata. Salio la mapato yako litaendelea kuongezeka hadi ufikie kima cha malipo. 

Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu Malipo

Je, ninaweza kulipwa mapema?

Hapana. Hatuwezi kutoa malipo nje ya ratiba yetu ya kawaida ya malipo kwa sababu yoyote.

Je, AdSense katika YouTube inaweza kunipa hati rasmi za malipo?

Ndiyo, tutakutumia Risiti ya Malipo kwa kila malipo kwenye akaunti yako ya AdSense katika YouTube. Ili uangalie Risiti ya Malipo, bofya Malipo kisha Angalia miamala, kisha ubofye kiungo cha ulipaji kiotomatiki kwenye ukurasa wako wa "Miamala".
Iwapo unahitaji kuonyesha mkataba kati yako na AdSense au AdSense katika YouTube, unaweza kuchapisha Sheria na Masharti ya AdSense au Sheria na Masharti ya AdSense katika YouTube (yoyote yanayotumika). Ulipojisajili kwenye AdSense au AdSense katika YouTube, ulikubali Sheria na Masharti. Sheria na Masharti haya yanatumika kama misingi ya kisheria ya mitagusano kati yako (biashara yako) na AdSense au AdSense katika YouTube.
Kumbuka: Hatuwezi kutoa hati zozote zilizochapishwa, kutiwa sahihi au kupigwa mihuri.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
3072636550078175733
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false