Weka lebo kwenye Video zako za YouTube

Lebo ni maneno muhimu yenye maelezo unayoweza kuweka kwenye video ili kuwasaidia watazamaji wapate maudhui yako. Jina, kijipicha na maelezo ya video yako ni sehemu muhimu sana za metadata kwa ajili ya ugunduzi wa video yako. Sehemu hizi kuu za maelezo huwasaidia watazamaji kuamua video zipi watatazama. 

Lebo zinaweza kuwa muhimu iwapo maudhui ya video yako yameendelezwa visivyo. Vinginevyo, lebo huwa na umuhimu mdogo katika ugunduzi wa video yako.
Kumbuka: Kuweka lebo nyingi mno kwenye maelezo ya video yako ni kinyume na sera zetu za taka, tabia za udanganyifu na ulaghai.

Weka lebo za video ya YouTube 

Video mpya

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Katika kona ya juu kulia, bofya TAYARISHA kisha Pakia Video.
  3. Chagua faili ambayo ungependa kupakia.
  4. Katika mchakato wa kupakia, bofya CHAGUO ZAIDI kisha uweke lebo zako. 

Video zilizopakiwa

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui kisha uchague video yako.
  3. Weka lebo zako. 

Unaweza pia kubadilisha lebo kwenye kifaa cha mkononi katika programu ya YouTube. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuhariri video ulizopakia kwenye kifaa cha mkononi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9178408288155812497
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false