Inayochezeka kwenye YouTube

Kipengele cha Inayochezeka ni michezo ya kucheza bila kulipia inayoweza kuchezwa moja kwa moja kwenye YouTube.

Jinsi ya kucheza

Michezo Inayochezeka inaweza kupatikana kwenye rafu ya Inayochezeka kwenye Ukurasa mkuu wa Kwanza wa YouTube au kwenye ukurasa mpya lengwa wa Inayochezeka inayoweza kufikiwa kutoka kwenye menyu ya Gundua. Kila wakati tunaongeza michezo, kwa hivyo endelea kufuatilia ili upate matoleo mapya.

Bofya kwenye kadi zozote za michezo ili uanze kucheza moja kwa moja. Unaweza pia kutuma mchezo kutoka kwenye kadi au unapocheza kupitia menyu ya nukta tatu ya Zaidi ''.

Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu Inayochezeka

Vifaa vinavyotumika na masharti

Huhitaji maunzi, programu au vipakuliwa vyovyote vya ziada ili utumie kipengele cha Inayochezeka. Unachohitaji tu ni toleo jipya zaidi la YouTube, kifaa kinachotumika na uwe umeunganishwa kwenye Wi-Fi au mpango wa data (huenda ukatozwa ada ya matumizi ya data).

Kwa sasa kipengele cha Inayochezeka kinatumika katika vifaa vifuatavyo:

  • Android
    • Toleo la programu ya YouTube: 18.33 na matoleo mapya zaidi
    • Mifumo ya uendeshaji ya vifaa vya mkononi:
      • Android S na matoleo mapya zaidi
      • Android O, P, Q, R (kwenye vifaa vyenye biti 64 au vifaa vya hifadhi ya juu vyenye biti 32 pekee)
  • iOS
    • Toleo la programu ya YouTube: 18.33 na matoleo mapya zaidi
    • Mifumo ya uendeshaji ya vifaa vya mkononi: iOS 14 na matoleo mapya zaidi
  • Wavuti wa kompyuta ya mezani
    • Vivinjari: Chrome, Safari na Firefox

Upatikanaji wa kipengele cha Inayochezeka

Kwa sasa, Inayochezeka ni kipengele cha majaribio kilichosambaza kwa watumiaji mahususi katika nchi au maeneo yanayostahiki. Pia, huenda baadhi ya watumiaji walio katika maeneo haya wasione kipengele cha Inayochezeka kinachoweza kugunduliwa kwenye YouTube lakini bado wanaweza kuzifikia kupitia viungo vinavyoweza kushirikiwa ambavyo ni vya kipekee katika kila mchezo. Lengo letu ni kuongeza upatikanaji siku zijazo.

Ikiwa umejisajili kwenye YouTube Premium na nchi au eneo lako linastahiki kipengele cha Inayochezeka, unaweza kujijumuisha kwenye vipengele vya majaribio kwa kufuata hatua hizi ili upate toleo la Beta la Inayochezeka.

Ikiwa ungependa kuona michezo michache Inayochezeka, unaweza kushusha hadhi ya rafu ya Inayochezeka au michezo mahususi Inayochezeka kwa kubofya “Haunivutii” kwenye YouTube.

Maendeleo ya mchezo na historia iliyohifadhiwa

Maendeleo ya mchezo yatahifadhiwa kiotomatiki na yatasawazishwa kwenye vifaa vyovyote vinavyotumika ambapo umeingia katika akaunti yako ya YouTube

Maendeleo yako yaliyohifadhiwa ya kila mchezo pia yanahifadhiwa kwenye Historia ya YouTube > Data ya Matumizi. Kuna faili moja pekee ya hifadhi kwa kila mchezo na maendeleo yako ya mchezo hayatatumika kwa mapendekezo. Ukifuta faili ya hifadhi ya mchezo, utapoteza maendeleo yote ya mchezo huo kwenye vifaa vyote.

Historia ya Inayochezeka inahifadhiwa kwenye Historia ya YouTube, ambapo ni rahisi kupata michezo uliyocheza hivi karibuni. Kipengele hiki kikiwashwa, historia hutuwezesha kutoa mapendekezo faafu ya michezo. Unaweza kudhibiti historia yako ya Inayochezeka kwa kufuta au kuzima historia yako. Michezo yoyote unayocheza wakati historia imezimwa haitaonekana kwenye Historia ya YouTube.  

Kubadilisha mipangilio yako ya Historia ya YouTube

  1. Nenda kwenye myactivity.google.com
  2. Bofya Historia ya YouTube kisha ubadilishe upendavyo. 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
16697182104820929119
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false