Utaratibu wa Kuwasilisha Malalamiko kuhusu Faragha

Kila siku, watu hutembelea YouTube ili kushiriki video na kuwasiliana na wengine. Tunataka ujihisi salama wakati unatumia YouTube, kwa hiyo tunakuhimiza utujulishe iwapo video au maoni kwenye tovuti yanakiuka faragha au usalama wako, ikiwa ni pamoja na wewe kurekodiwa bila kujua katika hali nyeti au za faragha.

Tunaelewa kuwa huenda usiridhishwe na maudhui yote yanayokuangazia kwenye YouTube, kwa hivyo tumebuni mchakato huu ili kukusaidia kuwasilisha malalamiko kuhusu faragha. Tafadhali hakikisha kuwa unaweza kutambulika kimahususi kwenye maudhui unayotaka kuripoti kabla ya kuendelea na Utaratibu wa Kuwasilisha Malalamiko kuhusu Faragha. 

Ili kuheshimu faragha na kumbukumbu ya watumiaji walioaga dunia, tunazingatia maombi kutoka kwa wanafamilia wa karibu zaidi au wawakilishi wa kisheria baada ya kuthibitisha kuwa mhusika amefariki.

Mtu fulani akinakili video uliyobuni au maudhui unayomiliki, unaweza kuwasilisha malalamiko kuhusu hakimiliki. Iwapo unaamini kuwa maudhui yanakiuka Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube, tunakuhimiza upate maelezo kuhusu jinsi ya kuripoti maudhui yasiyofaa.

Iwapo unahisi kuwa uko hatarini, wasiliana na mamlaka ya mahali ulipo ili upate usaidizi zaidi.

Endelea

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
false
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
4201430624172884077
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false