Kugundua mada za maoni

Mada za maoni hutumia akiliunde (AI) kupanga na kuandaa muhtasari wa maoni kuhusu video za YouTube. Kipengele hiki kinaweza kukusaidia ugundue mada katika sehemu za maoni na ujiunge na mjadala bila kusoma maoni yote.

Mada za maoni hazitaonekana kwenye video zote. Kwa sasa, kipengele hiki kinapatikana tu kwenye sehemu kubwa za maoni katika programu ya YouTube ya vifaa vya mkononi kwenye video na maoni katika lugha ya Kiingereza.

Ili uanze, fungua sehemu ya maoni kwenye video katika programu ya YouTube ya vifaa vya mkononi. Ikiwa zinapatikana, gusa Mada  ili uvinjari mada za maoni. 

Muhtasari wa mada hutayarishwa kwa AI na si binadamu, kwa hivyo ubora na usahihi vinaweza kutofautiana.

Maswali Yanayoulizwa Sana

Je, ninaweza kuzima mada za maoni?

Hapana. Kwa wakati huu, huwezi kuzima mada za maoni. 

Ikiwa kuna kitu chochote kuhusu mada ambacho ungependa kutuma maoni kukihusu, fuata hatua zilizo hapa chini. 

Ikiwa wewe ni mtayarishi, pata maelezo zaidi kuhusu kudhibiti mada za maoni.

Je, ninaweza kutuma maoni kuhusu mada za maoni?

Unaweza kutufahamisha unachofikiria kuhusu mada au kuripoti makosa, kwa kutuma tmaoni. 

Ili utoe maoni:

  1. Fungua sehemu ya maoni kwenye video katika programu ya YouTube. 
  2. Gusa Mada .
  3. Gusa Zaidi ''.
  4. Gusa Tuma maoni

Je, maoni yako yanatumikeje?

Maoni:

  • Yanakaguliwa na timu maalumu zilizopatiwa mafunzo. Uhakiki unaofanywa na binadamu ni muhimu ili kusaidia kutambua, kutatua na kuripoti matatizo yanayoweza kutokea kwenye maoni, ikijumuisha inavyohitajika kwa mujibu wa sheria husika.
  • Yanatumika kwa kuzingatia Sera yetu ya Faragha. YouTube hutumia data hii kutoa, kuboresha na kubuni bidhaa na huduma za YouTube pamoja na teknolojia za mashine kujifunza, kama ilivyofafanuliwa kwa kina zaidi katika Sera yetu ya Faragha.

 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
548361487198205334
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false