YouTube ni mahali ambapo watu wanashiriki simulizi zao, wanatoa maoni yao na kuwasiliana na wengine. Tunataka kuhakikisha kuwa watayarishi na watazamaji wanahisi wapo salama kufanya hivyo. Ingawa watayarishi na watazamaji wengi wa YouTube wanataka kushiriki, kujifunza na kuwasiliana, tunajua kuwa kuna matukio ya matumizi mabaya au hata unyanyasaji. Pata maelezo zaidi kuhusu sera na zana zinazotumika zilizo hapa chini ili kukulinda unapotumia YouTube.
Watayarishi na watumiaji pia wana wajibu wa kufanya YouTube iwe mfumo salama. Pata maelezo zaidi hapa kuhusu jinsi tunavyowawajibisha watayarishi na watumiaji katika kudumisha viwango hivi.
Ili kupata maelezo zaidi kuhusu sera za YouTube, angalia orodha yetu kamili ya Mwongozo wa Jumuiya.
Sera kuhusu chuki na unyanyasaji
YouTube ina sera mahususi za kusaidia kukulinda dhidi ya chuki na unyanyasaji.
- Matamshi ya chuki: Sera hii hulinda vikundi mahususi na wahusika walio kwenye vikundi hivi. Tunachukulia maudhui kuwa ni matamshi ya chuki yanapochochea chuki au vurugu dhidi ya vikundi kulingana na sifa zinazolindwa kama vile umri, jinsia, mbari, tabaka, dini, mwelekeo wa kingono au hali ya kuwa mwanajeshi aliyestaafu. Pata maelezo zaidi kuhusu sera yetu ya matamshi ya chuki.
- Unyanyasaji: Sera hii hulinda watu mahususi. Tunachukulia maudhui kuwa unyanyasaji yanapolenga mtu kupitia matusi makali au ya muda mrefu kulingana na sifa na maumbile, ikiwa ni pamoja na hali yake ya kuwa katika kikundi cha watu wanaolinda au hali za kimaumbile. Sera hii pia inajumuisha tabia hatari kama vile vitisho, uchokozi, upekuzi na utangazaji wa taarifa binafsi au kuhimiza tabia mbaya kwa mashabiki. Pata maelezo zaidi kuhusu sera yetu ya unyanyasaji.
Maudhui nyeti
Tunatumai kuwalinda watazamaji, watayarishi na hasa watoto. Hiyo ndiyo maana tumeweka sheria zinazolenga kuwalinda watoto, dhidi ya maudhui ya ngono na uchi na kujijeruhi. Pata maelezo kuhusu kinachoruhusiwa kwenye YouTube na hatua za kuchukua ukiona maudhui ambayo hayafuati sera hizi.
Nyenzo za usaidizi wa masuala ya kujiua na kujijeruhi
Lifuatalo ni shirika lililojitolea kusaidia watu wanaohitaji usaidizi nchini Singapoo. Shirika hili ni mshirika aliyetambuliwa anayetoa huduma nyakati za dharura.
1800-221-4444 |
Maudhui ya vurugu au hatari
YouTube hairuhusu matamshi ya chuki, tabia ya kunyatia, vurugu ya kuogofya, mashambulizi hasidi na maudhui yanayohimiza tabia hatari au za kudhuru.
Bidhaa zilizodhibitiwa
Kuripoti maudhui ya ukiukaji
Ukipata maudhui yanayokiuka sera zilizo hapo juu, pata maelezo kuhusu jinsi ya kuripoti video, vituo na maudhui mengine yasiyofaa kwenye YouTube.
Ukipata maudhui haramu, pata maelezo kuhusu jinsi ya kuandikisha malalamiko ya kisheria au yaripoti moja kwa moja.
Vidhibiti vya wazazi
Ikiwa wewe ni mzazi, pata maelezo zaidi kuhusu vidhibiti vya wazazi na mipangilio kwa ajili ya Wasifu kwenye YouTube Kids na akaunti zinazodhibitiwa.
Kituo cha Usalama cha Watayarishi
Ikiwa wewe ni mtayarishi unayetafuta vidokezo zaidi na video zinazoweza kukusaidia kuhisi uko salama zaidi kwenye YouTube, tembelea Kituo cha Usalama cha Watayarishi.