Kupata usaidizi kupitia @TeamYouTube kwenye Twitter

TeamYouTube, timu ya YouTube inayotoa usaidizi na elimu, hutoa taarifa za muda halisi na majibu kwa watayarishi, watazamaji na wanaolipia usajili kwenye Twitter kupitia @TeamYouTube. Yafuatayo ni maelezo zaidi kutuhusu:

  • Utambulisho wetu unafuatiliwa usiku na mchana kuanzia kila Jumatatu saa 3 asubuhi majira ya Pasifiki hadi Ijumaa saa 11 jioni majira ya Pasifiki.
  • Timu yetu hutuma taarifa na kujibu maswali kwa lugha ya Kiingereza, Kihispania, Kireno, Kijerumani, Kifaransa, Kijapani Kiindonesia, Kiarabu, Kihindi na Kikorea.
  • Ingawa tunajitahidi kufuatilia maswali na maombi ya usaidizi yanayotumwa kwa kuweka lebo kwenye vitambulishi vingine rasmi vya YouTube kama vile, @YouTube au @YouTubeCreators, njia ya haraka zaidi ya kupata usaidizi ni kuweka lebo kwenye @TeamYouTube.

Pata maelezo zaidi kuhusu @TeamYouTube kwenye Twitter

Je, ninafaa kujumuisha nini ninapowasiliana na @TeamYouTube?

Iwapo unatuma ujumbe wa twitter utakaoonekana hadharani, usijumuishe taarifa zozote binafsi zinazoweza kutumiwa kukutambua, kama vile anwani ya barua pepe, namba ya simu au maelezo ya kadi yako ya mikopo miongoni mwa taarifa nyinginezo.

Unapoweka lebo kwenye @TeamYouTube ili upate usaidizi, hakikisha umejumuisha taarifa muhimu kama vile:

  • URL ya chaneli au video.
  • Picha za skrini za mada au tatizo husika kama unavyoliona.
  • Kifaa unachotumia, kama vile iPhone.
  • Picha ya skrini ya Takwimu zako za Wajuaji ikiwa una tatizo na YouTube TV.

Je, kuna hali zozote ambazo @TeamYouTube haiwezi kusaidia nazo?

Kuna baadhi ya hali ambazo @TeamYouTube haiwezi kusaidia:

  • Matatizo yanayotokea kwenye bidhaa isiyo ya Google, kama vile Amazon Fire Stick au Roku au huduma nyingine.
  • Mizozo ya hakimiliki na mwenye haki.
  • Mizozo ya kisheria.
  • Kuwasha tena au kuondoa akaunti za Google AdSense.
  • Iwapo chaneli yako imedukuliwa, wasiliana na huduma ya Usaidizi kwa Watayarishi.
  • Ikiwa hukubaliani na uamuzi wa sera.

Nina tatizo na bidhaa inayolipiwa ya YouTube, je, @TeamYouTube inaweza kunisaidia?

Unaweza kuwasiliana na @TeamYouTube kwenye Twitter ili uulize maswali ya haraka au upate maoni kuhusiana na bidhaa zinazolipiwa.

Ikiwa una matatizo ya kipekee ya usaidizi yanayohusu akaunti au uanachama wako, ni vyema uwasiliane na Timu ya Usaidizi ya YouTube kwa kutuma barua pepe, kupiga simu au kupiga gumzo kwa bidhaa zinazolipiwa kwa sababu hizo huenda zikahitaji utume taarifa binafsi kama vile namba ya simu au anwani yako ya barua pepe. Haya yanaweza kujumuisha maswali yanayohusiana na

  • Malipo
  • Kuweka au kuondoa vifurushi
  • Kudhibiti usajili
  • Kusahau manenosiri au kufungiwa akaunti
  • Hatua ya kusimamishwa kwa kituo ambayo tayari rufaa imekatwa dhidi yake

Unaweza kuwasiliana na timu ya Usaidizi ya YouTube kupitia viungo vilivyo hapa chini:

Je, unahitaji usaidizi kuhusu kurejeshewa pesa?

@TeamYouTube haiwezi kukusaidia kuhusiana na masuala ya kurejeshewa pesa, lakini kwa bidhaa nyingi, unaweza kuanzisha mchakato huo mwenyewe. Yafuatayo ni maelezo zaidi kuhusu kurejeshewa pesa kutokana na bidhaa zinazolipiwa.

Je, kuna vitambulishi vingine vya YouTube?

Ndiyo, vitambulishi vingine rasmi vya YouTube ni pamoja na:
  • @YouTube
  • @YouTubeCreators
  • @YouTubeTV
  • @CreatorLiason
  • @YTCretadores
  • @YTCriadores
  • @YTCreatorsIndia
  • @YTCreatorsJapan
  • @YTCreatorsDe
  • @YouTubeIndia
  • @YouTubeJapan
  • @YouTubeKorea
  • @YouTubeLATAM
  • @YouTubeMusic
  • @YouTubeInsider

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
8284185716357054385
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false