Kipengele cha Sauti za lugha nyingi kinakuwezesha kupakia sauti katika lugha tofauti kwenye Video fupi au video moja. Kwa video ndefu, unaweza pia kupakia vijipicha katika lugha tofauti. Hii ni njia bora ya kupanua ufikiaji wako wa kimataifa bila kufungua na kudhibiti chaneli nyingi tofauti.
Je, sauti za lugha nyingi ni nini?
Sauti za lugha nyingi hukuwezesha kupakia sauti za ziada katika lugha nyingi kwenye video mpya na zilizopakiwa hapo awali.
- Jinsi zinavyofanya kazi kwa watazamaji: Sauti zitabadilika kiotomatiki kuwa katika lugha anayopendelea mtazamaji kwa chaguomsingi, hali ambayo hubainishwa na historia ya video alizotazama. Watazamaji wanaweza kubadilisha lugha wanayopendelea katika mipangilio yao. Wanaweza pia kubadili kati ya lugha katika mipangilio ya kicheza video.
- Utafutaji na Ugunduzi: Baada ya video zako kutafsiriwa, zinaweza kupatikana watazamaji wanapotafuta kwa kutumia jina na maelezo ya video yaliyotafsiriwa. Mifumo yetu ya utafutaji huangalia majina na maelezo haya yaliyotafsiriwa ili kutoa matokeo sahihi katika lugha wanayozungumza.
- Si uwekaji wa sauti kiotomatiki: Sauti za lugha nyingi hukuwezesha upakie sauti ulizotafsiri mwenyewe. Haitayarishi sauti hizi kiotomatiki, tofauti na kipengele cha kuweka sauti ya lugha nyingine kiotomatiki. Ni sharti urekodi sauti ulizotafsiri kabla ya kuzipakia. Ikiwa tayari kuna sauti ya lugha nyingine iliyowekwa kiotomatiki, ni lazima uifute kabla ya kupakia toleo lako.
Kutimiza masharti
Kwa sasa, kipengele cha sauti za lugha nyingi kinapatikana kwa watayarishi wachache walio na idhini ya kutumia Vipengele vya kina tunapopanua ufikiaji kwa utaratibu. Pata maelezo zaidi kuhusu Vipengele vya kina..
Weka sauti ya lugha
- Ingia katika Studio ya YouTube kwenye kompyuta yako.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Lugha
.
- Bofya video ambayo ungependa kuhariri.
- Bofya Weka Lugha kisha uchague lugha unayotumia.
- Karibu na "Sauti ya lugha nyingine," bofya Weka.
- Bofya Chagua faili.
- Chagua faili unayotaka kupakia. Ni lazima faili ziwe katika aina ya faili inayotumiwa ya sauti pekee na ziwe na takribani urefu sawa na wa video yako.
- Bofya Chapisha ukiwa tayari kupakia sauti yako.
Kubadilisha faili za sauti zilizopakiwa awali
- Ingia katika Studio ya YouTube kwenye kompyuta yako.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Lugha
.
- Bofya video ambayo ungependa kuhariri.
- Chini ya “Sauti,” bofya Futa
kwenye lugha husika.
- Rudia hatua ya kupakia sauti mpya ya lugha nyingi.
lli uhakikishe kuwa video zako zinafikiwa na watazamaji wengi zaidi, pata maelezo zaidi kuhusu kuweka manukuu na kutafsiri majina na maelezo ya video.
Kudhibiti vijipicha vilivyojanibishwa
Vijipicha vilivyojanibishwa vinakuwezesha kubuni vijipicha katika lugha tofauti. Ukiwa na vijipicha vilivyojanibishwa, watazamaji wataonyeshwa vijipicha vinavyolingana na mipangilio yao ya lugha.
Ili uanze kutumia vijipicha vilivyojanibishwa:
- Ingia katika Studio ya YouTube kwenye kompyuta yako.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui
.
- Bofya video ambayo ungependa kuhariri.
- Bofya Pakia kijipicha kisha upakie picha yako ya kijipicha.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Lugha
.
- Bofya jina la lugha ambayo ungependa kuwekea kijipicha maalum.
- Karibu na Kijipicha, bofya Weka kisha uchague picha ya kupakia.
- Bofya Sasisha.
Mikakati na Mbinu Bora
Sauti za lugha nyingi ni chaguo bora kwa watayarishi ambao wangependa kufikia watazamaji wa kimataifa katika maeneo mapya ya kijiografia. Unatimiza masharti ikiwa tayari una watazamaji kutoka maeneo mengi ya kijiografia au una maoni ya mara kwa mara katika lugha tofauti.
Manufaa Makuu ya sauti za lugha nyingi
- Fikia Hadhira za Kimataifa: Sauti za lugha nyingi hufanya video zako zifikiwe kwa urahisi zaidi na watazamaji kote duniani, hivyo kuwafikia watazamaji wapya wanaozungumza lugha tofauti.
- Ufikiaji Uliongezeka: Watayarishi waliopakia Sauti za lugha nyingi walipata zaidi ya asilimia 25 ya muda wao wa utazamaji kutokana na utazamaji katika lugha isiyo ya msingi ya video.
- Usimamizi Uliorahisishwa: Sauti za lugha nyingi hukuwezesha kuchapisha maudhui kwenye chaneli moja pamoja na sauti zote katika video moja, hali inayorahisisha usimamizi na ufuatiliaji wa takwimu ikilinganishwa na kudhibiti chaneli nyingi za lugha mahususi.
Mbinu bora za sauti za lugha nyingi
- Wekea kipaumbele uwekaji wa sauti nyingine: Weka juhudi zako katika lugha moja au mbili na ujitahidi kutafsiri maudhui mengi iwezekanavyo.
- Tafsiri orodha yako ya zamani: Ikiwa una nyenzo, kutafsiri nusu au zaidi ya orodha yako iliyopo ya video kunaweza kutoa fursa za ziada kwa watazamaji wapya kugundua maudhui yako.
- Usahihi wa tafsiri: Tunapendekeza kuwa sauti za lugha yako ya pili zilingane kwa karibu na tafsiri ya lugha ya msingi iwezekanavyo.
- Kuweka manukuu: Manukuu ya kiotomatiki yatapatikana katika lugha ya sauti halisi. Unaweza pia kuweka manukuu yako kwenye video.
- Maelezo ya sauti: Watayarishi walio na idhini ya kutumia Sauti za lugha nyingi wanaweza pia kupakia faili za Maelezo ya Sauti katika Studio ya YouTube. Pata maelezo zaidi kuhusu maelezo ya sauti.
- Kuhariri video yako: Unaweza kuweka sauti za lugha nyingi kwenye video ulizohariri. Ukipunguza au kubadilisha sauti mwenyewe kwenye video halisi, mabadiliko hayo yatatumika kwenye sauti za ziada.
- Kuchanganua utendaji: Tumia sehemu ya Takwimu za YouTube kufuatilia utazamaji na muda wako wa kutazama ulikiwa umeainishwa kulingana na lugha ya sauti ili ubaini ni watazamaji wa lugha gani walio wengi na uchanganue utendaji.
- Utangazaji unaoendelea: Wafahamishe watazamaji wako kwa kuwaeleza kuwa umeweka sauti za lugha nyingine kwenye maudhui yako au umeshirikiana na watayarishi katika lugha lengwa.