Maudhui huondolewa au kuzuiwa kwenye YouTube yanapobainishwa kuwa yanakiuka mojawapo ya sera zetu, kama vile Mwongozo wetu wa Jumuiya au yanapokiuka sheria fulani. Ili kubaini iwapo maudhui yanakiuka sera zetu, tunatumia mchanganyiko wa mifumo ya kiotomatiki na ukaguzi unaofanywa na binadamu.
Mifumo ya kiotomatiki
Mifumo yetu ya kiotomatiki hutumia mbinu ya mashine kujifunza, inayoiruhusu kutumia data kutoka kwa ukaguzi wa awali uliofanywa na binadamu kutambua maudhui ambayo huenda yana ukiukaji.
Mifumo yetu mingi huendelea kuwekewa mamilioni ya pointi za data kutoka kwa ukaguzi unaofanya na binadamu. Hii inamaanisha kuwa mifumo yetu ya kiotomatiki inaweza kutoa kiwango cha juu cha usahihi katika kutambua ukiukaji. Pia, mifumo ya kiotomatiki huwapa watumiaji wetu majibu kwa nyakati zinazofaa kwa kiwango kikubwa cha maudhui ambayo YouTube hupokea.
Mifumo yetu inapokuwa na imani ya juu sana kuwa maudhui fulani yana ukiukaji, inaweza kufanya uamuzi wa kiotomatiki. Hata hivyo, katika hali nyingi, mifumo yetu ya kiotomatiki itaripoti maudhui kwa mtu anayekagua ambaye amepewa mafunzo, ili ayakague kabla ya hatua yoyote kuchukuliwa.
Ukaguzi unaofanywa na binadamu
Mtu anayekagua anapokagua maudhui ambayo huenda yana ukiukaji, inamaanisha kuwa mtu aliyepewa mafunzo ametathmini maudhui na kufanya uamuzi kulingana na sera au sheria husika.
Iwapo maudhui yamepatikana kuwa yana ukiukaji, watu wetu wanaokagua wanaweza kuondoa maudhui hayo au kuyawekea mipaka ya umri ikiwa hayafai hadhira zote. Iwapo maudhui yana lengo la kuelimisha, kuelezea hali halisi, sayansi au sanaa, tunaweza kuyaruhusu yasalie kwenye YouTube.
Baada ya uamuzi kufanywa kuhusu maudhui, iwapo rufaa imekatwa dhidi ya uamuzi huo, binadamu atakagua rufaa hiyo na kuitathmini kulingana na hali mahususi.
Maswali Yanayoulizwa Sana (FAQ)
Maelezo zaidi
Mwongozo wa Jumuiya
Jinsi YouTube inavyotambua ukiukaji wa Mwongozo wa Jumuiya
Jinsi YouTube inavyotathmini maudhui ya Elimu, Hali Halisi, Sayansi na Sanaa (EDSA)
Hakimiliki
Jinsi YouTube inavyokagua maombi ya kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki
Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP)
Jinsi YouTube inavyotekeleza sera za uchumaji wa mapato kwenye YouTube
Jinsi YouTube inavyokagua maombi ya kujiunga kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP)
Faragha
Jinsi YouTube inavyobaini iwapo maudhui yanafaa kuondolewa kwa kukiuka faragha