Kuvinjari onyesho tulivu kwenye televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti na vifaa vingine

Unapotazama YouTube kwenye televisheni inayoweza kuunganisha kwenye intaneti, kifaa cha kutiririsha au kifaa cha michezo ya video, unaweza kuwa na vipindi ambapo kifaa hakina shughuli baada ya kufurahia video. Katika vipindi hivi ambapo kifaa hakina shughuli, wakati mwingine tunakuonyesha onyesho tulivu ili kusaidia kuzuia skrini kuchujua rangi. Onyesho tulivu huzunguka kupitia picha tulivu zinazoonyeshwa upya mara kwa mara kutoka kwenye video zenye mandharinyuma yanayoliwaza.

Ili utazame video iliyowasilishwa kama onyesho tulivu:

  • Bonyeza kitufe cha juu kwenye kidhibiti chako cha mbali.

Ili urudi kwenye skrini ambayo ulikuwa unatazama hapo awali:

  • Bonyeza kitufe cha kurudi nyuma kwenye kidhibiti chako cha mbali.

Ili uanzishe onyesho tulivu kimakusudi:

  • Chagua "Anzisha onyesho tulivu" unapoondoka kwenye programu ya YouTube.

Je, ni nini kinabainisha ikiwa video inapatikana kwenye onyesho tulivu?

Ingawa video nyingi mpya tulivu zinapakiwa kwenye YouTube siku yoyote, onyesho tulivu linaweza kuonyesha idadi ndogo pekee. Onyesho tulivu hulenga kuonyesha video ambazo:

  • Zinafaa kwenye skrini kubwa za televisheni za HD kulingana na ubora wa utayarishaji na usanifu

  • Huonyesha aina mbalimbali za mandhari, aina za vipindi na watayarishi

  • Zinaliwaza au zinatuliza

  • Hazipotoshi, si chambo cha kubofya au hazishtui

  • Zinafaa kwa watazamaji mbalimbali (kwa kuwa video za onyesho tulivu zinaonekana kwa hadhira ya kimataifa na hazijawekewa mapendeleo)

Onyesho tulivu hulenga kuzingatia vigezo hivi vyote kwa usawa. Ili kufikia lengo hili, onyesho tulivu huzingatia viashiria vingi, ikiwa ni pamoja na, (lakini si tu):

  • Mara ilizotazamwa

  • Muda wa video

  • Muda wa video kwenye YouTube baada ya kupakiwa

  • Utendaji wa video ikilinganishwa na video zingine katika aina zinazofanana

Pia, tuna wafanyakazi wanaohudumu kama wachujaji wa mwisho ili kuhakikisha usalama na ufaafu wa video.

YouTube haikubali mawasilisho au malipo ili kuwekwa kwenye onyesho tulivu na haipendelei watayarishi mahususi.

Mipangilio ya faragha ya video za onyesho tulivu

Video inaweza tu kuonekana katika hali ya onyesho tulivu ikiwa mipangilio yake ya faragha ni ya umma.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
6804573064640540658
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false