Tunabadilisha bei zetu za uanachama mara kwa mara ili kuendana na mabadiliko ya soko, yanayoweza kujumuisha mfumuko wa bei na mabadiliko ya kodi ya eneo ulipo.
Ili uone bei yako ya sasa au kufahamu jinsi unavyotozwa, nenda kwenye ukurasa wa Ununuzi na Uanachama kwenye akaunti yako. Pia, unaweza kughairi au kubadilisha uanachama wako wakati wowote.
Je, nitajuaje iwapo bei ya uanachama wangu inabadilika?
Tutakujulisha kupitia barua pepe angalau siku 30 kabla ya bei kuongezeka katika nchi au eneo uliko.
Kumbuka kuwa mabadiliko ya kodi katika eneo ulipo yanaweza kutokea na kusababisha kuongezeka kwa bei yako ya jumla. Ili upate taarifa za hivi punde kuhusu bei ya sasa ya uanachama wako unaojirudia, nenda kwenye ukurasa wa Ununuzi na Uanachama wa akaunti yako.Je, huduma yangu itakatizwa?
Je, lini nitaanza kutozwa gharama mpya?
Wanachama wapya watatozwa bei iliyoonyeshwa kwenye ofa wanapojisajili.
Wanachama waliopo watatozwa bei mpya ya kila mwezi katika kipindi cha kwanza cha kutozwa kinachofuata, angalau siku 30 baada ya ongezeko la bei ya mpango wa uanachama. Kwa mfano, tukiongeza bei kwa watumiaji wapya tarehe 1 Septemba, hutatozwa kiwango cha juu hadi kipindi cha kutozwa kinachofuata cha mwezi Oktoba.
Ikiwa uanachama wako umesimamishwa kwa sasa, hutatozwa hadi utakaporejesha uanachama wako. Utatozwa mara moja kwa bei ya awali, kisha utatozwa bei mpya kwenye vipindi vya kutozwa vitakavyofuata.