Kudhibiti Mpango wa Familia kwenye YouTube

Weka mipangilio ya mpango wa familia wa YouTube ili uwe msimamizi wa familia. Ukiwa msimamizi wa familia, unaweza kushiriki uanachama wako wa YouTube Premium au YouTube Music Premium. Unaweza kushiriki uanachama wako na hadi wanafamilia wengine 5 katika familia yako. Iwapo wewe ni mwanafamilia, unaweza kujiunga kwenye kikundi cha familia ili ushiriki mpango wa familia kwenye YouTube. 

Kumbuka: Iwapo wewe ni mwanachama wa kikundi kilichopo cha familia kwenye Google, huwezi kununua mpango wa familia kwenye YouTube. Msimamizi wa kikundi cha familia yako ndiye tu anayeweza kufanya ununuzi.

Mambo unayohitaji kujua kabla ya kuanza

  • Ni lazima wanafamilia wanaoshiriki mpango wa familia kwenye YouTube wawe wanaishi pamoja na msimamizi wa familia. Pata maelezo zaidi kuhusu masharti ya kikundi cha familia na hatua ya kuchukua ukikumbwa na hitilafu ukiweka mipangilio ya mpango wa familia
  • Unaweza tu kubadilisha vikundi vya familia mara moja katika kipindi cha miezi 12.
  • Kila jina, picha na anwani ya barua pepe ya mwanafamilia itashirikiwa na kikundi.
  • Iwapo unahitaji usaidizi kuhusu mpango wa familia yako kwenye YouTube TV, unaweza kuwasiliana na timu ya usaidizi wakati wowote. 

Jinsi ya Kuanzisha Vikundi vya Familia kwenye YouTube na YouTube TV

Fuatilia chaneli ya Watazamaji ya YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.

Wasimamizi wa familia: Kujisajili na kuanzisha kikundi cha familia

Wanachama wapya wa YouTube Premium au Music Premium

Ili uanze, chagua msimamizi wa familia ambaye ana umri wa miaka 18 au zaidi. Msimamizi wa familia ndiye tu anayeweza kununua mpango wa familia au kufanya uamuzi wa uanachama. Pata maelezo zaidi kuhusu kujisajili katika uanachama unaolipiwa kwenye YouTube.

Ili ujisajili kwenye uanachama wa YouTube Premium au Music Premium na uanzishe kikundi cha familia:

  1. Katika programu ya YouTube, gusa picha yako ya wasifu kisha Ununuzi na uanachama.
  2. Utaona chaguo za uanachama unaolipiwa kwenye YouTube Music Premium na YouTube Premium. Bofya Pata Maelezo Zaidi kuhusu usajili ambao ungependa kununua.
  3. Bofya Au uokoe pesa kwa kutumia mpango wa familia au wa wanafunzi.
  4. Bofya Pata mpango wa familia.
  5. Iwapo wewe ni msimamizi wa familia wa kikundi kilichopo cha familia kwenye Google, utaona kidirisha kitakachothibitisha kikundi cha familia yako. Chagua Endelea ili uendelee kufanya ununuzi na ushiriki mpango wa familia yako na wanachama wa kikundi chako kilichopo cha familia. Iwapo hatua ya 5 haitumiki kwako, nenda kwenye hatua ya 6.
  6. Iwapo tayari huna kikundi cha familia kwenye Google, fuata hatua ili ununue usajili wako kwanza. Kisha utaongozwa kwenye mchakato wa kuanzisha kikundi cha familia.
Kumbuka: Iwapo unatatizika kujisajili kwenye mpango wa familia, huenda ni kwa sababu una akaunti kadhaa za malipo kwenye Google Play. Iwapo ni hivyo, pata maelezo kuhusu jinsi ya kusasisha au kubadilisha akaunti katika nchi au eneo uliko.

Wanachama waliopo wa YouTube Premium au Music Premium

Ili usasishe uanachama wako binafsi wa Premium au Music Premium kwenye mpango wa familia:
  1. Katika programu ya YouTube, gusa picha yako ya wasifu kisha Ununuzi na uanachama.
  2. Gusa Pata mpango wa familia.
  3. Gusa Pata mpango wa familia tena.
  4. Gusa Nunua.
  5. Weka mipangilio ya kikundi cha familia yako kwenye Google.
    • Je, wewe ni msimamizi wa familia wa kikundi kilichopo cha familia kwenye Google? Chagua Endelea ili uendelee na ushiriki YouTube Premium na wanachama wa kikundi chako kilichopo cha familia.
    • Je, unaanzisha kikundi cha familia kwenye Google? Ili uweke mipangilio ya kikundi cha familia:
      • Waalike hadi wanafamilia watano wajiunge kwenye kikundi cha familia yako na uwatumie mialiko kupitia barua pepe au SMS.
      • Chagua Tuma.
      • Wanafamilia watapata mwaliko na wanaweza kuchagua Anza na wathibitishe akaunti zao.
      • Wanafamilia wanaokubali mwaliko wako watajiunga kwenye kikundi cha familia na wataweza kufikia YouTube Premium.
    • Je, wewe ni mwanafamilia wa kikundi kilichopo cha familia kwenye Google? Huwezi kununua YouTube Premium, lakini unaweza kumwambia msimamizi wa familia yako afanye ununuzi huo.
Vidokezo:
  • Ofa maalum haziwezi kuhamishiwa katika mipango ya familia kwenye YouTube. Ukianza kutumia mpango wa familia wakati wa jaribio linalozidi mwezi 1, muda wa jaribio lako utafupishwa kuwa mwezi 1. Ukighairi mpango wako wa familia baadaye, hutaweza kurudia jaribio lako. Pata maelezo zaidi kuhusu kusasisha uanachama wako unaolipiwa kwenye youTube.
  • Iwapo unatatizika kujisajili kwenye mpango wa familia, huenda ni kwa sababu una akaunti kadhaa za malipo kwenye Google Play. Iwapo ni hivyo, pata maelezo kuhusu jinsi ya kusasisha au kubadilisha akaunti katika nchi au eneo uliko.
  • Iwapo una mpango wa mwaka, utahitaji kusubiri hadi muda wa mpango wako utakapoisha kabla ya kupata toleo jipya la mpango wa familia.

Wasimamizi wa familia: Kuongeza au kuondoa wanafamilia

Kuongeza wanafamilia

Iwapo wewe ni msimamizi wa familia, unaweza kuwaalika hadi wanafamilia 5 kwenye kikundi cha familia yako.
Kuongeza mwanafamilia:
  1. Ingia katika Akaunti ya Google inayohusishwa na uanachama wako unaolipiwa kwenye YouTube.
  2. Katika programu ya YouTube, gusa picha yako ya wasifu kisha Ununuzi na uanachama.
  3. Gusa Badilisha karibu na mipangilio ya Kushiriki na familia.
  4. Gusa Alika wanafamilia.
  5. Weka anwani ya barua pepe au namba ya simu ya mtu ambaye ungependa kualika.
  6. Chagua Tuma. Utapokea arifa ya barua pepe mtu akijiunga kwenye familia yako.

Kuondoa wanafamilia

Iwapo wewe ni msimamizi wa familia, unaweza kuwaondoa watu kwenye kikundi cha familia yako wakati wowote.
Kuondoa mwanafamilia:
  1. Ingia katika Akaunti ya Google inayohusishwa na uanachama wako unaolipiwa kwenye YouTube.
  2. Katika programu ya YouTube, gusa picha yako ya wasifu kisha Ununuzi na uanachama.
  3. Gusa uanachama wako.
  4. Gusa Badilisha karibu na mipangilio ya Kushiriki na familia.
  5. Chagua jina la mtu ambaye ungependa kumwondoa.
  6. Bofya Ondoa mwanafamilia.

Wasimamizi wa familia: Majukumu mengine ya wasimamizi wa familia

Kubadilisha njia yako ya kulipa

Pata maelezo kuhusu jinsi ya kusasisha uanachama wako unaolipiwa kwenye YouTube, ikiwemo njia ya kulipa.

Kughairi uanachama wako unaolipiwa

Unaweza kukatisha uanachama wako unaolipiwa kwenye YouTube wakati wowote. Ukighairi, bado utaweza kufikia uanachama wako unaolipiwa kwenye YouTube hadi mwisho wa kipindi chako cha kutozwa kila mwezi. Baada ya kughairi, wanafamilia wote watapoteza uwezo wa kufikia uanachama unaolipiwa, lakini bado wataendelea kutumia Akaunti zao za Google.

 Wanafamilia: Kujiunga au kuondoka kwenye kikundi cha familia

Kujiunga kwenye kikundi cha familia

Iwapo mwanafamilia aliye na uanachama unaolipiwa kwenye YouTube amekualika ujiunge kwenye kikundi cha familia, utapata mwaliko kupitia barua pepe au SMS. Fuata maagizo katika mwaliko ili ujiunge kwenye kikundi cha familia.
Pata maelezo zaidi kuhusu kujiunga kwenye kikundi cha familia.

Kuondoka kwenye kikundi cha familia au kupata uanachama binafsi unaolipiwa kwenye YouTube

Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuondoka au kubadilisha vikundi vya familia. Ili upate uanachama wako binafsi unaolipiwa kwenye YouTube:
  1. Fuata maagizo ili uondoke kwenye kikundi cha familia yako.
  2. Jisajili kwenye uanachama wako binafsi unaolipiwa kwenye YouTube.
Kumbuka: Ukiondoka kwenye kikundi cha familia yako, unaweza kukubali mwaliko wa kujiunga kwenye kikundi tofauti cha familia au uanzishe kikundi chako mwenyewe. Unaweza kuhamia kwenye kikundi kingine cha familia mara moja tu katika kipindi cha miezi 12. Ukiondoka kwenye kikundi cha familia na ujiunge na kikundi kipya, huwezi kujiunga kwenye kikundi kingine cha familia kwa miezi 12.

Masharti ya mahali mahususi ya mipango ya familia

Masharti ya mahali mahususi ya mpango wa familia

Ili kuruhusiwa kushiriki uanachama wa familia kwenye YouTube, lazima kila mwanafamilia awe anaishi eneo ambako msimamizi wa familia anaishi. Kila baada ya siku 30, ukaguzi wa kielektroniki utathibitisha masharti haya.

Je, unatatizika kuweka mipangilio ya mpango wako wa familia? Iwapo unaona ujumbe kuhusu hitilafu kuwa:

  • "Familia hairuhusiwi"

Au

  • "Nchi hairuhusiwi"

Huenda nchi au eneo uliloorodhesha katika akaunti yako ya Google Pay halilingani na eneo uliko sasa.

Sasisha wasifu wako wa Google Pay ili ulingane na eneo uliko sasa na uendelee kuweka mipangilio ya mpango wako wa familia.

Iwapo eneo au nchi ambako mwanafamilia aliko hailingani na eneo uliko, hawezi kujiunga kwenye kikundi cha familia.

Wasiliana na timu ya usaidizi wakati wowote iwapo unahitaji usaidizi kuhusu mpango wa familia kwenye YouTube.

Wasiliana na timu ya usaidizi wakati wowote iwapo unahitaji usaidizi kuhusu mpango wa familia yako kwenye YouTube.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
1006289339108133539
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false