Kurejeshewa pesa za ununuzi wa filamu na vipindi kwenye YouTube

Pata maelezo zaidi kuhusu sera za kurejesha pesa na uombe kurejeshewa pesa za filamu na vipindi ulivyonunua kupitia akaunti yako.

Kuomba kurejeshewa pesa za filamu au kipindi cha televisheni kwenye YouTube

Fuatilia chaneli ya Watazamaji ya YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.

Sera ya kurejesha pesa za filamu na vipindi

Ikiwa video au vipengele vinavyohusiana na ununuzi wako kwenye YouTube havifanyi kazi, huenda ukatimiza masharti ya kurejeshewa pesa. Ikiwa ombi la kurejeshewa pesa limekubalika, tutaondoa ufikiaji wa maudhui na pesa zako zitarejeshwa ndani ya muda wa kurejesha pesa ulioorodheshwa hapa.

  • Ikiwa hujatazama kipindi au filamu, unaweza kuomba kurejeshewa pesa ndani ya siku 7 za kazi kuanzia siku uliyonunua.
  • Ununuzi na ukodishaji wa filamu na vipindi vya televisheni unaofanywa kwenye programu ya YouTube katika prrogramu ya Android utalipiwa kupitia Google Play. Nenda kwenye payments.google.com ili upate maelezo kuhusu ada mpya na uelewe jinsi unavyotozwa. Ununuzi unaofanywa kupitia Google Play unasimamiwa na sera zake za kurejesha pesa.

Omba urejeshewe pesa za vipindi na filamu kwenye YouTube

Ikiwa ulinunua filamu au kipindi kupitia Google Play, ni lazima uombe kurejeshewa pesa kupitia Duka la Google Play. Nenda kwenye payments.google.com ili upate maelezo kuhusu ada mpya na uelewe jinsi unavyotozwa.

Kwenye kompyuta yako:

  1. Nenda kwenye https://www.youtube.com/paid_memberships 
  2. Bofya Rejesha Pesa karibu na kipengee ambacho ungependa kurejeshewa pesa zake.
  3. Bofya Omba urejeshewe pesa.

Iwapo unalipwa kupitia Google Play, utaelekezwa kwenye fomu na utaombwa ujibu maswali machache kuhusu ununuzi wako. Weka maelezo yanayohitajika kisha ubofye thibitisha ili utume ombi lako.

Ukishatuma ombi lako la kurejeshewa pesa, utapokea barua pepe ya kuthibitisha.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
2822598784543380759
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false