Taarifa na ofa za YouTube Premium na Music Premium

Tumia makala haya ili upate habari kuhusu taarifa zote mpya za ofa na taarifa kuhusu uanachama wako wa YouTube Premium au YouTube Music Premium. Pata maelezo zaidi kuhusu YouTube (yenye matangazo) hapa.

Taarifa za hivi majuzi

Taarifa kutoka wiki 2 zilizopita

  • Sikiliza maudhui ya YouTube Music kwenye saa mahiri za Garmin: Ikiwa wewe ni mwanachama wa YouTube Music Premium au YouTube Premium, unaweza kusikiliza muziki na podikasti ulizopakua, kwenye saa mahiri za Garmin zinazotumika. Pata maelezo zaidi.
  • Mipango ya wanafunzi na familia inapatikana kwa ununuzi nchini Israeli: Mipango ya wanafunzi na familia ya Premium na Music Premium inapatikana kwa ununuzi nchini Israeli. Unaweza kufurahia manufaa yako pamoja na watu wengine 5 wa familia yako ukiwa na mpango wa familia. Ikiwa wewe ni mwanafunzi, unaweza kufurahia manufaa yako kwa ada iliyopunguzwa. Ukitumia Premium, unaweza kutazama YouTube bila matangazo, kufurahia muziki bila kikomo katika programu ya YouTube Music, kuhifadhi video nje ya mtandao na zaidi. Ukiwa na Music Premium, unaweza kusikiliza muziki bila matangazo, nje ya mtandao na ukiwa umezima skirini yako kwenye programu ya YouTube Music. Jisajili ili upate Premium au Music Premium na upate maelezo zaidi kuhusu manufaa ya Premium na manufaa ya Music Premium.

Taarifa za awali

Taarifa za miezi 6 iliyopita

Machi 2024

  • YouTube Premium na YouTube Music Premium zinapatikana katika nchi au maeneo mapya: Sasa YouTube Premium na YouTube Music Premium zinapatikana kwa watumiaji walioko Azabajani, Jamaika, Kazakistani, Libya, Moroko, Riyunioni, Tanzania, Uganda, Yemeni na Zimbabwe. Ukiwa na Premium, unaweza kutazama YouTube bila matangazo, kufurahia muziki bila kikomo katika programu ya YouTube Music, kuhifadhi video nje ya mtandao na zaidi. Ukiwa na Music Premium, unaweza kusikiliza muziki bila matangazo, nje ya mtandao na ukiwa umezima skirini yako kwenye programu ya YouTube Music. Jisajili ili upate Premium au Music Premium na upate maelezo zaidi kuhusu manufaa ya Premium na manufaa ya Music Premium.

Desemba 2023

  • Sasisho la bei ya uanachama nchini Korea Kusini: Kuanzia tarehe 8 Desemba 2023 majira ya KST, bei za uanachama wa YouTube Premium na YouTube Music Premium zitaongezeka. Huwa hatufanyi uamuzi kama huu bila kuzingatia masuala muhimu na sasisho hili litatuwezesha kuendelea kuboresha mpango wa Premium na kuwasaidia watayarishi na wasanii unaotazama maudhui yao kwenye YouTube. Wanachama waliopo wataona bei yao mpya ya kila mwezi katika kipindi chao cha kutozwa kinachofuata. Ili uone bei yako ya sasa au kufahamu jinsi unavyotozwa, nenda kwenye ukurasa wa Ununuzi na Uanachama kwenye akaunti yako. Pata maelezo zaidi kuhusu mabadiliko haya ya bei hapa.
  • YouTube Premium na YouTube Music Premium zinapatikana katika nchi au maeneo mapya: YouTube Premium na YouTube Music Premium sasa zinapatikana kwa watumiaji walio nchini Aljeria, Kambodia, Jojia, Ghana, Iraki, Yordani, Kenya, Laosi, Tunisia na Senegali. Ukitumia Premium, unaweza kutazama YouTube bila matangazo, kufurahia muziki bila kikomo katika programu ya YouTube Music, kuhifadhi video nje ya mtandao na zaidi. Ukiwa na Music Premium, unaweza kusikiliza muziki bila matangazo, ukiwa nje ya mtandao na skrini ikiwa imezima. Jisajili kwenye Premium au Music Premium na upate maelezo zaidi kuhusu manufaa ya Premium na manufaa ya Music Premium.

Novemba 2023

  • Angalia vipengele vyetu vipya zaidi vya Premium: Iwe ni toleo la Beta au vipengele vya majaribio vinavyowezeshwa na AI, udhibiti zaidi wa hali yako ya utazamaji, usikilizaji wa muziki bila matangazo, nje ya mtandao, uchezaji wa chinichini na bila kukatizwa, hivi ni baadhi ya vipengele vyetu vipya zaidi vya Premium kwa ajili ya watumiaji waliojisajili — ikiwa ni pamoja na masasisho mapya unayoweza kujaribu leo. Soma zaidi kuhusu vipengele hivi kwenye blogu yetu.
  • Sasisho la bei ya uanachama nchini Ajentina, Australia, Austria, Chile, Ujerumani, Polandi na Uturuki: Kuanzia tarehe 1 Novemba 2023, tutaongeza bei za mpango wa binafsi, familia na wa wanafunzi wa YouTube Premium na YouTube Music Premium. Nchini Ujerumani na Uturuki tutaongeza pia bei za mipango ya mwaka. Hatufanyi maamuzi haya bila kuzingatia na sasisho hili litatuwezesha kuendelea kuboresha Premium na Music Premium na kuwasaidia watayarishi na wasanii unaowatazama na kuwasikiliza kwenye YouTube. Wanachama waliopo watapata bei yao mpya ya kila mwezi katika kipindi chao cha kutozwa kinachofuata. Ili upate bei yako ya sasa au uelewe jinsi unavyotozwa, nenda kwenye ukurasa wa Ununuzi na Uanachama katika akaunti yako. Pata maelezo zaidi kuhusu mabadiliko ya bei ya bidhaa za YouTube zinazolipiwa hapa.

Oktoba 2023

  • Sikiliza maudhui ya YouTube Music kwenye HomePod na Fitbit: Ikiwa wewe ni mwanachama wa YouTube Music Premium au YouTube Premium, unaweza kusikiliza muziki na podikasti ulizopakua kwenye vifaa vya Fitbit na Apple HomePods vinavyotumika. Pata maelezo zaidi.

Septemba 2023

  • Sikiliza podikasti kwenye YouTube Music: Ikiwa unaishi Kanada, Amerika Kusini, Asia, au Visiwa vya Pasifiki, sasa utapata podikasti kwenye programu ya YouTube Music. Pata podikasti unazopenda na uzisikilize katika hali ya chinichini, bila kujali hali ya uanachama wako. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kupata podikasti kwenye YouTube Music.
  • Tazama video katika ubora wa 1080p Premium: Ukiwa na YouTube Premium, unaweza kutazama video katika ubora wa 1080p Premium kwenye kompyuta, televisheni na vifaa vya mkononi.  Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kubadilisha ubora wa video yako hapa.

Julai 2023

YouTube Premium inapatikana katika nchi au maeneo mapya: YouTube Premium sasa inapatikana kwa watumiaji nchini Bangladeshi, Nepali, Pakistani na Sirilanka. Ukitumia Premium, unaweza kutazama YouTube bila matangazo, kufurahia muziki bila kikomo katika programu ya YouTube Music, kuhifadhi video nje ya mtandao na zaidi. Jisajili kwenye YouTube Premium au upate maelezo zaidi kuhusu manufaa ya Premium.

Aprili 2023

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu