Kujisajili kwenye mpango wa mwaka wa YouTube

Mipango ya mwaka ya Premium ni uanachama usiorudiwa na unaolipiwa kabla ya kuitumia Baada ya kujisajili, unaweza kufurahia manufaa ya uanachama wa Premium kwa miezi 12 hadi muda wa mpango wako utakapoisha. Angalia hapa chini ili upate maelezo ya masharti ya kujisajili.

Kuangalia ikiwa unatimiza masharti ya kujisajili kwenye mpango wa mwaka

Ili ujisajili kwenye mpango wa mwaka, fuata hatua zilizo hapa chini. Baada ya kukamilisha ununuzi wako, unaweza kutumia manufaa yako ya YouTube Music Premium au YouTube Premium kila mahali unapoweza kuingia katika Akaunti ya Google uliyotumia kununua uanachama wako—ikijumuisha kwenye televisheni zinazoweza kuunganisha kwenye intaneti au vifaa cha michezo ya video vinavyooana.

Ili ujisajili kwenye mpango wa mwaka, ni sharti uwe:

  • Huna usajili wa sasa wa YouTube Premium au Music Premium. Ikiwa una uanachama unaotumika wa YouTube Premium au YouTube Music Premium na ungependa kubadilisha ili utumie mpango wa mwaka, pata maelezo kuhusu jinsi ya kufanya hivyo hapa.
  • Unaishi katika mojawapo ya maeneo yafuatayo:
    • Marekani, Kanada, Meksiko, Brazili, Urusi, Ujerumani, Tailandi, India na Japani.
    • Kidokezo kwa wanachama wanaoishi India: Iwapo umejiunga kwenye mpango wa kulipia mapema wa mwezi 1 au miezi 3, unaweza kujisajili kwenye mpango wa mwaka ambao utaanza baada ya muda wa mpango wako wa kulipia kuisha.
Kumbuka: Mipango ya mwaka inapatikana tu kwa watumiaji binafsi. Hatutoi mipango ya mwaka kwa watumiaji ambao wamejisajili kwenye mpango wa familia.

Mipango ya mwaka ya YouTube Premium inatumika vipi?

Unaponunua mpango wa mwaka, unalipia mapema ili upate usajili binafsi usiorudiwa. Hali hii inamaanisha kuwa manufaa yako ya uanachama unaolipiwa yataisha baada ya kipindi cha miezi 12 ulicholipia. Unaweza kununua hadi miaka 2 ya ufikiaji unaolipiwa kabla ya kutumia wa YouTube Music Premium au YouTube Premium kwa wakati mmoja. Ili uendelee kufikia manufaa yako, utahitaji kununua mpango mwingine baada ya muda wa uanachama wako kuisha.

Mipango ya mwaka haijumuishi urejeshaji wa pesa na mipango ya mwaka haiwezi kusitishwa. Ikiwa una maswali kuhusu mpango wako wa mwaka, wasiliana na Timu ya Usaidizi ya YouTube. Iwapo ungependa kuripoti muamala wa ulaghai, wasilisha dai hapa.

Pata maelezo zaidi hapa chini kuhusu jinsi ya kujisajili. Unaweza pia kugundua chaguo zetu za uanachama unaolipiwa ili ubaini inayokufaa.

Kujisajili kwenye mpango wa mwaka wa YouTube Premium

Ili ujisajili kwenye mpango wa mwaka wa Music Premium au YouTube Premium, fuata hatua zilizo hapa chini.

Kujisajili kwenye mpango wa mwaka wa YouTube Premium au YouTube Music Premium

  1. Kwenye simu au kishikwambi chako, fungua programu ya YouTube au YouTube Music.
  2. Ingia katika Akaunti ya Google ambayo ungependa kutumia ili kuanzisha uanachama wako.
  3. Gusa picha yako ya wasifu  kisha Pata YouTube Premium.
  4. Chagua “wa mwaka” kwenye chaguo za mipango.
  5. Kamilisha ununuzi wako.

Huenda ukaombwa uthibitishe pin ili kuimarisha usalama wa ununuzi wako. Ikiwa ndivyo, fuata hatua zilizo kwenye skirini ili ukamilishe mchakato wa uthibitishaji.

Baada ya kukamilisha ununuzi wako, unaweza kutumia manufaa yako ya YouTube Music Premium au YouTube Premium kwenye kompyuta, kifaa cha Apple au Android kwa kuingia katika Akaunti ya Google uliyotumia kununua uanachama wako. Unaweza kuangalia tarehe ya mwisho ya mpango wako kwenye sehemu ya Uanachama Unaolipiwa katika akaunti yako.

Kubadilisha aina ya uanachama wako

Iwapo una uanachama unaoendelea wa YouTube Premium au Music Premium na ungependa kubadilisha ili utumie mpango wa mwaka, kwanza utahitaji kuthibitisha kuwa uko katika eneo ambako mipango ya mwaka inapatikana:

  • Marekani
  • Kanada
  • Meksiko
  • Brazili
  • Urusi
  • Ujerumani
  • Tailandi
  • India
  • Japani

Iwapo umetimiza masharti ya kujiunga kwenye mpango wa mwaka, utahitaji kukatisha uanachama wako unaoendelea. Baada ya kukatisha uanachama wako unaweza kujisajili kwenye mpango wa mwaka wa YouTube Premium au Music Premium. Uwezo wako wa kufikia mpango wa mwaka utaanza baada ya mwisho wa kipindi chako cha sasa cha kutozwa.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
1459919302715474786
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false