Kuelewa mabadiliko ya akaunti za shule kwenye YouTube

Akaunti ya Google Workspace for Education ni anwani ya barua pepe uliyopewa na shule yako. Katika aina hii ya akaunti, msimamizi wa shule yako hudhibiti uwezo wako wa kufikia bidhaa za Google kama vile YouTube.

Kuanzia tarehe 1 Septemba, 2021, ikiwa msimamizi wa shule yako ataweka alama inayoashiria kuwa una umri wa chini ya miaka 18, akaunti yako ya YouTube ya shuleni itahamishiwa kwenye toleo linalodhibitiwa la YouTube. Chaneli yako ya YouTube haitaunganishwa tena kwenye akaunti yako ya shule na hutaweza kupakia video mpya kwenye chaneli hiyo. Mabadiliko haya yataathiri tu hali yako ya utumiaji wa YouTube kwenye akaunti yako ya shule kupitia Google Workspace for Education, na si akaunti yako binafsi.

Vizuizi vya akaunti kwa watumiaji walio na umri wa miaka chini ya 18

Ikiwa wewe ni mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari na msimamizi wa shule yako amekuwekea alama inayoashiria kuwa una umri wa chini ya miaka 18, utakuwa na vizuizi vya kuona vipengele na maudhui ya YouTube unapoingia katika akaunti yako ya Google Workspace for Education.

Hivi ni baadhi ya vipengele ambavyo havipatikani kwa ajili yako, ikiwa msimamizi wa shule yako amekuwekea alama inayoashiria kuwa una umri wa chini ya miaka 18:

Tazama

  • Video zinazotiririshwa moja kwa moja

Kushirikisha

  • Arifa (isipokuwa arifa zilizowekewa mapendeleo ambazo zina mihtasari ya shughuli)
  • Maoni
  • Gumzo la Moja kwa Moja
  • Buni
  • Kituo
  • Mtiririko mubashara
  • Machapisho
  • Orodha ya kucheza ya umma na ambayo haijaorodheshwa
  • Hadithi
  • Video Fupi
  • Upakiaji wa video

Nunua

  • Uanachama katika kituo
  • Bidhaa za mtayarishi
  • Ufadhili wa Uhisani wa YouTube
  • Filamu na Vipindi vya Televisheni
  • Super Chat na Super Stickers

Programu za YouTube

  • YouTube Music
  • Studio ya YouTube
  • YouTube TV
  • YouTube VR

Mengineyo

  • Tuma kwenye TV
  • Akaunti za michezo zilizounganishwa
  • Hali fiche
  • Matangazo yaliyowekewa mapendeleo
  • Hali yenye Mipaka

Pakua na uhifadhi maudhui yako

Ikiwa una umri wa miaka zaidi ya 18:

Wasiliana na msimamizi wa shule yako:

  • Mwombe msimamizi wa shule yako aweke alama kwenye akaunti yako inayoashiria kuwa una umri unaozidi miaka 18.

Baada ya msimamizi wako kubadilisha mipangilio yako:

  • Ingia katika akaunti ya YouTube.
  • Nenda kwenye fungua kituo, kisha ujaze fomu ya taratibu za kazi. Akaunti yako itaonyeshwa na utaweza kuendelea kutayarisha video kwenye chaneli ya YouTube ya akaunti yako ya shule.

Ikiwa una umri wa chini ya miaka 18:

  • Tumia Google Takeout kupakua na kuhifadhi video zako na data nyinginezo (kama vile maoni na historia ya mambo uliyotafuta) ambayo umetayarisha kwenye YouTube. Ikiwa akaunti yako iliundwa baada ya Septemba 2021, utakuwa na siku 60 za kupakua data yako kuanzia wakati ambapo msimamizi wa shule yako atakuwekea alama inayoashiria kuwa una umri wa chini ya miaka 18.
Kumbuka: Programu ya Google Takeout inapatikana ikiwa msimamizi wa shule yako ataiwezesha ili uweze kuifikia ukitumia akaunti yako.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
7976828714472970888
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false