Mbinu bora za utayarishaji maudhui ya watoto na familia

Katika YouTube tunaamini kuwa watoto wanaweza kugundua mambo mapya yanayowavutia, kujifunza na kukuza hisia ya kujihisi kuwa sehemu ya maudhui wanayotazama kupitia video za mtandaoni. Tunajitahidi kuwasaidia watayarishi kuelewa jinsi ya kutengeneza video bora, zinazovutia na zinazohamasisha zinazofaa kwa watoto na familia.

Mbinu Bora za Utayarishaji Maudhui ya Watoto na Familia (Kanuni za Maudhui yenye Ubora wa Juu na Ubora wa Chini)

Kama sehemu ya juhudi hizi zinazoendelea, tumeunda kanuni za ubora hapa chini ili kuwaongoza watayarishi wa maudhui ya watoto na familia kwenye YouTube. Kanuni hizi zimeundwa na wataalamu wa maendeleo ya watoto na zinatokana na utafiti wa kina.

Orodha ifuatayo inakusudia kukupa ufahamu bora wa kile kinachoweza kuzingatiwa kama maudhui ya ubora wa chini au juu, lakini si kamilifu. Kanuni hizi zinatumika pamoja na Mwongozo wetu wa Jumuiya ambao husaidia kuweka hali salama ya utazamaji kwa kila mtu na hutumika kwa video ndefu pamoja na Video Fupi za YouTube.

Ili upate maelezo zaidi kuhusu mbinu bora za kubuni Video Fupi za YouTube zinazowalenga watoto, angalia mwongozo huu.

Una wajibu wa kufuata Mwongozo wetu wa Jumuiya kuhusu maudhui yote unayotayarisha. Tutaendelea kutathmini upya na kusasisha kanuni kwenye ukurasa huu.

Kanuni za maudhui ya ubora wa juu

Maudhui ya ubora wa juu yanapaswa kuwa bora, yaambatane na umri, yavutie na yahamasishe. Maudhui haya yanaweza kutayarishwa katika miundo tofauti na kuhusisha mada mbalimbali, lakini yanapaswa kuhamasisha:

  • Kuwa mtu mwema: Maudhui haya yanaonyesha au kuhimiza heshima, tabia njema na tabia nzuri. Mifano ni pamoja na maudhui kuhusu kushiriki au kuwa rafiki mwema. Pia, video zinaweza kuhusu upigaji mswaki au kuhimiza watoto kula mboga za majani.
  • Kujifunza na kuhamasisha udadisi: Maudhui haya hukuza fikra makini, kujadili mawazo yanayohusiana na kuchunguza ulimwengu. Maudhui yanapaswa yaambatane na umri na yawe yamebuniwa kwa ajili ya hadhira ya watoto. Yanaweza pia kuwa mafunzo kulingana na asili au mafunzo ya kimapokeo (kwa mfano, mafunzo ya kitaaluma, mafunzo yasiyo rasmi, uchunguzi wa mambo yanayovutia na mafunzo ya mazoezi).
  • Ubunifu, michezo na hali zenye kufikirisha: Maudhui haya ni ya kuibua ubunifu au yanachochea fikira. Maudhui haya yanaweza pia kuwahimiza watoto kutengeneza, kuunda au kufanya kitu katika njia bora na yenye kuvutia. Mifano ni pamoja na kutengeneza vitu vya kufikirika, kusimulia hadithi, mbinu za soka, kuimba pamoja na shughuli za ubunifu kama vile sanaa na ufundi.
  • Mwingiliano na masuala ya-ulimwengu halisi: Maudhui haya yanajumuisha masomo ya maisha na wahusika thabiti, au yanayohimiza kujenga stadi za kijamii na kihisia, utatuzi wa changamoto na kuwa na fikra huru. Mara nyingi hujumuisha masimulizi kamili (kama vile kumvisha uhusika mhusika, mpangilio wa matukio, hitimisho la simulizi) na funzo au somo.
  • Utofauti, usawa, na ujumuishwaji: Maudhui haya huhusudu na kuchochea uwakilishi na ushiriki wa makundi na mitazamo mbalimbali ya watu. Maudhui haya huonyesha watu mbalimbali wenye umri, jinsia, mbari, dini na mwelekeo wa kingono ulio tofauti. Pia, hutetea usawa kwa watu wa makundi hayo. Mifano ni pamoja na maudhui ambayo yanajadili manufaa ya kuwa watu aina tofauti na kuwajumuisha kwenye nyanja mbalimbali au yanayoonyesha hadithi/wahusika ambapo mada hizi zimeonyeshwa.

Kanuni za maudhui yenye ubora wa chini

Epuka kutayarisha maudhui yenye ubora wa chini. Maudhui yenye ubora wa chini ni:

  • Yanayolenga kutangaza biashara au ofa kwa kiasi kikubwa: Maudhui ambayo yanalenga zaidi ununuzi wa bidhaa au kukuza chapa na nembo (kama vile vifaa vya kuchezea watoto na chakula). Pia, inajumuisha maudhui yanayolenga ununuzi wa bidhaa kupita kiasi.
  • Kuhimiza tabia au mitazamo hasi: Maudhui yanayohimiza shughuli hatari, ubadhirifu, uchokozi, udanganyifu au kukosea wengine heshima. Kwa mfano, maudhui haya yanaweza kujumuisha mizaha iliyo hatari au isiyo salama na ulaji usiofaa.
  • Mafunzo yanayopotosha: Maudhui yanayodai kuwa ya mafunzo katika sehemu ya jina au kijipicha chake, lakini hayana mwongozo au maelezo au hayafai kutazamwa na watoto. Kwa mfano, vichwa au vijipicha ambavyo vinaahidi kuwasaidia watazamaji "kujifunza rangi" au "kujifunza nambari," lakini badala yake video inaelezea maelezo yasiyo sahihi.
  • Maudhui yasiyoeleweka: Maudhui yasiyojitosheleza, yenye masimulizi yasiyooana au yasiyoeleweka kama vile kuwa na sauti isiyosikika. Aina hii ya video mara nyingi hutokana na uandaaji wa maudhui mengi kwa pamoja au utayarishaji wa kiotomatiki.
  • Maudhui yanayoshtua au yanayopotosha: Maudhui ambayo si ya kweli, yaliyotiwa chumvi, ya ajabu au yanayotokana na maoni na yanayoweza kuchanganya hadhira ya watoto. Yanaweza pia kujumuisha "uwekaji wa maneno muhimu", au matumizi ya maneno muhimu maarufu ya kuvutia watoto kwa kurudiwa, kubadilishwa au kutiwa chumvi. Maneno muhimu yanaweza pia kutumika kwa njia isiyo na maana.
  • Matumizi ya ajabu ya wahusika ambao ni watoto: Maudhui ambayo yanawaweka watoto maarufu (wahusika, waliohuishwa au halisi) katika hali zisizokubalika.

Athari kwenye utendaji wa kituo

Kanuni za ubora wa maudhui ya watoto na familia zinaweza kuathiri utendaji wa kituo chako. Maudhui ya ubora wa juu "yanayolenga watoto" huwekwa katika mapendekezo. Pia, huchochea maamuzi ya kujumuishwa kwenye YouTube Kids na uchumaji wa mapato katika kituo na video. Iwapo kituo kitapatikana kinaangazia sana maudhui ya ubora wa chini "yanayolenga watoto", kinaweza kusimamishwa katika Mpango wa Washirika wa YouTube. Iwapo video mahususi itapatikana kuwa inakiuka kanuni hizi za ubora, inaweza kupata matangazo machache au isipate kabisa.

Tunategemea kila mmoja wenu atayarishe maudhui bora na yanayohamasisha ya watoto na familia kwenye YouTube.

Kanuni za ubora wa video na Video Fupi za YouTube

 Kumbukua kuwa kanuni hizi za ubora kwa maudhui ya watoto na familia zinatumika kwa video ndefu na Video Fupi za YouTube.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
16847217699458976764
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false