Content ID inapopata video inayolingana na faili ya marejeleo ya kipengee chako, dai hufunguliwa. Video unayodai ni ile iliyo na dai moja au zaidi.
Kwenye Kidhibiti Maudhui cha Studio, unaweza kuangalia orodha ya video zako unazodai na uchuje orodha ili upate video mahususi. Ili udhibiti video unazodai, unaweza kuzisasisha kila moja kivyake au kwa wingi, kudhibiti madai yake na kuhamisha data inayozihusu.
Kutafuta video unazodai
Unaweza kugawanya orodha ya video zako unazodai kulingana na nyenzo, kisha utumie vichujio unavyopendelea ili upate video unazotafuta. Ili utafute video unazodai:
- Ingia katika Kidhibiti Maudhui cha Studio.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Video unazodai .
- Kwenye upau wa kuchuja , bofya Chanzo ili uchague chanzo cha video unazodai:
- Video za wengine: Video ulizodai
- Video zilizowekwa na mshirika: Video zilizopakiwa na chaneli zilizounganishwa na mmiliki wa maudhui
- Bofya upau wa kuchuja kisha uchague kichujio kimoja au zaidi, kama vile:
- Hali ya dai: Pata maelezo zaidi kuhusu hali za madai.
- Aina ya dai: Ili uchuje kulingana na iwapo dai lilikuwa la sauti, video au sauti na video.
- Dai jipya lililowekwa au lililosasishwa: Ili uchuje kulingana na tarehe dai lako la mwisho la video husika liliwekwa au lilisasishwa.
- Idadi ya madai yangu, yanayoendelea au yaliyokoma: Ili upate video zenye zaidi ya dai moja.
- Tarehe ya kuchapishwa: Ili uchuje kulingana na tarehe ya kuchapishwa kwa video unayodai.
- Weka idadi TUMIA.
Kupata Video fupi zenye madai
Video wima zenye urefu wa kati ya dakika 1 hadi 3 zitazuiwa ikiwa zina madai. Ili upate madai kwenye Video zako fupi,
- Ingia katika Kidhibiti Maudhui cha Studio.
- Gusa Maudhui Video fupi.
- Video zilizo na lebo za “Hakimiliki” zinajumuisha maudhui yenye hakimiliki na zimezuiwa. Gusa aikoni ili upate maelezo zaidi kuhusu zuio.
Pata maelezo zaidi kuhusu Video fupi zenye urefu wa dakika tatu au kukagua na kuchukua hatua kuhusu masuala ya madai.
Kudhibiti video unazodai
Ili udhibiti video unazodai, unaweza kuzisasisha kila moja kivyake au kwa wingi, kudhibiti madai yake na kuhamisha data inayozihusu.
Kusasisha video unazodai- Fuata hatua zilizo hapo juu ili utafute video unazodai unazohitaji.
- Bofya kisanduku kimoja au zaidi cha kuteua karibu na video unazodai ambazo ungependa kusasisha.
- Ili uchague video binafsi unazodai, teua visanduku vilivyo katika safu wima ya kushoto.
- Ili uchague video zote unazodai kwenye ukurasa mmoja, teua kisanduku cha "Chagua zote" katika sehemu ya juu.
- Ili uchague video zote unazodai kwenye kurasa zote, teua kisanduku cha "Chagua Zote" katika sehemu ya juu Chagua zote zinazolingana.
- Kwenye bango lililo sehemu ya juu, bofya Badilisha kisha uchague kitendo:
- Aina ya dai: Hubainisha iwapo unadai maudhui ya sauti (Sauti), ya video (Video) au aina zote mbili (Sauti na Video).
- Kusasisha sera ya video unayodai: Husasisha sera inayotumika kwenye video unayodai.
- Kuondoa madai: Huondoa madai uliyochagua.
- Chagua mipangilio ya kitendo ulichochagua.
- Iwapo ulichagua Aina ya dai au Kusasisha sera ya video unayodai, chagua:
- Sasisha madai yako yote kwenye video ulizochagua: Iwapo video zina madai mengi, kitendo ulichochagua kitatumika kwenye video zote ulizochagua.
- Sasisha tu madai yako kwenye video ulizochagua zinazolingana na vichujio: Hupatikana tu iwapo umetumia vichujio vya ziada kwenye orodha yako ya video unazodai.
- Mfano: Ikiwa unataka tu kusasisha madai ya kudai mwenyewe kwenye video unazodai, tumia kichujio cha Chanzo Kudai Mwenyewe. Unapochagua mipangilio ya Sasisha tu madai yako kwenye video ulizochagua zinazolingana na vichujio, ni madai uliyofanya mwenyewe tu kwenye video ulizochagua ndiyo yatasasishwa.
- Iwapo ulichagua Kuondoa madai, chagua:
- Ondoa madai yote kwenye video ulizochagua: Iwapo video zina madai mengi, madai yote yataondolewa kwenye video zote ulizochagua.
- Ondoa tu madai yako kwenye video ulizochagua zinazolingana na vichujio: Hupatikana tu iwapo umetumia vichujio vya ziada kwenye orodha yako ya video unazodai.
- Mfano: Ikiwa unataka tu kuondoa madai ya kudai mwenyewe kwenye video unazodai, tumia kichujio cha Chanzo Kudai Mwenyewe. Unapochagua mipangilio ya Ondoa tu madai yako kwenye video ulizochagua zinazolingana na vichujio, ni madai ya kudai mwenyewe tu kwenye video ulizochagua yatakayoondolewa.
- Iwapo ulichagua Aina ya dai au Kusasisha sera ya video unayodai, chagua:
- Bofya SASISHA VIDEO UNAZODAI.
- Fuata hatua zilizo hapo juu ili utafute video unazodai unazohitaji.
- Bofya video unayodai. Ukurasa wa maelezo utafunguka na kuonyesha muhtasari wa madai ya video hiyo, yaliyopangwa kulingana na hali ya dai.
- Kumbuka: Unaweza pia kubofya kichupo cha Historia ili uangalie shughuli za awali.
- Chini ya Madai kwenye video, bofya MAELEZO ili uangalie maelezo zaidi kuhusu madai kwenye video.
- Kulingana na hali ya dai, huenda vitendo vifuatavyo vikapatikana:
- Kuondoa dai: Chagua ONDOA MADAI (#) ili uondoe dai moja au zaidi kwenye video.
- Kuondoa na kufutilia mbali dai: Bofya kishale kando ya ONDOA DAI. Chagua Ondoa na ufutilie mbali dai ili uondoe dai na ufutilie mbali sehemu ya rejeleo iliyoweka dai.
- Wasilisha ombi la kuondoa video: Bofya ONDOA VIDEO UNAYODAI uwasilishe ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki kwa YouTube ili utume ombi la kuondoa video.
- Kubadilisha sera ya dai: Bofya kichupo cha Sera kisha ubofye WEKA SERA MAHUSUSI YA VIDEO UNAYODAI.
- Ili uweke sera iliyopo, chagua sera kwenye orodha, kisha bofya TUMIA.
- Ili uweke sera mpya, bofya WEKA SERA MAALUM, tunga sera yako, kisha ubofye HIFADHI TUMIA.
- Kufungua tena dai: Wakati mwingine unaweza kufungua tena madai yaliyokoma kwa kubofya DAI TENA MADAI (#). Kwa mfano, katika hali kadhaa, unaweza kudai tena mwenyewe madai yaliyofungwa na ambayo muda wake umeisha.
- Kumbuka: Huwezi kufungua tena madai yaliyoondolewa na mtu mwenyewe wakati wa mchakato wa kupinga dai.
Pata maelezo zaidi kuhusu kukagua na kuchukua hatua kuhusu masuala ya madai.
Unaweza kuhamisha video zisizozidi milioni 1 unazodai kwa wakati mmoja. Ili kuhamisha faili yenye data ya video unazodai:
- Fuata hatua zilizo hapo juu ili upate video unazodai unazohitaji.
- Bofya kisanduku kimoja au zaidi cha kuteua karibu na video unazodai ambazo ungependa kuhamisha data inayozihusu.
- Ili uchague video binafsi unazodai, teua visanduku vyao vilivyo katika safu wima ya kushoto.
- Ili uchague video zote unazodai kwenye ukurasa mmoja, teua kisanduku cha "Chagua zote" katika sehemu ya juu.
- Ili uchague video zote unazodai kwenye kurasa zote, teua kisanduku cha "Chagua Zote" katika sehemu ya juu Chagua zote zinazolingana.
- Katika bango lililo sehemu ya juu, bofya Hamisha kisha uchague:
- Video unazodai (.csv) au Video unazodai (Majedwali ya Google) ili uhamishe orodha ya video unazodai ikiwa na video moja unayodai kwa kila safu mlalo.
- Madai (.csv) au Madai (Majedwali ya Google) ili uhamishe orodha ya madai ikiwa na dai moja kwa kila safu mlalo.
- Faili itaanza kuchakatwa. Unaweza kuondoka kwenye ukurasa au kutekeleza vitendo vingine wakati faili inachakatwa.
- Baada ya faili kuchakatwa:
- Kwa faili ya .csv: Bofya PAKUA kwenye bango la sehemu ya juu.
- Kwa faili ya Majedwali ya Google: Bofya FUNGUA MAJEDWALI YA GOOGLE KATIKA DIRISHA JIPYA kwenye bango lililo sehemu ya juu.