Kwa ajili ya watoto na familia: Kulipia bidhaa zitangazwe katika maudhui ni nini?

Je, kulipia bidhaa ili zitangazwe katika maudhui ni nini? (Kwa ajili ya Watoto)

Fuatilia chaneli ya Watazamaji ya YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.

Unapotazama video, huenda ukaona alama hii ikiibuka inayosema “Kituo hiki kilipata pesa au vitu bila malipo ili kutengeneza video hii” au "Inajumuisha matangazo yanayolipiwa." Inamaanisha kuwa huenda aliyetayarisha video hiyo akapokea pesa au bidhaa bila malipo kutoka kwa kampuni.

Kwa mfano, ikiwa video inaonyesha kitu cha watoto kuchezea, aliyeitayarisha anaweza kupokea pesa ili akuonyeshe kitu hicho. Kitu hicho cha watoto kuchezea kinaonyeshwa kwenye video kwa sababu kampuni iliyokitengeneza inataka ukinunue. 

Kwa wazazi au walezi: Fahamu bidhaa zilizolipiwa ili zitangazwe katika maudhui, ufadhili na maudhui yaliyoidhinishwa

Kuwa Mtayarishi wa YouTube kunaweza kuwa ajira ya kudumu na vituo vingi maarufu huwa na timu zinazovisaidia kutayarisha video. Ufadhili, matangazo na ushirika ni baadhi ya njia ambazo Watayarishi wanaweza kutumia ili wajikimu kimaisha wanapoandaa maudhui bora kwenye YouTube. Ni muhimu kwa watoto kuelewa kwamba Watayarishi wanaweza kupewa bidhaa au huduma ili wazitangaze. Watoto wanapaswa wajue tofauti iliyopo kati ya video zenye bidhaa zilizolipiwa ili zitangazwe katika maudhui na maudhui yaliyoidhinishwa na video ambazo hazina vitu hivi. Ufumbuzi dhahiri utaonekana kwenye maudhui yoyote yenye matangazo yanayolipiwa inapobainishwa na mtayarishi.

Vidokezo kwa wazazi na walezi

  • Zungumza na watoto wako kuhusu matangazo yanayolipiwa yaliyopo kwenye video na uwafundishe jinsi ya kutambua kiashirio cha matangazo yanayolipiwa kilichopo kwenye video. Tazama video hii fupi kisha muulize mtoto wako akueleze jinsi atakavyoweza kufahamu iwapo maudhui anayoyatazama yana matangazo yanayolipiwa.
  • Ongea na mtoto wako kuhusu Watayarishi anaowapenda na umweleze ni Watayarishi wangapi wanatayarisha maudhui ya YouTube kama ajira yao ya kudumu. Utaratibu huu humaanisha kwamba wanafanya kazi na biashara pamoja na washirika wengine ili wapate pesa za kuendesha vituo vyao.
  • Tafuta maneno kama vile "imefadhiliwa na", "ameshirikiana na", au #tangazo, yanayoweza kuashiria kuwa kampuni imemlipa Mtayarishi kutangaza bidhaa yao.

Kwa vidokezo zaidi kuhusu namna unavyoweza kumsaidia mtoto wako kutumia YouTube, pakua na usome mwongozo wetu wa familia.

Je, kulipia bidhaa ili zitangazwe katika maudhui, ufadhili na maudhui yaliyoidhinishwa ni nini?

Kulipia bidhaa ili zitangazwe katika maudhui
  • Video zilizotengenezwa kwa ajili ya kampuni au biashara kwa lengo la kupokea malipo au kupokea bidhaa au huduma husika bila malipo. 
  • Video ambapo chapa, ujumbe au bidhaa ya kampuni au biashara hiyo imejumuishwa moja kwa moja kwenye maudhui. Kampuni imempa mtayarishi pesa au bidhaa bila malipo ili atengeneze video hiyo.
Maudhui yaliyoidhinishwa: Video zilizotengenezwa kwa ajili ya mtangazaji na kujumuisha ujumbe unaoonyesha maoni, imani au hali zinazohusu utumiaji wa bidhaa au huduma kwa mtayarishi au mhusika anayeidhinisha maudhui.
Ufadhili: Video ambazo gharama zote au sehemu ya gharama za utayarishaji zimelipwa na kampuni, bila kujumuisha chapa, ujumbe au bidhaa ya kampuni hiyo moja kwa moja kwenye maudhui. Kwa kawaida ufadhili unatangaza:
  • Chapa husika
  • Ujumbe
  • Bidhaa ya mhusika mwingine

Je, hii inamaanisha nini kwa mtoto wangu?

Matangazo yote yanayolipiwa na kuonekana kwenye video zinazowalenga watoto huwa na ufumbuzi ambao watoto wanaweza kuuelewa. 
Matangazo yote yanayolipiwa yanapaswa kufuata Sera zetu za Matangazo, zinazozuia matangazo ya aina fulani. Utangazaji unaofanyika kwenye maudhui yaliyobainishwa kuwa "Yanalenga Watoto" hautakiwi kuwa wa kidanganyifu, usio wa haki, usiofaa kwa hadhira inayokusudiwa  na haupaswi kutumia vifuatiliaji vyovyote kutoka kwa wahusika wengine. Maudhui haya hayapaswi kukusanya taarifa binafsi bila kupata idhini ya mzazi, na ni lazima yatii sheria na kanuni zote. Watayarishi na chapa wanazoshirikiana nazo wanapaswa kuelewa na kutii wajibu wa kisheria wa mahali walipo ili kutoa ufumbuzi wa matangazo yanayolipiwa katika maudhui yao. Wajibu huu unajumuisha wakati, jinsi na hadhira mahususi inayostahili kupewa ufumbuzi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
11829842898870704441
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false