Kuwekea Mapendeleo Onyesho lako la Kwanza

Unaweza kunufaika kwenye Onyesho la kwanza kwa kuliwekea mapendeleo. Chagua mandhari tofauti ya muda uliosalia, chuma mapato kupitia Onyesho lako la kwanza au onyesha kionjo.

Kuchagua mandhari ya muda uliosalia

Dakika mbili kabla ya Onyesho lako la kwanza kuanza, wewe na watazamaji wako mtaona video ya moja kwa moja ikihesabu kuelekea wakati wa video yako Kuonyeshwa kwa mara ya kwanza. Unaweza kuchagua kutoka kwenye orodha ya mandhari ya muda uliosalia. 

  1. Kwenye Studio ya YouTube, pakia video.
  2. Katika hatua ya “Uonekanaji”, ratibu upakiaji wako kama Onyesho la kwanza.
  3. Bofya Weka mipangilio ya Onyesho la kwanza.
  4. Chini ya “Chagua mandhari ya muda uliosalia,” teua kipima muda.

Kuonyesha kionjo

Ichangamshe hadhira yako inayotazama mtiririko mubashara kuhusu video yako ijayo kwa kuonyesha kionjo chake kwenye ukurasa wa Onyesho la kwanza. Kionjo chako kitachezwa kwa watazamaji kwenye ukurasa wa kutazama kabla ya Onyesho la kwanza halijaanza.

  1. Kupakia kionjo chako kwenye kituo chako cha YouTube sawa na unavyopakia video ya kawaida.
  2. Kwenye Studio ya YouTube, pakia video unayotaka iwe onyesho la kwanza.
  3. Katika hatua ya “Uonekanaji”, ratibu kama Onyesho la kwanza.
  4. Bofya Weka mipangilio ya Onyesho la kwanza.
  5. Chini ya “Weka kionjo,” bofya Weka kisha uchague kionjo chako.
Masharti ya Kujiunga

Kipengele hiki kinapatikana kwa watayarishi walio na zaidi ya watu 1,000 wanaofuatilia na hawana maonyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya

Masharti
  • Aina ya video: Tumia aina yoyote ya video inayoruhusiwa kwenye YouTube.
  • Urefu wa video: sekunde 15 – dakika 3.
  • Uwiano na ubora: Tunapendekeza uwiano na ubora ule ule uliotumia kwenye video ya Onyesho la kwanza.
  • Haki za sauti na video: Hakikisha kuwa kionjo hakikiuki haki za maudhui mengine.
  • Hakikisha kuwa hakuna maudhui yatakayokiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya.

Kuchuma mapato kupitia Onyesho lako la kwanza

Kuna njia kadhaa ambazo unaweza kuchuma mapato kupitia onyesho la kwanza la video yako:

Matangazo

Iwapo kituo chako kimetimiza masharti ya Mapato ya utangazaji, unaweza kuwasha matangazo ili kuonyesha matangazo kabla ya video kucheza wakati wa Onyesho la kwanza. Matangazo ya katikati na baada ya video hayapatikani wakati wa Onyesho la kwanza.

Onyesho la kwanza linapokamilika, tunafuata mipangilio chaguomsingi ya video zinazopakiwa ya kituo chako kwa ajili kucheza matangazo.

Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuwasha matangazo kwenye video yako au jinsi ya kubadilisha mipangilio yako chaguomsingi ya video zinazopakiwa.

Super Chat na Super Stickers

Super Chat na Super Stickers ni njia za kuunganisha mashabiki na watayarishi, wakati wa gumzo la moja kwa moja. Watazamaji wanaweza kununua Super Chat ili kuangazia ujumbe wao ndani ya gumzo la moja kwa moja. Unaweza kuwasha Super Chat na Super Stickers kwa watazamaji kabla na wakati wa Onyesho la kwanza.

Kuangalia ikiwa unastahiki kutumia Super Chat na Super Stickers.

Uanachama katika kituo

Ikiwa unastahiki, unaweza kufaidika na manufaa ya uanachama katika kituo kama vile gumzo la wanachama pekee. Pia, utapata manufaa kama vile emoji na beji maalum ya uaminifu.

Pata maelezo zaidi kuhusu uanachama katika kituo.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
10815103069029798707
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false