Pata maelezo kuhusu majaribio na ofa za YouTube Premium

YouTube Premium huboresha utazamaji na usikilizaji wako wa video na muziki kwa kukupa vipengele vya kipekee, kukuonyesha yaliyoendelea wakati wa maandalizi, na mengine mengi. Ikiwa hujawahi kutumia YouTube Premium au YouTube Music Premium, unaweza kujisajili ili ujaribu uanachama. Pata maelezo zaidi hapa chini.

Jinsi majaribio yanavyofanya kazi

  • Unapojisajili kwa jaribio, utafurahia manufaa ya uanachama kama mwanachama wa YouTube Premium au YouTube Music Premium.
  • Wakati wa kujisajili, unaombwa uweke njia ya kulipa ili iwekwe kwenye faili. Huenda ukaona tozo la kuthibitisha akaunti kwenye akaunti yako, ambalo hutuwezesha kuthibitisha kuwa njia yako ya kulipa ni halali. Utozaji huu hautachakatwa na utatoweka ndani ya siku 1 hadi 14.
  • Kipindi chako cha kujaribu kinapoisha, uanachama wako utajisasisha kiotomatiki kwa kutumia maelezo ya njia ya kulipa yaliyo kwenye faili. Utatozwa bei ya sasa ya uanachama kila mwezi isipokuwa ughairi kabla ya kipindi cha kujaribu kuisha.
  • Ukighairi uanachama wako wakati wa kipindi cha kujaribu, utapoteza idhini ya kufikia manufaa yako ya Premium mwishoni mwa kipindi chako cha kujaribu.
Kumbuka: Ikiwa hujatimiza masharti ya kujiunga hapo chini, ombi lako la kujaribu halitaendelea.

Maelezo kuhusu kutimiza masharti ya vipindi vya kujaribu

Dokezo: Unaweza tu kujisajili katika kipindi kimoja cha kujaribu kwa njia ya kulipa kwa vipindi vya kujaribu vya mwezi 1 au vipindi vya kujaribu vya muda mrefu.

Kwa watumiaji walio na akaunti za Workspace:

  • Huwezi kujisajili kupata uanachama binafsi au wa familia kwenye YouTube Premium ukitumia akaunti ya Workspace, isipokuwa kama ni akaunti ya toleo binafsi la Workspace.
  • Unaweza kujisajili ili upate mpango wa wanafunzi wa YouTube Premium ukitumia akaunti yoyote ya Workspace.
  • Iwapo unafikiri kuwa unastahiki kipindi cha kujaribu lakini huoni chaguo lake, badilisha utumie akaunti yako binafsi na ujisajili katika youtube.com/premium.

Majaribio ya mwezi 1 ya YouTube Premium na Music Premium:

  • majaribio ya mwezi 1 yanapatikana kwa:
    • wanachama wa mara ya kwanza
    • watumiaji walioghairi uanachama wa YouTube Premium, Music Premium au Google Play angalau miezi 6 iliyopita
  • Unaweza kujaribu mara 1 pekee ndani ya miezi 12

Majaribio ya muda mrefu zaidi ya YouTube Premium na Music Premium: Wakati mwingine, tutatoa jaribio la muda mrefu zaidi ambalo hudumu kwa zaidi ya mwezi 1.

  • Majaribio ya muda mrefu zaidi yanapatikana kwa wanachama wa mara ya kwanza AU wanaorejea miaka 3 baada ya kughairi uanachama wako awali.
  • Jaribio 1 pekee linalozidi mwezi moja linapatikana ndani ya miaka 3.
Kumbuka: Ikiwa hujatimiza masharti ya kujiunga, ombi lako la kujaribu halitaendelea.

Angalia ikiwa umetimiza masharti ya kufanya jaribio

Kuangalia ustahiki wako wa jaribio ukitumia kompyuta:

  1. Ingia kwenye akaunti yako ya YouTube.
  2. Nenda kwenye youtube.com/paid_memberships.
  3. Kwenye sehemu ya Ofa za YouTube, tutaorodhesha majaribio unayostahiki.
  4. Chagua ofa moja kisha ufuate hatua ulizopewa ili uitumie.
Kumbuka: Ikiwa hujatimiza masharti ya kujiunga, ombi lako la kujaribu halitaendelea.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu
16519516870831746758
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true