Maswali Yanayoulizwa Sana na wazazi kuhusu akaunti zinazodhibitiwa

Kuna tofauti gani kati ya akaunti inayodhibitiwa na akaunti ya kawaida ya YouTube au YouTube Music?

Akaunti inayodhibitiwa ya mtoto wako itaonekana kama akaunti ya kawaida ya YouTube au YouTube Music lakini itatofautiana katika vipengele na mipangilio inayopatikana.

Maudhui ambayo mtoto wako anaweza kucheza yatategemea mipangilio ya maudhui utakayochagua kwa ajili ya akaunti yake inayodhibitiwa. Baadhi ya vipengele vinavyopatikana kwa kawaida kwenye YouTube na YouTube Music havitapatikana. Ili ufiikie orodha ya vipengele visivyopatikana, nenda kwenye Je, matumizi yanayosimamiwa kwenye YouTube ni nini?.

Kwa kuzingatia kuwa uhuru wa kujieleza na jumuiya ni vipengele muhimu katika YouTube, tunashirikiana na wazazi na wataalamu tunapofanya maamuzi kuhusu vipengele vinavyopaswa kujumuishwa kwenye akaunti zinazodhibitiwa.

YouTube Kids ni nini? Inatofautiana vipi na akaunti inayodhibitiwa kwenye YouTube?

YouTube Kids ni programu yetu maalum iliyobuniwa kwa ajili ya watoto. Kwa kutumia akaunti inayodhibitiwa, wazazi huchagua mipangilio ya maudhui inayoweka mipaka ya maudhui ambayo watoto wanaweza kupata na kucheza kwenye YouTube na YouTube Music.

YouTube Kids inajumuisha video mbalimbali lakini za chaguo chache ukilinganisha na zinazopatikana kwenye akaunti ya kawaida ya YouTube. Video huchaguliwa kwa kutumia mchanganyiko mbalimbali. Video hizi huchaguliwa kwa uhakiki unaofanywa na binadamu pamoja na orodha iliyoratibiwa kutoka kwa wataalamu. Pia, uchujaji wa kialgoriti utasaidia kuchagua video zinazofaa.

Ili upate maelezo zaidi kuhusu utofauti kati ya YouTube Kids na akaunti zinazodhibitiwa, nenda kwenye Fahamu chaguo zenu kama familia.

Je, Hali yenye Mipaka ni nini? Inatofautiana vipi na akaunti inayodhibitiwa kwenye YouTube?

Hali yenye Mipaka ni mipangilio isiyo ya lazima inayopatikana kwenye YouTube. Husaidia kuchuja maudhui ya watu wazima ambayo usingependa kuyaona au hutaki watu wengine wanaotumia kifaa chako wayaone. Watumiaji wanaohitaji hali mahususi ya utumiaji kwenye YouTube, kama vile maktaba, shule na taasisi za umma, kwa kawaida huwasha kipengele cha Hali yenye Mipaka.

Wazazi wa vijana walio na umri wa zaidi ya miaka 13 ambao wameongeza usimamizi kwenye Akaunti za Google za vijana wao wanaweza pia kutumia Hali yenye Mipaka ili kusaidia kuchuja maudhui ambayo huenda yakawa ya watu wazima.

Akaunti zinazodhibitiwa hazipatikani kwa vijana wanaozidi umri unaofaa katika nchi au eneo waliko ambao wana usimamizi ulioongezwa kwenye Akaunti zao za Google. Akaunti zinazodhibitiwa zinapatikana kwa watoto walio na umri chini ya miaka 13 (au umri unaofaa katika nchi au eneo waliko) na huwapa wazazi vidhibiti vya kusimamia hali ya utumiaji ya watoto wao kwenye YouTube.

Je, chaguo zangu ni zipi kwa ajili ya mipangilio ya maudhui ninapofungua akaunti inayodhibitiwa ya mtoto wangu?

Kuna mipangilio ya maudhui ya aina 3 unayoweza kuchagua:

  • Gundua: Hulingana kwa jumla na ukadiriaji wa maudhui kwa watazamaji walio na umri wa miaka 9 na zaidi. Video zinajumuisha blogu za video, mafunzo, video za michezo, video za muziki, habari na zaidi. Hamna mitiririko mubashara, isipokuwa kwa Maonyesho ya Kwanza. Baadhi ya video zina matukio kiasi ya vurugu, lugha ya kukera na dawa zinazodhibitiwa. Baadhi ya video pia zinaweza kuwa na maudhui ya elimu yanayohusiana na taswira na mabadiliko ya mwili, afya ya akili na afya ya kingono.
  • Gundua zaidi: Hulingana kwa jumla na ukadiriaji wa maudhui kwa watazamaji walio na umri wa miaka 13 na zaidi. Mipangilio hii inajumuisha kundi kubwa la video. Video zinajumuisha mitiririko mubashara, blogu za video, mafunzo, video za michezo, video za muziki, habari, video za elimu, video za kujifanyia mwenyewe (DIY), sanaa na ufundi, dansi na zaidi. Baadhi ya video zina matukio kiasi ya vurugu katika mazingira halisi, lugha chafu isiyokithiri au dawa zinazodhibitiwa. Marejeleo ya ngono isiyo dhahiri na mada zinazohusiana na siha pamoja na afya ya mwili, akili na kingono zinaweza kuwepo.
  • Maudhui zaidi ya YouTube: Mipangilio hii inajumuisha karibu kila kitu kwenye YouTube isipokuwa kwa video zilizowekewa alama ya 18+ na video zingine ambazo huenda hazifai kwa watazamaji wanaotumia hali za utumiaji zinazosimamiwa. Video zinajumuisha mitiririko mubashara, blogu za video, mafunzo, video za michezo, video za muziki, habari, video za elimu, video za kujifanyia mwenyewe (DIY), sanaa na ufundi, dansi na zaidi. Baadhi ya video zitakuwa na mada nyeti ambazo zinaweza kufaa tu kwa vijana wakubwa, kama vile vurugu zinazoogofya, maudhui ya watu wazima, uchi, lugha chafu iliyokithiri na mada kama vile magonjwa ya afya ya akili, maelezo ya kula kiafya na afya ya kingono.

Pata maelezo zaidi katika Mipangilio ya maudhui ya familia zinazotumia matumizi yanayosimamiwa.

Je, ninaweza kuipa akaunti inayodhibitiwa ya mtoto wangu ruhusa ya kufikia YouTube Music au YouTube TV?

Akaunti zinazodhibitiwa zinatumika kwenye YouTube Music. Mipangilio ya maudhui unayochagua kwa ajili ya akaunti inayodhibitiwa ya mtoto wako itatumika pia kwenye maudhui ya YouTube Music anapoingia katika akaunti kwenye programu au tovuti.

Itakuwaje ikiwa siwezi kupakua YouTube au YouTube Music kwenye kifaa cha iOS cha mtoto wangu?

Ili kupakua programu ya YouTube au YouTube Music, wazazi wanapaswa kukagua mipangilio yao ya Vizuizi vya Faragha na Maudhui kwenye kifaa cha iOS cha mtoto wao.

Ikiwa mtoto wangu ana akaunti inayodhibitiwa, je anaweza kutumia YouTube kwenye Televisheni yangu?

Akaunti zinazodhibitiwa zinaweza kutumia YouTube kwenye televisheni nyingi zinazoweza kuunganisha kwenye intaneti ambazo zinastahiki, Microsoft Xbox, Nintendo Switch na Sony PlayStation. Akaunti zinazodhibitiwa haziwezi kutumika kwenye vifaa vya zamani vya Android TV.

Ninawezaje kufungua akaunti inayodhibitiwa kwa kutumia kifaa ambacho kina programu ya Mratibu wa Google?

Ili umwongeze mtoto wako, fuata hatua zilizo kwenye Ruhusu mtoto wako atumie Mratibu wa Google kwenye vifaa vyako.  Ukiongeza Akaunti ya Google ya mtoto wako na sauti kwenye kifaa, akaunti zinazodhibitiwa zinaweza kutumia programu ya Mratibu wa Google kwenye vifaa vinavyotumiwa kwa pamoja.

Je, YouTube huchuja vipi maudhui yasiyofaa?

Mwongozo wetu wa Jumuiya unabainisha maudhui yanayoruhusiwa na yasiyoruhusiwa kwenye YouTube. Mwongozo huu unatumika kwa kila mtumiaji, bila kujali umri wao. Ikiwa umefungua akaunti inayodhibitiwa kwa ajili ya mtoto wako, kuna sera zinazobainisha aina mbalimbali za maudhui yanayofaa kwa mipangilio tofauti ya maudhui.

Tunawajali sana watumiaji wetu na tunajitahidi kuondoa maudhui yasiyofaa, lakini hakuna mfumo wa kiotomatiki wa vichujio ambao ni timilifu. Unaweza kubadilisha ruhusa za programu na mipangilio ya maudhui ya akaunti ya mtoto wako wakati wowote. Iwapo utaona maudhui unayoamini kuwa hayafai kwenye YouTube, unaweza kuyaripoti.

Je, matangazo hufanyaje kazi kwenye akaunti zinazodhibitiwa?

Ili kuwalinda vizuri watoto, aina fulani za matangazo haziruhusiwi na matangazo yaliyowekewa mapendeleo huzimwa. Watazamaji wa maudhui "yaliyoundwa kwa ajili ya watoto" wanaweza kuona bamba la tangazo kabla na baada ya tangazo la video kuonyeshwa. Bamba hili husaidia kuwaarifu tangazo linapoanza na linapomalizika. Ikiwa una mpango wa familia wa YouTube Premium, mtoto wako ataweza kuona maudhui bila matangazo na kutumia manufaa mengine ya pamoja ya uanachama.

Video ambazo mtayarishi amebainishwa kuwa zinalipia bidhaa ili zitangazwe katika maudhui au maudhui yaliyoidhinishwa kwenye video zake yataonyeshwa kwenye akaunti zinazodhibitiwa katika YouTube. Pia, video hizi ni lazima zitii sera ya matangazo kuhusu video zinazolenga watoto.

Je, YouTube inalinda vipi faragha ya mtoto wangu?

YouTube ni sehemu ya Google na inatii kanuni na sera za faragha za Google. Tunafahamu ni muhimu uelewe taarifa binafsi tunazokusanya kuhusiana na Akaunti ya Google ya mtoto wako. Tunafahamu pia kuwa unahitaji kujua ni kwa nini tunakusanya data hiyo, na jinsi unavyoweza kudhibiti na kuifuta.Sera ya Faragha ya Google na Ilani yetu ya Faragha ya Akaunti za Google kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka 13 (au umri unaofaa katika nchi au eneo waliko) inafafanua desturi zetu za faragha.

Mtoto wako anaweza kudhibiti na kupata maelezo zaidi kuhusu mipangilio yake ya faragha na vidhibiti chini ya "Data yako kwenye YouTube" katika akaunti yake. Ukurasa huu unajumuisha muhtasari wa video yake, data ya shughuli na mipangilio ili kusimamia data hii. Pia, ukurasa huu una maelezo ya jinsi data yake inavyotumiwa kuboresha hali yake ya utumiaji kwenye YouTube, kama vile kuwakumbusha maudhui waliyotazama na kutoa mapendekezo.

Ukiwa mzazi na msimamizi wa Akaunti ya Google ya mtoto wako, unaweza kusitisha au kufuta historia ya mambo aliyotafuta na kutazama kwenye Family Link. Unaweza pia kufuta historia katika ukurasa wa Mipangilio ya Wazazi kwenye YouTube.

Je, akaunti zinazodhibitiwa zinapatikana kwa ajili ya shule na taasisi za elimu?

Akaunti zinazodhibitiwa kwa sasa zinapatikana kwa akaunti binafsi pekee. Akaunti zinazodhibitiwa hazipatikani kwa ajili ya shule au taasisi za elimu. Jinsi unavyoingia katika akaunti yako kwenye kifaa kunaweza kuathiri namna ambavyo YouTube inaweza kutumika. Pata maelezo zaidi kuhusu akaunti zinazodhibitiwa.

Ni nani anastahili kuwa na akaunti inayodhibitiwa kwenye YouTube?

Unaweza kufungua akaunti inayodhibitiwa kwenye YouTube kwa ajili ya mtoto wako aliye na umri wa chini ya miaka 13 (au umri unaofaa katika nchi au eneo aliko).

Utakuwa hujakidhi vigezo vya kuwa na akaunti inayodhibitiwa kwenye YouTube ikiwa:

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9170666490574615991
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false