Kuweka mipangilio ya maudhui ya matumizi yanayosimamiwa

Tunawapa wazazi chaguo za kuwaongoza watoto wao wanapotumia YouTube. Tunaamini kuwa watoto wanaweza kugundua mambo mapya yanayowavutia, kujifunza mitazamo anuai na kujihisi kuwa sehemu ya maudhui wanayotazama kupitia video kwenye YouTube. Ikiwa unaamini kuwa mtoto wako anaweza kuwa tayari kugundua ulimwengu mpana wa maudhui kwenye YouTube, kuna machaguo kadhaa. Unaweza kuchagua kati ya kutumia programu yetu ya YouTube Kids kwa hali salama na rahisi ya utumiaji au kuunda na kudhibiti matumizi yanayosimamiwa kwenye YouTube.

Mipangilio ya maudhui kwa ajili ya familia zinazotumia matumizi yanayosimamiwa

Fuatilia chaneli ya Watazamaji ya YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.

Katika YouTube, tunaamini kuwa maudhui mbalimbali na kupata maoni kutoka vyanzo tofauti kunaweza kutusaidia kujifunza kuhusu watu wengine. Utofauti huu pia unamaanisha kufahamu mitazamo ambayo huenda usikubaliane nayo. Tuna Mwongozo wa Jumuiya unaosaidia kujenga hali salama ya utazamaji kwa kila mtumiaji. Pia, tuna sera zaidi za maudhui zilizofafanuliwa hapa chini ambazo zinatumika mahususi kwa watazamaji wadogo katika hali ya utumiaji inayosimamiwa. Ikiwa ungependa mtoto wako atumie YouTube katika hali ya utumiaji inayosimamiwa, tunakuhimiza upitie mwongozo huu na familia yako kabla ya kuanza kutumia.

Utaratibu wetu

YouTube imeandaa mkusanyiko wa sera za ufaafu kwa maudhui yanayolingana kwa ujumla na ukadiriaji wa maudhui ya Televisheni na filamu. Sera hizi zinasaidia kuelekeza video ipi imetimiza masharti katika mipangilio tofauti ya maudhui inayopatikana kwa ajili ya familia. Kupata ushauri kwa wataalamu wa nje wanaoshughulikia masuala ya malezi ya watoto, maudhui ya watoto, mafunzo dijitali na uraia kuliboresha zaidi sera hizi. Mfumo wetu wa kiotomatiki ambao unazingatia sera hizi za maudhui, kisha hutambua video zinazofaa kujumuishwa kwenye kila mipangilio ya maudhui. Tunafahamu kuwa mifumo yetu si timilifu na itafanya makosa. Tuna timu ya wahandisi na wakaguzi wanaoshirikiana pamoja ili kuendelea kuboresha mifumo yetu. Pia, tunatathmini upya sera zetu mara kwa mara, hivyo sera zilizoorodheshwa hapa chini zinaweza zisiwe kamilifu.

Ikiwa utaona maudhui unayoamini kuwa hayafai kwenye YouTube, unaweza kuyaripoti.

Mipangilio ya maudhui

Gundua Hulingana kwa jumla na ukadiriaji wa maudhui kwa watazamaji walio na umri wa miaka 9 na zaidi
Gundua zaidi Hulingana kwa jumla na ukadiriaji wa maudhui kwa watazamaji walio na umri wa miaka 13 na zaidi
Maudhui zaidi ya YouTube Karibia video zote kwenye YouTube isipokuwa maudhui yaliyowekewa alama ya 18+ na video nyingine ambazo huenda hazifai kwa watazamaji wanaotumia hali za utumiaji zinazosimamiwa.

Sera za Maudhui

Sera zetu za maudhui zinatofautiana kati ya mipangilio tofauti ya maudhui inayopatikana kwa ajili yako unapofungua akaunti inayodhibitiwa ya mtoto wako. Mfumo wetu wa kiotomatiki ambao unazingatia sera hizi za maudhui, kisha hutambua maudhui yanayofaa kujumuishwa kwenye kila mipangilio ya maudhui. Tunafahamu kuwa mifumo yetu si timilifu na itafanya makosa. 

Gundua

Kipengele cha “Gundua” kinalenga familia zilizo tayari kuacha kutumia YouTube Kids na kuanza kugundua maudhui mbalimbali kwenye YouTube. Mipangilio hii inajumuisha aina mbalimbali za video ambazo hulingana kwa jumla na ukadiriaji wa maudhui kwa watazamaji walio na umri wa miaka 9 na zaidi. Video zinajumuisha blogu ya video, mafunzo, video za michezo, habari, maudhui ya elimu, video za kujifanyia mwenyewe (DIY), sanaa na ufundi, dansi na zaidi. Huenda baadhi ya video zikajumuisha:

Maudhui ya watu wazima: Video zenye maudhui ya mapenzi, ikiwa ni pamoja na maonyesho mafupi ya mvuto wa kimapenzi na huba. Video za elimu zinazoambatana na umri kuhusu maudhui ya ngono au utambulisho wa kijinsia na mada za Elimu ya Ngono kama vile kubalehe na uzazi.

Vurugu: Video zinazoambatana na umri kuhusiana na matukio ya sasa au ya kihistoria ambayo ni ya kielimu lakini huenda yana vurugu kidogo katika muktadha wa tukio. Vurugu zisizo za kuogofya katika video zilizoandikwa na kuhuishwa kwenye katuni, michezo ya video, vipindi vya televisheni na filamu.

Silaha: Video zinazoangazia silaha zisizo halisi katika muktadha wa watoto kuchezea vitu, michezo ya video, uhuishaji na silaha za kisanii katika muktadha wa kihistoria.

Maudhui Hatari: Video zinazoangazia vitendo vya hatari kama vile matendo ya kustaajabisha, mzaha na mashindano ambayo si rahisi kuigwa na watoto au kanusho dhahiri lenye ufumbuzi unaofaa wa usalama. Video zinazoonyesha pombe na tumbaku kwa ufupi.

Lugha Isiyofaa: Video zenye matumizi yasiyojirudia mara kwa mara ya lugha inayokera kiasi, kama vile "shenzi" au "bure" katika muktadha ambao si wa unyanyasaji.

Lishe, Siha na Urembo: Video zinazoangazia maoni kuhusu bidhaa za urembo, mafunzo ya vipodozi yanayoambatana na umri, pamoja na maudhui ya kielimu kuhusu siha. Maudhui haya yanajumuisha ulaji bora na mazoezi.

Mada Nyeti: Video zinazoambatana na umri zinazojadili masuala nyeti kama vile afya ya akili, uraibu, matatizo ya ulaji, pamoja na huzuni na maumivu. Video katika mipangilio hii haziangazii picha za kuogofya na zinaangazia mbinu za kukabiliana na kudhibiti hali hizi, na umuhimu wa kutafuta usaidizi.

Video za Muziki: Video za Muziki zinaweza kujumuisha maneno ya wimbo yenye lugha ya kukera kiasi au mitajo ya pombe au tumbaku. Video zinaweza pia kuangazia dansi yenye maudhui ya ngono ambayo hayajakithiri, na maonyesho ya pombe au tumbaku yasiyojirudia mara kwa mara.

Gundua zaidi

Kipengele cha “Gundua zaidi” ni kwa ajili ya watoto walio tayari kugundua ulimwengu mpana zaidi wa YouTube. Mipangilio hii inajumuisha kila kitu katika kipengele cha Gundua, na video mbalimbali ambazo hulingana kwa jumla na ukadiriaji wa maudhui kwa watazamaji walio na umri wa miaka 13 na zaidi. Video zinajumuisha mtiririko mubashara, blogu ya video, mafunzo, video za michezo ya video, habari, video za elimu, video za kujifanyia mwenyewe (DIY), sanaa na ufundi, dansi na zaidi. Huenda baadhi ya video zikajumuisha:

Maudhui ya Watu Wazima: Video zenye maudhui ya kingono, kama vile simulizi zisizo dhahiri za matukio ya kingono na maonyesho ya kugusana kimwili. Video za kielimu kuhusu ngono na utambulisho wa kijinsia na mada za Elimu ya Ngono kama vile kupevuka maumbile, afya ya uzazi, kujizuia na mihemko ya kingono na magonjwa.

Vurugu: Video zisizoogofya zinazohusiana na matukio ya sasa au ya kihistoria. Vurugu inayoogofya kwa muda mfupi ni video zilizoandikwa na kuhuishwa katika michezo ya video, vipindi vya televisheni na filamu.

Silaha: Video zinazoangazia silaha halisi na zisizo halisi kwenye video zilizoandikwa ambazo huonekana mara nyingi kwenye vipindi vya televisheni na filamu. Video zinazoangazia bunduki halisi zinapotumiwa katika muktadha wa michezo au elimu kuhusu usalama wa bunduki.

Maudhui Hatari: Video zinazoangazia vitendo vya hatari kama vile matendo ya kustaajabisha, mzaha na mashindano ambayo yanaweza kusababisha majeraha makubwa ya mwili lakini si rahisi kuigwa na watoto. Video zinazoonyesha au kuangazia matumizi ya pombe au tumbaku mara kwa mara.

Lugha Isiyofaa: Video zenye matumizi ya mara kwa mara ya lugha inayokera au lugha chafu kama vile "malaya" au "mjinga" katika muktadha usio wa unyanyasaji na usiochochea ngono. Ikiwa si mara kwa mara na yanatumiwa katika muktadha usio wa unyanyasaji, maneno yanayodhalilisha yanaweza kutumika katika muktadha wa kielimu au video ya muziki.

Lishe, Siha na Urembo: Video zinazoangazia mafunzo ya vipodozi, vidokezo vya urembo, mbinu za maisha na video zinazohusiana na ulaji bora na mazoezi.

Mada Nyeti: Video zisizoogofya zinazohusiana na masuala nyeti kama vile afya ya akili, kufikiria kujiua, kujijeruhi, uraibu, matatizo ya ulaji na maumivu au huzuni. Video hizi zinaangazia mbinu chanya za kukabiliana na kudhibiti hali hizo na umuhimu wa kuomba usaidizi.

Video za Muziki: Video za muziki zinaweza kujumuisha maneno ya wimbo yenye marejeleo ya kingono, lugha chafu iliyokithiri ambayo haijirudii mara kwa mara au maneno yenye udhalilishaji katika muktadha usio wa unyanyasaji au chuki. Video zinaweza kuangazia pia dansi yenye maudhui ya ngono na matumizi ya pombe, tumbaku au bangi.

Maudhui zaidi ya YouTube
“Maudhui zaidi ya YouTube'' ni kwa ajili ya watoto walio tayari kugundua ulimwengu mpana wa YouTube, ikiwa ni pamoja na maudhui kwa ajili ya vijana wakubwa. Mipangilio hii inajumuisha karibia kila kitu kwenye YouTube isipokuwa video zilizowekewa alama ya 18+ na video nyingine ambazo huenda hazifai kwa watazamaji wanaotumia hali za utumiaji zinazosimamiwa. Video zinajumuisha mitiririko mubashara, blogu za video, mafunzo, video za michezo, habari, video za elimu, video za kujifanyia mwenyewe (DIY), sanaa na ufundi, dansi na zaidi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
17565931965008281612
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false