Kuzuia kupakia tena video zilizoondolewa

Ikiwa kazi yako inayolindwa kwa hakimiliki imechapishwa kwenye YouTube bila idhini yako, unaweza kuwasilisha ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki. Ukifanya hivyo kwa kutumia fomu yetu ya wavuti, unaweza kuteua chaguo la kuzuia nakala za maudhui yanayofanana zisipakiwe tena.

Kuteua chaguo hili kunamaanisha kuwa YouTube itajaribu kuzuia kiotomatiki nakala za maudhui yanayofanana unazoomba ziondolewe ili zisipakiwe tena baadaye. Kumbuka kuwa ombi lako la kuondoa video lazima liwe limekamilika na liwe sahihi kabla ya video zozote kuondolewa au kabla ya nakala zozote kuzuiwa zisipakiwe tena.

Matumizi mabaya ya kipengele hiki yanaweza kusababisha upoteze uwezo wa kukitumia kuomba video ziondolewe katika siku zijazo. Matumizi mabaya ya fomu ya wavuti, kama vile kutoa taarifa za uongo, yanaweza kusababisha kusimamishwa kwa akaunti yako au kuchukuliwa hatua nyinginezo za kisheria.
Jinsi ya Kuzuia Video Ulizoziondoa Zisipakiwe Tena

Kuteua chaguo la Zuia Nakala

Kabla ya kuteua chaguo la Zuia Nakala, hakikisha una haki za kipekee za kimataifa za video unazoripoti kwenye ombi lako la kuondoa video. Ili uteue chaguo la Zuia Nakala:

  1. Anza kujaza fomu ya wavuti ya maombi ya kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki.
  2. Chini ya Chaguo za kuondoa video, chagua kisanduku kilicho karibu na "Zuia nakala za video hizi zisionekane kwenye YouTube kuanzia sasa."
  3. Bofya TUMA ukimaliza kujaza fomu.
    • Kumbuka: Ni lazima ombi lako la kuondoa video liidhinishwe kabla ya mfumo wetu kuanza kutafuta na kuzuia nakala zisipakiwe.
  • Unaweza pia kufikia fomu ya wavuti kwenye ukurasa wa Hakimiliki wa Studio ya YouTube. Kwenye kichupo cha Maombi ya Kuondoa Video, bofya OMBI JIPYA LA KUONDOA VIDEO.
  • Katika baadhi ya matukio, tunaweza pia kuzuia mchakato wa kupakia upya video ambayo ina nakala ya maudhui ya video iliyoondolewa awali kwa kukiuka hakimiliki hata kama hujateua chaguo la Zuia Nakala.

Kuangalia nakala zilizozuiwa zisipakiwe upya

Ikiwa ulichagua Zuia Nakala kwenye ombi lako la kuondoa video na ombi hilo limeidhinishwa, unaweza kuona idadi ya nakala zilizozuiwa kiotomatiki kupakiwa upya:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Hakimiliki .
  3. Bofya kichupo cha Maombi ya kuondoa video.
  4. Bofya safu mlalo. Safu mlalo hupanuka ili kuonyesha maelezo zaidi kuhusu video iliyoombwa kuondolewa.
  5. Katika safu wima ya Zilizozuiwa kiotomatiki , unaweza kupata idadi ya video ambazo zimezuiwa kiotomatiki zisipakiwe upya.
    • Hali ya safu wima hii ikiwa Inatumika, inamaanisha kuwa YouTube inafanya jitihada zote kuwazuia watu wengine wasipakie upya nakala za video hizi.
Pata maelezo zaidi kuhusu kukagua video zinazoonyeshwa kwenye safu wima ya Tafuta zinazolingana.

Kuzima chaguo la Zuia Nakala

Ikiwa uliteua chaguo la Zuia Nakala kwenye ombi lako la kuondoa video, unaweza kuzima chaguo hilo wakati wowote. Hatua ya kuzima itaruhusu nakala zozote za video zilizoondolewa zipakiwe katika siku zijazo. Ili kuzima chaguo:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Hakimiliki .
  3. Bofya kichupo cha Maombi ya kuondoa video.
  4. Bofya safu mlalo. Safu mlalo hupanuka ili kuonyesha maelezo zaidi kuhusu video iliyoombwa kuondolewa.
  5. Batilisha uteuzi wa kisanduku kilicho karibu na kipengele cha Zuia nakala.
Vidokezo:
  • Kuzima kipengele cha Zuia nakala kunaathiri tu video zilizopakiwa kuanzia muda huo na kuendelea. Video ambazo tayari zimeondolewa hazitarejeshwa.
  • Hatua ya Kufuta ombi lako la kuondoa video pia itazima kipengele hiki kiotomatiki.

Maswali Yanayoulizwa Sana

Ikiwa uliwasilisha ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki:

Nilisahau kuteua chaguo la "Zuia Nakala" nilipowasilisha ombi langu la kuondoa video. Je, ninaweza kurudi na kuteua chaguo hilo?

Ikiwa mwanzoni hukuteua chaguo la Zuia Nakala, huwezi kuliteua kwa ombi la kuondoa video ambalo tayari umetuma. Ukipata video nyingine ambayo ina maudhui yanayokiuka hakimiliki yako, tumia fomu ya wavuti ili utume ombi jipya la kuondoa video. Hakikisha umeteua chaguo la Zuia Nakala kabla ya kutuma ombi lako.

Kwa nini sioni video zozote ambazo zimezuiwa kiotomatiki kupakiwa upya?

Huenda usione nakala zozote za maudhui sawa yaliyozuiwa kiotomatiki yasipakiwe upya ikiwa:

  • Ombi lako la kuondoa video halijaidhinishwa.
  • Hatujapata nakala zozote za maudhui yaliyoondolewa.

Niliteua chaguo la "Zuia Nakala", lakini nimepata nakala ya video yangu ambayo haikuondolewa kiotomatiki. Kwa nini haikutambuliwa?

Kipengele cha Zuia Nakala hujaribu kuzuia nakala za maudhui yaliyoondolewa ili zisipakiwe tena. Kipengele hiki huanza kutumika baada ya ombi lako la kuondoa video kuidhinishwa. Inawezekana video uliyoibaini ilipakiwa kabla ya ombi kuidhinishwa.

Klipu fupi za maudhui yako huenda zisizuiwe kupakiwa. Mfumo wetu huenda usizingatie hizi kuwa nakala ya maudhui yaliyoondolewa.

Ikiwa umebaini nakala ya maudhui iliyoondolewa, unaweza kuiripoti ukitumia fomu yetu ya wavuti. Unaweza pia kuangalia iwapo video uliyobaini inaonekana kwenye kichupo chako cha Zinazolingana na uwasilishe ombi la kuondoa video ukiwa hapo.

Je, kuna tofauti gani kati ya safu wima ya “Zilizozuiwa kiotomatiki” na safu wima ya “Tafuta zinazolingana”?

Safu wima ya Zilizozuiwa kiotomatiki huonyesha idadi ya nakala za maudhui yaliyoondolewa. Video hizi zilizuiwa kiotomatiki zisionekane kwenye YouTube mtumiaji alipojaribu kuzipakia.

Hali ya Zilizozuiwa kiotomatiki inapoonyesha kuwa Inatumika, inamaanisha kuwa YouTube inajaribu kuwazuia wengine wasipakie nakala hizi.

Safu wima ya Tafuta zinazolingana huonyesha iwapo YouTube inatafuta maudhui ambayo huenda ni nakala za maudhui yaliyoondolewa.

Hali ya Tafuta zinazolingana inapoonyesha kuwa Inatumika, inamaanisha kuwa YouTube inatafuta maudhui ambayo huenda ni nakala za maudhui yaliyoondolewa. Maudhui haya ambayo huenda ni nakala hayakuzuiwa kiotomatiki yasipakiwe kwa sababu hayakubainishwa kuwa ni nakala, lakini yanachukuliwa kuwa yanaweza kuwa maudhui yanayolingana.

Kumbuka: Hali ya safu wima hizi inaweza kuonyesha kuwa Hazitumiki ombi lako la kuondoa video linapoondolewa. Hali hii inaweza kutokea ikiwa umefuta ombi lako la kuondoa video au ikiwa video imerejeshwa kutokana na arifa ya kukanusha.

Kwa nini si kila video inayotumia maudhui yangu inazuiwa isipakiwe, ikiwa ni pamoja na video ambazo hazijabainishwa kuwa ni nakala?

Si matumizi yote ya maudhui yako yanakiuka hakimiliki yako. Kuna hali zisizofuata kanuni za hakimiliki kama vile matumizi ya haki, ambayo yanaweza kumaanisha kuwa matumizi ya maudhui yako ni halali.

Mfumo wetu utakuonyesha maudhui ambayo huenda ni nakala ya maudhui yaliyoondolewa, lakini ni jukumu lako kuamua hatua utakayochukua. Ikiwa unaamini kuwa video ambayo huenda ni nakala inakiuka hakimiliki yako, unaweza kutuma ombi la kuondoa nakala husika.

Kwa nini siwezi kujua ni nakala gani mahususi zilizuiwa kiotomatiki zisipakiwe?

Kwa kuwa video hizi hazikupakiwa, hakuna hatua yoyote unayoweza kuchukua. Idadi ya video zilizoonyeshwa kwenye safu wima ya Zimezuiwa kiotomatiki itakuongezea ufahamu kuhusu idadi ya nakala za video zilizozuiwa kupakiwa tena.

Je, nakala ya maudhui yaliyoondolewa itazuiwa ili isipakiwe ikiwa imewekwa kuwa ya faragha?

Bila kujali mipangilio ya faragha, mfumo wetu utajaribu kutambua nakala ya maudhui yaliyoondolewa na kuzizuia kiotomatiki zisipakiwe upya.

Kwa video zinazolingana ambazo zinahitaji ukaguzi wako, tutaonyesha tu video zinazopatikana kwa umma.

Je, kipengele cha "Zuia Nakala" kitazuia kiotomatiki video zinazojumuisha maudhui yangu yenye hakimiliki yasiyo ya video, kama vile picha?

Ndiyo, kipengele cha Zuia Nakala kinaweza kuzuia nakala na kuonyesha video ambazo huenda ni nakala iwapo maudhui yako yenye hakimiliki yasiyo ya video yanapatikana katika video.

Kumbuka, mfumo wetu hukagua tu video zilizopakiwa kwenye YouTube. Ikiwa maudhui yako yasiyo ya video yanapatikana katika maelezo au kijipicha au mahali popote ambapo si kwenye video yenyewe mfumo wetu hautaweza kuyatambua.

Je, inamaanisha nini kuwa na haki za kipekee za kimataifa kwa maudhui ninayoomba yaondolewe? 

Kuwa na haki za kipekee za kimataifa kunamaanisha kuwa ni wewe tu au mteja unayemwakilisha ndiye anayedhibiti matumizi na usambazaji wa maudhui duniani kote.

Kwa nini sina uwezo wa kufikia Content ID?

Zana za udhibiti wa hakimiliki za YouTube zimebuniwa kwa ajili ya aina mbalimbali za watayarishi kutoka kwa wapakiaji wa mara chache hadi kampuni za maudhui. Mfumo wa Content ID unapatikana kwa wenye hakimiliki walio na mahitaji makubwa ya udhibiti wa hakimiliki.

Ili kustahiki kutumia mfumo wa Content ID, wenye hakimiliki lazima wamiliki haki za kipekee za maudhui halisi kwa sehemu kubwa ambayo hupakiwa mara kwa mara kwenye YouTube. Ni lazima pia wawe na ujuzi wa kina wa hakimiliki na nyenzo zinazohitajika ili kutumia Content ID, miongoni mwa vigezo vingine. Pata maelezo zaidi kuhusu ustahiki wa Content ID.

Mimi ni mwanamuziki. Je, ninaweza kutumia kipengele hiki kuzuia kupakiwa upya kwa nyimbo zangu?

Ndiyo. Baada ya kufaulu kuondoa video ukitumia aina ya kazi ya “Wimbo Halisi” kwenye fomu ya wavuti, YouTube itajaribu kuzuia nakala za nyimbo zile zile zisipakiwe tena. 

Pia, zana ya Copyright Match Tool itaonyesha video zenye sauti ambazo huenda zikalingana na wimbo au maudhui yako ya sauti. Kumbuka kwamba, ikiwa mtu alitumia sehemu ya wimbo au maudhui yako ya sauti kwenye video yake, haitaonyeshwa na zana ya Copyright Match Tool.

Iwapo video yako ilizuiwa isipakiwe:

Ninaweza kupata wapi maelezo zaidi kuhusu sababu ya video yangu kuzuiwa isipakiwe?

Unaweza kupata maelezo zaidi kwenye Studio ya YouTube:

  1. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
  2. Katika safu wima ya Vizuizi, wekelea kiashiria juu ya Sheria na masharti pamoja na sera. Dirisha ibukizi litakufahamisha kuwa video yako haikuweza kupakiwa kwa sababu ina nakala ya maudhui ya video tuliyoiondoa awali kutokana na ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki. Litakuonyesha ni nani aliyetuma ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki, wakati tuliopokea ombi na jina la kazi ya mlalamikaji inayolindwa kwa hakimiliki.

Pia, tutakutumia barua pepe video yako itakapozuiwa isipakiwe, ambayo itajumuisha maelezo haya.

Ikiwa mojawapo ya video zangu ilizuiwa isipakiwe, je, hiyo inamaanisha kuwa nitapewa onyo la hakimilki?

Hapana, video ikizuiwa kiotomatiki isipakiwe, hatua hiyo haitaathiri chaneli yako na haitasababisha upewe maonyo ya hakimiliki au Maonyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya.

Ikiwa ninaamini kuwa video yangu inapaswa kupakiwa, ninaweza kufanya nini?

Ikiwa unaamini kuwa video yako inapaswa kupakiwa, unaweza kukata rufaa kwa kutumia kiungo kilicho kwenye dirisha ibukizi.

Katika rufaa yako, unapaswa kutupatia maelezo yafuatayo:

  1. Maelezo yako ya mawasiliano

Iwapo YouTube itakubali rufaa uliyokata, tutaisambaza kwa mlalamikaji aliyetuma ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki, ikiwa ni pamoja na taarifa zako binafsi. Anaweza kutumia taarifa hizi kuwasiliana nawe kuhusiana na rufaa uliyokata. Ikiwa una wasiwasi kuhusu kushiriki taarifa zako binafsi na mlalamikaji, unaweza kuteua mwakilishi aliyeidhinishwa (kama vile wakili) ili akate rufaa kwa niaba yako. Mwakilishi aliyeidhinishwa ni lazima atumie akaunti yake mwenyewe ya YouTube kutuma ombi. Pia, anatakiwa abainishe uhusiano wake nawe.

  1. URL sahihi ya video iliyozuiwa isipakiwe

URL hii inapaswa kuonekana kiotomatiki baada ya kubofya kiungo cha kukata rufaa kilicho kwenye dirisha ibukizi.

  1. Sababu za kuamini kuwa una haki zote zinazohitajika kupakia video

Kwa maneno yako mwenyewe, fafanua ni kwa nini unaamini kuwa una haki zote zinazohitajika kupakia video na uambatishe hati za kuthibitisha. Maelezo haya yatatumwa kwa mlalamikaji ili ayakague.

  1. Taarifa

Ni lazima ukubali taarifa 2 zifuatazo:

  • Ninakiri kuwa nina haki zote zinazohitajika kupakia maudhui husika kwenye YouTube.
  • Ninakiri kuwa maelezo yaliyo katika rufaa hii ni kamili na ya kweli. Ninaelewa kuwa kukata rufaa yenye taarifa za uongo kunaweza kusababisha kufungwa kwa akaunti yangu ya YouTube.
  1. Sahihi Yako

Kuandika jina lako rasmi kamili au la mwakilishi wako aliyeidhinishwa (ikiwa yupo), kutachukuliwa kama sahihi dijitali. Jina rasmi kamili linapaswa kuwa jina la kwanza na la mwisho, si jina la kampuni au chaneli.

 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
1955790104490542641
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false