Michezo ya video na uchumaji wa mapato

Michezo ya video ni mada maarufu za video kwenye YouTube. Ukurasa huu huwasaidia watayarishi wa video za michezo kufahamu masharti mbalimbali yanayotumika kuhusiana na uchumaji mapato. Hizi si sera mpya, bali ni kanuni zilizopo ambazo zinatokana na Mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji wa YouTube. Ingawa ukurasa huu unaangazia mada za kawaida katika video za michezo, kumbuka kwamba mwongozo wote wa maudhui yanayofaa watangazaji unaendelea kutumika kwa video zako zote.

Kukiuka masharti yaliyo hapa chini kunaweza kusababisha watangazaji wachague kuonyesha matangazo machache au kutoyaonyesha kabisa kwenye video zako zinazochuma mapato. Tunapendekeza uthibitishe kuwa video zako hazikiuki Mwongozo wa Jumuiya kwenye YouTube, kwa sababu hili linaweza pia kuathiri hali ya uchumaji wa mapato.

Vidokezo kuhusu kuchuma mapato kupitia video za michezo

Ifuatayo ni mifano kutoka katika mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji inayohusiana na mada za michezo. Mabadiliko yote ya aikoni ya uchumaji wa mapato yaliyo hapa chini yanaweza kutekelezwa kwa video zinazoangazia maudhui halisi au yaliyotengenezwa na kompyuta iwapo kuna ukiukaji wa sera kwenye maudhui ya sauti au yanayoonekana (ikiwa ni pamoja na maandishi). Hii inajumuisha kwenye jina na kijipicha cha video.

Lugha isiyofaa

Kutumia lugha chafu au isiyofaa mwanzoni mwa video au katika sehemu kubwa ya video zako za michezo huenda kukasababisha mabadiliko ya hali ya uchumaji wa mapato. Matumizi madogo au yasiyo ya mara kwa mara ya lugha chafu (kama vile video za muziki, nyimbo zinazosindikiza, muziki wa utangulizi au utamatishaji au wimbo unaochezwa chinichini) katika maudhui yako hayatasababisha video yako isifae matangazo.

Hii hapa ni baadhi ya mifano (orodha haijataja vipengele vyote):

Mwongozo wa matangazo Maelezo na chaguo za dodoso

Maudhui haya yanaweza kutumika kuchuma mapato ya matangazo

Lugha chafu iliyofupishwa au iliyobanwa au maneno kama vile “bure” au “shenzi” kwenye jina, kijipicha au video. Lugha chafu kiasi kama vile “malaya”, “bwege”, “mpumbavu” na “shonde” inayotumiwa mara kwa mara kwenye video. Lugha chafu inayotumiwa ndani ya muziki au maudhui ya video ya ucheshi.

Ufafanuzi:

  • “Lugha chafu iliyobanwa” inarejelea mambo kama vile kuzima sauti au kuweka sauti nyingine ya mashine inayozuia neno na pia kufunika maneno yaliyoandikwa kwa kutumia pau nyeusi, ishara, au maandishi yanayowekwa baada ya kurekodi.
  • “Lugha chafu yenye maneno yaliyofupishwa” inarejelea ufupisho kama vile WTF (“matusi ya kingono”) ambapo neno halisi linafupishwa kwa kutumia baadhi ya herufi zake.

Maudhui haya yanaweza kuchuma mapato machache au yasichume kabisa mapato ya matangazo

Lugha chafu zaidi (kama vile matusi ya kingono) inayotumiwa katika sekunde 7 za kwanza au lugha chafu kiasi (kama vile "shonde") kwenye jina au kijipicha.

Baadhi ya mifano ya maudhui yanayopatikana pia katika aina hii:

  • Matumizi ya lugha chafu kwenye video yote (kama vile lugha chafu inayotumiwa katika sentensi nyingi).
  • Lugha chafu iliyotumiwa kwenye jina au kijipicha cha muziki au maudhui ya vichekesho vya jukwaani.

Maudhui haya hayatachuma mapato ya matangazo

Lugha chafu zaidi (kama vile matusi ya kingono ) inayotumiwa katika vijipicha au majina. Matumizi yoyote ya lugha chafu iliyokithiri, ambayo inajumuisha lugha ya chuki au maneno ya kukashifu kwenye video, kijipicha au jina kama vile  "mfi***wa" au "mku**u”.

Ili upate maelezo ya ziada kuhusu lugha ya chuki au kashfa, unaweza pia kurejelea mwongozo wetu kuhusu maudhui ya chuki na ya kudhalilisha ndani ya kituo chetu cha usaidizi.

Maudhui ya watu wazima

Mwongozo wa matangazo Maudhui yanayochochea ngono Uchi Maelezo na chaguo za dodoso

Maudhui haya yanaweza kutumika kuchuma mapato ya matangazo

Mada kuhusu sehemu za siri bila kudhihirisha ngono (kama vile simulizi kuhusu kumtembelea daktari wa uzazi).

Matukio ya kawaida ya kimahaba (kama vile busu lenye hisia kati ya wahusika).

Matumizi ya mizaha na madokezo ya kingono (kama vile kuiga vitendo vya ngono katika hali ya ucheshi kwa kutumia mikono) ambayo hayatumii maneno machafu.

Miili iliyo uchi ambapo sehemu za siri zimefunikwa kabisa.

Picha zisizosisimua hisia zinazoonyesha sehemu ya mwili katika mandhari yanayofaa kama vile bwawa la kuogelea (wahusika wa mchezo wakiwa wamevaa bikini kama sehemu ya matukio).

Maudhui yaliyochujwa kabisa ambapo sehemu za siri zimefunikwa ili kutoonyesha uchi (kama vile mtu aliye uchi kabisa ambaye sehemu zake za siri zimefunikwa).

Mahaba au kupiga busu; mazungumzo kuhusu uhusiano wa kimahaba au kimapenzi bila kurejelea tendo la ngono; uchi uliofichwa kabisa usioonekana na usiolenga kuchochea hadhira kingono; uchi unaohusisha tendo la kunyonyesha ambapo mtoto anaonekana; elimu kuhusu ngono bila kudhihirisha tendo lenyewe; kucheza dansi katika hali inayohusisha miondoko ya sehemu za mwili ambazo kwa kawaida huhusishwa na tendo la ngono katika juhudi za kutaka kutamaniwa au kuvutia, lakini hazionyeshwi dhahiri kingono; kucheza dansi ya kingono katika mazingira ya kitaaluma, kama vile katika dansi au video ya muziki iliyopangwa.

Maudhui haya yanaweza kuchuma mapato machache au yasichume kabisa mapato ya matangazo

Dansi za kimahaba (kama vile kutingisha makalio) zinazoangazia mavazi yasiyoficha uchi kabisa katika muktadha wa kitaalamu kama vile studio ya dansi au matukio ya moja kwa moja.

Hakuna.

Sanaa ya zamani inayoonyesha tendo la ngono linaloweza kutambuliwa (kama vile picha ya tendo la ngono) au kuangazia sehemu za siri kwenye vijipicha; elimu kuhusu ngono isiyo ya kusisimua yenye vitendo vya ngono vilivyohuishwa; mizaha inayohusisha mada za ngono; kucheza dansi kwa kuangazia mavazi yasiyoficha uchi kabisa; kugusa kimakusudi au kuangazia sana sehemu za siri kwenye dansi.

Maudhui haya hayatachuma mapato ya matangazo

Vitendo dhahiri vya ngono au ugiligili wa mwili unaohusiana na ngono.

Matukio ya mchezo yanayoangazia burudani inayohusisha ngono (kama vile vilabu ambako watumbuizaji wako uchi) kama sehemu ya matukio (hata ikiwa ni kwa ufupi).

Maonyesho au mijadala kuhusiana na mapendeleo ya ngono.

Majina yanayotumia lugha chafu kama vile “hot s3x” (ikiwa ni pamoja na kuandika maneno visivyo kwa makusudi) au mkusanyiko wa video za “KUPIGA PUNYETO.”

Metadata inayopotosha (kama vile jina linaloashiria kuwa video ina vitendo vya ngono) hata ikiwa video yenyewe haina maudhui ya watu wazima.

Majina au vijipicha vilivyo na vielelezo vingi vya kingono (kama vile “18+,” “wakubwa tu”).

Michezo ya video za ngono inayowalenga watu wazima au kuhusisha ngono katika utendaji wa wahusika wa mchezo wa video kwa nia ya kuchochea hisia ya ngono au kuridhisha hadhira.

Matumizi ya lugha ya matusi inayojumuisha maneno machafu (kama vile neno linalotaja viungo vya siri linalotamkwa au kuzungumzwa wakati wa mchezo).

Vifaa vya kingono au vitu vingine vinavyokusudia kuchochea shughuli ya ngono haviruhusiwi (kama vile vifaa vya michezo au maudhui yanayoonekana katika mandharinyuma).

Vitendo vinavyoashiria ngono (kama vile watu wanaosogeasogea ndani ya blanketi) au sauti za vitendo vya ngono (kama vile kuguna).

Mada za ufafanuzi wa ngono katika uchezaji (kama vile kupiga punyeto au kuelezea mada ya ngono kulingana na mhusika au tukio kwenye mchezo).

Kutoficha sehemu nyeti za mwili (kama vile kuonyesha wazi sehemu za siri).

Picha za uchi zilizobanwa au kupunguzwa ubora ambapo sehemu nyeti za mwili bado zinaweza kutambulika (kama vile matukio yanayoonyesha uchi uliotiwa nyota au ukungu, lakini bado unaweza kutambulika kwenye kivuli chake).

Maonyesho ya picha za sehemu za siri za mwili kama vile picha zinazorudiwa au zinazolenga sehemu za katikati ya matiti au maumbo yanayolenga kuchochea hisia za kingono kwa hadhira (kama vile matiti yanayoonekana dhahiri au picha za sehemu nyeti zinazoweza kutambuliwa za wahusika wa mchezo).

Sehemu za siri za mwili zilizofunikwa kidogo au uchi kabisa; uchi wakati wa kunyonyesha bila mtoto kuwepo katika tukio; vitendo vya kingono (hata kama vimetiwa ukungu au kukisiwa), majadiliano ya mada za ngono, kama vile mapendeleo ya ngono yasiyo ya kawaida, vidokezo, hali za kushiriki tendo hili; kijipicha cha video kilicho na maudhui ya ngono (ikiwa ni pamoja na maandishi au viungo); ishara na matukio yanayochochea ngono; kuonyesha vifaa vya ngono; maudhui yanayohusiana na tasnia na wafanyakazi wa ngono; ngono kati ya wanyama inayoangazia sehemu za siri au matukio ya kujamiiana; kuiga mienendo au vitendo vya ngono katika kucheza dansi; dansi za wazi zenye ashiki za ngono zinazolenga kuchochea hadhira kingono.

Vurugu

Mwongozo wa matangazo Vurugu kwenye michezo Maelezo na chaguo za dodoso

Maudhui haya yanaweza kutumika kuchuma mapato ya matangazo

Vurugu zinazoangazia michezo isiyo ya kuogofya: Michezo isiyo ya kuogofya ni pamoja na:

  • Matukio ya kuogofya (kama vile mashambulizi ya kikatili kwa mtu) baada ya sekunde 15 za mwanzo kwenye video.

Klipu zinazoficha vurugu za kuogofya (kama vile matukio ya mauaji au tukio la kukata kichwa lililotiwa ukungu).

Mchezo wa kawaida ambao hauhusishi vurugu za kuogofya (angalia sehemu ya “Maudhui haya yanaweza kuchuma mapato machache au yasipate kabisa mapato ya matangazo” hapa chini ili upate maelezo kuhusu vurugu za kuogofya).

Vurugu isiyo ya kweli, ya mzaha na kwa jumla inakubalika kwa umri wote (kama vile michezo ya video inayofaa familia inayoonyesha kukimbia ili kutoroka mazimwi).
Utekelezaji wa sheria, ikiwa ni pamoja na jukumu la kawaida likifanywa (kama vile kukamatwa kwa lazima, kudhibiti umati, kuzozana na afisa, kuingia kwa lazima); vurugu zinazotokea kama sehemu ya uchezaji wa video ambayo haijahaririwa; vurugu isiyokithiri yenye kiasi kidogo cha damu; maiti ambazo zimebanwa kabisa, kutiwa ukungu, kuandaliwa kwa kuzikwa au kuonyeshwa katika matukio ya historia kama vile vita, ikiwa kama sehemu ya video ya elimu.
Maudhui haya yanaweza kuchuma mapato machache au yasichume kabisa mapato ya matangazo

Vurugu ya mchezo inayoogofya kwenye kijipicha au katika sekunde 8 hadi 15 za mwanzo za video.

  • “Vurugu za mchezo unaoogofya” ni pamoja na mauaji ya kikatili au majeraha mabaya yanayoangazia ugiligili na sehemu za mwili kama vile kukatwa vichwa na kukatwa kwa viungo vya mwili.
Utekelezaji wa sheria kwa njia ya kuogofya kama vile majeraha yanayoonekana, maiti zilizo na majeraha au madhara dhahiri katika miktadha ya elimu au hali halisi (kama vile chaneli ya kujifunza historia); vurugu za mchezo za kuogofya katika kijipicha au kuonekana mapema katika maudhui; video ghafi ya mapambano kwa silaha bila majeraha; ufafanuzi wa maelezo ya kuogofya ya majanga; maudhui ya kuigiza yanayoonyesha majeraha mabaya na ya kushtua.
Maudhui haya hayatachuma mapato ya matangazo

Huangazia uchezaji uliobuniwa ili kutengeneza hali ya kushtua. Mifano ni kama:

  • Kujumuisha wahusika wasioweza kudhibitiwa na mchezaji katika mauaji ya halaiki.

Vurugu za kuogofya za michezo kwenye kijipicha au katika sekunde saba za mwanzo za video.

  • “Vurugu za kuogofya za michezo” ni pamoja na majeraha mabaya (kama vile kukatwa vichwa, kukatwa kwa viungo vya mwili) yanayoangazia ugiligili na/au sehemu za mwili zilizo na maumivu makali au ya muda mrefu.

Uchezaji wa video unaoonyesha vurugu za kingono (kama vile kumnyanyasa kingono mhusika ambapo kunaweza kuwepo kwa maumivu makali).

Uchezaji wa video unaoonyesha vurugu zinazochochewa na chuki au vurugu zinazolenga kikundi cha watu wanaolindwa (kama vile kufanya mauaji ya kikundi maalum cha dini kutokana na hisia za chuki).

Uchezaji wa video unaoonyesha mateso ya kuogofya.

Uchezaji wa video unaoonyesha vurugu za kuogofya zinazowalenga watoto (kama vile kuwapiga wahusika watoto).

Uchezaji wa video unaoonyesha vurugu za kutisha zinazowalenga watu halisi waliotajwa (kama vile kuua mhusika aliyepewa jina linalolingana na jina la mtu mashuhuri).

Maiti za kuogofya katika video isiyo ya elimu; uchezaji wa video unaoangazia mada zilizopigwa marufuku (kama vile unyanyasaji wa kingono).

Matendo ya vurugu yanayoogofya zaidi (ikiwa ni pamoja na yanayojumuisha utekelezaji wa sheria) na majeraha.

Uchochezi au kusifu vurugu.

Masuala yanayotatanisha

Mwongozo wa matangazo Masuala yanayotatanisha Maelezo na chaguo za dodoso

Maudhui haya yanaweza kutumika kuchuma mapato ya matangazo

Kurejelea mada au matukio yoyote yanayoonyeshwa kwa muda mfupi, ambayo hayajafafanuliwa na si ya kuogofya yaliyoorodheshwa katika sehemu ya Hakuna Matangazo.

  • Matumizi ya neno “kujiua” katika uchezaji wa video (kama vile kuua mhusika wa mchezo ili kuanza upya).
  • Wahusika au wachezaji wakisema “Nitajiua.”

Maudhui yanayohusiana na jinsi ya kuzuia masuala tata. Maudhui ambapo masuala tata yanatajwa kwa kifupi katika video na hayajafafanuliwa na si ya kuogofya. Maudhui ambayo hayajafafanuliwa na si ya kuogofya yanayohusiana na unyanyasaji nyumbani, kujijeruhi, unyanyasaji wa kingono kwa watu wazima, kutoa mimba na dhuluma za kingono.

Maudhui haya yanaweza kuchuma mapato machache au yasichume kabisa mapato ya matangazo

Maonyesho dhahiri au maelezo ya masuala tata katika maudhui au kijipicha isipokuwa unyanyasaji wa watoto.

  • Picha ya mtu akipigwa kwenye kijipicha.
Maudhui kuhusu masuala tata ambayo hayasababishi hofu yanapotazamwa, japo huenda yanatoa ufafanuzi. Masuala tata yaliyowakilishwa kwa njia ya maigizo, kisanaa, kielimu, hali halisi au kisayansi. Mada kuu ambayo haijafafanuliwa na si ya kuogofya inayohusiana na unyanyasaji wa watoto. Maudhui yasiyo ya kuogofya lakini yamefafanuliwa yanayohusiana na unyanyasaji wa kingono kwa watu wazima, dhuluma za kingono au unyanyasaji nyumbani.
Maudhui haya hayatachuma mapato ya matangazo

Maudhui ya kuogofya (kama vile jeraha la damu) au maelezo ya kina kuhusu masuala tata.

  • Unyanyasaji wa watoto
  • Pedofilia
  • Ndoa za watoto
  • Kujijeruhi
  • Kujiua
  • Unyanyasaji nyumbani
  • Eutanasia

Kuonyesha mhusika katika mchezo akijijeruhi kwa kujikata viganja vya mikono na kutokwa na damu hadi kufa.

Kutangaza au kuhimiza masuala tata katika maudhui, mada au kijipicha.

  • Mitajo kama vile “Nitampiga mke wangu, anastahili kupigwa.”

Maonyesho ya masuala tata yaliyohuishwa yanayowasilishwa ili kuibua mihemko.

  • Onyesho la wahusika wanaochokoza wahusika wengine.

Maudhui ya kuogofya au ufafanuzi wa kina kuhusu masuala tata kama mada kuu; marejeleo ya wazi ya matatizo ya ulaji yanayoambatana na marejeleo au muktadha wowote ufuatao:

  • BMI au uzito mdogo zaidi.
  • Kuonyesha mwili mwembamba au uliodhoofika sana.
  • Uchokozi unaohusiana na uzito au ukubwa wa mwili.
  • Marejeleo ya ulaji wa chakula kingi kwa haraka, kuficha au kuweka akiba ya chakula.
  • Kufanya mazoezi ili kufikia kiwango cha chini mno cha kalori.
  • Kutapika au kutumia vibaya dawa zinazosaidia kitendo cha kwenda choo.
  • Kuangalia hatua alizopiga mtu katika kupoteza uzito.
  • Urejeleaji wa jinsi ya kuficha tabia yoyote kati ya zilizotajwa hapo juu.

Ufafanuzi muhimu:

  • Lengo kuu au kuangazia inamaanisha kuwa sehemu fulani ya video au video nzima inahusu mada fulani, na mada hiyo inarejelewa na kujitokeza mara kadhaa. Kuangazia kwa kifupi mojawapo ya mada zilizoorodheshwa kuwa nyeti au za kutatanisha si sababu ya video kuainishwa kuwa Hakuna Matangazo. Kwa mfano, hatua ya kukubali kwa muda mfupi mada nyeti au ya kutatanisha (k.m. “Katika video ya wiki ijayo tutajadiliana kuhusu kupungua kwa visa vya watu kujiua.”) haitachukuliwa kuwa lengo kuu, lakini sehemu ya video inayozungumzia kuhusu mada kama hiyo itachukuliwa kuwa lengo kuu. Si lazima lengo liwe sauti. Iwapo kuna picha au maandishi yanayolenga suala nyeti, yatachukuliwa pia kuwa yanaangazia. Baadhi ya mifano ni pamoja na:

    • Video inayolenga jinsi ya kujijeruhi.
    • Maudhui yanayolenga tu kutumia lugha chafu zaidi bila muktadha au sababu nyinginezo.
  • Kurejelea kwa kifupi humaanisha matukio yasiyolengwa kwenye maudhui (hayaangaziwi) na yanajumuisha kudokeza kuhusu mada zinazochukuliwa kuwa nyeti au za kutatanisha. Kwa mfano, kutaja kwa kifupi mada nyeti au ya kutatanisha (k.m. “Katika video ya wiki ijayo tutajadiliana kuhusu kupungua kwa idadi ya watu wanaojiua.”) kutachukuliwa kuwa kurejelea kwa kifupi na wala si lengo kuu.

Ili upate maelezo zaidi kuhusu istilahi muhimu zinazotumika kwenye mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji, angalia jedwali la ufafanuzi.

Aina zinazotumika

Angalia maelezo kuhusu aina za video zinazotumika kwa mujibu wa sera zetu za uchumaji wa mapato yanayotokana na video za michezo.

Aina za video zinazotumika

Mtiririko au uonyeshaji wa picha kwenye mchezo

Uhuishaji ulioongezwa katika uchezaji pia umejumuishwa kwenye mwongozo wa sera zetu. Kuzihariri na kuziondoa ili kushiriki maudhui ya kuogofya au kuunda klipu kutokana na matukio ya kutisha kutasababisha video yako kutiwa aikoni ya manjano.

Video za maoni

Iwapo klipu halisi iliyopachikwa kwenye video yako ya maoni ina matukio yanayokiuka sera zetu, mwongozo na masharti yetu yatatumika; kwa hivyo itapata aikoni ya manjano licha kuwa huenda si wewe uliyetengeneza klipu hiyo inayokiuka sera.

Mazungumzo au masimulizi kwenye mchezo

Klipu za sauti ambazo hazipo kwenye mchezo bali umezitengeneza mwenyewe ili zitumike wakati wa kucheza (rekodi ya sauti) zinapaswa pia kuzingatia mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji.

Maandishi au michoro inayowekwa kwenye video

Kuwepo kwa maudhui yasiyoruhusiwa katika maandishi (kama vile manukuu yenye maelezo yaliyowekwa na mtayarishi au manukuu yaliyopachikwa kwenye video), sauti (wimbo unaotanguliza video, n.k.), au picha za kuogofya (kama vile aikoni ya chapa yako, kauli mbiu, n.k.) zinazowekwa kwenye video yako kutasababisha itiwe aikoni ya manjano.

Maoni yanayoonekana na kusomeka kwenye video yako

Hatutakagua maoni ya watazamaji (kama vile mfululizo wa maoni, madirisha ibukizi ya michango ya watumiaji, n.k.) yanayoonyeshwa kwenye video yako isipokuwa ibainishwe dhahiri kwa njia fulani (kama vile kusomwa kwa sauti katika video au kuangaziwa kwa kuvutwa karibu). Pia, hatudhibiti maudhui katika sehemu za maoni yanayohusiana na video kwa mujibu wa mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji na ni wajibu wako kuyachuja ukiona maoni yasiyofaa (angalia hapa ili upate maelezo zaidi).

Maudhui ya kamari yanayohusiana na mchezo

Video za jinsi ya kufanya kitu, mafunzo na viungo vinavyoelekeza katika tovuti za kucheza kamari (kama vile kuweka dau ya mechi kwa kutumia bidhaa pepe kama sarafu) au kuweka dau ukitumia sarafu za ndani ya mchezo kunachukuliwa kuwa ukiukaji wa sera dhidi ya “maudhui yanayokiuka sheria”. Kupata bidhaa pepe nje ya utaratibu wa kawaida wa uchezaji pia ni ukiukaji wa sera (hii haijumuishi msimbo wa mtayarishi kama vile programu za washirika). Watumiaji wa YouTube wanatakiwa wazingatie sheria za sera zetu na kukosa kufanya hivyo kutasababisha vikwazo vya matumizi. Pata maelezo zaidi kwenye ukurasa huu.

Video ndefu

Urefu wa video ni muhimu, lakini cha muhimu zaidi ni lengo na muktadha wa video. Iwapo video ina maudhui ya kukera, itachukuliwa kuwa isiyowafaa watangazaji. Kwa mfano, hata video za michezo zinazochukua takribani saa moja, ikiwa zinatumia lugha inayodhihirisha ubaguzi wa rangi zitatiwa aikoni ya manjano.

Ukiukaji unaowasilishwa kama mada kuu

Tunachukulia kuwa maudhui yanayokiuka sera ndiyo lengo kuu ikiwa yako katika mojawapo ya aina zifuatazo:

  • Kutaja au kuonyesha jambo la kuwashtua watazamaji (kama vile kuonyesha kwa ukaribu shambulizi kali lenye majeraha mabaya na umwagikaji wa damu kwenye mchezo).
  • Maudhui yanayokiuka sera ndiyo mada kuu ya video (kama vile video za watu kukatwa vichwa kwenye mchezo).

Iwapo huwezi kuacha kujumuisha matukio haya kwenye video yako, unapaswa kutia mwenyewe aikoni ya manjano kwenye video yako.

Vijipicha na majina ya video

Mara nyingi, vifungu vya maneno ya kutisha na kusisimua hutumika kwenye vijipicha au majina ya video ili kuwavutia watazamaji. Hata hivyo, kama ilivyo kwa maudhui ya video, ukiukaji ukigunduliwa kwenye vijipicha au majina ya video, maudhui yatapata mapato machache au yakose kabisa mapato ya matangazo.

Baadhi ya mifano ya Vijipicha ni pamoja na (orodha hii haijataja vipengele vyote):

  • Kuashiria au kuwavutia watazamaji (kama vile kuonyesha sehemu nyeti zilizotiwa ukungu)
  • Maandishi machafu yanayohusiana na vitendo vya kingono (kama vile “tazama mhusika huyu akitokwa shahawa”)
  • Picha za kushtua, kama vile vitendo vya ngono au vurugu ya kuogofya

Kwa mfano Majina ya videoni pamoja na (orodha hii haijataja vipengele vyote):

  • Kutumia lugha chafu kwa kuandika maneno kamili, kuchuja maneno au kuendeleza maneno vibaya kimakusudi (kama vile "kmmk#*")
  • Majina yanayopotosha kwa kudai maudhui ni ya ngono
  • Majina yanayoonyesha kuwa maudhui ni ya watu wazima pekee (kama vile kwa waliofikisha umri wa miaka 19 na zaidi au WATU WAZIMA PEKEE)
  • Kutumia herufi kubwa ili kuwavutia watazamaji (kama vile “USHINDI MKUU WA KIPEKEE”)

Pata maelezo zaidi

Je, ungependa kujisajili ili upokee taarifa kuhusu sera zetu? Jisajili kwenye Jukwaa letu la Jumuiya ya YouTube hapa ili upokee arifa ya barua pepe kila tunaposasisha sera. Unaweza pia kutufuatilia kwenye X kupitia @teamyoutube au @youtubecreators.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
4528509356071905574
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false