Kutatua matatizo ya utiririshaji na video

Ikiwa filamu, kipindi au maudhui yako ya kutazama unapohitaji yanaendelea kuakibisha, kusitasita au hayachezi ipasavyo, jaribu mojawapo ya njia hizi za kutatua matatizo kwenye kompyuta au kifaa chako cha mkononi. Ikiwa unapata matatizo kwenye televisheni yako, jaribu hatua hizi. Hatua hizi za utatuzi zinaweza kusaidia kutatua hitilafu na matatizo mengi ya kucheza.

Ikiwa umejaribu hatua hizi na bado video yako haichezi ipasavyo, unaweza kujaribu kutazama kwenye kifaa tofauti kinachotumika.

Kurekebisha matatizo ya video kwenye kompyuta yako

Mifano ya ujumbe wa kawaida kuhusu hitilafu:
  • Samahani, hitilafu imetokea wakati wa kupatia video hii leseni.
  • Video hii inahitaji malipo.
  • Hitilafu fulani imetokea. Tafadhali jaribu tena baadaye.
  • Tuna matatizo katika seva zetu. Tafadhali jaribu tena baadaye.
  • Hitilafu fulani imetokea.

Ukipata hitilafu inayofanana na zilizo hapo juu, jaribu hatua hizi:

  1. Hakikisha kuwa kompyuta yako imesasishwa.
  2. Funga kisha ufungue tena kivinjari chako.
  3. Ikiwa umefungua vichupo vingi vya kivinjari, jaribu kufunga vichupo vingine isipokuwa kichupo unachotumia kwa ajili ya YouTube.
  4. Sasisha kivinjari chako kiwe toleo jipya zaidi.
  5. Tumia Google Chrome kama kivinjaro chako.
  6. Washa upya kifaa chako.

Kurekebisha hitilafu za kuakibisha au kupakia video

Jaribu kutazama video yako ukitumia Google Chrome kama kivinjari chako. Ikiwa umeshindwa kutumia Chrome au bado unatatizika, jaribu hatua zilizo hapa chini.

  1. Kwenye kompyuta yako, onyesha upya au ufunge kisha ufungue kivinjari chako cha intaneti.
  2. Angalia kasi ya intaneti yako. Ikiwa unatumia muunganisho wa intaneti wenye kasi ndogo, jaribu kufunga programu, vichupo na vivinjari vingine. Unaweza pia kujaribu kuzima kisha uwashe modemu au kisambaza data chako.
  3. Sasisha kivinjari chako kiwe toleo jipya zaidi.
  4. Jaribu kufuta akiba na vidakuzi vyako.
  5. Jaribu kupunguza ubora wa video yako.
  6. Washa upya kifaa chako.

Kurekebisha hitilafu za filamu yako kukwama

Kwenye kipindi cha muda cha filamu yako, bofya peleka mbele kwa kasi uende kwenye matukio kadhaa yanayofuata ili uone iwapo filamu itaanza kucheza kawaida tena.

Kitendo hiki kisiposaidia, jaribu kufunga kisha ufungue kivinjari chako. Ikiwa bado unatatizika, angalia iwapo kuna masasisho ya kivinjari au ujaribu kutumia kivinjari tofauti kinachotumika, kama vile Chrome. Vitendo hivi vyote visipokusaidia, jaribu kufuta akiba na vidakuzi vyako.

Kurekebisha hitilafu za ununuzi usioonekana katika maktaba

Ili uone maudhui uliyonunua, hakikisha umeingia katika akaunti binafsi iliyotumika kufanya ununuzi. Akaunti za Biashara haziruhusu kutazama filamu au vipindi, kwa hivyo utahitaji kubadilisha ili utumie akaunti yako binafsi.

Ili ubadilishe utumie akaunti yako binafsi:

  1. Katika kona ya juu kulia ya YouTube, bofya aikoni ya kituo chako.
  2. Kando ya picha yako ya wasifu, gusa Badili akaunti kisha. Utaona orodha ya Akaunti unazodhibiti na utambulisho wa Akaunti yako ya Google.
  3. Bofya akaunti unayotaka kutumia. Ukichagua Akaunti ya Biashara ambayo haina kituo, unaweza kufungua kituo kwa ajili ya ukurasa huo.

Kurekebisha matatizo ya video kwenye televisheni yako

Angalia muunganisho wako wa intaneti

Tunapendekeza muunganisho wenye kasi isiyopungua Mbps 7 kwa utiririshaji wa HD. Unaweza kufanya jaribio la kasi ya muunganisho wako hapa.
Tunapendekeza ufanye jaribio hili ukiwa karibu na televisheni yako. Ikiwa kasi ya intaneti yako iko chini, tunapendekeza uhakikishe kuwa kifaa au televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti ipo karibu na kisambaza data chako na hakuna vitu vinavyokikatiza (k.m., hujaweka ndani sana ya ukuta, hakijazuiwa na chuma, n.k.). Jaribu kusogeza kifaa chako ili uone ikiwa hatua hii itaboresha muunganisho. Unaweza pia kujaribu kupunguza idadi ya vifaa vingine vilivyounganishwa kwenye mtandao wako.

Kuangalia ubora wa utiririshaji wako

Jaribu kurekebisha ubora mwenyewe.
  1. Chagua Mipangilio  kwenye kicheza video.
  2. Chagua Ubora na uone ikiwa una chaguo la kurekebisha ubora mwenyewe.

Funga kisha ufungue upya programu ya YouTube

  1. Bonyeza kitufe cha ukurasa wa mwanzo kwenye kidhibiti chako cha mbali.
  2. Fungua upya programu ya YouTube.
  3. Jaribu kucheza tena video.

Ondoka katika akaunti ya programu ya YouTube, kisha uingie katika akaunti tena

  1.  Fungua programu ya YouTube.
  2. Chagua picha yako ya wasifu  kisha aikoni iliyo chini ili udhibiti wasifu wako.
  3. Chagua Endelea ili uendelee na uondoke kwenye akaunti.
  4. Rudi kwenye Mipangilio kisha uchague Ingia katika akaunti. Unaweza pia kuweka msimbo.
  5. Jaribu kucheza tena video.

Washa upya kifaa chako

  1. Chomoa kifaa chako kwenye umeme.
  2. Subiri sekunde kadhaa.
  3. Unganisha tena kifaa chako.
  4. Rudi kwenye programu ya YouTube kisha ujaribu kucheza tena video yako.

Kusasisha programu ya mfumo ya kifaa chako

Angalia iwapo kuna masasisho yoyote ya mfumo wa kifaa chako. Unaweza kuangalia masasisho kwa kwenda kwenye sehemu ya sasisho la mfumo kwenye mipangilio ya kifaa chako. Ikiwa kuna sasisho, fuata maagizo yaliyo kwenye skrini ili usasishe mfumo, kisha ujaribu kucheza video yako tena.

Ikiwa unatatizika kusasisha au unaona hitilafu za utiririshaji katika huduma kadhaa tofauti, angalia tovuti ya usaidizi ya mtengenezaji wa kifaa chako ili upate usaidizi wa utatuzi.

Unaweza pia kujaribu kutumia njia nyingine kucheza video kwenye televisheni yako:

  • Ikiwa una Chromecast, icheze kwenye kifaa kingine kisha utume kwenye televisheni yako.
  • Ikiwa una kebo ya HDMI, cheza kutoka kwenye kompyuta ya kupakata kisha uunganishe kwenye televisheni yako.

Vilevile, jaribu kutazama kwenye kifaa kingine ili uone ikiwa tatizo hilo litaendelea.

Kupunguza hali ya kuchelewesha kupeperusha kwenye televisheni yako katika Chaneli za Primetime

Kuchelewesha kupeperusha ni hali ya kuchelewa kati ya kamera kunasa tukio na tukio kuonyeshwa kwenye skrini unapotazama kwenye televisheni yako. 

Hali ya kuchelewesha kupeperusha ikipungua zaidi, matukio ya kicheza video kuakibisha yatapungua. Hali ya kuchelewesha kupeperusha ikipungua, kuna uwezekano mkubwa zaidi kuwa uchezaji wa video utakatizwa.

Msongamano kwenye mtandao na vigezo vingine pia vinaweza kusababisha matatizo ya kupeperusha vipindi mubashara, hali inayoweza kusababisha kuchelewa kwa mtiririko. Ucheleweshaji unaweza kutokea hata wakati mtandao wako ni shwari.

Kusasisha hali ya kuchelewesha kupeperusha kwenye programu ya YouTube kwenye televisheni yako

  1. Kwenye sehemu ya chini kulia, chagua Mipangilio.
  2. Chagua Kuchelewesha Kupeperusha.
  3. Chagua Punguza au Chaguomsingi.

Chaguo la “Chaguomsingi” ni bora zaidi ili kupunguza kukatizwa kwa video inapocheza. Chaguo la "Punguza" ni bora zaidi ili kupunguza vitu vinavyoharibu mtiririko mubashara. Teua chaguo la “Punguza” ikiwa ungependa hali ya kuchelewesha kupeperusha isiyokatiza sana video inapocheza.

Tuma maoni

Unaweza kutuma maoni kuhusu hitilafu za kutazama video kwenye programu ya YouTube kwa kwenda kwenye aikoni ya wasifu wako kisha Usaidizi na Maoni kisha Tuma Maoni moja kwa moja baada ya tatizo lako la uchezaji.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
13714444764645461985
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false