Kuweka lebo kwenye bidhaa zilizo katika maudhui yako

Ikiwa umetimiza masharti, unaweza kuweka lebo kwenye bidhaa zilizoangaziwa katika maudhui yako. Unapoweka lebo kwenye bidhaa zilizo katika maudhui yako, lebo ya "Angalia Bidhaa itaonekana katika kona ya kulia ya maudhui yako. Watazamaji wanaweza kuchagua lebo ili wakague orodha ya bidhaa ulizowekea lebo.

Kipengele hiki kinaonekana tu kwa watazamaji wanaoishi katika nchi au maeneo mahususi. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi watazamaji wanavyovinjari na kununua bidhaa kwenye YouTube.

Mwongozo wa Kuweka Lebo

Ikiwa umetimiza masharti ya kipengele hiki, weka lebo tu kwenye bidhaa katika maudhui yako ikiwa:

  • Bidhaa zinaweza kutambuliwa kwa urahisi na kuangaziwa mara kwa mara kwenye maudhui yako.
  • Bidhaa zinahusiana kikamilifu na maudhui yako.
  • Mtazamaji anaweza kuhitaji kupata maelezo zaidi au kununua bidhaa kulingana na mwonekano wake kwenye maudhui yako.
  • Bidhaa zinatumika ipasavyo. Hii inamaanisha kwamba matumizi yako ya bidhaa yanawiana na lengo la mtengenezaji na yanakuza matumizi salama.

Kutimiza Masharti ya Mwongozo

Tunakagua lebo za bidhaa na tunaweza kuondoa zile ambazo hazifuati mwongozo huu. Tunataka kuhakikisha kuwa watazamaji wako wanagundua bidhaa ambazo zimeangaziwa kwenye maudhui yako ili kuwapa hali ya utumiaji inayofaa zaidi. Tukibaini lebo za bidhaa zinazokiuka mwongozo mara kwa mara, tunaweza kuziondoa kwenye maudhui yako na chaneli yako inaweza kupoteza idhini ya kufikia mpango wa washirika.

Kutatua matatizo ya lebo za bidhaa

Kumbuka kuwa lebo za bidhaa hazitaonyeshwa kwenye maudhui yako ikiwa:

  • Mipangilio ya hadhira ya maudhui yako imewekwa kuwa inalenga watoto.
  • Maudhui yako tayari yanaonyesha Vipengele vya Tiketi au Ufadhili.
  • Kuna dai la hakimiliki dhidi ya maudhui yako.
  • Maudhui yako yanachukuliwa kuwa yamedhibitiwa au hayastahiki uchumaji wa mapato.
  • Maudhui yako yanajumuisha wimbo unaoweza kutumika katika ugavi wa mapato kwenye kipengele cha Muziki wa Watayarishi.
  • Mtazamaji wako hayupo katika nchi au eneo linalostahiki.
  • Mtazamaji wako anatazama maudhui yako kwenye kivinjari cha kifaa cha mkononi, televisheni inayoweza kuunganisha kwenye intaneti au kifaa cha michezo ya video.
  • Huna bidhaa zilizoidhinishwa ambazo ziko dukani.
Kumbuka: Kabla ya kujumuisha bidhaa zilizolipiwa ili zitangazwe kwenye maudhui, hakikisha kuwa unakagua wajibu wowote wa kimkataba ambao unaweza kuwa nao. Weka ufumbuzi unaofaa kwenye maudhui yako, ikiwa ni pamoja na ufumbuzi wa YouTube wa kulipia bidhaa zitangazwe katika maudhui na ufumbuzi wa maudhui yaliyoidhinishwa.
Kumbuka: Masasisho haya yanapatikana kwa watayarishi walio nchini Marekani na tutapanua upatikanaji wake duniani kote katika wiki chache zijazo.

Kufikia maktaba ya Sauti za ununuzi za kutumia kwenye Video Fupi

Chaneli Rasmi za Wasanii na watayarishi wanaoruhusiwa kufanya Ununuzi kwenye YouTube wanaweza kufikia maktaba ya Sauti za ununuzi. Unaweza kupata sauti unazoweza kutumia katika Video Fupi ukitumia vipengele vya Ununuzi katika maktaba ya Sauti za ununuzi.

Ili ufikie maktaba ya Sauti za ununuzi za kutumia kwenye Video Fupi:

  1. Ingia katika programu yako ya YouTube ya vifaa vya mkononi.
  2. Gusa Tayarisha  kisha  Tayarisha Video fupi.
  3. Gusa Weka sauti katika upande wa juu wa ukurasa wa Kamera au Sauti katika sehemu ya chini ya ukurasa wa Mhariri ili ufikie Maktaba ya Sauti.
  4. Bofya bango la Sauti Zote katika sehemu ya juu ya Maktaba ya Sauti ili ufikie maktaba ya Sauti za ununuzi.
  5. Vinjari sauti zilizopo kisha uchague.
  6. Chagua “wekea bidhaa lebo" ili ufanye Video yako fupi iweze kununulika.
  7. Chapisha Video yako Fupi.

Maktaba ya Sauti za ununuzi haiwezi kutumika katika video ndefu na mitiririko mubashara inayoonyesha vipengele vya Ununuzi. Unaweza kutumia madoido ya sauti na muziki usiokuwa na mirahaba kutoka kwenye Maktaba ya Sauti ili uonyeshe vipengele vya Ununuzi katika video ndefu na mitiririko mubashara.

Kumbuka: Tumia toleo jipya zaidi la programu ya YouTube ya vifaa vya mkononi ili ufikie maktaba ya Sauti za ununuzi na uhakikishe kuwa unaweka sauti hizi kupitia zana za utayarishaji wa Video Fupi za YouTube. Ikiwa hutumii zana za utayarishaji wa Video Fupi za YouTube, unaweza kupokea madai ya hakimiliki. Vipengele vya ununuzi havitaonekana kwenye maudhui yaliyo na madai ya hakimiliki. Baadhi ya miziki katika maktaba ya Sauti za ununuzi haitimizi masharti yanayotatikana kwa bidhaa zilizowekewa lebo katika nchi zote. Watazamaji wa Video Fupi wanaotumia aina hii ya miziki hawataweza kuona vipengele vya Ununuzi.

Kuwekea lebo, kuondoa na kupanga upya bidhaa wakati unapakia maudhui mapya

Kuweka lebo kwenye bidhaa unapopakia maudhui mapya:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Pakia video au Video fupi.
  3. Ukifika kwenye ukurasa wa "Vipengele vya video", nenda kwenye Weka lebo kwenye Bidhaa na ubofye Weka.
  4. Weka jina la bidhaa unayotaka kuiwekea lebo kwenye kisanduku cha kutafutia.
  5. Chagua bidhaa kisha iburute uipeleke kwenye eneo ambalo limeonyeshwa kwenye zana. Unaweza kuwekea lebo hadi bidhaa 30.

Kuweka mihuri ya wakati kwenye bidhaa ulizowekea lebo

Ili uwasaidie watazamaji wako kununua bidhaa ulizowekea lebo kwenye video zako kwa wakati unaofaa, weka mihuri ya wakati kwenye bidhaa ulizowekea lebo:

  1. Kwenye sehemu ya ‘Wekea Bidhaa Lebo’, bofya WEKA MIHURI YA WAKATI karibu na bidhaa ulizowekea lebo.
  2. Bofya Weka muhuri wa wakati karibu na bidhaa mahususi unayotaka kuwekea muhuri wa wakati.
  3. Weka wakati ambapo bidhaa inaonyeshwa kwenye video yako. 
    1. Huwezi kuweka muhuri wa wakati kwenye sekunde 30 za kwanza za video yako na lazima kuwe na muda wa angalau sekunde 30 kati ya mihuri ya wakati.
  4. Bofya Nimemaliza and then Hifadhi.

Madokezo:

  • Unaweza tu kutumia kompyuta kuweka mihuri ya wakati kwenye bidhaa ulizowekea lebo.
  • Mihuri ya wakati inapatikana tu kwenye video ndefu ambazo zina urefu wa angalau dakika 1.

Kuondoa bidhaa:

  1. Tafuta bidhaa ambayo umeshaiwekea lebo.
  2. Ili uiondoe kwenye orodha, bofya kitufe cha Futa kilicho karibu na bidhaa.

Kupanga upya bidhaa mbili au zaidi:

  1. Tafuta bidhaa ambayo umeshaiwekea lebo.
  2. Iburute uipeleke kwenye sehemu unayopendelea.
  3. Chagua Endelea ili uhifadhi badiliko.

Kuweka lebo, kuondoa na kupanga upya bidhaa kwenye maudhui yaliyopo

Ili uwekee lebo bidhaa kwenye maudhui yaliyopo:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
  3. Bofya jina au kijipicha cha video.
  4. Bofya Bidhaa ili ufungue sehemu ya 'Wekea bidhaa lebo'.
  5. Weka jina la bidhaa unayotaka kuiwekea lebo kwenye kisanduku cha kutafutia.
  6. Chagua bidhaa kisha iburute uipeleke kwenye eneo ambalo limeonyeshwa kwenye zana. Unaweza kuwekea lebo hadi bidhaa 30.

 Kuweka mihuri ya wakati kwenye bidhaa ulizowekea lebo

Ili uwasaidie watazamaji wako kununua bidhaa ulizowekea lebo kwenye video zako kwa wakati unaofaa, weka mihuri ya wakati kwenye bidhaa ulizowekea lebo:

  1. Kwenye sehemu ya ‘Wekea Bidhaa Lebo’, bofya WEKA MIHURI YA WAKATI karibu na bidhaa ulizowekea lebo.
  2. Bofya Weka muhuri wa wakati karibu na bidhaa mahususi unayotaka kuwekea muhuri wa wakati.
  3. Weka wakati ambapo bidhaa inaonyeshwa kwenye video yako. 
    1. Huwezi kuweka muhuri wa wakati kwenye sekunde 30 za kwanza za video yako na lazima kuwe na muda wa angalau sekunde 30 kati ya mihuri ya wakati.
  4. Bofya Nimemaliza and then Hifadhi.

Madokezo:

  • Unaweza tu kutumia kompyuta kuweka mihuri ya wakati kwenye bidhaa ulizowekea lebo.
  • Mihuri ya wakati inapatikana tu kwenye video ndefu ambazo zina urefu wa angalau dakika 1.

Kuondoa bidhaa:

  1. Tafuta bidhaa ambayo umeshaiwekea lebo.
  2. Ili uiondoe kwenye orodha, bofya kitufe cha Futa kilicho karibu na bidhaa.

Kupanga upya bidhaa mbili au zaidi:

  1. Tafuta bidhaa ambayo umeshaiwekea lebo.
  2. Iburute uipeleke kwenye sehemu unayopendelea.
  3. Chagua Endelea ili uhifadhi badiliko.

Kuwekea bidhaa zako lebo kwa wingi

Okoa muda kwa kuwekea lebo bidhaa zilizopendekezwa ukitumia kipengele cha kuwekea lebo bidhaa nyingi. Ili utumie kipengele cha kuwekea lebo bidhaa nyingi:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Bofya kichupo cha Ununuzi.
  3. Bofya Wekea bidhaa lebo .
  4. Kagua video zilizo na mapendekezo ya bidhaa za kuwekea lebo, zinazopatikana kwenye maelezo ya video.
  5. Ili uweke lebo kwenye bidhaa fulani:
    1. Bofya picha ya bidhaa.
    2. Bofya WEKEA LEBO karibu na bidhaa husika au WEKEA LEBO ZOTE kwa bidhaa zote.
  6. Ili uwekee bidhaa lebo bidhaa kwenye video moja au zaidi: 
    1. Chagua video husika au uchague video zote.
    2. Bofya WEKEA LEBO.

Kuweka lebo kwenye bidhaa katika mitiririko mubashara

Ukishakuwa sehemu ya mpango, unaweza kuanza kuwekea lebo bidhaa katika mitiririko mubashara. Watazamaji wanaweza kukagua orodha ya bidhaa ambazo umeziwekea lebo kwa kuchagua Ununuzi Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuwekea lebo bidhaa katika mitiririko mubashara

Utendaji na mapato kutokana na ununuzi

Unaweza kutumia ripoti zilizopanuliwa kwenye Takwimu za YouTube ili kupima hali ya kushirikisha bidhaa zako zilizowekewa lebo na ufahamu idadi ya watazamaji wako inayotokana na kurasa za bidhaa.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
31785912354151255
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false