Sheria na Masharti ya Ziada ya Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida

Mara ya Mwisho Kubadilishwa: 7 Februari 2021

ili kutuma ombi la akaunti ya Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida au kutumia vipengele vya mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida, ni sharti ukubali (1) Sheria na Masharti ya Google na (2) Sheria na Masharti haya ya Ziada ya Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida (“Sheria na Masharti ya Ziada ya Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida”). 

Tafadhali soma kila moja ya hati hizi kwa umakini. Kwa pamoja, hati hizi zinajulikana kama “Sheria na Masharti”. Zinabainisha utakachotarajia kutoka kwetu unapotumia  akaunti na vipengele vyako vya Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida na tunachotarajia kutoka kwako.
Iwapo Sheria na Masharti haya ya Ziada ya Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida yanakinzana na Sheria na Masharti ya Google, Sheria na Masharti haya ya Ziada ya Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida yataongoza mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida. 

Ingawa si sehemu ya Sheria na Masharti haya, tunapendekeza usome Sera yetu ya Faragha ili uelewe zaidi jinsi unavyoweza kusasisha, kudhibiti, kuhamisha na kufuta maelezo yako.

Umri na uhusiano

Sharti uwe umetimiza umri wa kisheria wa mtu mzima katika nchi yako (au uwe na umri wa zaidi ya miaka 18, yoyote iliyo juu) ili uwe na akaunti ya Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida.

Zaidi ya hayo, sharti uwe mwakilishi aliyeidhinishwa ambaye anaweza kuwashurutisha wengine kwa niaba ya huluki iliyoorodheshwa katika akaunti yako ya Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida na wasifu wa shirika lisilo la faida.

Kuwashurutisha wengine na Faragha ya Msimamizi

Iwapo ombi la shirika lako la kupata akaunti ya Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida litaidhinishwa, utakuwa msimamizi wa akaunti ya shirika lako ya Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida. Kama utaongeza au kuidhinisha watumiaji wengine baadaye kuwa wasimamizi wenza wa akaunti ya shirika lako, sharti uwashurutishe watumiaji hao kwenye Sheria na Masharti haya kabla ya kuwaongeza au kuwaidhinisha kuwa wasimamizi wenza. Wasimamizi wenza watakuwa na haki sawa kama wewe za kudhibiti akaunti ya shirika lako, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kukuondoa usiwe msimamizi. Kwa kukubali kuweka wasimamizi wenza kwenye akaunti ya shirika lako ya Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida unakubali wasimamizi wenza waone jina lako na maelezo yako ya shughuli za usimamizi ikiwa ni pamoja na kuondoa wasimamizi wenza, kukataa maombi ya watumiaji ya kutaka wawe wasimamizi wenza na maombi ya shirika lako ya bidhaa za Google zinazotolewa kupitia Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida.

Mambo tunayotarajia kutoka kwako

Pamoja na kufuata sheria za msingi za kanuni katika Sheria na Masharti ya Google, lazima, unapotumia akaunti ya shirika lako ya Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida na wasifu wa shirika lisilo la faida, uhakikishe kuwa:

  • Maelezo unayowasilisha kwenye ombi la shirika lako la Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida ni ya kweli na sahihi na maudhui yaliyo katika wasifu wa shirika lako lisilo la faida ni sahihi, yamesasishwa na yamekamilika
  • Shirika lako halibagui mtu au kundi lolote la watu kupitia utaratibu wa kuajiri wafanyakazi au katika utekelezaji wa mipango na huduma, ikiwa ni pamoja na kutobagua kwa misingi ya mwelekeo wa ngono na utambulisho wa jinsia
  • Matumizi ya shirika lako ya Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida yanatii sera zake na hayataathiri vibaya uwezo wa Google wa sasa au wa baadaye wa kufanya biashara na shirika lako
  • Hutatumia mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida (i) kushawishi mfanyakazi yeyote wa serikali kwa njia yoyote ya ufisadi ili upate manufaa ya biashara au udumishe biashara au upate manufaa yoyote kwa njia isiyo halali (ii) kupata au kudumisha biashara (iii) kusababisha mfanyakazi wa serikali afanye au akose kufanya jambo kwa kutumia mamlaka yake rasmi au (iv) kupata mapendeleo mengine yoyote. 

Matumizi ya umma ya wasifu wako wa shirika lisilo la faida

Unakubali kuwa ukijumuisha maudhui kwenye wasifu wa shirika lako lisilo la faida, huenda maudhui unayotoa yakatumiwa katika bidhaa zingine za Google na yanaweza kuonyeshwa hadharani (kama vile vipengele vya mchango katika YouTube). 

Ingawa Google haiwajibikii wasifu wako wa shirika lisilo la faida iwapo umetoa maelezo kuhusu shirika lako katika wasifu wa shirika lako lisilo la faida, unaelewa kuwa tunayo haki, lakini siyo wajibu wa kudhibiti maudhui hayo. 

Bidhaa au huduma zingine

Sheria na Masharti yanaongoza matumizi yako ya akaunti na vipengele vya shirika lako vya Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida (kama vile wasifu wa shirika lisilo la faida). Huenda bidhaa za Google zinazotolewa kupitia mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida zikahitaji hatua za ziada ili kuanza kutumia, ikiwa ni pamoja na kukubali sheria na masharti ya kila bidhaa mahususi. 

Ufikiaji wa Google

Kwa kushiriki katika mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida au kwa kutumia vipengele vyake, unaruhusu Google kufikia akaunti ya shirika lako, ikiwa ni pamoja na wasifu wa shirika lako lisilo la faida, ili kukusaidia kudhibiti akaunti na maelezo ya shirika lako uliyotoa kuhusu shirika lako.

Maswali au malalamiko

Iwapo una maswali au malalamiko yoyote kuhusu Mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida, akaunti ya shirika lako au Wasifu wa Shirika Lisilo la Faida tafadhali tembelea Kituo chetu cha Usaidizi na iwapo maswali yako hayajajibiwa hapo, unaweza kuwasiliana nasi kwa kutumia fomu ya  “kuwasiliana nasi” inayoweza kufikiwa katika Kituo cha Usaidizi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu
1268917784784843633
true