Arifa

Mshirika wetu wa uthibitishaji wa mashirika yasiyo ya faida, Percent, amebadilisha jina la chapa kuwa Goodstack. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ambavyo Google kwa mashirika yasiyo ya faida inashirikiana na Goodstack

Matumizi ya AI kwa kuwajibika kwa mashirika yasiyo ya faida

Utangulizi

Mara kwa mara, mashirika yasiyo ya faida yanatafuta njia za kuboresha shughuli na kuongeza tija kwenye kazi yanazoshughulikia. Akiliunde (AI), hasa AI zalishi, inaweza kuwa zana inayofaa na yenye gharama ndogo au isiyo na gharama kabisa ya kusaidia kufikia malengo haya. Hata hivyo, unapotumia AI ni muhimu kuzingatia jinsi ya kuitumia AI kwa kuwajibika. Maelezo yaliyo kwenye makala haya ya kituo cha usaidizi yataongoza shirika lako lisilo la faida kujumuisha AI kwenye mifumo yake ya kazi kwa kuwajibika.

AI zalishi ni nini?

Zana nyingi za AI zinazokusudiwa kwa matumizi ya kila siku hujumuisha AI zalishi. AI zalishi ni aina ya akiliunde ambayo inatambua mitindo kuanzia viwango vikubwa vya data na hutumia mitindo hiyo ili kubuni maudhui mapya kama vile maandishi, picha na maudhui mengine.

AI zalishi inalipatia shirika lako lisilo la faida uwezo, si tu wa kuokoa muda lakini pia kuongeza tija ya kazi yako. Zana hizi hutumika kama washirika dijitali, wanaowezesha wafanyakazi wakamilishe majukumu changamano kwa ufanisi zaidi, kufanya uamuzi unaotokana na data pamoja na kufikia viwango vipya vya ubunifu. Fikiria kuandaa rasimu za mapendekezo ya ruzuku yanayovutia kwa maarifa yanayotokana na utafiti, kutayarisha kampeni bora zilizowekewa mapendeleo, zinazowavutia zaidi wafadhili au kuchanganua data ya mpango ili kubainisha maeneo ya kuboresha – vyote kwa usaidizi wa AI.

Mikakati na mbinu za kutumia AI kwa kuwajibika

Ingawa AI zalishi hukupatia uwezekano mkubwa wa kuboresha ufanisi na tija kwenye shirika lako lisilo la faida, ni muhimu kuweka mbinu za uwajibikaji wakati wa kutumia zana za AI zalishi. Mbinu zinazozingatia zaidi usawa, usahihi, ulinzi wa faragha na njia za jumla za kimaadili zitakazosaidia shirika lako lisilo la faida kutumia AI zalishi kwa kuwajibika. 

Kupunguza Upendeleo

Kama ilivyo kwenye mifumo yote inayotegemea data, ni muhimu kuzingatia upendeleo unaoweza kutokea ambao unaweza kuathiri matokeo yanayotokana na zana za AI. Upendeleo unaweza kutokana na data ya mafunzo iliyotumika kubuni AI au kutokana na vidokezo pamoja na maelezo ambayo watumiaji wanaweka. Mikakati ifuatayo inaweza kusaidia shirika lako litumie AI zalishi kwa kuwajibika na kuhakikisha matokeo unayopata yana usawa na yana uwakilishi.

  • Fuatilia vidokezo vyako. Matokeo ya AI zalishi yanaweza kuonyesha upendeleo ulio kwenye maelezo inayofikia. Zingatia aina ya data unayoweka kwenye kidokezo na jinsi inavyoweza kuathiri matokeo. Weka muktadha wa kutosha kwenye vidokezo vyako ili uisaidie AI itayarishe jibu lenye usawa zaidi.
  • Kagua na uchuje. Kagua matokeo yote ya AI kwa umakini na uangalie upendeleo wowote unaoweza kuwepo. Kagua ili uone ikiwa kuna hali za upendeleo au uwakilishi usio na usawa na usisite kuchuja vidokezo vyako au kujaribu zana tofauti ili upate matokeo yenye usawa na yaliyo sahihi.
  • Hakikisha kuna uanuai katika matokeo. Zana nyingi za AI hutoa matoleo mengi ya jibu kulingana na vidokezo vya mtumiaji. Inapowezekana, linganisha matoleo na uchague matokeo ambayo yanawakilisha mitazamo mbalimbali.

Kuhakikisha usahihi

Wakati mwingine, AI zalishi inaweza "kuota," ikimaanisha kuwa inaweza kutoa matokeo ambayo huenda yanaonekana kuwa ya uhakika na sahihi, lakini kimsingi si sahihi. Kuota huku kunaweza kutokea kwa sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na data ambayo haijakamilika inayotumiwa na zana ya AI. Mikakati ifuatayo inaweza kusaidia shirika lako lizingatie usahihi linapotumia AI zalishi katika kazi zako.
 
  • Weka vidokezo dhahiri na mahususi. Unapoandika vidokezo vya zana za AI zalishi, tumia lugha ya kawaida katika hali inayoeleweka na kwa ufupi na uweke muktadha wa kutosha kwenye ombi lako. Epuka kuweka vidokezo vyenye muktadha mpana au maelezo marefu ambayo yanaweza kusababisha matokeo yasiyo sahihi.
  • Hakikisha ukweli wa matokeo yako. Thibitisha usahihi wa maelezo yoyote yaliyotayarishwa na AI. Tumia vyanzo vinavyoaminika kupitia utafiti wako ili uthibitishe maelezo.
  • Fahamu kuhusu vikomo. Elewa kuwa AI zalishi bado inabuniwa na ina vikomo. Kwa majukumu yanayohitaji usahihi wa viwango vya juu, tunapendekeza utumie vyanzo vingine isipokuwa AI ili vikusaidie kukamilisha jukumu lako.

Kuheshimu faragha

Iwapo unatumia AI zalishi ili ikusaidie kutekeleza majukumu ya msingi au kutayarisha maudhui mapya, zingatia jinsi matumizi haya yanavyoweza kuathiri faragha na usalama wa watu katika shirika lako lisilo la faida na wale unaowahudumia. Mikakati ifuatayo inaweza kusaidia kuhakikisha kuwa shirika lako linapunguza mashaka kuhusu faragha na usalama linapotumia AI.

  • Kagua sera za faragha. Soma hati yote ya zana za AI ili upate maelezo kuhusu kinga za faragha ambazo wasanidi programu wamebuni, ikiwa ni pamoja na sheria na masharti. Fanya utafiti ili uendelee kufahamu kuhusu sheria za faragha na mbinu bora za kutumia AI.
  • Dhibiti uwekaji wa data yako. Ondoa taarifa za siri, za faragha au zinazoweza kumtambulisha mtu pamoja na data nyeti ya shirika au ya mnufaika unapotumia zana za AI.

Kufumbua matumizi ya AI

Kufumbua matumizi yako ya AI zalishi huhamasisha uaminifu na hudumisha mbinu za kimaadili kwenye shirika lako lisilo la faida. Mikakati ifuatayo inaweza kusaidia kuhakikisha uwazi unapotumia AI zalishi katika kazi zako.

  • Bainisha kuhusu matumizi. Bainisha kwa udhahiri muda wowote shirika lako lisilo la faida linapotumia AI. Fumbua kwa watumiaji wako kuwa unatumia zana za AI na sababu za kuzitumia. 
  • Toa maelezo. Fafanua aina ya zana uliyotumia na lengo la kuitumia. Toa maelezo mengine yoyote ambayo yanaweza kumsaidia mtu yeyote anayeweza kufikia kazi yako atathmini hatari zinazoweza kutokea.
  • Epuka kunakili kazi za wengine. Dumisha uhakiki unaofanywa na wanadamu unapotumia matokeo ya AI kwenye shirika lako lisilo la faida, ikiwa ni pamoja na kukagua na kurekebisha matokeo bila kuyanakili na kuyabandika moja kwa moja.

Nyenzo za Kutumia AI kwa kuwajibika

Mashirika ya aina zote yanatafuta mbinu za jinsi ya kutumia AI zalishi kwenye kazi yanazofanya. Mwongozo wa matumizi ya AI kwa kuwajibika unaweza kulisaidia shirika lolote libaini sera na mbinu bora za AI. Nyenzo zifuatazo kutoka mashirika mbalimbali hutoa mwongozo wa ziada wa kuzingatia ili kuelewa jinsi ya kutumia AI kwa kuwajibika. 

 




 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
765485566774662729
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
false
false