Arifa

Hivi majuzi tulitangaza mabadiliko kwenye kurasa za uchapishaji. Tafadhali soma hapa ili upate maelezo zaidi.

Chapisha Maudhui yako kwenye Google News

Google News inaweza kukusaidia ufikie hadhira na uvutie wasomaji wa habari wenye shauku kwenye tovuti yako. Kupitia Google News, watumiaji wanaweza:

  • Kugundua matukio ya sasa, habari za kimataifa na maudhui mbalimbali kutoka kwa wachapishaji tofauti.
  • Kufuatilia watoa habari na mada mahususi.
  • Kualamisha na kushiriki makala.
  • Weka mapendeleo kwenye maudhui katika sehemu ya “Kwa ajili yako”.

Jinsi inavyofanya kazi

Kupitia vipengele mbalimbali, Google News huwaruhusu watumiaji wawasiliane na wapate maelezo kukuhusu. Matumizi ya Google News ni pamoja na fursa za uwekaji chapa na uchumaji wa mapato kama vile mauzo ya usajili maalum na matangazo kupitia kipengele cha Jisajili kupitia Google.

Unaweza kutumia zana ya Kituo cha Wachapishaji kushiriki maudhui yako kwenye Google News kwa kutuma mipasho ya RSS, URL za tovuti au video.

Hata ikiwa hujawasilisha chapisho kwenye Kituo cha Wachapishaji, Google inaweza kupata tovuti yako kupitia njia yetu ya kawaida ya kutambaa kwenye wavuti. Ikiwa hungependa maudhui yako yaonekane kwenye Google News, unaweza kuzuia ufikiaji wa maudhui kwenye tovuti yako bila kuathiri nafasi na farahasa katika huduma ya Tafuta na Google.

Ingawa huhitaji kujisajili kupitia Kituo cha Wachapishaji ili maudhui yako yapate nafasi kwenye Google News, hatua hiyo ina manufaa fulani:

  • Udhibiti wa chapa na maudhui:Buni, weka chapa na uweke mapendeleo kwenye chapisho lako katika Google News.
  • Fursa za kuchuma mapato: Wachapishaji wanaweza kutumia ulingo wa malipo kwenye Google News kupitia kipengele cha Jisajili kupitia Google.
  • Ustahiki wa kupata nafasi ya kuorodheshwa: Wachapishaji ambao wameweka na kuwasilisha Machapisho ya Google News kwenye Kituo cha Wachapishaji wanastahiki kuorodheshwa katika programu kwenye sehemu ya Rafu ya Google Play katika nchi na maeneo husika.
    • Muhimu: Hatukuhakikishii kuwa utapata nafasi ya kuorodheshwa. Algoriti huweka mapendeleo kwenye machapisho yanayoonekana katika Rafu ya Google Play kulingana na mapendeleo ya mtumiaji.

Mambo ya kuzingatia

  • Mipasho au URL unayotuma katika Kituo cha Wachapishaji haijahakikishiwa kuonyeshwa au kuorodheshwa kwenye Google News.
  • Ili kuonyesha maudhui yako kwenye Google News, ni lazima yafuate Sera za Tafuta na Habari. Google inaweza kuzuia maudhui yanayokiuka sera pale ukaguzi wa kiotomatiki unapofanywa baada ya maudhui kuwasilishwa.
  • Iwapo unaendesha tovuti katika lugha nyingi, usiwaelekeze kiotomatiki wanaotembelea tovuti kwenda kwenye matoleo tofauti ya lugha. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kudhibiti tovuti za kikanda na za lugha nyingi.
  • Zifanye URL za kuelekeza kutoka kikoa kimoja kwenda kingine katika kifaa cha mkononi zilingane na kwenye kompyuta ya mezani. Kwa mfano, ikiwa example.com inaelekeza kwenye example1.com kwenye kifaa cha mkononi, inapaswa kuwa hivyohivyo kwenye kompyuta ya mezani. Kuwa na URL za kuelekeza ambazo hazilingani kwenye mifumo yote kunaweza kuwazuia watumiaji pamoja na mitambo ya kutafuta isiangalie maudhui kwenye tovuti yako.

Pata maelezo kuhusu jinsi maudhui yako yanavyoweza kuonekana kwenye huduma zingine za Google News.

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
6981012076207618190
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
100499
false
false