Jinsi daraja la maudhui linavyokabidhiwaIli upokee ukadiriaji wa maudhui, ni lazima ujaze dodoso la ukadiriaji kwenye Dashibodi ya Google Play lililo na maswali kuhusu hali ya maudhui ya programu yako. Programu yako itakabidhiwa daraja la maudhui kutoka mamlaka mbalimbali za ukadiriaji kulingana na majibu utakayojaza kwenye dodoso. Usipotoa maelezo sahihi kuhusu maudhui ya programu yako, inaweza kuondolewa au kusimamishwa. Kwa hivyo, ni muhimu utoe majibu sahihi katika dodoso la ukadiriaji wa maudhui. Ili kuzuia programu yako isiorodheshwe kuwa “Haijakadiriwa”, ni lazima ujaze dodoso la daraja la maudhui kwa kila programu mpya unayowasilisha kwenye Dashibodi ya Google Play, pamoja na programu zote zilizoko zinazotumika kwenye Google Play. Programu zisizo na daraja la maudhui zitaondolewa kwenye Duka la Google Play. Ukibadilisha maudhui au vipengele vya programu yako ambavyo vitaweza kuathiri majibu kwenye dodoso ya ukadiriaji, ni lazima uwasilishe dodoso jipya la ukadiriaji wa maudhui katika Dashibodi ya Google Play. Tembelea Kituo cha Usaidizi ili upate maelezo zaidi kuhusu mamlaka mbalimbali za ukadiriaji na jinsi ya kujaza dodoso la ukadiriaji wa maudhui. |