Unda ukurasa maalum wa programu katika Google Play ili ulenge watumiaji mahususi

Kwa kutumia kurasa maalum za programu katika Google Play, unaweza kuweka maelezo ya kuwavutia watumiaji mahususi au wanaotembelea ukurasa wa programu yako katika Google Play kupitia URL maalum.

Ikiwa programu yako inalenga hadhira katika nchi mbalimbali, unaweza kutumia kurasa maalum za programu katika Google Play ili uonyeshe kwa usahihi vipengele vya programu yako na ueleze kuhusu umahiri wa programu yako kwa njia zinazowavutia hadhira tofauti. Unaweza kutumia kurasa maalum za programu katika Google Play ili uwafikie watumiaji katika nchi tofauti ambao wamejisajili mapema, watumiaji wanaotafuta maneno muhimu mahususi au watumiaji waliosita kutumia programu.

Njia nyingine ya kutumia kurasa maalum za programu katika Google Play ni kuonyesha ukurasa maalum wa programu katika Google Play kwa watumiaji wanaotembelea ukurasa huo kupitia URL maalum au katika kampeni mahususi ya Google Ads. Hii inaweza kuwa njia bora ya kuangazia vipengele vinavyohusiana na programu yako kulingana na kurasa za programu yako ambazo watumiaji wanatembelea katika Google Play.

Kumbuka: Ukurasa maalum wa programu katika Google Play ni mojawapo ya njia mbili ambazo Dashibodi ya Google Play inaweza kukusaidia kubuni huduma za kipekee kwa watumiaji katika maeneo mbalimbali. Ili kubuni ukurasa wa programu katika Google Play na maudhui ya programu yanayolingana na mapendeleo ya lugha ya mtumiaji (au jozi za lugha zinazopendelewa katika eneo fulani), tunapendekeza ujumuishe tafsiri za programu yako.
Angalia mifano kuhusu jinsi unavyoweza kutumia kurasa maalum za programu katika Google Play

Ili kukusaidia ubaini njia bunifu za kutumia kurasa maalum za programu katika Google Play, ifuatayo ni mifano kadhaa kuhusu jinsi ya kuzitumia:

Mfano wa 1: Angazia vipengele kwa wanaozungumza Kiingereza katika nchi mbalimbali

Chukulia kuwa una programu ya kutiririsha video ambayo huenda ikavutia hadhira kubwa Marekani na Singapoo, nchi mbili ambako kuna idadi kubwa ya watumiaji wanazungumza Kiingereza.

Ili uweze kutangaza ukurasa wa programu yako katika Google Play kwa watumiaji katika nchi hizi mbili, unataka kuangazia vipengele na maudhui mbalimbali (kwa mfano vipindi maarufu vya televisheni) yanayowavutia watumiaji wengi katika kila nchi. Unaweza kufuata utaratibu ufuatao ukitumia ukurasa wa programu yako katika Google Play:

  • Tunga ukurasa mkuu wa programu katika Google Play kwa Kiingereza: Kwa kuwa unalenga haswa watumiaji nchini Marekani, unaweza kutunga ukurasa mkuu wa programu katika Google Play kwa watumiaji walio Marekani na nchi nyingine ambako Kiingereza (en-US) kinatumika kama lugha ya chaguomsingi. Unaweza kujumuisha watu mashuhuri nchini Marekani katika picha zako za skrini na utaje kuwa programu yako inatumia “hali ya kutazamwa nje ya mtandao” kwenye maelezo mafupi kuhusu programu yako kwa sababu kipengele hiki ni maarufu nchini Marekani.
  • Tunga ukurasa maalum wa programu yako katika Google Play kwa Watumiaji walio Singapoo: Ili uweze kutangaza programu yako Singapoo, tunga ukurasa maalum wa programu katika Google Play unaolenga watumiaji nchini Singapoo. Kwa kuwa kuna uwezekano kuwa watumiaji unaolenga wanazungumza Kiingereza, teua Kiingereza (en-US) kuwa lugha chaguomsingi kwenye ukurasa maalum wa programu yako katika Google Play. Unaweza pia kujumuisha watu mashuhuri nchini Singapoo katika picha zako za skrini, na utaje video ya 4K kwenye maelezo mafupi kuhusu programu yako kwa sababu kipengele hiki ni maarufu nchini Singapoo.

Matokeo

Ukurasa mkuu wa programu katika Google Play Ukurasa maalum wa programu katika Google Play
  • Watumiaji walio Marekani wanaozungumza Kiingereza wataona ukurasa kuu wa programu yako katika Google Play ukiwa na watu mashuhuri ambao wanatambua na kusoma kuhusu "hali ya kuangalia nje ya mtandao."
  • Watumiaji walio Marekani wanaozungumza Kihispania wataona ukurasa mkuu wa programu yako katika Google Play ukiwa na maudhui sawa yaliyotafsiriwa kiotomatiki katika Kihispania.
  • Watumiaji walio Singapoo wanaozungumza Kiingereza wataona ukurasa wako maalum katika Google Play ukiwa na watu mashuhuri ambao wanatambua na kusoma kuhusu video za 4K.
  • Watumiaji walio Singapoo wanaozungumza Kimalei wataona ukurasa maalum wa programu yako katika Google Play kwa Kiingereza kwa sababu kurasa maalum za programu katika Google Play hazijumuishi tafsiri za kiotomatiki. Iwapo ungependa waone ukurasa maalum wa programu yako kwenye Google Play katika Kimalei, unaweza kuongeza tafsiri.

Mfano wa 2: Tumia lugha nyingi chaguomsingi kutangaza programu yako

Chukulia kuwa una programu ya kitabu cha mapishi ambacho ni maarufu Marekani na nchi za Amerika Kusini, haswa Meksiko, Ajentina na Brazili.

Ili uwavutie watumiaji kupitia mapishi na maelezo, unataka kuweka mapendeleo kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play ili ulenge watumiaji katika maeneo mahususi. Unaweza kufuata utaratibu ufuatao ukitumia ukurasa wa programu yako katika Google Play:

  • Tunga ukurasa mkuu wa programu katika Google Play kwa Kiingereza: Kwa kuwa unalenga haswa watumiaji nchini Marekani, tunga ukurasa mkuu wa programu katika Google Play kwa Kiingereza (en-US) unaolenga watumiaji walio Marekani na nchi zingine.
  • Tunga ukurasa maalum wa programu yako katika Google Play kwa watumiaji walio Amerika Kusini wanaozungumza Kihispania na Kireno cha Brazili: Ili utangaze programu yako kwa watumiaji nchini Meksiko, Ajentina na Brazili, tunga ukurasa maalum wa programu yako katika Google Play unaoitwa “Amerika Kusini” ambao unalenga watumiaji katika nchi hizo. Weka Kihispania cha Amerika Kusini (es-419) kuwa lugha chaguomsingi kisha ujumuishe tafsiri ya Kireno cha Brazili (pt-br). Unaweza pia kujumuisha picha za skrini na maelezo yanayowavutia watumiaji walio Amerika Kusini.

Matokeo

Ukurasa mkuu wa programu katika Google Play Ukurasa maalum wa programu katika Google Play
  • Watumiaji walio Marekani na nchi nyingine mbali na Meksiko, Ajentina na Brazili, wanazozungumza Kiingereza, wataona ukurasa kuu wa programu yako katika Google Play.
  • Watumiaji walio Amerika Kusini wanaozungumza Kihispania wataona ukurasa kuu wa programu yako katika Google Play pamoja na tafsiri za kiotomatiki kwa lugha ya Kihispania kwa sababu hukuweka tafsiri kwenye ukurasa kuu wa programu yako katika Google Play.
  • Watumiaji walio Amerika Kusini wanaozungumza Kihispania, nchini Meksiko, Ajentina na Brazili, wataona ukurasa maalum wa programu yako kwenye Google Play katika Kihispania, lugha chaguomsingi ya ukurasa wako maalum wa programu katika Google Play.
  • Watumiaji walio Meksiko, Ajentina na Brazili wanaozungumza Kireno cha Brazili wataona ukurasa maalum wa programu yako kwenye Google Play katika Kireno cha Brazili kwa sababu umeongeza tafsiri katika lugha yao.
  • Watumiaji walio Meksiko, Ajentina na Brazili wanaozungumza Kiingereza wataona ukurasa maalum wa programu yako kwenye Google Play katika lugha chaguomsingi ya Kihispania cha Amerika Kusini kwa sababu ukurasa maalum wa programu yako katika Google Play haujumuishi tafsiri za kiotomatiki. Weka tafsiri ikiwa ungependa ukurasa maalum wa programu yako katika Google Play uwe kwa Kiingereza.

Mfano wa 3: Angazia vipengele vya programu yako kulingana na jinsi watumiaji wako wanavyotembelea ukurasa wako wa programu katika Google Play

Chukulia kuwa una programu ya mazoezi ambayo inajumuisha shughuli mbalimbali kama vile kuogelea, kukimbia, kuendesha baiskeli, mazoezi ya yoga au shughuli zinazofanana na hizo. Shughuli hizi mbalimbali hutangazwa kwa hadhira tofauti nje ya Google Play.

Ili ufanye ukurasa wako wa programu katika Google Play uwe faafu zaidi kulingana na kinachowavutia watumiaji wako, ungeangazia shughuli mahususi kulingana na iwapo mtumiaji alitembelea ukurasa wako wa programu katika Google Play kupitia kiungo cha Google Play kilichopachikwa kwenye ukurasa unaozungumzia shughuli hiyo mahususi.

  • Tunga ukurasa mkuu wa programu katika Google Play kwa Kiingereza: Tunga ukurasa mkuu wa kawaida wa programu katika Google Play kwa ajili ya watumiaji wanaotembelea kurasa zako bila kupitia URL ya ukurasa maalum wa programu katika Google Play. Huenda ukurasa huu wa programu katika Google Play ukajumuisha shughuli zote unazoweza kutekeleza kwa kutumia programu.
  • Tunga ukurasa maalum wa programu katika Google Play kwa kila shughuli yako: Kwa kila ukurasa maalum wa programu katika Google Play, weka picha za skrini na maelezo yanayolingana na shughuli husika. Chagua jina la kipekee la kigezo cha URL linalolingana na shughuli husika katika ukurasa wa programu katika Google Play.
  • Shiriki URL ya kipekee ya ukurasa maalum wa programu katika Google Play kwenye kurasa zinazofaa: Kila URL ya kipekee itamwelekeza mtumiaji kwenye ukurasa maalum wa programu katika Google Play wa shughuli husika. Pachika URL hizi za kipekee za ukurasa maalum wa programu katika Google Play kwenye kurasa husika za wavuti zinazofafanua au kutangaza kila shughuli.

Mfano wa 4: Weka hali ya utumiaji wa duka inayolingana na Kampeni mahususi ya Programu ya Google Ads

Chukulia kuwa unaendesha kampeni ya mtandaoni inayoangazia kipengele kipya cha programu yako kwa demografia mahususi ukitumia kampeni ya kutangaza programu ya Google Ads.

Ili ufanye ukurasa wako wa programu katika Google Play ulingane na ujumbe wa kampeni yako, unapaswa kujumuisha faili husika za tangazo kwenye vipengee vyako vya ukurasa wa programu katika Google Play. Kwa njia hii, mtumiaji anapobofya kwenye tangazo, ataendelea kuona taarifa zinazofanana huku akiamua iwapo ataweka programu au mchezo wako kwenye kifaa.

  • Fungua ukurasa kuu wa programu katika Google Play: Fungua ukurasa kuu wa kawaida wa programu katika Google Play wa kutumiwa na watumiaji wanaotembelea kurasa zako bila kubofya Tangazo. Huenda ukurasa huu wa programu katika Google Play ukajumuisha shughuli zote unazoweza kutekeleza kwa kutumia programu.
  • Fungua ukurasa maalum wa programu katika Google Play kwa kila kampeni zako za Google Ads: Kwa kila ukurasa maalum wa programu katika Google Play, weka picha za skrini na maelezo yanayolingana na faili husika za tangazo za Google Ads. Utaombwa ubandike kwenye AdGroupID ya Google Ads, unayoweza kupata kwenye dashibodi ya Google AdWords.
  • Hifadhi na uchapishe ukurasa wako wa programu katika Google Play: Baada ya kuhifadhiwa na kuchapishwa, watumiaji wanaobofya tangazo lililo na AdGroupIDs yako wataona vipengele vya ukurasa wako maalum wa programu katika Google Play kwenye mifumo mbalimbali ya Google Play.

Matokeo

Ukurasa mkuu wa programu katika Google Play Ukurasa maalum wa programu katika Google Play
Watumiaji wanaotembelea ukurasa wa programu katika Google Play bila kubofya Tangazo wataona picha za skrini na maelezo yako chaguomsingi. Watumiaji wanaobofya Tangazo linalohusiana na kufikia ukurasa wako wa programu katika Google Play wataona picha za skrini na maelezo unayotoa yanayolingana na kampeni waliyoona.


Kumbuka: Kurasa za programu katika Google Play zilizo na ulengaji wa matangazo bado hazitumii miundo yote ya Google Ads katika kampeni za kutangaza programu. Unapaswa kutarajia kuona vipengee maalum unapofika kwenye ukurasa wako wa programu katika Google Play kutoka Mtandao wa AdMob wa Google kwenye Android. Miundo zaidi itatumika siku zijazo.

Mwongozo

Unaweza kubuni hadi kurasa 50 maalum za programu katika Google Play. Ikiwa tayari umeunda programu yenye ukurasa wa programu katika Google Play, ukurasa wake wa programu uliopo katika Google Play utakuwa ukurasa mkuu unaoonyeshwa kwa watumiaji katika nchi ambako hujalenga kupitia ukurasa maalum wa programu katika Google Play.

Kabla hujabuni ukurasa wa kwanza maalum wa programu katika Google Play, yafuatayo ni baadhi ya mambo muhimu unayohitaji kufahamu:

Unachoweza kuwekea mapendeleo
  • Kwa kila ukurasa maalum wa programu katika Google Play, unaweza kuweka mapendeleo kwenye jina, aikoni, maelezo na vipengee vya picha vya programu yako.
  • Maelezo ya mawasiliano, sera ya faragha na aina ya programu yako hutumwa kwenye matoleo yote ya ukurasa wa programu yako katika Google Play.
Ulengaji kupitia URL ya kipekee ya ukurasa maalum wa programu katika Google Play
  • Ili ulenge ukitumia URL ya kipekee ya ukurasa maalum wa programu katika Google Play, unapaswa kuweka kigezo cha mfuatano ambacho ni cha kipekee kwenye kurasa zako zote maalum za programu katika Google Play.
  • Data sahihi ya kigezo inajumuisha herufi ndogo na namba pamoja na alama zifuatazo: [".", "-", "_", "~"].
  • Baada ya kubuni ukurasa maalum wa programu yako katika Google Play, unaweza kufikiwa na watumiaji kupitia URL ifuatayo: https://play.google.com/store/apps/details?id=[packageName]&listing=[parameter]
Ulengaji wa Nchi
  • Unaweza kulenga nchi kadhaa ukitumia ukurasa maalum wa programu katika Google Play, lakini unaweza tu kulenga nchi fulani ukitumia ukurasa mmoja maalum wa programu katika Google Play kwa wakati mmoja.
  • Kwa mfano, ikiwa una ukurasa mmoja maalum wa programu katika Google Play unaolenga Marekani na Kanada, huwezi kulenga Marekani na Kanada ukitumia kurasa zingine maalum za programu katika Google Play.
Tafsiri
  • Kurasa maalum za programu katika Google Play hazitafsiriwi kiotomatiki, kwa hivyo unahitaji kuchagua lugha chaguomsingi unapoziweka.
  • Usipojumuisha tafsiri kwenye kurasa zako maalum za programu katika Google Play, kurasa hizo zitaonyeshwa kwa watumiaji kwenye nchi utakazochagua katika lugha chaguomsingi ya ukurasa maalum wa programu yako katika Google Play.
  • Tunapendekeza ujumuishe tafsiri za lugha zote zinazozungumzwa katika nchi unazolenga kupitia ukurasa maalum wa programu katika Google Play.

Kutayarisha ukurasa maalum wa programu katika Google Play

Ili utayarishe ukurasa maalum wa programu katika Google Play:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play.
  2. Chagua programu unayotaka.
  3. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Kuza > Upatikanaji katika Duka la Google Play > Kurasa maalum za programu katika Google Play.
    • Iwapo huna ukurasa mkuu wa programu yako katika Google Play, unahitaji kuuanzisha kisha uchapishe programu yako kabla hujaanzisha ukurasa maalum wa programu katika Google Play.
  4. Chagua Tayarisha ukurasa maalum wa programu katika Google Play.
  5. Teua chaguo:
    • Tayarisha ukurasa mpya: Weka vipengee vyote vinavyohitajika.
    • Toa nakala ya ukurasa uliopo wa programu katika Google Play: Utaanza kwa kutumia nakala ya vipengee kutoka katika mojawapo ya kurasa za programu yako katika Google Play (ikiwa ni pamoja na ukurasa mkuu wa programu yako katika Google Play).
    • Tayarisha ukurasa mpya wa programu katika Google Play kwenye kikundi: Ukurasa huu utatumia vipengee vya kikundi vinavyopatikana kwa chaguomsingi. Ili upate maelezo zaidi, angalia sehemu ya Anzisha kikundi cha kurasa za programu katika Google Play.
  6. Katika sehemu ya “Maelezo ya ukurasa wa programu katika Google Play”, andika jina la ukurasa maalum wa programu yako katika Google Play.
    • Kidokezo: Jina la ukurasa maalum wa programu yako katika Google Play linatumika tu kurejelea na halionekani kwa watumiaji, kwa hivyo chagua jina linalokufaa, kama vile “Amerika ya Kaskazini” au “Nchi zilizoko Asia.” Huwezi kubadilisha jina baada ya kuliweka.
  7. Karibu na chaguo la "Ulengaji," teua kundi la watumiaji ambao ungependa waone ukurasa maalum wa programu yako katika Google Play, kwa kuchagua nchi, URL, neno kuu la utafutaji na/au hali ya mtumiaji.
    • Kumbuka: Mipangilio ya majaribio na usambazaji wa programu yako inaweza kuathiri uwezo wako wa kuteua chaguo fulani au miseto fulani ya chaguo. Hii ni baadhi ya mifano inayofafanua kwa nini vipengele fulani huenda visipatikane:
      • Kutumiwa kwenye ukurasa mwingine maalum wa programu katika Google Play: Nchi au eneo halipatikani kwa kuwa tayari umelenga nchi hiyo kupitia ukurasa mwingine maalum wa programu katika Google Play.
      • Kujisajili mapema: Ulengaji kulingana na hali ya mtumiaji hukuwezesha uonyeshe ukurasa tofauti wa programu katika Google Play kwa watumiaji walio katika nchi au maeneo ambako programu yako iko katika hali ya usajili wa mapema. Watumiaji katika nchi au maeneo ambako programu yako imechapishwa kuwa toleo la umma au inafanyiwa majaribio na watumiaji wengi au watumiaji mahususi, hawataona ukurasa huu wa programu katika Google Play.
      • Programu bado haijachapishwa kuwa toleo la umma: Nchi au eneo halipatikani kwa sababu bado hujachapisha programu kuwa toleo la umma huko.
      • Haipatikani kwenye Google Play: Nchi haipatikani kwa sababu husambazi programu huko.
      • Watumiaji waliosita kutumia programu: Hawa ni watumiaji ambao wamefanya mambo yafuatayo:
        • Walipakua programu yako zaidi ya siku 28 zilizopita.
        • Hawajaitumia ndani ya siku 28 zilizopita au wameiondoa kwenye vifaa vyao vyote
  8. Kwenye sehemu ya "Maelezo ya programu", teua lugha chaguomsingi kwa kuchagua Dhibiti tafsiri > Badilisha lugha chaguomsingi.
    • Kumbuka: Usipoweka tafsiri, watumiaji katika nchi ulizochagua wataona ukurasa wa programu yako katika Google Play kwa lugha chaguomsingi. Iwapo ungependa kujumuisha tafsiri kwenye programu yako, chagua Dhibiti tafsiri zako mwenyewe.
  9. Karibu na "Maelezo ya programu," andika jina na maelezo mafupi na kikamilifu.
  10. Katika sehemu ya "Michoro", pakia vipengee vyako vya picha.
  11. Chagua Anzisha.

Kuanzisha ukurasa wa programu katika Google Play wa maneno makuu ya utafutaji

Ukiwa na ulengaji wa neno kuu la utafutaji, unaweza kufafanua seti ya Maneno makuu ya utafutaji ya Google Play yatakayoelekeza kwenye ukurasa maalum wa programu yako katika Google Play.

  1. Unapochagua hadhira yako, chagua Maneno makuu ya utafutaji.
  2. Bofya Chagua maneno makuu ya utafutaji.
  3. Chagua kwenye maneno makuu yanayopatikana, kwa kuyabofya, tunakuletea wanaoona ukurasa. Kumbuka yafuatayo:
  • Unaweza pia kuweka na kutekeleza utafutaji wa maneno makuu mapya
  • Unaweza kubofya sehemu ya Angalia mabadiliko kwenye neno lolote kuu ili uangalie usahihishaji wa tahajia na tafsiri ambao pia umejumuishwa kwenye kifurushi hiki cha maneno makuu. Unaweza kuchagua na kuacha kuchagua vipengee kama vinavyohitajika kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play.
  • Bofya Hifadhi ili uhifadhi chaguo za mabadiliko yako na urudi kwenye skrini iliyotangulia.
  1. Bofya Hifadhi.
  2. Kwenye ukurasa mpya wa kuweka mipangilio ya orodha yako mpya ya maneno makuu ya utafutaji, weka maelezo yanayofaa na vipengee kama inavyohitajika kwa kufuata hatua zilizo kwenye sehemu iliyotangulia.
  • Kumbuka: Huenda ukaona kisanduku cha kuangazia kinachotoa chaguo la "Kuzalisha maelezo kwa kutumia Gemini." Tunatumia miundo ya Gemini kuzalisha seti mpya ya maelezo kwa kutumia maandishi yako yaliyochapishwa ya ukurasa mkuu wa programu katika Google Play na hoja kuu za utafutaji ulizochagua. Unaweza kuweka mapendekezo haya na kuyabadilisha au kuyaondoa.

Anzisha kikundi cha ukurasa wa programu katika Google Play

Unaweza kuanzisha vikundi kwa kutumia vigezo vyovyote muhimu. Kwa mfano, kikundi kinachohusu likizo, kilicho na picha maalum za skrini zinazoonyesha kila nchi.

Programu zote huanza kwa kikundi chaguomsingi kinachoitwa "Kikundi kikuu cha ukurasa wa programu katika Google Play," kilicho na vipengee vinavyopatikana kwenye ukurasa mkuu wa programu katika Google Play. Tumia kikundi hiki kutayarisha haraka kurasa mbadala za ukurasa mkuu wa programu yako katika Google Play.

Unapotayarisha ukurasa wa programu katika Google Play katika kikundi, ukurasa huo utatumia aikoni, picha za skrini, maelezo na vipengee vingine vya kikundi hicho kwa chaguomsingi. Kisha unaweza kuongeza vipengee maalum ili ubadilishe ukurasa wowote mahususi wa programu katika Google Play. Kusasisha kipengee katika kikundi kutasasisha kipengee hicho katika kurasa zote za programu katika Google Play kwenye kikundi hicho. Kwa mfano, unaweza kusasisha aikoni ya kurasa zote za programu kwenye kikundi kwa kubadilisha aikoni ya kikundi pekee.

Ili kuanzisha kikundi maalum cha ukurasa wa programu katika Google Play:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play.
  2. Chagua programu unayotaka.
  3. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Kuza > Upatikanaji katika Duka la Google Play > Kurasa maalum za programu katika Google Play.
    • Iwapo huna ukurasa mkuu wa programu yako katika Google Play, unahitaji kuuanzisha kisha uchapishe programu yako kabla hujaanzisha ukurasa maalum wa programu katika Google Play.
  4. Chagua Anzisha kikundi.
  5. Teua chaguo:
    • Anzisha kikundi kipya: Utaweka vipengee vyote vinavyohitajika.
    • Toa nakala ya ukurasa uliopo wa kikundi: Utaanza kwa nakala za vipengee ambavyo vipo katika mojawapo ya vikundi vyako.
  6. Katika sehemu ya "Vipengee vya kikundi", andika jina la kikundi cha ukurasa maalum wa programu yako katika Google Play.
    • Kidokezo: Jina la kikundi chako linatumika tu kwa marejeleo yako na halionekani kwa watumiaji, kwa hivyo chagua jina linalokufaa, kama vile "Kikundi cha Amerika Kaskazini" au "Kikundi cha Likizo." Huwezi kubadilisha jina hili baada ya kulitunga.
  7. Kwenye sehemu ya "Maelezo ya kikundi", teua lugha chaguomsingi kwa kuchagua Dhibiti tafsiri > Badilisha lugha chaguomsingi.
    • Kumbuka: Usipoweka tafsiri, watumiaji katika nchi ulizochagua wataona ukurasa wa programu yako katika Google Play kwa lugha chaguomsingi. Ikiwa ungependa kuongeza tafsiri kwa kurasa za programu katika Google Play, chagua Dhibiti tafsiri zako mwenyewe.
  8. Karibu na "Vipengee vya kikundi," andika jina na maelezo mafupi na kikamilifu.
  9. Katika sehemu ya "Michoro", pakia vipengee vyako vya picha.
  10. Chagua Anzisha kikundi.

 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
14219056217106319394
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false