Weka vipengee vya kukagua ili uonyeshe programu yako

Kwa kuweka vipengee vya kukagua vinavyoonyesha utendaji na vipengele vya programu yako kwenye ukurasa wake wa programu katika Google Play, unaweza kusaidia programu yako ivutie watumiaji wapya kwenye Google Play.

Video, picha za skrini, maelezo mafupi na picha zinazoangaziwa hutumiwa kuangazia au kutangaza programu yako kwenye Google Play na chaneli zingine za matangazo kwenye Google.

Dhibiti vipengee vya kukagua

Kabla hujaweka vipengee vya kukagua kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play, kumbuka:

  • Vipengee huonyeshwa kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play kwenye vikundi vyote vya majaribio baada ya kuviweka kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play.
  • Unaweza kubatilisha uteuzi kisanduku cha "Utangazaji wa nje” kwenye ukurasa wa Mipangilio ya Google Play (Kuza > Upatikanaji katika Google Play > Mipangilio ya Google Play) ili uzuie utangazaji wa programu yako kwenye bidhaa inayomilikiwa na Google.

Unaweza kudhibiti vipengee vya kukagua programu yako kwenye Ukurasa mkuu wa programu katika Google Play (Kuza > Upatikanaji katika Google Play > Ukurasa mkuu wa programu katika Google Play) kwenye Dashibodi ya Google Play. Unaweza kupakia picha na kuweka onyesho la kukagua video katika sehemu ya “Picha”.

Mwongozo wa maudhui na matumizi ya kipengee cha kukagua

Vipengee tofauti vya kukagua vina masharti tofauti na yataonyeshwa kwenye mifumo tofauti. Tafadhali soma maudhui yaliyo hapa chini ili uelewe jinsi vipengee vyako vitakavyotumiwa na unachohitaji kukumbuka unapoweka vipengee kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play.

Mwongozo wa maudhui: Masharti na mapendekezo

  • “Masharti” yaliyoorodheshwa kwenye ukurasa huu ni ya lazima; usipotimiza masharti haya, mchezo au programu yako inaweza kuondolewa au kusimamishwa kwenye Google Play.
  • Mwongozo ulioorodheshwa chini ya "Zinazopendekezwa zaidi" kwenye ukurasa huu unaweza kusaidia kufanya mchezo au programu yako istahiki zaidi kupendekezwa na kutangazwa kwenye Google Play. Usipotii mwongozo huu, ukurasa wa programu yako katika Google Play hautaathiriwa, lakini huenda mabadiliko yakatokea kuhusu jinsi vipengee vyako vya kukagua vinaonekana kwenye Google Play au kupunguza fursa za matangazo.
  • Lazima maudhui yote yatii Sera zetu za Mpango wa Wasanidi Programu.

Vipengee vya kukagua

Aikoni ya programu

Lazima uweke aikoni ya programu ili uchapishe ukurasa wa programu yako katika Google Play. Aikoni ya programu haichukui nafasi ya aikoni ya kifungua programu lakini inapaswa kuwa toleo lenye ubora wa juu zaidi ambalo linafuata Vigezo vya muundo wa aikoni ya Google Play.

Matumizi

Aikoni ya programu yako hutumiwa katika maeneo tofauti kwenye Google Play, ukiwemo ukurasa wa programu yako katika Google Play, matokeo ya utafutaji na chati maarufu.

Mwongozo wa maudhui

Masharti

  • PNG ya biti 32 (pamoja na alpha)
  • Vipimo: pikseli 512 kwa pikseli 512
  • Kiwango cha juu cha ukubwa wa faili: KB 1024
  • Inatimiza Vigezo vya muundo wa aikoni kwenye Google Play
  • Haijumuishi beji au maandishi yanayopendekeza nafasi, bei, aina za Google Play au vinginevyo kupotosha watumiaji. Kwa maelezo zaidi, angalia sera ya Metadata.
Maelezo mafupi

Lazima uweke maelezo mafupi ili uchapishe ukurasa wa programu yako katika Google Play. Maelezo yako mafupi ni muhtasari wa haraka unaolenga kuvutia watumiaji kwa kuangazia thamani muhimu ya mchezo au programu.

Matumizi

Maelezo yako mafupi ni maandishi ya kwanza ambayo watumiaji huona wanapoangalia ukurasa wa maelezo ya programu yako kwenye Duka la Google Play na yanaweza kupanuliwa na watumiaji ili waangalie maelezo yote ya programu yako.

Maelezo yako mafupi yanaweza kuonekana katika maeneo mengine kando na ukurasa wa programu yako katika Google Play. Hivyo basi, mtumiaji yeyote anapaswa kuyatumia kuelewa kwa haraka lengo kuu la mchezo au programu yako.

Mwongozo wa maudhui

Masharti

  • idadi ya juu ya herufi ni 80

Inapendekezwa zaidi

  • Toa muhtasari wa utendaji au lengo kuu la mchezo au programu yako katika lugha rahisi na inayoeleweka, ukiangazia vipengee vyovyote vinavyoifanya iwe ya kipekee. 
    • Kwa programu, vipengee vya kipekee vinaweza kuwa vipengele, utendaji, maudhui na manufaa yanayoitofautisha na zingine
    • Kwa michezo, vipengee vya kipekee vinaweza kuwa uchezaji, muundo, hali za wachezaji, vipengele vya kijamii, IP, mandhari na mipangilio, hadithi na muunganisho (kama vile ukiwa ndani au nje ya mtandao).
    • Usitumie lugha ya mtaani au istilahi, isipokuwa iwe inaeleweka kwa urahisi na watumiaji unaolenga.
  • Epuka kurudia ujumbe kwenye maelezo mafupi, picha za skrini, picha zinazoangaziwa au video ya msanidi programu. Kumbuka kuwa vipengee hivi vinaweza kuonyeshwa sambamba.
  • Angazia hali ya sasa ya mchezo au programu yako. 
    • Usitumie nakala inayozingatia muda ambayo inaweza kupitwa na wakati kwa haraka, ili upunguze haja ya kusasisha.
  • Usitumie lugha ambayo haihusiani na utendaji au lengo la programu yako, ikiwa ni pamoja na: 
    • Lugha inayoonyesha au kupendekeza utendaji, nafasi, sifa kuu au tuzo, maoni ya watumiaji, au bei na maelezo ya utangazaji, kwa mfano “Bora zaidi,” “#1,” “Inaongoza,” “Maarufu,” “Mpya,” “Punguzo,” “Mauzo,” au “Imepakuliwa mara Milioni Moja”.
    • Mwito wa kuchukua hatua, kwa mfano, “pakua sasa”, “sakinisha sasa”, “cheza sasa”, au “jaribu sasa.”
    • Maneno muhimu yasiyotakikana kama njia ya kurajibu kuboresha matokeo ya utafutaji; hayataathiri nafasi na hutoa hali mbaya ya utumiaji.
  • Janibisha maelezo yako yafae masoko na lugha tofauti.
  • Hakikisha kuwa maelezo yako mafupi yamepangwa kwa njia sahihi:
    • Tumia tu nukta mwishoni mwa sentensi iwapo maelezo yako mafupi yana sentensi nyingi.
    • Weka nafasi ikitakikana baada ya neno, nukta (.), koma (,) na herufi maalum (kwa mfano, &).
    • Usiweke herufi maalum, alama za kuanzisha mistari, emoji, vikaragosi, uakifishaji unaorudiwa (kwa mfano, ?, !!, ?!, !?!, <>, \\, --,***, +_+, …, ((, !!, $%^, ~&~, ~~~), au ishara (kwa mfano ★ au ☆).
      • Tunaruhusu tu herufi za kawaida zinazotumiwa katika tahajia, sarufi na nahau za lugha yako (kwa mfano, ¿, æ, Ø, or ¡ ).
      • Panapohitajika, tunaruhusu hali zisizofuata kanuni kwa sababu za Hakimiliki (©), Chapa ya Biashara Iliyosajiliwa (®) na Chapa ya Biashara (™).
    • Usitumie herufi kubwa kusisitiza:
      • Weka herufi kubwa kwa njia ya kawaida jinsi ilivyo katika lugha ambayo unatumia kuandika.
      • Vifupisho vinaweza kuandikwa kwa herufi kubwa.
      • Andika tu jina la programu yako kwa herufi kubwa iwapo jina la programu yako katika ukurasa wa Google Play limeandikwa pia kwa herufi kubwa.
Picha inayoangaziwa

Lazima uweke picha inayoangaziwa ili uchapishe ukurasa wa programu yako katika Google Play. Picha yako inayoangaziwa ni zana thabiti ya kuonyesha hali za utumiaji za mchezo au programu na kuwavutia watumiaji wapya.

Matumizi

Picha yako inayoangaziwa huonyeshwa katika maeneo mbalimbali kwenye Google Play, ikiwa ni pamoja na:

  • Kama picha ya jalada la video yako ya kukagua, iwapo ipo.
  • Kwenye programu, tunaonyesha mkusanyiko wa programu katika muundo mkubwa pamoja na picha yako inayoangaziwa, yakiwemo matangazo.
  • Kwenye michezo, tunaonyesha makundi ya michezo inayopendekezwa katika muundo mkubwa yanayoangazia picha za skrini na video za kukagua, ambako tunaonyesha picha yako inayoangaziwa.

Mwongozo wa maudhui

Masharti

  • JPEG au PNG ya biti 24 (alpha hairuhusiwi)
  • Vipimo: pikseli 1024 kwa pikseli 500

Inapendekezwa zaidi

  • Tumia picha ambazo zinaonyesha hali za mchezo au programu na uangazie uboreshaji mkuu wa thamani, muktadha unaofaa au vipengele vya masimulizi panapohitajika.
    • Usitumie chapa dhahiri ambayo inafanana na aikoni ya programu yako, kwa kuwa hatua hii itasababisha urudiaji inapoonyeshwa katika muktadha pamoja na aikoni ya programu yako. Boresha kwa ajili ya vipengele vya chapa ambavyo vinatumika kama viendelezi vya aikoni ya programu yako.
    • Usiweke maelezo mengi mno ya kina kwenye picha. Maelezo haya hayataonekana kwenye skrini nyingi za simu.
  • Weka maudhui ili uvipe kipaumbele vipengele vikuu na uepuke maeneo ya kukatwa.
    • Weka matukio muhimu ya video na sehemu ya kuangaziwa katikati ya picha:

    • Usiweke vipengele muhimu (kwa mfano nembo ya chapa, jina la programu, kaulimbiu msingi na kiolesura kikuu) katika maeneo ya kukatwa (maeneo mekundu katika mfano ulio hapa chini), vinaweza kukatwa kulingana na mfumo wa kiolesura.

    • Baadhi ya miundo inaweza kutumia vipengele vya ziada vya kiolesura kuwekelewa. Usipotii masharti ya sehemu inayoangaziwa na maeneo ya kukatwa, programu yako inaweza kukosa kustahiki kuonekana katika miundo hii.
    • Weka tu vipengele vya mandharinyuma kwenye ncha za picha.
  • Tunakushauri utumie rangi za kupendeza zaidi kwenye picha zako ili ziwe za kuvutia na kuchangamsha na usitumie rangi nyeupe kabisa au ya kijivu kilichokolea. Rangi hizi zinaweza kuingiliana na mandharinyuma ya Google Play.
    • Tumia muundo na mandhari ya rangi zinazoingiliana au zinazofanana kwenye picha inayoangaziwa, aikoni ya programu na kwenye programu yenyewe, ili watumiaji waweze kuzihusisha mara moja na programu na chapa yako.
    • Usitumie rangi nyeupe, nyeusi au kijivu kilichokolea kwa kuwa rangi hizi zinaweza kuingiliana kwa urahisi na mandharinyuma ya Google Play.
  • Tafsiri maandishi ya chapa na picha yako kulingana na masoko na lugha mbalimbali.
  • Usiweke maudhui yoyote yanayoonyesha au kupendekeza utendaji, nafasi, maoni ya watumiaji, sifa kuu au tuzo, au bei na maelezo ya matangazo kwenye Google Play. Kwa mfano, usitumie maneno kama vile “Bora zaidi,” “Inaongoza,” “Maarufu,” “Mpya,” “Bila Malipo,” “Punguzo,” “Ofa,” au “Imepakuliwa Mara Milioni Moja”.
  • Usitumie maudhui yanayozingatia muda ambayo yanaweza kupitwa na wakati kwa haraka, ili upunguze haja ya kusasisha.
    • Maudhui yanayotegemea muda (kama taarifa mahususi za likizo) yanapaswa kuwekwa na kuondolewa kwa muda unaofaa.
  • Usitumie vipengele vya picha vinavyojirudia au visivyofaa, kama vile:
    • Herufi zilizo na chapa ya biashara au nembo za kampuni nyingine bila ya idhini inayofaa.
    • Picha ya kifaa (kwa kuwa hii inaweza kupitwa na wakati kwa haraka au kuwatenga baadhi ya watumiaji).
    • Aikoni au beji ya Google Play au duka jingine lolote.
  • Jumuisha matini mbadala na kila kipengee cha picha. Matini mbadala ni muhimu kwa watumiaji wa kisoma skrini ambao hawawezi kuona vipengee vyako vilivyopakiwa. Kwa sababu hiyo, kutumia maelezo ya matini mbadala ya kila kipengee cha picha kutaboresha sana mwonekano wa programu yako miongoni mwa watumiaji wa teknolojia ya usaidizi. Unaweza kutumia vidokezo hivi kuandika matini mbadala: 

    • Usitumie "picha ya"; visoma skrini tayari vinatoa maelezo haya.

    • Tumia muktadha kutambua sehemu muhimu ya picha, ukitumia herufi zisizozidi 140. Kwa mfano, "Skrini ya muamala umekamilika."

Picha za skrini

Tumia picha za skrini ili uonyeshe uwezo, mwonekano na muundo na hali ya utumiaji ya programu yako kwa watumiaji wanaotarajiwa ili wagundue programu kwa njia bora. Unaweza kuweka hadi picha nane za skrini kwa kila aina ya kifaa kinachotumika. Aina za vifaa vinavyoweza kutumika ni pamoja na simu, kompyuta vibao (inchi saba na inchi 10), Android TV na saa zinazotumia mfumo wa Wear OS.

Ili upakie picha za skrini kwenye aina mbalimbali za vifaa, chini ya Picha nenda kwenye sehemu ya kifaa mahususi:

  • Skrini kubwa:
    • Kwa Chromebook na vishikwambi, unaweza kuweka picha za skrini zisizopungua 4 ili uonyeshe hali yako ya utumiaji wa ndani ya programu.
    • Pakia picha za skrini zenye ubora wa kati ya pikseli 1,080 na 7,680
    • Tumia uwiano wa 16:9 kwa picha mlalo na 9:16 kwa picha wima
    • Usijumuishe maandishi ya ziada ambayo si sehemu ya matumizi yako ya msingi ya programu, kwa sababu yanaweza kukatwa kwenye kurasa za nyumbani za Google Play kwenye ukubwa fulani wa skrini
    • Usisahau kuimarisha ubora wa programu yako kwa ajili ya skrini kubwa kwa kukagua orodha yetu hakikishi ya ubora wa programu
  • Wear OS: Ikiwa unasambaza programu kwenye vifaa vya Wear OS, ukurasa wa programu yako ya Wear OS katika Google Play ni sharti:
    • Uwe na angalau picha moja ya skrini inayoonyesha kwa usahihi toleo la sasa la programu kwenye Wear OS.
    • Utoe picha za skrini zinazoonyesha kiolesura cha programu pekee.
    • Usiweke picha za skrini ndani ya fremu za kifaa, au kujumuisha maandishi, picha au mandharinyuma mengine ambayo si sehemu ya kiolesura cha programu.
    • Ujumuishe picha za skrini zilizo na uwiano wa 1:1 na ukubwa wa usiopungua pikseli 384 x 384.
    • Ikiwa programu yako inatoa huduma ya Vigae, basi tunapendekeza utume picha ya skrini ya utendaji wa Vigae.
    • Usijumlishe mandharinyuma au kuficha sehemu wazi.
  • Sura za saa zinazotumia mfumo wa Wear OS: Ukurasa wa programu wa sura za saa katika Google Play ni sharti:
    • Uwe na angalau picha moja ya skrini inayoonyesha kwa usahihi toleo la sasa la sura ya saa.
    • Uonyeshe zaidi ya mojawapo ya mabadiliko yanayopatikana, ikiwa uso wa saa unaweza kubadilishwa upendavyo.
    • Utoe picha za skrini zinazoonyesha hali ya utumiaji ya sura ya saa pekee.
    • Usiweke picha za skrini ndani ya fremu za kifaa, au kujumuisha maandishi, picha au mandharinyuma mengine ambayo si sehemu ya kiolesura cha programu.
    • Ujumuishe picha za skrini zilizo na uwiano wa 1:1 na ukubwa wa usiopungua pikseli 384 x 384.
    • Usijumlishe mandharinyuma au kuficha sehemu wazi.
  • Android TV: Iwapo unasambaza programu kwenye vifaa vya Android TV, unahitaji kuweka angalau picha moja ya skrini ya Android TV kabla kuichapisha.
    • Picha ya bango la Android TV pia inahitajika.
    • Picha za skrini za TV zitaonyeshwa kwenye vifaa vya Android TV pekee.

Matumizi

Picha za skrini zinaweza kuonyeshwa kwenye Google Play, kwa mfano katika utafutaji au kwenye ukurasa wa kwanza, mbali na ukurasa wa programu yako katika Google Play. Wakati Google Play inaonyesha onyesho lako la kukagua na picha za skrini pamoja, kwa mfano kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play na iwapo video ya kukagua inapatikana, basi picha zako za skrini zitaonyeshwa baada ya video ya kukagua, zikifuatwa kushoto kuelekea kulia na picha za skrini zinazofaa kifaa ambacho mtumiaji anatumia kuvinjari.

Mwongozo wa maudhui

Masharti

Ili uchapishe ukurasa wa programu yako katika Google Play, ni lazima uweke idadi ya chini zaidi ya picha za skrini mbili kwenye maumbo yote ambayo yanatimiza masharti yafuatayo:

  • JPEG au PNG ya biti 24 (alpha hairuhusiwi)
  • Kipimo cha chini: Pikseli 320
  • Kipimo cha juu: Pikseli 3840 
    • Kipimo cha juu zaidi cha picha yako ya skrini hakiwezi kuzidi mara mbili kipimo cha chini zaidi.

Inapendekezwa zaidi

  • Baadhi ya sehemu za Google Play huonyesha vikundi vya michezo na programu zinazopendekezwa katika muundo mkubwa kwa kutumia picha za skrini. Ili utimize masharti ya kuonyesha mapendekezo katika miundo inayotumia picha za skrini, ni sharti ufuate mwongozo huu:
    • Kwenye programu, lazima uweke angalau picha nne za skrini zenye ubora wa angalau pikseli 1080. Picha hizi zinapaswa kuwa na uwiano wa 16:9 zikiwa picha mlalo za skrini (ubora wa angalau pikseli 1920x1080) na uwiano wa 9:16 zikiwa picha wima za skrini (ubora wa angalau pikseli 1080x1920).
    • Kwenye michezo, lazima uweke angalau picha tatu mlalo za skrini za uwiano wa 16:9 (ubora wa angalau pikseli 1920x1080) au picha tatu wima za skrini za uwiano wa 9:16 (ubora wa angalau pikseli 1080x1920). Hakikisha kuwa picha hizi za skrini zinaonyesha hali ya ndani ya mchezo ili watumiaji waweze kuelewa jinsi uchezaji utakavyokuwa iwapo watapakua na kucheza
  • Lazima picha za skrini zionyeshe hali halisi ya matumizi ya ndani ya programu au mchezo, ikizingatia maudhui na vipengele vya msingi ili watumiaji waweze kukisia jinsi hali ya matumizi ya mchezo au programu itakavyokuwa.
    • Tumia video iliyorekodiwa ya mchezo au programu yenyewe. Usiweke watu wanaotumia kifaa (kwa mfano, vidole vinavyogusa kifaa), isipokuwa matumizi ya msingi ya programu au uchezaji hayafanyiki kwenye kifaa.
  • Tunaruhusu picha za skrini zilizowekewa mitindo zinazogawanya kiolesura kwenye picha nyingi zilizopakiwa, lakini kipe kiolesura kipaumbele katika picha tatu za kwanza za skrini kadri uwezavyo.

 

  • Weka tu kaulimbiu iwapo zinahitajika kuonyesha sifa muhimu za mchezo au programu. Kaulimbiu hazipaswi kuchukua zaidi ya asilimia 20 ya sehemu ya picha.
    • Usiweke maudhui yoyote yanayoonyesha au kupendekeza utendaji, nafasi, sifa kuu au tuzo, maoni ya watumiaji, au bei na maelezo ya matangazo kwenye Google Play.  Kwa mfano, usitumie maneno kama vile “Bora zaidi,” “Inaongoza,” “Maarufu,” “Mpya,” “Punguzo,” “Ofa,” au “Imepakuliwa Mara Milioni Moja.” 
    • Usiweke njia yoyote ya kuchukua hatua, kwa mfano "Pakua sasa," "Sakinisha sasa," "Cheza sasa," au "Jaribu sasa."
    • Usiweke maandishi mengi kwenye picha ya skrini katika fonti ndogo au mandharinyuma yanayokinzana na maandishi. Maelezo haya hayataonekana kwenye skrini nyingi za simu.
  • Usitumie kaulimbiu au maudhui yanayozingatia muda, ambayo yanaweza kupitwa na wakati kwa haraka ili upunguze haja ya kusasisha.
    • Maudhui yanayotegemea muda (kama taarifa mahususi za likizo) yanapaswa kuwekwa na kuondolewa kwa muda unaofaa.
  • Tafsiri maandishi ya chapa na picha yako kulingana na masoko na lugha mbalimbali.
    • Kiolesura cha ndani ya mchezo hakipaswi kujanibishwa kulingana na soko, lakini kaulimbiu au maandishi yoyote yanayowekelewa juu yanapaswa kujanibishwa.
  • Badilisha vipengele vya ziada katika sehemu ya arifa kabla ya kutuma. Usionyeshe arifa au watoa huduma. Betri, Wi-Fi na nembo za huduma za simu zinapaswa kuwa kamili.

 

  • Tumia picha za ubora wa juu zilizo na uwiano sahihi.
    • Usiweke picha za skrini ambazo zina ukungu, ni kombo, au zilizopunguzwa ubora kwa njia ambayo hailengi hali ya chapa yako. 
    • Usiweke picha ambazo zimepanuliwa au kubanwa.
    • Zungusha picha za skrini ipasavyo. Usipakie picha zilizoinama, zinazoegemea upande au zilizo kombo.
  • Usitumie vipengele vya picha vinavyojirudia au visivyofaa, kama vile:
    • Nembo au herufi zilizo na chapa za biashara za kampuni nyingine bila ruhusa inayofaa. 
    • Picha ya kifaa (kwa kuwa inaweza kupitwa na wakati kwa haraka au kuwatenga baadhi ya watumiaji). 
    • Aikoni au beji ya Google Play au duka jingine lolote.
  • Jumuisha matini mbadala na kila picha ya skrini. Matini mbadala ni muhimu kwa watumiaji wa kisoma skrini ambao hawawezi kuona picha za skrini ulizopakia. Kwa sababu hiyo, kutumia maelezo ya matini mbadala kutaboresha sana mwonekano wa programu yako miongoni mwa watumiaji wa teknolojia ya usaidizi. Unaweza kutumia vidokezo hivi kuandika matini mbadala: 

    • Usitumie "picha ya"; visoma skrini tayari vinatoa maelezo haya.

    • Tumia muktadha kutambua sehemu muhimu ya picha, ukitumia herufi zisizozidi 140. Kwa mfano, "Skrini ya muamala umekamilika."

Video ya kukagua

Video ya kukagua ni bora katika kuonyesha uwezo, mwonekano na muundo na hali ya programu yako kwa watumiaji wanaotarajiwa ili wagundue programu na kufanya maamuzi bora. Tunapendekeza zaidi uweke video ya kukagua hasa kwa michezo, japo si lazima. Mchezo wako unahitaji video ya kukagua ionyeshwe katika sehemu fulani za Google Play.

Unaweza kuweka video moja ya kukagua kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play kwa kuweka URL ya YouTube katika sehemu ya "video ya kukagua".

  • Tumia URL ya video ya YouTube, wala si URL ya kituo au orodha ya kucheza ya YouTube.
  • Usiweke vigezo vya ziada kama vile muda kwenye URL ya YouTube. 
  • Tumia kiungo kamili cha video kwenye YouTube badala ya kiungo kilichofupishwa.
    • Tumia: https://www.youtube.com/watch?v=yourvideoid
    • Usitumie: https://youtu.be/yourvideoid
  • Weka video iliyojanibishwa inayofaa watumiaji kwenye masoko mbalimbali duniani kote.

Matumizi ya vipengee

Video yako ya onyesho la kukagua huonyeshwa kabla ya picha zako za skrini kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play. Watumiaji wanaweza kutazama video yako ya kukagua kwa kugusa kitufe cha kucheza ambacho kimewekelewa kwenye picha yako inayoangaziwa.

Pia, yafuatayo yanaweza kutekeleza jinsi video yako ya kukagua inaweza kuonekana kwenye Google Play:

  • Huenda pia video yako ya kukagua ikaonyeshwa kwenye ukurasa wa kwanza na utafutaji.
  • Huenda video yako ya kukagua ikacheza kiotomatiki bila kutoa sauti kwa hadi sekunde 30 kulingana na kifaa cha mtumiaji, mipangilio, muunganisho wa mtandao na upana wa eneo kazi. Wakati ambapo video yako haichezi kiotomatiki, kitufe cha kucheza huwekelewa kwenye picha yako inayoangaziwa.
  • Kwenye michezo, baadhi ya sehemu za Google Play huonyesha vikundi vya michezo inayopendekezwa katika muundo mkubwa kwa kutumia video za kukagua.

Mwongozo wa maudhui

Masharti

  • Zima matangazo ili video yako ionyeshwe kwenye Google Play. Watumiaji wanapovinjari Google Play, tungependa waone video inayohusu programu yako, wala si tangazo la mtu mwingine, kwa kuwa hali hii inaweza kuwakanganya watumiaji. Ili uzime matangazo, utahitaji:
    • Kuzima uchumaji wa mapato katika video yako, au
    • Kupakia video tofauti isiyo na madai ya uchumaji wa mapato na usasishe URL katika Dashibodi ya Google Play.
      Muhimu: Iwapo video yako inatumia maudhui yaliyo na hakimiliki, hatua ya kuzima uchumaji wa mapato katika video yako haitatosha kuzuia matangazo. Katika hali hiyo, utahitaji kutumia video tofauti (isiyo na maudhui yaliyo na hakimiliki, ambayo yana madai ya uchumaji wa mapato).
  • Weka mipangilio ya faragha ya video yako kuwa ya umma au ambayo haijaorodheshwa. Usiiweke kuwa ya faragha.
  • Usitumie video iliyo na masharti ya umri.
  • Hakikisha kuwa video yako inaweza kupachikwa kwenye Google Play.

Inapendekezwa zaidi

  • Video yako inapaswa kuweka matarajio sahihi na ionyeshe thamani ya mchezo au programu yako ikilinganishwa na michezo au programu kama yako. 
    • Onyesha hali ya ndani ya programu au ya ndani ya mchezo, ukiangazia vipengele na maudhui ya msingi mapema iwezekanavyo ndani ya sekunde 10 za kwanza za video.
    • Lenga angalau asilimia 80 ya video iwakilishe hali ya utumiaji. 
      • Punguza skrini za mada, nembo, matukio ya msuko au maudhui mengine ya matangazo au yaliyotekelezwa mapema. 
      • Unapotumia video inayowekwa mapema, matukio ya msuko na vipengee vya picha, ni lazima viwe sehemu na vichangie katika hali halisi ya uchezaji.
    • Fanya video zako ziwe fupi na mahususi kwa kuwa hucheza kiotomatiki kwa sekunde 30 za kwanza pekee. Watumiaji wanaweza kuendelea kutazama video kamili kwa kuigusa lakini tunapendekeza uweke video fupi.
    • Usiweke watu wanaotumia kifaa (kwa mfano, vidole vinavyogusa kifaa), isipokuwa matumizi ya msingi ya programu au uchezaji hayafanyiki kwenye kifaa.
    • Hakikisha kuwa video yako ina ubora wa juu na imehaririwa vizuri zaidi. Si lazima video iwe imerekodiwa na mtaalamu, lakini kasi, madoido ya video, madoido ya sauti au muziki, mabadiliko au maandishi yaliyowekelewa juu yanapaswa kuwa laini na yafanye kazi pamoja kwa utaratibu unaofaa.
  • Rekodi video ya mlalo badala ya wima, kwa kuwa itaonyeshwa katika kicheza video za mlalo. 
    • Hata kama mkao wa mchezo au programu yako ni wima, rekodi video ya mlalo ambayo imevutwa karibu kwenye hali ya mchezo au programu.
    • Usiache pau nyeusi katika upande wowote wa video ya wima. 
  • Tunakushauri utumie nakala kumpa mtumiaji muktadha ikiwa video imezimwa sauti (kwa mfano, inapochezwa kiotomatiki). Unapotumia nakala:
    • Usiweke maudhui yoyote yanayoonyesha au kupendekeza utendaji, nafasi, sifa kuu au tuzo, maoni ya watumiaji, au bei na maelezo ya matangazo kwenye Google Play. Kwa mfano, usitumie maneno kama vile “Bora zaidi,” “Inaongoza,” “Maarufu,” “Mpya,” “Punguzo,” “Ofa,” au “Imepakuliwa Mara Milioni Moja.” Tuzo kutoka Google Play kama vile “Bora Katika” zinaruhusiwa kuonyeshwa.
    • Usitumie wito wa kuchukua hatua, kwa mfano, "Pakua sasa," "Sakinisha sasa," "Cheza sasa," au "Jaribu sasa."
    • Hakikisha kuwa maandishi yanasomeka kwa kutumia fonti zinazosomeka, fonti zenye ukubwa unaofaa na uonyeshe maandishi kwa muda mrefu ili mtumiaji ayasome.
  • Usitumie maudhui yanayozingatia muda au kaulimbiu ambazo zinaweza kupitwa na wakati kwa haraka ili upunguze haja ya kusasisha. 
    • Maudhui yanayotegemea muda (kama taarifa mahususi za likizo) yanapaswa kuwekwa na kuondolewa kwa muda unaofaa.
  • Janibisha video ipasavyo ikiwa ni pamoja na kiolesura, kaulimbiu na sauti.
  • Tumia manukuu kwa video za kukagua ili kuwasaidia watumiaji ambao ni viziwi au walio na tatizo la kusikia, pamoja na wale walio katika mazingira ya kelele.

Bango la TV

Unahitaji kipengee cha bango ili uchapishe programu inayotumia Android TV. Unapotengeneza kipengee cha bango, kichukulie kuwa kama aikoni ya programu yako kwenye Android TV.

Kumbuka: Kipengee cha bango la programu yako kitaonyeshwa kwenye vifaa vya Android TV pekee.

Mwongozo wa maudhui

Masharti

  • JPEG au PNG ya biti 24 (alpha hairuhusiwi)
  • Vipimo: pikseli 1280 kwa 720
Picha ya mtindo wa stereo ya digrii 360

Ili uchapishe programu inayoweza kutumia Daydream, utahitaji kuweka Picha ya mtindo wa stereo ya digrii 360 kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play.

Unapoweka picha ya mtindo wa stereo ya digrii 360, ichukulie kama picha ya mandharinyuma ya programu yako katika Google Play kwenye kifaa cha Daydream.

Mwongozo wa maudhui

Masharti

  • JPEG au PNG ya biti 24 (alpha hairuhusiwi)
  • Vipimo: pikseli 4096 kwa 4096
  • Stereo 360°
  • Ukubwa wa juu unaoruhusiwa wa faili: MB 15

 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
2490414573490087347
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false