Tayarisha programu yako ifanyiwe ukaguzi

Ukurasa wa Maudhui ya programu ni mahali ambapo unatoa na kudhibiti maelezo tunayohitaji ili kuhakikisha kuwa programu yako ni salama kwa watumiaji inaowalenga, inatii Sera za Mpango wa Wasanidi Programu wa Google Play na inatimiza mahitaji ya kisheria.

Muhtasari

Ukurasa wa Maudhui ya programu hutufahamisha kuhusu maudhui ya programu yako. Unaweza kukamilisha taarifa kuhusu sera na kutoa maelezo mengine, kama vile maagizo maalum ya ufikiaji kwa wakaguzi, kwenye ukurasa huu. Ifuatayo ni baadhi ya mifano mingine ya vitu unavyoweza kufanya kwenye ukurasa wa Maudhui ya programu ili kuhakikisha kuwa programu yako inatii sera za Google Play: 

  • Kuweka sera yako ya faragha ili kuruhusu kufikiwa kwa maelezo ya jinsi unavyoshughulikia data nyeti ya watumiaji na ya kifaa. 
  • Bainisha iwapo programu yako ina matangazo au haina.
  • Weka na udhibiti maagizo kuhusu jinsi ya kufikia sehemu zenye vizuizi katika programu yako.
  • Kutoa maelezo kuhusu maudhui na hadhira ambayo programu yako inalenga.
  • Kufafanua jinsi unavyolenga kutumia ruhusa zozote nyeti au zinazoweza kuwa na hatari zaidi kama vile ruhusa za SMS na Rekodi ya Namba za Simu.
  • Kupokea madaraja ya maudhui kutoka kwa mamlaka rasmi za ukadiriaji.
  • Kutueleza kuhusu mbinu za usalama na faragha kwenye programu yako.

Ukurasa wa Maudhuii ya programu una vichupo viwili: 

  • Inafaa kushughulikiwa: Taarifa kuhusu sera ambazo unahitaji kushughulikia zinaonyeshwa hapa. Unapaswa kukamilisha taarifa kabla ya makataa husika ili kutii sera za Google Play.
  • Zilizoshughulikiwa: Taarifa kuhusu sera ambazo umezishughulikia zinaonyeshwa hapa. Tutakufahamisha ikiwa tutabaini matatizo yoyote. Ili utii sera za Google Play, unapaswa kukagua mara kwa mara maelezo uliyoweka na uhakikishe kuwa yamesasishwa.

Kuweka maelezo ya programu

Sera ya faragha

Kuweka sera ya faragha kwenye ukurasa wa programu katika Google Play kutakusaidia kutoa maelezo kwa uwazi kuhusu jinsi unavyoshughulikia data nyeti ya watumiaji na ya kifaa.

Ni sharti sera ya faragha, ikiwa ni pamoja na ufumbuzi wowote wa ndani ya programu, ifafanue kwa kina jinsi programu yako inavyokusanya, kutumia na kushiriki data ya watumiaji. Hii inajumuisha aina za vikundi unavyoshiriki navyo. Ni lazima uwasiliane na mwakilishi wako wa kisheria ili akupe mawaidha kuhusu mambo yanayohitajika.

  • Kwa programu ambazo zinaomba idhini ya kufikia data au ruhusa nyeti (jinsi inavyoelezwa kwenye sera za data ya mtumiaji): Ni lazima uunganishe sera ya faragha kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play na ndani ya programu yako. Hakikisha kuwa sera yako ya faragha inapatikana kwenye URL inayotumika, inahusu programu yako na inaelezea faragha ya mtumiaji kwa njia mahususi.
  • Kwa programu zinazolenga watoto: Ni lazima uunganishe sera ya faragha kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play na ndani ya programu yako, bila kujali idhini ya programu yako ya kufikia ruhusa au data nyeti. Hakikisha kuwa sera yako ya faragha inapatikana kwenye URL inayotumika, inahusu programu yako na inaelezea faragha ya mtumiaji kwa njia mahususi. Kumbuka kwamba hata programu ambazo hazifikii data yoyote nyeti au binafsi zinapaswa pia kuwasilisha sera ya faragha. 

Weka sera ya faragha

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Maudhui ya programu (Sera > Maudhui ya programu).
  2. Chini ya "Sera ya Faragha," chagua Anza
    • Kumbuka: Iwapo uliweka sera ya faragha hapo awali na ungependa kufanya mabadiliko, utaona na uchague Dhibiti badala ya anza.
  3. Weka URL ya ilipo sera ya faragha mtandaoni.
  4. Hifadhi mabadiliko uliyofanya.

Matangazo 

Lazima ubainishe iwapo programu yako ina matangazo au haina. Hii ni pamoja na matangazo yanayotumwa kupitia SDK za wengine za matangazo, (Zana za Usanidi wa Programu) matangazo ya kuonyeshwa, matangazo yanayojumuishwa katika maudhui na/au matangazo ya mabango). Programu zilizo na matangazo zitaonyesha lebo ya "Ina matangazo" kwenye ukurasa wa programu katika Google Play. Lebo hii itaonekana kwa watumiaji wote katika Duka la Google Play.

Kumbuka: Lebo ya "Ina matangazo" haitumiki kueleza ikiwa programu ina aina nyingine ya maudhui ya biashara, kama vile kulipia bidhaa zijumuishwe katika maudhui au ofa za kufanya ununuzi wa ndani ya programu au matoleo mapya. Kama programu yako ina huduma ya kulipia bidhaa zijumuishwe katika maudhui, hakikisha kuwa zinatii sheria za nchi husika.

Bainisha iwapo programu yako ina matangazo au haina

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Maudhui ya programu (Sera > Maudhui ya programu)
  2. Chini ya "Matangazo," chagua Anza.
    • Kumbuka: Iwapo ulibainisha hapo awali kuwa programu yako ina matangazo au haina na ungependa kufanya mabadiliko, utaona na uchague Dhibiti badala ya Anza.
  3. Soma Sera ya matangazo ili uhakikishe kuwa programu yako inatii, kisha uchague Ndiyo au La
  4. Hifadhi mabadiliko uliyofanya.

Mifano

Ifuatayo ni baadhi ya mifano ya wakati unapopaswa kujibu "ndiyo" kuhusu kuwa na matangazo kwa ajili ya lebo ya "Ina matangazo" . Orodha hii haijataja kila kitu lakini ina mifano kadhaa kulingana na aina maarufu za matangazo.

  • Mabango na matangazo unganishi: Programu yangu hujumuisha SDK ya matangazo ili kuonyesha mabango na/au matangazo unganishi. Mimi hutumia miundo ya matangazo kupokea mapato na/au kutangaza bidhaa au programu zangu mwenyewe.
  • Matangazo yanayojumuishwa katika maudhui: Programu yangu ina matangazo yanayojumuishwa katika maudhui mengine, ambayo hayawezi kutofautishwa na maudhui mengine (kwa mfano, makala yanayodhaminiwa, matangazo katika mipasho, n.k.).
  • Matangazo ya bidhaa za kampuni yenyewe: Programu yangu hutumia bango dogo la matangazo, tangazo unganishi, tangazo la skrini nzima, na/au wijeti inayotangaza programu zangu nyingine.

Unapaswa kujibu "la" kwa swali linalouliza ikiwa una matangazo kwa ajili ya lebo ya "Ina matangazo" ikiwa tu utatangaza programu zako nyingine katika vyombo mbalimbali vya habari kwa njia zifuatazo:

  • Programu inaonyesha sehemu ya Programu Zaidi* katika menyu kuu inayomwelekeza mtumiaji kwenye programu zako nyingine
  • Chaguo la Programu Zaidi* halitatizi uchezaji
  • Chaguo la Programu Zaidi* halitatanishi mtumiaji kwa kujipachika ndani ya uchezaji

*Vipengee vingine vinavyokubalika badala ya 'Programu Zaidi' ni pamoja na Michezo Zaidi, Mengine ya Kugundua, Toleo Kamili, Zaidi, Kutuhusu, au Aikoni yako ya Msanidi Programu.

Ufuatiliaji wa ziada

Ingawa ni jukumu lako kuhakikisha kuwa umesema ukweli kuhusu uwepo wa matangazo katika programu zako, Google inaweza kuthibitisha haya wakati wowote na kuonyesha lebo ya "Ina matangazo" panapohitajika.

Kama unafikiri kuwa programu yako imewekewa lebo kwa makosa na mfumo wetu, wasiliana na timu yetu ya usaidizi.

Utekelezaji

Ikiwa hutasema ukweli kuhusu uwepo wa matangazo kwenye programu zako, hii itakuwa ukiukaji wa sera za Google Play na inaweza kusababisha kusimamishwa kwa programu zako.

Ufikiaji wa programu

Ikiwa sehemu za programu yako au programu yote imewekewa masharti kwa misingi ya kitambulisho cha kuingia katika akaunti, maelezo ya kuingia katika akaunti, uanachama, mahali au mbinu nyingine za uthibitishaji, lazima uweke maelezo yote yanayohitajika ili kuwezesha ufikiaji wa programu yako.

Weka maelezo ya ufikiaji wa programu

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Maudhui ya programu (Sera > Maudhui ya programu).
  2. Chini ya "Ufikiaji wa programu," chagua Anza.
    • Kumbuka: Iwapo uliweka maagizo ya ufikiaji wa programu hapo awali na ungependa kuyabadilisha, utaona na uchague Dhibiti badala ya Anza.
  3. Bofya + Weka maagizo mapya na utoe maelezo yako ya ufikiaji.
    • Kumbuka: Tumia sehemu ya "Maagizo mengine yoyote" ili kutufahamisha iwapo kuna jambo lolote maalum kuhusu mbinu zako za kuingia katika akaunti, kama vile kutumia nenosiri la wakati mmoja, uthibitishaji wa vigezo vingi au kuingia katika akaunti kwa kutumia zaidi ya sehemu mbili.
  4. Hifadhi mabadiliko uliyofanya.

Iwapo mabadiliko uliyofanya yamekataliwa au programu yako imeondolewa, tafadhali fuata maagizo yaliyo hapa chini ili utume upya programu yako ikaguliwe.  Unaweza kukamilisha hatua hizi bila kuwasiliana au kusubiri jibu kutoka kwa timu ya usaidizi wa sera.

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Ufikiaji wa programu
  2. Sasisha maelezo yako ya ufikiaji wa programu na ubofye Hifadhi.
  3. Ikiwa hali ya mabadiliko yako uliyofanya ni "Yako tayari kutumwa ili yakaguliwe," au iwapo ukurasa wako wa Muhtasari wa uchapishaji una sehemu ya "Mabadiliko yako tayari kutumwa ili yakaguliwe", lazima ubofye Tuma ili yakaguliwe kutoka kwenye ukurasa wa Muhtasari wa uchapishaji ili utume mabadiliko uliyofanya yakaguliwe.

Madokezo: 

  • Unaweza kuweka hadi vikundi vitano vya maagizo.
  • Iwapo kitambulisho chako cha kuingia katika akaunti si cha nambari au mseto wa nambari na herufi (kwa mfano, msimbo wa QR au msimbopau), tengeneza URL isiyobadilika na uipakie kwenye Dashibodi ya Google Play.
  • Iwapo programu yako kwa kawaida inahitaji msimbo wa Uthibitishaji wa hatua mbili au Nenosiri la Wakati Mmoja, tupe kitambulisho cha kuingia katika akaunti kinachoweza kutumiwa tena ambacho ni cha kudumu.
  • Iwapo programu yako kwa kawaida inatumia nenosiri linalotegemea mahali alipo mtumiaji (kwa mfano, geo-gate), toa kitambulisho cha kuingia katika akaunti ambacho kinatumika bila kujali mahali alipo mtumiaji (kwa mfano, kitambulisho “kikuu” cha kuingia katika akaunti).
  • Ikiwa kitambulisho chako cha kuingia katika akaunti kwa kawaida huwa kwa lugha isiyo ya Kiingereza, toa toleo la Kiingereza la vitambulisho vyote muhimu vya kuingia katika akaunti kupitia Dashibodi ya Google Play.

Maudhui na hadhira lengwa

Ni lazima ubainishe rika linalolengwa na programu yako. Programu zozote ambazo zinalenga hadhira ya watoto lazima zitii Masharti ya sera ya Familia kwenye Google Play.

Ni muhimu kuweka maelezo sahihi kuhusu programu yako. Kulingana na chaguo zako za hadhira lengwa, programu yako inaweza kuhitajika kutii sera za ziada za Google Play. Unaweza kujifahamisha na sera hizo na upate maelezo kuhusu jinsi ya kujaza sehemu ya "Maudhui na hadhira lengwa" ya ukurasa wa Maudhui ya programu ukurasa. 

Unaweza pia kupata maelezo kuhusu mchakato na ukague orodha hakikishi inayoshirikisha mtumiaji katika Mafunzo kwa Wasanidi wa Google Play.

Fomu ya taarifa za ruhusa

Maombi ya ruhusa hutathminiwa katika mchakato wa kuchapisha baada ya kuweka Android App Bundle yako. Iwapo programu yako inaomba kutumia ruhusa zozote nyeti au zinazoweza kuwa hatari zaidi (kwa mfano Rekodi ya Nambari za Simu au SMS), huenda ukatakiwa kujaza Fomu ya Taarifa za Ruhusa na upokee idhini kutoka Google Play.

Hapa ndipo unaweza kupata maelezo kuhusu mchakato na jinsi ya kujaza Fomu ya Taarifa za Ruhusa kwenye ukurasa wa Maudhui ya programu ukurasa.

Madaraja ya Maudhui

Unaweza kuwasiliana na watumiaji walio katika eneo uliko kuhusu ukadiriaji wa maudhui yanayojulikana na yanayowafaa ili usaidie kuboresha shughuli kwenye programu kwa kulenga watumiaji mwafaka wa maudhui yako.

Ili uzuie programu zako zisiorodheshwe kuwa “Hazijakadiriwa,” ingia katika Dashibodi yako ya Google Play na ujaze dodoso kwa kila mojawapo ya programu hizo haraka iwezekanavyo. Huenda tukaondoa programu ambazo “Hazijakadiriwa” kwenye Google Play.

Nenda kwenye Madaraja ya maudhui ya programu na michezo ili upate maelezo zaidi kuhusu mamlaka na ufafanuzi wa ukadiriaji mahususi, pia upate maagizo kuhusu jinsi ya kujaza sehemu hii ya ukurasa wa Maudhui ya programu.

Programu za hali ya COVID-19 na programu za kufuatilia waliotangamana na aliyeambukizwa COVID-19

Ni sharti utufahamishe iwapo programu yako ina utendaji wa hali ya COVID-19 na kufuatilia waliotangamana na aliyeambukizwa COVID-19. 

Soma Masharti ya programu za ugonjwa wa Virusi vya Korona 2019 (COVID-19) kabla ukamilishe sehemu hii.

Ili ukamilishe taarifa ya programu za hali ya COVID-19 na za kufuatilia waliotangamana na aliyeambukizwa COVID-19:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Maudhui ya programu (Sera > Maudhui ya programu).
  2. Chini ya "programu za hali ya COVID-19 na za kufuatilia waliotangamana na aliyeambukizwa COVID-19," chagua Anza.
    • Kumbuka: Ikiwa ulikamilisha taarifa hapo awali na ungependa kufanya mabadiliko, utaona na uchague Dhibiti badala ya Anza.
  3. Chagua taarifa zote zinazozingatiwa kwenye programu yako.
  4. Hifadhi mabadiliko uliyofanya

Ikiwa programu yako ina utendaji wa hali ya COVID-19 au wa kufuatilia waliotangamana na aliyeambukizwa COVID-19, ni sharti utoe arifa ya mapema kwa timu ya Ukaguzi wa Programu ya Google Play.

Maudhui yanayohusiana

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
11299853480756601266
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false