Tayarisha na usambaze toleo

Ukiwa na toleo, unaweza kudhibiti Android App Bundle ya programu yako (au APK kwa programu zilizoweka kabla ya Agosti 2021) kisha usambazae programu yako kwenye kikundi maalum.

Hatua ya Kwanza: Unda toleo

Toleo ni mchanganyiko wa toleo moja au zaidi la programu utakalotayarisha ili kuzindua programu au kusambaza sasisho la programu. Unaweza kuweka toleo kwenye vikundi vitatu tofauti vya majaribio au kwenye toleo la umma:

  • Jaribio la watu wengi: Matoleo ya majaribio ya wengi yanapatikana kwa wanaojaribu kwenye Google Play. Watumiaji wanaweza kujiunga na majaribio kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play.
  • Jaribio la watumiaji mahususi: Matoleo ya majaribio ya watumiaji mahususi yanapatikana kwa wachunguzaji wachache unaowachagua, ambao wanaweza kujaribu toleo la mapema la programu yako na kutoa maoni.
  • Jaribio la ndani: Matoleo ya majaribio ya ndani yanapatikana kwa hadi watumiaji 100 unaochagua ambao wanajaribu ndani ya kampuni.
  • Toleo la umma: Matoleo ya umma yanapatikana kwa watumiaji wote wa Google Play katika nchi ulizochagua.

Muhimu:

  • Lazima uwe na ruhusa ya Kusambaza programu kwenye vikundi vya majaribio ili uunde toleo jipya.
  • Wasanidi programu walio na akaunti za binafsi zilizofunguliwa kabla ya tarehe 13 Novemba 2023, lazima watimize masharti mahususi ya kujaribu kabla ya kuchapisha programu zao kwenye Google Play. Soma makala haya ya Kituo cha Usaidizi ili upate maelezo zaidi.
  • Huwezi kuunda toleo jipya ukiwa na matoleo ambayo bado hayajachapishwa. Sambaza matoleo yoyote yanayosubiri kuchapishwa hadi asilimia 100 au uondoe mabadiliko kwenye ukurasa wa Muhtasari wa uchapishaji na ufute kwanza matoleo yoyote ambayo hayajachapishwa.

Ili uanzishe toleo lako:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye kundi ambako ungependa kuanzisha toleo lako: 
  2. Karibu na sehemu ya juu kulia kwenye ukurasa, bofya Weka toleo jipya.
    • Kumbuka: Iwapo sehemu ya Weka toleo jipya imezimwa, unaweza kutekeleza majukumu kadhaa ili ukamilishe. Majukumu haya yanaweza kuorodheshwa kwenye ukurasa wa Dashibodi.

Ukitaka kubadilisha toleo lililopo, unaweza kwenda kwenye ukurasa unaofaa wa toleo kama ilivyoorodheshwa katika hatua ya 1 hapo juu na ubofye Badilisha toleo.

Kidokezo: Ili upate maelezo zaidi kuhusu majaribio, nenda kwenye weka mipangilio ya majaribio ya watu wengi, wachache au jaribio la ndani.

Hatua ya 2: Tayarisha toleo la programu yako

  1. Fuata maagizo yaliyo kwenye skrini ili utayarishe toleo lako: 
    • Ikiwa hili ni toleo lako la kwanza la programu hii, fuata maagizo ya kuweka mipangilio ya mpango wa Google Play wa Kuambatisha Cheti kwenye Programu.
    • Weka App Bundles zako.
      • Kumbuka: Programu zilizoundwa kabla ya Agosti 2021 zinaweza kuweka App Bundles au APK za masasisho ya programu.
    • Si lazima: Ikiwa hii ni mara yako ya kwanza ya kuweka toleo, una chaguo la kubadilisha ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye programu. Katika sehemu ya "Uadilifu wa programu", bofya Badilisha ufunguo wa kuambatisha cheti kwenye programu. Kabla ya kubadilisha ufunguo wako, elewa kwamba:
      • Watumiaji wa jaribio la ndani na jaribio la watumiaji wachache ambao tayari wamesakinisha programu yako hawatapokea tena masasisho. Watumiaji hawa watapaswa kuondoa na kusakinisha upya programu ili wapokee masasisho.
      • Hutaweza kutumia matoleo yoyote ya programu yaliyopakiwa mapema. Utapaswa kupakia upya matoleo ya programu.
    • Andika jina la toleo lako. 
    • Weka maelezo kuhusu toleo.
    • Kwa maelezo zaidi kuhusu mojawapo ya sehemu hizi, chagua mada ya sehemu husika kwenye “Tayarisha” hapa chini.
  2. Ili kuhifadhi mabadiliko yoyote unayofanya kwenye toleo lako, chagua Hifadhi kuwa rasimu.
  3. Baada ya kutayarisha toleo lako, chagua Inayofuata.

Kumbuka: Baada ya kuchapisha programu kwenye toleo la jaribio la watumiaji wengi, ufunguo wake hauwezi kubadilishwa.

Tayarisha

Chagua mada ya sehemu hapo chini ili upate maelezo zaidi.

Uadilifu wa Programu

Sehemu hii huonyesha hali ya mpango wa Google Play wa Kuambatisha Cheti kwenye Programu. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kutumia mpango wa Google Play wa Kuambatisha Cheti kwenye Programu.

App Bundle

Katika sehemu hii, unaweza kupakia App Bundles mpya au uziweke kutoka kwenye maktaba yako. Unaweza pia kubofya aikoni ya nukta tatu ili:

  • upakie faili ya uunganishaji wa ReTrace (.txt)
  • upakie alama za utatuzi wa mfumo (.zip)
  • upakie faili ya upanuzi (.obb)
  • uondoe App Bundle

Kumbuka: Programu zilizowekwa kabla ya Agosti 2021 zinaweza kutumia App Bundles au APK kwenye matoleo.

Ili upate maelezo zaidi kuhusu sababu ya kupakia faili za Uunganishaji wa ReTrace na alama za utatuzi za mfumo, nenda kwenye Fanya ufuatiliaji wa rafu za matukio ya programu kuacha kufanya kazi ufumbuliwe kupitia ishara.

Zinazojumuishwa

Katika sehemu hii, angalia maelezo kuhusu App Bundle kutoka toleo lako la awali ambazo zitajumuishwa katika toleo hili.

Kubofya Ondoa kutaondoa App Bundle kutoka kwenye toleo hili. Unaweza kupata App Bundle au APK tena kwenye Kichunguzi cha App Bundle.

Ambazo hazijumuishwi

Katika sehemu hii, angalia maelezo kuhusu App Bundle kutoka toleo lako la awali ambazo hazitajumuishwa katika toleo hili.

Kubofya Jumuisha kutaweka App Bundle kwenye toleo hili.

Bainisha ruhusa za programu yako (si lazima)

Maombi ya ruhusa hutathminiwa wakati wa kuchapisha toleo, baada ya kuweka APK au App Bundle zako. Ikiwa programu yako itaomba kutumia ruhusa nyeti au zinazoweza kuwa hatari zaidi (kwa mfano, Rekodi ya Nambari za Simu au SMS), huenda ukatakiwa kujaza Fomu ya Taarifa za Ruhusa na upokee idhini kutoka Google Play.

Jina la toleo

Jina la toleo litatumika katika Dashibodi ya Google Play pekee na halitaonekana kwa watumiaji.

Tutaweka data kiotomatiki kwenye sehemu ya jina la toleo la APK au App Bundle ya kwanza uliyoweka kwenye toleo.

Ili kufanya iwe rahisi kutambua toleo lako, weka jina la toleo ambalo linakufaa, kama vile toleo la muundo ("3.2.5-RC2") au jina la msimbo wa ndani ("Banana").

Nini kipya katika toleo hili?

Muhtasari

Waruhusu watumiaji wako wajue masasisho ya hivi majuzi ambayo ulifanya katika toleo hili la programu yako. Maelezo kuhusu matoleo hayapaswi kutumika kwa malengo ya matangazo au kuomba vitendo kutoka kwa wateja wako.

Weka maelezo kuhusu toleo na udhibiti tafsiri

Weka maelezo kuhusu toleo la programu yako katika lebo za lugha husika. Lebo za lugha zitaonekana katika kisanduku cha maandishi kwa kila lugha ambayo programu inatumia.

Ili ubadilishe lugha zinazotumika katika programu yako, ni lazima kwanza uweke tafsiri. Wakati unarejea kwenye ukurasa wa Tayarisha toleo, lugha zilizowekwa hivi karibuni zitaonekana kwenye kisanduku cha maandishi.

Unapoweka maandishi, hakikisha kuwa lebo za lugha zimewekwa kwenye mistari isiyo na maelezo kuhusu toleo. Unastahili kufuata muundo ufuatao:

<en-US>

Maelezo kuhusu toleo yanaweza kuandikwa kwenye mistari mingi.

</en-US>

Kumbuka: Unaweza kuweka maelezo kuhusu toleo ukitumia herufi hadi 500 za Unicode kwa kila lugha.

Nakili kutoka kwenye toleo lililotangulia

Ili kunakili maelezo kuhusu toleo kutoka kwenye toleo la awali, chagua Nakili kutoka kwenye toleo la awali. Kwenye skrini inayofuata, hatua ya kuchagua toleo itasababisha kunakiliwa kwa maelezo kuhusu toleo na tafsiri zozote katika kisanduku cha maandishi ili yakaguliwe zaidi. Maelezo haya yatatumika badala ya maelezo yoyote kuhusu toleo ambayo huenda uliweka.

Hatua ya 3: Kagua na usambaze toleo lako

Masharti: Kabla ya kusambaza toleo lako, hakikisha kuwa umeweka mipangilio kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play, umetayarisha programu yako ikaguliwe kwenye ukurasa wa Maudhui ya programu na umeweka mipangilio ya bei za programu yako

Muhimu: Unapotayarisha toleo lako, unaweza kuwa na chaguo la Kuhifadhi au Kuchapisha kulingana na ikiwa mabadiliko uliyofanya kwenye programu yako yanahitaji kukaguliwa au la. Uchapishaji utapelekea mabadiliko yako yaonekane moja kwa moja papo hapo. Kuhifadhi mabadiliko yako kutayaweka kwenye "Mabadiliko yaliyo tayari kutumwa kwa ajili ya ukaguzi" katika ukurasa wa Muhtasari wa uchapishaji, ambapo unaweza kuamua ni lini unataka kutuma mabadiliko ili yakaguliwe. Pata maelezo zaidi kuhusu kudhibiti wakati mabadiliko yatakapochapishwa moja kwa moja.

Ukiwa tayari kuchapisha programu yako:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Muhtasari wa Matoleo .
  2. Karibu na toleo ambalo ungependa kusambaza, chagua kishale cha kulia ili ufungue ukurasa wa Maelezo ya toleo
    • Kidokezo: Tumia upau wa kutafutia iwapo umeshindwa kupata toleo lako. 
  3. Kwenye sehemu ya “Muhtasari wa toleo”, chagua Angalia dashibodi ya toleo.
  4. Chagua kichupo cha Matoleo, kisha Badilisha.
  5. Kagua rasimu ya toleo lako, fanya mabadiliko yoyote yanayohitajika na uchague Inayofuata. Utaelekezwa kwenye skrini ya "Kagua kwanza na uthibitishe", ambapo unaweza kuhakikisha kuwa toleo lako halina matatizo yoyote kabla ya kulisambaza kwa watumiaji.
  6. Ukiona mada “Muhtasari wa hitilafu” katika sehemu ya juu ya ukurasa, bofya Onyesha zaidi ili ukague maelezo na utatue matatizo yoyote. 
    • Kumbuka: Unaweza pia kuangalia ubora unaopendekezwa au unaohitajika, ikiwa upo. Huwezi kuchapisha programu yako hadi usuluhishe hitilafu. Iwapo una maonyo, matatizo madogo au yote mawili, basi unaweza kuchapisha programu yako, lakini tunapendekeza uyashughulikie kabla ya kuchapisha.
  7. Kama unasasisha programu iliyopo, chagua asilimia ya usambazaji.
  8. Chagua Anza kusambaza.
    • Iwapo unasambaza toleo la kwanza la programu yako katika toleo la umma, kubofya Anza usambazaji wa toleo la umma kutasambaza pia programu yako kwa watumiaji wote wa Google Play katika nchi ulizochagua.

Hatua ya 4: Kagua maelezo ya toleo

Baada ya kuunda toleo, utaona maelezo yafuatayo ya toleo jipya la programu ulilosambaza kwa kila kikundi kwenye jedwali chini ya “Matoleo mapya” katika ukurasa wa Muhtasari wa matoleo.

  • Toleo: Jina la kutambua toleo kwenye Dashibodi ya Google Play pekee, kama vile jina la msimbo wa ndani au toleo la muundo.
  • Kikundi: Kikundi ambacho toleo limesambazwa.
  • Hali ya toleo: Hali ya sasa ya toleo lako.
  • Mara ya mwisho kusasishwa: Tarehe na muhuri wa wakati unaonyesha tukio la mwisho la usambazaji kwa toleo lako.
  • Nchi au maeneo: Idadi ya nchi au maeneo ambayo usambazaji wa mwisho wa toleo lako unapatikana. Baada ya kusambaza toleo la programu yako kwenye Toleo la umma, Jaribio la watumiaji wengi au toleo la jaribio la watumiaji mahususi, unaweza kulenga toleo lako katika kila kundi kwa watumiaji katika nchi mahususi. Soma makala haya ili uelewe jinsi ya kudhibiti upatikanaji wa programu yako katika nchi au maeneo tofauti.

Unaweza kuangalia maelezo zaidi ya kina kwa kuchagua kishale cha kulia ili ufungue ukurasa wa Maelezo ya toleo, ambao unajumuisha:

  • Muhtasari wa toleo: Kikundi cha vipimo vinavyohusiana na idadi ya usakinishaji na masasisho, matatizo ya utendaji na ukadiriaji uliopimwa dhidi ya matoleo ya awali ya programu.
  • App Bundle na APK: Orodha ya App Bundle na APK mpya, zilizohifadhiwa na zilizozimwa zinazohusishwa na toleo lako.
  • Maelezo kuhusu toleo: Orodha ya maelezo kuhusu toleo la awali.
  • Historia ya usambazaji: Rekodi ya matukio inayoonyesha mihuri ya wakati ambayo toleo la programu yako lilisimamishwa, kurejeshwa au kutolewa kwa asilimia mpya ya watumiaji.

Si lazima: Kufuta toleo

Ikiwa, wakati wa kuweka mipangilio ya toleo lako, utaamua kuwa usingependa kuendelea na toleo lako, unaweza kulifuta. Mchakato wa kufuta toleo unatofautiana kulingana na hali ya toleo:

  • Rasimu: Bofya Futa rasimu ya toleo karibu na sehemu ya juu kulia mwa ukurasa. Unapofanya hivi, utapoteza mabadiliko uliyofanya kwenye toleo hili.
  • Ukiwa tayari kutuma ili likaguliwe: Bofya Futa toleo kwenye muhtasari wa toleo. Toleo lako litaondolewa kwenye ukurasa wa Muhtasari wa uchapishaji na halitajumuishwa kwenye mabadiliko ya kutuma ili yakaguliwe.
  • Linakaguliwa au Lipo tayari kuchapishwa: Kwanza, ni lazima uondoe mabadiliko ambayo yanakaguliwa au yaliyo tayari kuchapishwa kwenye Muhtasari wa uchapishaji. Mabadiliko yakishaondolewa, unaweza kubofya Futa toleo kwenye muhtasari wa toleo.
  • Kumbuka: Unaweza tu kufuta toleo jipya zaidi kwenye kikundi, ikiwa ni pamoja na rasimu za matoleo. Matoleo ambayo ni sehemu ya sasisho lililokataliwa hayawezi kufutwa.

Kufuatilia na kudhibiti matoleo kwenye ukurasa wako wa muhtasari wa Matoleo

Iwapo umesambaza matoleo kadhaa, ukurasa wa Muhtasari wa matoleo (chini ya “Toleo” katika menyu ya kushoto) hukusaidia kupata matoleo yote katika sehemu moja. Ni sehemu moja unayoweza kufuatilia upatikanaji wa programu zako kwenye vikundi tofauti, kuangalia nchi au maeneo ambako inapatikana na kuchagua matoleo maalum ili uone maelezo mahususi.

Kufuatilia na kudhibiti mabadiliko ya programu kwenye ukurasa wa Muhtasari wa uchapishaji

Unaweza pia kutumia ukurasa wa Muhtasari wa uchapishaji ili udhibiti wakati ambao mabadiliko ya programu yako yanatumwa ili yakaguliwe na kuchapishwa. Pata maelezo zaidi kuhusu ukurasa wa Muhtasari wa uchapishaji.

Maudhui yanayohusiana

 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
5416237254685264406
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false