Tafsiri na ujanibishe programu yako

Ili uwape watumiaji wa programu yako maelezo yaliyojanibishwa popote walipo, unaweza kuongeza tafsiri za ukurasa wa programu yako katika Google Play, faili za APK, vifungu au bidhaa za ndani ya programu. Unaweza kuziongeza mwenyewe au uzinunue na uzitumie kupitia Dashibodi ya Google Play. Pia, unaweza kutumia huduma ya tafsiri ya mashine ya Dashibodi ya Google Play bila malipo ili utafsiri programu yako kwenda baadhi ya lugha.

Ongeza tafsiri za programu yako

Iwapo mapendeleo ya lugha ya mtumiaji yanalingana na tafsiri ya lugha ulizoongeza, wataona toleo la programu yako lililotafsiriwa. Unaweza pia kuongeza vipengee vya picha vilivyo janibishwa kwenye kurasa zako za programu katika Google Play.

Ukiongeza maandishi ya tafsiri bila vipengele vya picha vilivyojanibishwa, vipengee vya picha vya programu yako vitaonyeshwa katika lugha chaguomsingi.

Kumbuka: Ujanibishaji wa ukurasa wa programu katika Google Play ni mojawapo ya njia mbili ambazo Dashibodi ya Google Play inaweza kukusaidia kuweka hali za kipekee za utumiaji kwa watu katika maeneo mbalimbali. Ili utume kurasa tofauti za programu katika Google Play kulingana na nchi au eneo (ikilinganishwa na lugha), tunapendekeza uweke kurasa maalum za programu katika Google Play.

Weka tafsiri zako mwenyewe za maandishi na vipengee vya picha vilivyojanibishwa
  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Huduma ya tafsiri (Kuza > Upatikanaji katika Duka la Google Play > Huduma ya kutafsiri).
  2. Katika sehemu ya juu ya ukurasa, bofya Weka tafsiri na uchague Weka maandishi ya tafsiri yako mwenyewe kwenye menyu kunjuzi.
    • Kumbuka: Iwapo uliweka tafsiri awali, utaona Dhibiti tafsiri na Dhibiti maandishi ya tafsiri yako mwenyewe kwenye menyu kunjuzi.
  3. Chini ya “Weka au ondoa lugha,” chagua lugha unazotaka kuweka kwenye orodha. 
  4. Bofya Tekeleza.
  5. Hifadhi mabadiliko uliyofanya.
Angalia orodha ya lugha zinazopatikana

Ikiwa unaweka tafsiri zako mwenyewe, unaweza kufanya hivyo katika lugha zifuatazo:

  • Kiafrikana – af
  • Kialbania – sq
  • Kiamhari – am
  • Kiarabu – ar
  • Kiarmenia – hy-AM
  • Kiazabajani – az-AZ
  • Kibangla – bn-BD
  • Kibaski – eu-ES
  • Kibelarusi – be
  • Kibulgaria – bg
  • Kibama – my-MM
  • Kikatalani – ca
  • Kichina (Hong Kong) – zh-HK
  • Kichina (Kilichorahisishwa) – zh-CN
  • Kichina (Cha jadi) – zh-TW
  • Kikorasia – hr
  • Kicheki – cs-CZ
  • Kideni – da-DK
  • Kiholanzi – nl-NL
  • Kiingereza – en-IN
  • Kiingereza – en-SG
  • Kiingereza – en-ZA
  • Kiingereza (Australia) – en-AU
  • Kiingereza (Kanada) – en-CA
  • Kiingereza (Uingereza) – en-GB
  • Kiingereza (Marekani) – en-US
  • Kiestonia – et
  • Kifilipino – fil
  • Kifini – fi-FI
  • Kifaransa (Kanada) – fr-CA
  • Kifaransa (Ufaransa) – fr-FR
  • Kigalisi – gl-ES
  • Kijojia – ka-GE
  • Kijerumani – de-DE
  • Kigiriki – el-GR
  • Kigujarati – gu
  • Kiyahudi – iw-IL
  • Kihindi – hi-IN
  • Kihungari – hu-HU
  • Kiaisilandi – is-IS
  • Kiindonesia – id
  • Kiitaliano – it-IT
  • Kijapani – ja-JP
  • Kikanada – kn-IN
  • Kikazakhi – kk
  • Kikhema – km-KH
  • Kikorea – ko-KR
  • Kirigizi – ky-KG
  • Kilao – lo-LA
  • Kilativia – lv
  • Kilitwania – lt
  • Kimasedonia – mk-MK
  • Kimalesia – ms
  • Kimalei (Malesia) – ms-MY
  • Kimalayalamu – ml-IN
  • Kimarathi – mr-IN
  • Kimongolia – mn-MN
  • Kinepali – ne-NP
  • Kinorwe – no-NO
  • Kiajemi – fa
  • Kiajemi – fa-AE
  • Kiajemi – fa-AF
  • Kiajemi – fa-IR
  • Kipolandi – pl-PL
  • Kireno (Brazili) – pt-BR
  • Kireno (Ureno) – pt-PT
  • Kipunjabi – pa
  • Kiromania – ro
  • Kiromanshi – rm
  • Kirusi – ru-RU
  • Kiserbia – sr
  • Kisinhala – si-LK
  • Kislovakia – sk
  • Kislovenia – sl
  • Kihispania (Amerika Kusini) – es-419
  • Kihispania (Uhispania) – es-ES
  • Kihispania (Amerika) – es-US
  • Kiswahili – sw
  • Kiswidi – sv-SE
  • Kitamili – ta-IN
  • Kitelugu – te-IN
  • Kitai – th
  • Kituruki – tr-TR
  • Kiukraini – uk
  • Kiurdu – ur
  • Kivietinamu – vi
  • Kizulu – zu
Nunua na utumie tafsiri zinazofanywa na binadamu

Nunua tafsiri

Kwa kutumia huduma za tafsiri inayofanywa na binadamu inayolipiwa, unaweza kuagiza tafsiri za ubora wa juu kwenye mifuatano ya programu, ukurasa wa programu katika Google Play na bidhaa ya ndani za programu kutoka kwa mtaalamu mwingine wa tafsiri. Kuagiza huchukua dakika chache, bei huanzia USD 0.07 kwa kila neno na tafsiri hukamilishwa ndani ya siku saba.

Vidokezo:

  • Utafanya kazi moja kwa moja na mtoa huduma ili udhibiti tafsiri na ushughulikie masuala yoyote yanayohitaji usaidizi.
  • Tafsiri hazipatikani katika jozi zote za lugha chanzo na lengwa.

Ili ununue tafsiri kupitia Dashibodi ya Google Play:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Huduma ya tafsiri (Kuza > Upatikanaji katika Duka la Google Play > Huduma ya tafsiri).
  2. Bofya Anza kutafsiri.
  3. Chagua Tafsiri inayofanywa na binadamu inayolipiwa kuwa aina ya tafsiri yako.
  4. Katika sehemu ya "Chagua Lugha": 
    • Bainisha lugha chanzo uliyotumia katika maandishi halisi.
    • Chagua lugha zinazolengwa katika tafsiri. 
    • Ukimaliza kuchagua lugha, bofya Endelea.
  5. Katika sehemu ya "Chagua maudhui ya kutafsiri", chagua vipengee unavyotaka kutafsiri:
    • Ukurasa wa programu katika Google Play: Weka jina, maelezo mafupi na maelezo kamili ya programu yako yanayoonyeshwa kwa watumiaji kwenye Google Play.
    • Mifululizo ya programu: Ongeza maandishi kutoka kwenye programu yako kama faili ya XML au CSV.
    • Bidhaa za ndani ya programu: Weka jina na maelezo ya bidhaa zako za ndani ya programu.
    • Maelezo ya ziada: Ongeza picha za skrini au hati zingine kama faili ya GIF, JPEG, PNG au ZIP. Hatua ya kuongeza picha ya skrini huwapa wana isimu muktadha wa jinsi maandishi yanaonyeshwa kwenye programu yako.
    • Tumia tena vifungu vilivyotafsiriwa kwenye maagizo ya awali: Teua kisanduku ili utumie tena vifungu ambavyo tayari vimetafsiriwa ili uokoe pesa. Utatozwa tu kwa tafsiri zozote mpya na utaona gharama ya jumla kabla ya kutuma agizo lako.
    • Ukimaliza kuchagua maudhui ya kutafsiri, bofya Kagua agizo.

      Madokezo: 
    • Unapochagua, bei inayokadiriwa itasasishwa karibu na upande wa juu kulia wa ukurasa. Unaweza kubofya Angalia maelezo ili uone maelezo ya makadirio, ikiwa ni pamoja na lugha hizo, bei kwa kila neno na jumla. 
    • Unaweza kubofya Angalia watoa huduma wengine ili uone orodha ya watoa huduma wengine wa tafsiri na bei zao.
       
  6. Katika sehemu ya "Kukagua na kulipa": 
    • Kagua muhtasari wa agizo lako la tafsiri na uondoe maudhui yoyote usiyoyataka. 
    • Kumbuka tarehe inayotarajiwa kukamilika.
    • Weka msimbo wa vocha iwapo unao.
  7. Bofya Thibitisha na ulipe ili ukamilishe agizo lako. Utapokea barua pepe ya kuthibitisha malipo na utapokea barua pepe nyingine tafsiri zako zinapokamilika.

Tumia tafsiri

Baada ya tafsiri zako kukamilishwa, hivi ndivyo unavyoweza kuzitumia:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Huduma ya tafsiri (Kuza > Upatikanaji katika Duka la Google Play > Huduma ya tafsiri).
  2. Kwenye jedwali, chagua safu mlalo ya lugha ambayo ungependa kutumia. 
  3. Bofya Pakua ili uhifadhi faili yako ya tafsiri kwenye kifaa.
  4. Karibu na lugha ambayo ungependa kutumia, bofya Tumia.

Baada ya kuongeza tafsiri za mifuatano yako ya programu, unaweza kupakia faili ya APK iliyotafsiriwa kwenye Google Play. Ikiwa mapendeleo ya lugha ya mtumiaji yanalingana na lugha za tafsiri ulizoongeza, ataona toleo lililotafsiriwa la programu yako.

Tumia huduma ya tafsiri ya mashine ya Dashibodi ya Google Play bila malipo

Kwa kutumia huduma yetu ya tafsiri ya mashine bila malipo, unaweza kuagiza tafsiri za papo hapo, zinazofanywa na binadamu zenye ubora wa juu za mifuatano ya programu, ukurasa wa programu katika Google Play na bidhaa za ndani ya programu. Kutumia tafsiri za mashine ni njia nzuri ya kuongeza tafsiri zenye ubora wa juu ili kutoa huduma bora kwa watumiaji wa kimataifa wa programu yako bila malipo.

 Lugha zifuatazo zinapatikana (tunajitahidi kuongeza lugha zingine katika siku zijazo):

  • Kichina (Kilichorahisishwa) – zh-CN
  • Kifaransa (Ufaransa) – fr-FR
  • Kijerumani – de-DE
  • Kiindonesia – id
  • Kijapani – ja-JP
  • Kireno (Brazili) – pt-BR
  • Kihispania (Uhispania) – es-ES

Muhimu: Tafsiri hii ni ya mashine, kwa hivyo haijakaguliwa au kuidhinishwa na binadamu.

Ili uongeze tafsiri ya mashine kwenye Dashibodi ya Google Play bila malipo:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Huduma ya tafsiri (Kuza > Upatikanaji katika Duka la Google Play > Huduma ya kutafsiri).
  2. Bofya Anza kutafsiri.
  3. Chagua Tafsiri inayofanywa na binadamu bila malipo kuwa aina ya tafsiri yako.
  4. Katika sehemu ya "Chagua Lugha": 
    • Bainisha lugha chanzo uliyotumia katika maandishi halisi.
    • Chagua lugha zinazolengwa katika tafsiri. 
    • Ukimaliza kuchagua lugha, bofya Endelea.
  5. Katika sehemu ya "Chagua maudhui ya kutafsiri", chagua vipengee unavyotaka kutafsiri:
    • Ukurasa wa programu katika Google Play: Weka jina, maelezo mafupi na maelezo kamili ya programu yako yanayoonyeshwa kwa watumiaji kwenye Google Play.
    • Mifululizo ya programu: Ongeza maandishi kutoka kwenye programu yako kama faili ya XML au CSV.
    • Bidhaa za ndani ya programu: Weka jina na maelezo ya bidhaa zako za ndani ya programu.
    • Ukimaliza kuchagua maudhui ya kutafsiri, bofya Tazama tafsiri.
  6. Katika ukurasa wa Huduma za tafsiri, bofya Kukagua na kutumia ili ukague na utumie maandishi ya ukurasa wa programu katika Google Play na tafsiri za bidhaa ya ndani ya programu. Ikiwa huwezi hutaki kufanya mabadiliko yoyote, bofya Tumia bila kufanya mabadiliko yoyote katika maandishi ya tafsiri ya mashine. Pia, unaweza kupakua mifuatano yako ya tafsiri ya mashine kwenye ukurasa wa Huduma za tafsiri.
Kama hutaki kuweka au kununua tafsiri

Ingawa ni vizuri zaidi kutumia tafsiri zinazofanywa na wazungumzaji wa lugha ya asili, tafsiri za kiotomatiki za maelezo yaliyo kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play zitapatikana kwa watumiaji wa Google Play.

Watumiaji wakitembelea ukurasa wa programu yako katika Google Play kwa kutumia lugha ambayo hujatafsiri, wanaweza kuchagua kuangalia ukurasa wa programu yako uliotafsiriwa kiotomatiki. Karibu na sehemu ya juu ya ukurasa, kutakuwa na arifa inayoeleza kuwa tafsiri imefanywa kiotomatiki, pamoja na chaguo ya kuangalia orodha ya duka katika lugha ya chaguomsingi badala yake.

Kumbuka: Tafsiri za kiotomatiki hazitumiki katika lugha za Kiarmenia, Kiroma cha Raeto, Kitagalogi na Kizulu.

Mapendekezo ya lugha

Katika baadhi ya matukio, unaweza kuona bango kwenye Dashibodi ya Google Play na mapendekezo ya tafsiri ambayo yanaweza kuongeza usakinishaji. 

Data ya kutosha itakapopatikana, mapendekezo haya yatatokana na vigezo vifuatavyo:

  • Mgawanyo wa sasa wa usakinishaji wa programu yako kwa kila lugha unalinganishwa na programu zingine za aina moja.
  • Ukuaji wa sasa wa usakinishaji wa programu yako kwa kila lugha unalinganishwa na programu zingine za aina moja.
  • Aina ya programu yako na mapendeleo ya lugha kwa aina hiyo.
  • Kiwango cha sasa cha kushawishika cha programu yako kwa kila lugha.
  • Soko inayotarajiwa kwa kila lugha.

Tafsiri zilizosasishwa

Ikiwa unawasilisha ombi la tafsiri kwa programu iliyo na tafsiri zilizofanywa hapo awali, kumbuka:

  • Ni sharti utafsiri maandishi yoyote ambayo yamesasishwa tangu toleo la awali kuchapishwa. Huhitaji kuwasilisha mifuatano ya tasfiri iliyofanywa awali.
  • Wakati unapowasilisha agizo, tunalinganisha maandishi na maagizo ya awali. Maandishi yoyote yaliyopo yataondolewa kwenye agizo, kwa hivyo unalipia maandishi mapya pekee.
  • Ukitaka kuwasilisha maandishi yote ili yatafsiriwe (ikiwa ni pamoja na mifutano iliyotafsiriwa), batilisha uteuzi wa kisanduku kilicho karibu na "Tumia tena mifuatano iliyotafsiriwa kwenye maagizo ya awali" kwenye ukurasa wa Chagua maudhui ya kutafsiriwa unaponunua tafsiri yako.

Kagua hali ya agizo

Kuangalia hali ya tafsiri ulizoagiza:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Huduma ya tafsiri (Kuza > Upatikanaji katika Duka la Google Play > Huduma ya tafsiri).
  2. Kwa kila agizo, utaona tarehe ya ununuzi, lugha zilizoombwa, hali na bei iliyolipwa. Unaweza kuchagua safu mlalo ili uone maelezo zaidi.

Kuwasiliana na mtoa huduma za tafsiri

Ili uwasiliane na mtoa huduma wako wa tafsiri:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Huduma ya tafsiri (Kuza > Upatikanaji katika Duka la Google Play > Huduma ya tafsiri).
  2. Karibu na agizo lako, bofya aikoni ya nukta tatu  > Wasiliana na mtoa huduma.

Kuangalia au kukagua tafsiri zako

Ili kuangalia programu yako katika lugha nyingine na kukagua tafsiri za programu yako, utahitaji kubadilisha lugha kwenye kifaa chako cha Android. Ili kufanya hivyo:

  1. Kwenye kifaa chako, fungua programu ya Mipangilio .
  2. Chagua Lugha na mbinu ya kuweka data > Lugha.
  3. Chagua lugha unayotaka kuangalia.
  4. Kagua programu yako.

Omba ankara ya VAT

Kama unahitaji ankara yenye kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa ajili ya agizo lako la tafsiri, nenda kwenye Kituo cha Usaidizi wa Malipo ya Google.

Maudhui yanayohusiana

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
14842770708017154005
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false