Tumia ripoti ya kabla ya uzinduzi ili kubaini matatizo

Makala haya yanafafanua jinsi ya kutayarisha na kutekeleza ripoti ya kabla ya jaribio. Ikiwa umetekeleza ripoti ya kabla ya uzinduzi na ungependa kufahamu jinsi ya kufasiri matokeo, nenda kwenye sehemu ya Fahamu ripoti ya kabla ya uzinduzi.

Ripoti ya kabla ya uzinduzi hutayarishwa kiotomatiki unapochapisha programu kwenye jaribio la ndani, la watumiaji mahususi au la watumiaji wengi. Husaidia kubaini matatizo kabla programu yako iwafikie watumiaji. Inajumuisha majaribio ya:

  • Matatizo ya uthabiti
  • Matatizo ya uoanifu wa Android
  • Matatizo ya utendaji
  • Matatizo ya ufikivu
  • Athari za kiusalama
  • Matatizo ya faragha

Jinsi ripoti ya kabla ya jaribio inavyofanya kazi

Baada ya kupakia na kuchapisha Android App Bundle ya kujaribu, tunaisakinisha kwenye kundi la vifaa vya Android katika maabara yetu ya kujaribu. Kisha tunafungua na kutambaa kiotomatiki kwenye programu yako kwa dakika kadhaa. Programu ya kutambaa hutekeleza vitendo vya msingi kama vile kuandika, kugusa na kutelezesha kidole. Unaweza pia kuweka kitambulisho cha akaunti ya kujaribu au majaribio maalum ili programu ya kutambaa itumie.

Baada ya mchakato wa kutambaa kukamilika, tunaweka matokeo yako kwenye ripoti ya kabla ya jaribio. Tunaondoa pia programu yako kwenye vifaa vyote.

Kukagua ufaafu wa programu yako kwa ripoti ya kabla ya jaribio

Ripoti ya kabla ya uzinduzi itafanya kazi mradi tunaweza kusakinisha na "kutambaa" kwenye programu yako. Hata hivyo, huenda programu fulani zikahitaji mabadiliko madogo kwenye misimbo. Mifano ya kawaida ni pamoja na programu zinazohitaji uthibitishaji wa nchi au usakinishaji. Ili upate maelezo zaidi, nenda kwenye sehemu yetu ya maswali yanayoulizwa sana.

Kumbuka kuwa vifaa vya majaribio haviwezi kutekeleza majaribio kwenye programu zisizo na shughuli kuu ya uzinduzi, zikiwemo vifungua programu, wijeti, kibodi, na sura za saa.

Kunja Zote Panua Zote

Kutekeleza ripoti ya kabla ya jaribio

Jaribu programu yako

Ili utayarishe ripoti ya kabla ya jaribio ya programu yako, chapisha programu yako kwa majaribio ya watumiaji wengi au wachache.

Utapokea kiotomatiki ripoti ya kabla ya jaribio ya programu yoyote unayochapisha kwenye kikundi cha majaribio usipojiondoa. Kwa kawaida utapokea matokeo ya jaribio ndani ya saa moja baada ya kupakia App Bundle yako. Wakati mwingine, utapokea matokeo saa kadhaa baada ya kupakia.

Jisajili kupata barua pepe za ripoti ya kabla ya jaribio

Unaweza kupokea arifa za barua pepe kuhusu ripoti zinazopatikana za kabla ya majaribio kwa kufuata hatua hizi:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play > Arifa.
  2. Sogeza chini hadi kwenye "Ripoti ya kabla ya uzinduzi" kisha uteue kisanduku kilicho karibu nayo. Unaweza kuchagua kupokea barua pepe za majaribio yote au za majaribio yenye matatizo pekee.
Zima ripoti za kabla ya jaribio

Ripoti za kabla ya jaribio hutayarishwa kiotomatiki unapochapisha programu kwenye kikundi cha majaribio ya watumiaji wengi au wachache. Ili uzime ripoti zote za kabla ya jaribio za programu yako:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play> Ripoti ya kabla ya uzinduzi > Mipangilio.
  2. Nenda chini hadi kwenye "Mapendeleo," na ubatilishe uteuzi wa kisanduku cha "Washa ripoti ya kabla ya uzinduzi" ili uzime ripoti ya programu yako.
  3. Bofya Hifadhi.

Weka mapendeleo kwenye majaribio yako

Unaweza kuweka mapendeleo kwenye majaribio yako ili ufanye ripoti yako ya kabla ya uzinduzi iwe ya kina zaidi na ihusiane na programu yako.

Hatua ya Kwanza: Weka vitambulisho vya akaunti ya kujaribu ikiwa programu yako ina skrini ya kuingia katika akaunti

Iwapo programu yako ina skrini ya kuingia katika akaunti na unataka programu ya kutambaa ijaribu mchakato wa kuingia katika akaunti au maudhui husika, unahitaji kuweka vitambulisho vya akaunti.

Kumbuka: Huhitaji kuweka vitambulisho iwapo programu yako inatumia kipengele cha "Ingia ukitumia akaunti ya Google,” (ambacho huruhusu programu ya kutambaa iingie kiotomatiki katika akaunti), au ikiwa tayari umeweka kitambulisho kwenye Ukurasa wa maudhui ya programu.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo muhimu ya kukumbuka unapojaribu vitambulisho:

  • Vitambulisho unavyoweka hutumiwa kwa madhumuni ya majaribio pekee.
  • Tunapojitahidi kuhifadhi vitambulisho vya majaribio kwa usalama, tunapendekeza kuwa usiweke vitambulisho vyovyote rasmi kwenye ripoti ya kabla ya jaribio. Badala yake, unda jina la mtumiaji na nenosiri la akaunti ya majaribio.
  • Vitambulisho vinaweza tu kuwekwa kiotomatiki kwenye programu za Android ambazo zinatumia wijeti za kawaida za Android. Huwezi kutumia vitambulisho katika programu zinazotumia OpenGL kutekeleza programu au vidhibiti maalum ambavyo vinatumia Mwonekano wa Wavuti katika utaratibu wa uthibitishaji unaotokana na wavuti.
  • Google itaingia katika akaunti kiotomatiki iwapo programu inatumia kipengele cha "Ingia ukitumia akaunti ya Google."
Kuweka kitambulisho
  1. Fungua Dashibodi ya Google Play.
  2. Chagua programu unayotaka.
  3. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Majaribio > Ripoti ya kabla ya jaribio > Mipangilio.
  4. Kwenye sehemu ya “Vitambulisho vya akaunti ya kujaribu”, chagua Weka vitambulisho.
  5. Weka yafuatayo:
    • Jina la mtumiaji: Jina la mtumiaji linalohusishwa na akaunti yako ya kujaribu.
    • Nenosiri: Nenosiri linalohusishwa na akaunti yako ya kujaribu.
  6. Bofya Hifadhi. Vitambulisho hivi vitatumika kwa majaribio yote ya baadaye usipovibadilisha.
Badilisha au uondoe vitambulisho
  1. Fungua Dashibodi ya Google Play.
  2. Chagua programu unayotaka.
  3. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Majaribio > Ripoti ya kabla ya uzinduzi > Mipangilio.
  4. Fanya mabadiliko unayotaka:
    • Ili ubadilishe vitambulisho: Katika sehemu ya “Vitambulisho vya akaunti ya kujaribu”, weka vitambulisho ulivyobadilisha kwenye sehemu za jina la mtumiaji na nenosiri.
    • Ili uondoe vitambulisho: Katika sehemu ya “Vitambulisho vya akaunti ya kujaribu”, chagua Usiweke vitambulisho.
      • Kumbuka: Ikiwa utaondoa vitambulisho vya kujaribu programu yako, utahitaji kuweka vitambulisho vipya kabla ya majaribio yoyote ya baadaye kufanyika kwenye programu yako.
  5. Bofya Hifadhi. Vitambulisho hivi vitatumika kwa majaribio yote ya baadaye usipovibadilisha.

Hatua ya Pili: Weka hati ya Robo au utaratibu wa mchezo

Iwapo unataka kudhibiti hatua ambazo programu ya kutambaa inachukua wakati inajaribu programu yako, unaweza kuweka hati ya Robo au utaratibu wa mchezo.

Weka hati ya Robo ili uweke mapendeleo kwenye njia ya majaribio ya programu ya Java

Unaweza kudhibiti hatua ambazo programu ya kutambaa inachukua wakati wa kujaribu programu yako kwa kuweka hati ya Robo ili itekeleze vitendo mahususi kama vile kujaribu safari ya mtumiaji wa kawaida au sehemu mpya ya programu yako.

Unapotekeleza jaribio ukiwa umeambatisha hati, programu ya kutambaa itatekeleza kwanza vitendo ulivyobainisha mapema kisha ikague programu kama kawaida.

Ili upakie hati kwenye ripoti yako ya kabla ya jaribio:

  1. Rekodi hati yako ukitumia zana ya Firebase katika Studio ya Android (Studio ya Android > Zana > Firebase > Maabara ya Kujaribu > Rekodi Hati ya Robo). Ili upate maelezo zaidi, nenda kwenye Kituo cha Usaidizi wa Firebase.
    • Kumbuka: Huhitaji kuwa na akaunti ya Firebase ili kubuni hati ya Robo.
  2. Hati yako inapokuwa tayari, fungua Dashibodi ya Google Play.
  3. Chagua programu unayotaka.
  4. Chagua Majaribio > Ripoti ya kabla ya jaribio > Mipangilio. Katika sehemu ya "Dhibiti jinsi ripoti ya kabla ya jaribio inavyokagua programu yako, pakia hati yako. Unaweza kuburuta na udondoshe faili yako au uchague Pakia.
  5. Bofya Hifadhi.
Weka utaratibu wa mchezo ili ujaribu mchezo au programu ya OpenGL

Iwapo unajaribu mchezo au programu inayotumia OpenGL, unahitaji kuweka utaratibu wa mchezo ili upate ripoti bora ya kabla ya jaribio. Utaratibu wa mchezo hubainisha vitendo ambavyo ungependa programu ya kutambaa itekeleze. Unaweza kujaribu zaidi ya utaratibu mmoja wa mchezo kwenye programu sawa.

Ili utumie taratibu za mchezo kwenye ripoti yako ya kabla ya jaribio:

  1. Badilisha mchezo wako ufanye yafuatayo:
    • Kuanzisha utaratibu
    • Kutekeleza utaratibu
    • Kufunga mfululizo (si lazima). Utafanya mabadiliko haya kwenye mazingira yako ya kusanidi. Ili upate maelezo zaidi, nenda kwenye Kituo cha Usaidizi wa Firebase.
      • Kumbuka: Huhitaji akaunti ya Firebase ili utumie taratibu za mchezo kwenye ripoti ya kabla ya jaribio.
  2. Chapisha toleo la mchezo wako ukitumia utaratibu wa mchezo kwa toleo la jaribio la watumiaji wachache au wengi. Programu ya kutambaa itatambua na kutekeleza kiotomatiki utaratibu wa mchezo.

Hatua ya Tatu: Weka mapendeleo ya eneo unakoanzia kujaribu ukitumia viungo mahususi

Unaweza kuweka hadi viungo vitatu mahususi katika ripoti yako ya kabla ya uzinduzi ili ujaribu maeneo zaidi ya kuanzia katika programu yako.

Programu ya kutambaa hufanya kazi kama kawaida kwa dakika kadhaa, kisha huzima programu na kutembelea kila kiungo mahususi kwa zamu na kutambaa kwa sekunde 30 zaidi. Matatizo yoyote yanayopatikana wakati wa shughuli hizi za ziada za kutambaa hujumuishwa kwenye ripoti kama kawaida.

Ili upate maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kubuni na kujaribu viungo mahususi vya programu yako, tembelea tovuti ya Wasanidi wa Android.

Hatua ya Nne: Angalia ripoti za jaribio katika lugha mahususi

Iwapo ungependa kuangalia matokeo ya kujaribu ya lugha mahususi, unaweza kuweka mapendeleo ya lugha kwenye ukurasa wa Mipangilio ya ripoti ya kabla ya uzinduzi. Unaweza kuchagua hadi lugha tano.

Kidokezo: Kwa kuwa ripoti ya kabla ya uzinduzi hutayarishwa kiotomatiki unapopakia App Bundle yako ya majaribio, unaweza kuweka mapendeleo ya lugha baada ya jaribio la kwanza kukamilika.

Weka mapendeleo ya lugha
  1. Fungua Dashibodi ya Google Play.
  2. Chagua programu unayotaka.
  3. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Majaribio > Ripoti ya kabla ya uzinduzi > Mipangilio.
  4. Chini ya sehemu ya "Jaribu programu yako katika lugha mahususi," chagua + Weka lugha.
  5. Chagua hadi lugha tano. Kwa majaribio yatakayofanywa baadaye, utaona matokeo ya majaribio katika lugha hizi pekee.
    • Kumbuka: Ikiwa hutachagua lugha yoyote, tutachagua kiotomatiki lugha ambazo zimetumiwa sana kusakinisha programu yako.
  6. Bofya Hifadhi.

Angalia ripoti yako ya kabla ya jaribio

Wakati ripoti yako ya kabla ya jaribio inapatikana, unaweza kuona muhtasari wa jaribio ambao unajumuisha idadi ya hitilafu, maonyo na matatizo madogo yaliyopatikana wakati wa kujaribu, yakiwa yamepangwa kulingana na aina ya tatizo. Utaona pia pendekezo la kuzindua kulingana na matokeo ya jaribio la programu yako.

Angalia muhtasari wa ripoti ya kabla ya jaribio

Ili uone muhtasari wa ripoti yako ya kabla ya jaribio:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play.
  2. Chagua programu unayotaka.
  3. Chagua Majaribio > Ripoti ya kabla ya uzinduzi > Muhtasari.
  4. Kagua kila sehemu:
    • Uthabiti
    • Utendaji
    • Ufikivu
    • Usalama na uaminifu
  5. Ikiwa sehemu yoyote ina tatizo, chagua Onyesha muhtasari ili upanue.
  6. Chagua Angalia maelezo ili uone maelezo zaidi ya kina kuhusu matatizo yako.
  7. Ili uone ripoti za awali za kabla ya uzinduzi, nenda kwenye jedwali katika sehemu ya “Maelezo ya ripoti” chini ya ukurasa.

Kumbuka: Ukiona "Jaribio linaendelea," inamaanisha kuwa haijakamilisha jaribio la sasa. Iwapo jaribio lako jipya halijatekelezwa, huenda ukaona "Imeshindwa kujaribu." Ili utekeleze jaribio jingine, chapisha App Bundle nyingine.

Angalia maelezo ya ripoti ya kabla ya jaribio

Ili uone matokeo ya kina ya ripoti yako ya kabla ya jaribio:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play.
  2. Chagua programu unayotaka.
  3. Chagua Majaribio > Ripoti ya kabla ya jaribio > Maelezo.
  4. Kagua vichupo vya Uthabiti, Utendaji, Ufikivu, Picha za skrini na Usalama na uaminifu. Katika kila ukurasa, utaona maelezo kamili ya matokeo ya jaribio lako jipya, yakiwemo ufuatiliaji wa rafu, picha za skrini na chati.

Kumbuka: Ukiona "Jaribio linaendelea," inamaanisha kuwa haijakamilisha jaribio la sasa. Iwapo jaribio lako jipya halijatekelezwa, huenda ukaona "Imeshindwa kujaribu." Ili utekeleze jaribio jingine, chapisha App Bundle nyingine.

Maswali yanayoulizwa sana

Kunja Zote Panua Zote

Majaribio ya programu

Jaribio linapaswa kuchukua muda gani?

Kwa kawaida utapokea matokeo ya jaribio ndani ya saa moja baada ya kupakia App Bundle yako. Wakati mwingine, utapokea matokeo saa kadhaa baada ya kupakia. Iwapo ripoti haijakamilika baada ya siku mbili, jaribu kupakia vizalia vyako vya programu tena. Hatua hii itaanzisha ripoti mpya.

Programu zinazotekeleza uthibitishaji wakati wa kufunguliwa

Je, ninaweza kutekeleza ripoti ya kabla ya jaribio kwa programu ambayo inatekeleza uthibitishaji wa nchi?

Bado unaweza kupata ripoti ya kabla ya jaribio kama ungependa kufanya mabadiliko madogo kwenye msimbo wako.

Vifaa vya majaribio vinapatikana Marekani. Kama programu yako hutumia kitambulisha mahali au ina vizuizi vya maudhui kulingana na nchi, vifaa vya majaribio vinaweza tu kuonyesha maudhui yanayopatikana mahali vilipo.

Iwapo unahitaji kujaribu programu yako kwenye kitambulisha mahali nje ya eneo ambako vifaa vya majaribio vinapatikana, unaweza kuchapisha App Bundle ambayo inaondoa masharti ya mahali kwa madhumuni ya majaribio. Kuna njia mbili za kutambua kuwa ripoti zako za kabla ya jaribio zinatekelezwa kwenye Maabara ya Majaribio:

Je, ninaweza kupata ripoti ya kabla ya jaribio ya programu inayokagua vifaa vilivyozibuliwa?

Mfumo wa kujaribu hauwezi kutumia programu ambazo zinakagua ikiwa kifaa kina udhibiti maalumu (idhini maalum ya kudhibiti) kwenye Android.

Programu zilizo na matangazo au chaguo za ununuzi

Programu yangu ina matangazo. Ninaweza kuhakikisha vipi kuwa jaribio la ripoti ya kabla ya jaribio halichangii katika idadi ya mibofyo na maonyesho (ambayo kituo changu cha matangazo kinaweza kugundua au kukosa kufurahia)?

Tayari Google Ads hutenga watumiaji kutoka makundi ya anwani za ripoti ya kabla ya uzinduzi. Kwa vituo vingine vya matangazo, unahitaji kubainisha makundi ya anwani ya IP zitakazotengwa.

Kuna kitu chochote ninachohitaji kufahamu kuhusu kujaribu programu zenye matangazo ya kuonyesha?

Kwa maelezo kuhusu namna ya kukabiliana na ulaghai wa mapato ya matangazo na jaribio la kiotomatiki la programu, tembelea tovuti ya Wasanidi Programu wa Google.

Je, majaribio hujumuisha usajili wa ununuzi au bidhaa za ndani ya programu?

Vifaa vya majaribio haviwezi kufanya ununuzi wakati wa majaribio. Kama programu yako inatoa huduma ya usajili au bidhaa za ndani ya programu ili kufikia baadhi ya sehemu za programu yako, hali za majaribio zinaweza kuwa chache.

Utendaji mwingine wa programu

Msimbo wangu umefumbwa (Java) au kupunguzwa (wa asili). Je, bado ninaweza kutumia ripoti ya kabla ya jaribio?

Ndiyo. Majaribio ya ripoti ya kabla ya jaribio yatatekelezwa bila tatizo.

Hata hivyo, iwapo msimbo wako umefumbwa au kupunguzwa, ANR au matukio yoyote ya kuacha kufanya kazi yanayopatikana wakati wa majaribio yatakuwa na ufuatiliaji wa rafu ambao pia umefumbwa au kupunguzwa. Ili utusaidie kurahisisha utatuzi wa ufuatiliaji wa rafu yako, tunapendekeza kuwa upakie faili ya kufumbua msimbo au kubadilisha anwani katika faili za uchunguzi na kuweka thamani zinazoweza kusomeka na binadamu.

Unaweza kupata maelezo kuhusu jinsi ya kupakia faili za kufumbua msimbo au kubadilisha anwani katika faili za uchunguzi na kuweka thamani zinazoweza kusomeka na binadamu.

Je, kuna njia ya kupakia mapema vifaa vya majaribio vilivyo na maudhui au programu za ziada zilizosakinishwa mapema?

Hapana. Mfumo wa kujaribu hautumii vifaa vinavyopakia mapema vilivyo na maudhui au programu zilizosakinishwa mapema.

Hata hivyo, iwapo unataka kutekeleza majaribio kwenye programu iliyo na data iliyopakiwa mapema, unaweza kuchapisha toleo la jaribio la programu yako ukitumia faili zako za maudhui zilizopachikwa katika App Bundle yake.

Itakuwaje iwapo programu yangu hutumia huduma ya utoaji leseni ya Google Play?

Iwapo programu yako inafanyiwa jaribio na watumiaji wengi au imechapishwa katika toleo la umma, ripoti ya kabla ya uzinduzi itatumia kitambulisho ambacho kinatumika kama leseni ya programu yako.

Iwapo programu yako haifanyiwi jaribio na watumiaji wengi au haina App Bundle inayotumika ambayo imechapishwa katika toleo la umma, programu hiyo haitapita ukaguzi wa leseni. Bado utapokea matokeo ya ripoti ya kabla ya uzinduzi lakini programu yako haitakuwa na leseni. Ili ufanye majaribio kwenye programu hizi, unaweza kuchapisha toleo la watumiaji wachache la programu yako wakati huduma za leseni zimezimwa.

Je, vifaa vya majaribio vinaweza kutekeleza majaribio katika programu zinazotumia mipangilio ya ukurasa wa mkao mlalo?

Vifaa vya kujaribu hubainishwa mapema ili kutekeleza majaribio kwenye ukurasa wa mkao wima usiobadilika kwa chaguomsingi. Hata hivyo, ikiwa programu yako imefungwa katika ukurasa wa mkao wa mlalo, unapaswa kuona video na picha za skrini katika mkao wa mlalo.

Uteuzi wa kifaa

Je, nyinyi huamua kwa njia gani vifaa mtakavyotumia kujaribu programu yangu?

Sisi huchagua vifaa vya majaribio ambavyo vinatumika sana kwenye mfumo wetu na huzingatia umaarufu wa kifaa, idadi ya matukio ya kuacha kufanya kazi, ubora wa skrini, watengenezaji, toleo la Mfumo wa Uendeshaji wa Android na zaidi. Uteuzi wa vifaa vya majaribio unaweza kutofautiana.

Itakuwaje iwapo sijajumuisha baadhi ya vifaa kwenye orodha ya watumiaji lengwa katika faili ya maelezo ya programu yangu?

Iwapo hujajumuisha baadhi ya vifaa kwenye orodha ya watumiaji lengwa katika faili ya maelezo ya programu yako, basi ripoti ya kabla ya uzinduzi pia haitavijumuisha kwenye majaribio, lakini haitalenga vifaa vyovyote vya ziada kwa ajili ya programu yako.

Je, ninaweza kuweka mapendeleo kwenye kikundi cha vifaa vya majaribio?

Ripoti ya kabla ya jaribio inatolewa kwa hisani ya Firebase Test Lab. Ili uweke mapendeleo kwenye vifaa vinavyofanyiwa jaribio, tunakushauri ufanye majaribio yako mwenyewe kwenye dashibodi ya Firebase.

Je, ninaweza kutekeleza ripoti za kabla ya uzinduzi kwenye programu zinazolenga vifaa vya x86?

Ndiyo, tutatekeleza programu kwenye kiigaji na kuitambaza jinsi ambavyo tungefanya kwenye kifaa halisi.

Je, ninaweza kujaribu programu yangu kwenye maumbo gani?

Vifaa vyetu ni pamoja na simu, vishikwambi, Wear OS na Kompyuta za aina yoyote kama vile Chromebook. Huwezi kujaribu programu moja kwa moja kwenye vifaa vya Android Auto au Android TV.

Je, ninaweza kujaribu programu yangu kwenye matoleo ya zamani ya Android?

Vifaa vyetu ni pamoja na vifaa vya Android 9 na matoleo mapya zaidi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
8484996339039286255
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false