Bainisha ruhusa zinazotakiwa na programu yako

Maombi ya ruhusa hutathminiwa wakati wa kuchapisha toleo baada ya kuweka Android App Bundle. Ikiwa programu yako itaomba kutumia ruhusa nyeti au zinazoweza kuwa hatari zaidi (kwa mfano, Rekodi ya Nambari za Simu au SMS), huenda ukatakiwa kujaza Fomu ya Taarifa za Ruhusa na upokee idhini kutoka Google Play.

Kuhusu mchakato huu

Fomu ya Taarifa za Ruhusa huonyeshwa wakati wa kuchapisha toleo iwapo programu ina App Bundle inayoomba ruhusa ambazo hazijatolewa kwenye Fomu ya Taarifa za Ruhusa katika Google Play.

Iwapo una App Bundle inayotumika inayohitaji Taarifa ya Ruhusa, ikiwa ni pamoja na matoleo kwenye Jaribio la watu wengi, Jaribio la watu mahususi au matoleo ya jaribio la ndani, arifa huonyeshwa kwenye menyu ya kushoto chini ya Maudhui ya Programu. Huwezi kuchapisha mabadiliko yoyote kwenye programu yako, yakiwemo mabadiliko kuhusu Upatikanaji katika Duka la Google Play (kwa mfano, Bei, Usambazaji na Ukurasa wa Programu Katika Google Play) hadi ushughulikie arifa hii kwa kubuni toleo ambalo lina Taarifa za Ruhusa au lisilo na ruhusa.

Unaweza kuzima vikundi vyovyote vya Jaribio la Ndani, la Wachache au la Wengi ambavyo havitumiki kwa sasa iwapo havitii sera hii.

Iwapo unachapisha programu kwa kutumia API ya Uchapishaji wa Wasanidi Programu wa Google Play, soma maagizo haya maalum.

Jaza Fomu ya Taarifa za Ruhusa

 

Hatua ya 1: Tathmini ruhusa zinazotakikana

Panapohitajika, utapata historia ya ruhusa zilizobainishwa awali na pia ruhusa zilizoombwa hivi majuzi katika orodha inayoweza kupanuliwa chini ya sehemu ya "Fomu ya Taarifa za Ruhusa" ya ukurasa wa Maudhui ya programu.

  • Ruhusa zilizo na alama ya kuteua zimebainishwa katika matoleo ya awali.

  • Ruhusa zilizo na arifa zimeongezwa hivi majuzi. Maombi haya ya ruhusa yatajumuishwa katika fomu yako ya taarifa ili yakaguliwe na timu ya Google Play na yatathminiwe kwa kuzingatia mwongozo uliochapishwa.
Iwapo utaona ruhusa zilizoombwa katika orodha ya ruhusa mpya zinazoombwa, ambazo hutarajii kujumuisha katika Fomu yako ya Taarifa za Ruhusa, unapaswa kuondoa APK au App Bundle hiyo kisha upakie App Bundle mpya iliyo na orodha sahihi ya ruhusa zinazoombwa kabla hujaendelea.

 

Hatua ya Pili: Bainisha utendaji wa msingi wa programu yako

Ni sharti ubainishe utendaji wa msingi wa programu yako kwenye orodha ya utumiaji unaokubalika. Chagua visanduku vyote vya kuteua ambavyo vinatumika katika utendaji wa msingi wa programu yako.

Hatua ya 3: Weka maagizo ya ukaguzi wa programu

Pindi unapotuma Fomu ya Taarifa za Ruhusa, timu ya Google Play hukagua utendaji wa msingi wa programu yako ili kuhakikisha kuwa ruhusa zinazoombwa zinatakikana katika hali ya utumiaji inayokubalika. 
Iwapo maagizo maalum yanatakikana ili kuashiria utendaji huu wa msingi, unaweza kujumuisha maagizo hayo katika sehemu hii.

Hatua ya nne: Weka onyesho la video ya programu yako

Lazima uweke onyesho la video ili timu ya ukaguzi wa Google Play iweze kutathmini kwa urahisi utendaji wa msingi wa programu yako.

Miundo ya video inayokubalika: Viungo vya YouTube (inapendekezwa), kiungo cha hifadhi ya wingu kuelekea katika mp4 au aina yoyote ya faili ya video ya kawaida

Hatua ya 5: Weka maagizo ya kufikia maudhui ya programu yanayodhibitiwa

Iwapo utendaji wa msingi wa programu yako unatumiwa tu na watu wanaoingia katika akaunti, ni sharti uweke maagizo ya kufikia maudhui hayo yanayodhibitiwa. Timu ya ukaguzi wa Google Play itatumia maagizo haya kutathmini utendaji unaodhibitiwa.

Iwapo programu yako itahitaji mtumiaji aingie katika akaunti, chagua Imedhibiti baadhi ya utendaji au utendaji wote na maelezo sahihi ya jina la mtumiaji au nambari ya simu, nenosiri na maagizo yoyote yanayohitajika ili kufikia maudhui ya programu zinazodhibitiwa.

Weka tu vitambulisho vya akaunti vinavyotumika kwenye jaribio. Usiweke vitambulisho vyovyote vya mtumiaji wa toleo la umma.
Vinginevyo, chagua Utendaji wote unapatikana bila idhini maalum ili uendelee bila kuweka vitambulisho vya jaribio.

Hatua ya 6: (APK Nyingi pekee) Omba hali ya kutofuata kanuni katika APK za zamani 

Kumbuka: Sehemu hii itaonekana tu ikiwa unatumia mipangilio ya APK nyingi katika toleo lako na moja ya vibadala vya APK vinaomba ruhusa ya kutumia data ya Rekodi ya Nambari za Simu au SMS.

Unaweza kutuma ombi la kutofuata kanuni katika hali ambapo mipangilio yako ya APK nyingi inatumia APK za zamani ambako huwezi kufanya mabadiliko ya misimbo. Soma masharti ya kutofuata kanuni katika hali hii kabla ya kuendelea. Soma masharti ya kutofuata kanuni katika hali hii kabla hujaendelea, rejelea makala ya Utumiaji wa vikundi vya ruhusa za SMS au Rekodi ya Nambari za Simu na Kuomba ufikiaji wa mahali chinichini ili upate maelezo zaidi.

APK zozote ambazo hazitimizi masharti ni lazima zizimwe ili zitii sera za Ruhusa.

Iwapo umetimiza masharti ya kutofuata kanuni, weka misimbo ya toleo, ikiwa imetenganishwa kwa koma, katika sehemu ya Kutofuata Kanuni za APK. 

Hatua ya 7: Thibitisha taarifa unayotoa

Chagua visanduku vya kuteua vinavyoambatana ili uthibitishe kuwa maelezo ya taarifa yako ni sahihi na kuwa unakubali sheria na masharti ya matumizi yanayofaa ya ruhusa ulizobainisha.

Andaa na usambaze toleo lako

Baada ya kukamilisha hatua zote zinazotakikana katika Fomu ya Taarifa za Ruhusa, kamilisha hatua zilizosalia ili kuandaa programu yako kwa ukaguzi na uandae na usambaze toleo lako.

Mchakato wa kukagua ruhusa

Baada ya kujaza Fomu ya Taarifa za Ruhusa na kusambaza toleo lako, programu yako itakaguliwa kwa kina na timu ya Google Play. Huenda ikachukua wiki kadhaa kuchakata ombi lako. Katika kipindi hiki, programu yako mpya au sasisho la programu litakuwa katika hali ya linasubiri kuchapishwa hadi ombi lako likaguliwe. Pia, programu yako itafanyiwa ukaguzi wa kawaida ili kubaini iwapo inatii Sera za Mpango wa Wasanidi Programu wa Google Play.

Ikiwa utabatilisha programu inayosubiri kuchapishwa kwa kuwasilisha toleo jipya, huenda tukachelewesha zaidi mchakato wa ukaguzi. Iwapo unahitaji kuchapisha haraka sasisho la programu, lazima uondoe ruhusa nyeti au zilizo hatari kwenye App Bundle yako na usambaze toleo jipya. Toleo hili jipya litakaguliwa tu kubaini ikiwa linatii sera za kawaida na litachapishwa ndani ya saa kadhaa.

Ikiwa programu yako haitii sera ya Ruhusa, timu ya Google Play itatuma barua pepe iliyo na matokeo ya ukaguzi kwa Mmiliki wa Akaunti kupitia anwani ya barua pepe iliyo kwenye akaunti yako ya msanidi programu. Ikiwa ombi lako limethibitishwa na programu yako inatii sera za Mpango wa Wasanidi Programu, programu yako mpya au sasisho la programu litachapishwa kiotomatiki kwenye Google Play.

Maagizo muhimu kwa ajili ya watumiaji wa API ya Uchapishaji ya Wasanidi Programu wa Google Play

Ikiwa utasambaza toleo ukitumia API ya Uchapishaji ya Wasanidi Programu wa Google Play na Google Play haijathibitisha awali utumiaji wa ruhusa nyeti au zinazoweza kuwa na hatari kubwa katika App Bundle, utapokea ujumbe wa hitilafu.

Ili uendelee kudhibiti matoleo ukitumia API ya Uchapishaji, ni lazima uondoe maombi yoyote ya ruhusa nyeti au yenye hatari kubwa katika programu yako kisha uunde toleo jipya lenye App Bundle iliyosasishwa. Unaweza pia kutayarisha na kusambaza toleo lako ukitumia kiolesura cha wavuti cha Dashibodi ya Google Play kwa kufuata hatua hizi:

  1. Pakia App Bundle yako yenye hatari kubwa au ruhusa nyeti iliyoombwa

  2. Jaza Fomu ya Taarifa za Ruhusa kama ilivyoelezwa hapo juu

  3. Kamilisha usambazaji wa toleo ukitumia kiolesura cha wavuti kwenye Dashibodi ya Google Play

Baada ya kuthibitisha Taarifa za Ruhusa na programu kuthibitishwa kuwa inatii sera, toleo lako litachapishwa na utaweza kutumia tena API ya Uchapishaji kudhibiti matoleo yako. Vinginevyo, timu ya Google Play itakuarifu iwapo ombi la Taarifa za Ruhusa limekataliwa na ikupe maelezo ya ziada.

Kumbuka: Wakati wowote ambapo programu yako itaomba ruhusa zozote mpya, utahitajika kutumia kiolesura ili ujaze Fomu ya Taarifa za Ruhusa iliyosasishwa, inayoshughulikia hasa ruhusa mpya zinazoombwa.

Maudhui yanayohusiana

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
10103430421380120863
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false