Matatizo ya kugundulika na kuonekana kwa programu

Unaweza kupata majibu ya maswali mengi kuhusu matatizo ya kugundulika na kuonekana kwa programu katika Kituo cha Usaidizi wa Dashibodi ya Google Play. Timu yetu ya usaidizi inaweza kutatua yaliyosalia.

Vidokezo kuhusu matatizo ya kawaida

  • Unapochapisha programu au sasisho, tunakufahamisha muda ambao mchakato wa ukaguzi utachukua kabla ya mabadiliko uliyofanya kuchapishwa. Iwapo sasisho lako linachukua muda zaidi ya vile tulivyobaini na bado hujaona mabadiliko uliyofanya kwenye Google Play, tatua tatizo mahususi hapa chini.
  • Ikiwa ungependa programu yako ipatikane na kutafutwa kwenye Google Play, hakikisha imechapishwa katika toleo la umma. Kama unafanya jaribio la watumiaji wachache au jaribio la ndani na ungependa kufanya programu yako ipatikane hadharani, unda toleo la umma.
Siipati programu yangu kwenye baadhi ya vifaa

Iwapo hupati programu yako katika baadhi ya vifaa vya Android, inawezekana kuwa vifaa hivyo haviwezi kuitumia au havijajumuishwa kwenye programu yako. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kukagua uoanifu wa kifaa cha programu yako na vifaa ambavyo havijajumuishwa.

Pia, hakikisha kwamba vifaa vya Android unavyotumia vinaweza kutumia Google Play.

Ikiwa bado huipati programu yako, tafadhali wasiliana na timu yetu ya usaidizi.

Siipati programu yangu nikitumia huduma ya Tafuta na Google au Nafasi ya programu yangu imebadilika katika matokeo ya utafutaji

Kama vile unapotafuta kwenye Google, huduma ya utafutaji kwenye Google Play huzingatia vipengee kadhaa, kama vile majina ya programu, majina ya wasanidi programu na ufafanuzi wa programu. Ili tusaidie programu yako kugundulika, hakikisha unafuata mbinu bora za kuunda ukurasa wa programu katika Google Play ambao una maelezo ya kina.

Kwa kuwa programu mpya zinachapishwa kila siku na kuna mabadiliko yanayoendelea kuhusu jinsi matokeo ya utafutaji yanavyoorodheshwa, unaweza kutarajia matokeo ya utafutaji kubadilika mara kwa mara. Pia, watu wanaweza kupata matokeo tofauti ya utafutaji kulingana na vifaa, maeneo, watoa huduma, uwezo wa kutumia vipengele vinavyopatikana na zaidi.

Ikiwa una programu inayolipishwa, kumbuka kwamba ingawa programu zinazolipishwa zinapatikana katika nchi nyingi, hazipatikani katika nchi zingine. Ili upate maelezo zaidi, nenda katika Vichujio kwenye Google Play..

Ili kuhakikisha kwamba programu yako imeorodheshwa kwenye Google Play, hivi ndivyo unavyoweza kutembelea ukurasa wa programu yako katika Google Play:

  1. Ingia katika akaunti ya Dashibodi ya Google Play.
  2. Chagua programu unayotaka.
  3. Chini ya jina la programu, bofya Angalia kwenye Google Play.
Programu yangu inaweza kuangaziwa kwenye Google Play kwa njia gani?

Ingawa haturuhusu uteuzi wa kibinafsi kuangaziwa kwenye Google Play, unaweza kuisaidia programu yako igunduliwe kwenye Google Play kwa kubuni ukurasa wa programu katika Google Play ambao unaridhisha kwa kutumia aina sahihi ya picha na video. Programu maarufu zinaweza kuangaziwa na timu ya Google Play kwenye orodha kadhaa za bidhaa zinazotangazwa

Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kusambaza programu yako kwenye Google Play katika Tovuti ya Wasanidi Programu wa Android.

Programu yangu imeondolewa, imekataliwa au imesimamishwa kwenye Google Play

Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu kukataliwa, kuondolewa na kusimamishwa kwa programu katika Kituo chetu cha Usaidizi.

Matatizo yanayohusiana na programu zilizowekewa vikwazo vya kijiografia au vya IP

Kutumia huduma ya kutambulisha mahali au IP kufanya programu yako itumike katika nchi mahususi hulazimu baadhi ya watumiaji kutegemea seva mbadala kuifikia. Wakati mwingine, hali hii inaweza kusababisha mifumo yetu kuripoti kuwa ununuzi wa wateja umefanywa kwa ulaghai. Ili kuzuia matatizo kutokea, usiweke vikwazo vya IP au vya kutambulisha mahali katika programu yako.

Pia, ili kuhakikisha kwamba unasambaza programu yako katika nchi sahihi, hakikisha kuwa unakagua nchi ambapo programu yako inapatikana

Matatizo ya kufanya jaribio la watumiaji wengi, watumiaji wachache au jaribio la ndani

Unaweza kupata maagizo kamili kuhusu jinsi ya kufanya majaribio ya watumiaji wengi, watumiaji wachache au majaribio ya ndani katika Kituo chetu cha Usaidizi.

Kama una maswali mahususi ambayo ungependa tuyajibu, wasiliana na timu yetu ya usaidizi.

Matatizo yanayohusiana na kutoa sasisho la programu ukitumia njia ya kusambaza kwa hatua

Unaweza kupata maagizo yote kuhusu jinsi ya kutoa sasisho la programu ukitumia njia ya kusambaza kwa hatua katika Kituo chetu cha Usaidizi.

Kama una maswali mahususi ambayo ungependa tuyajibu, wasiliana na timu yetu ya usaidizi.

Maudhui yanayohusiana

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
10447409813691983520
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false