Kagua utendakazi wa usajili wa ndani ya programu

Kwenye dashibodi yako ya usajili, unaweza kuona jumla ya usajili, usajili mpya na usajili ulioghairiwa wa programu yako katika kipindi mahususi pamoja na maelezo ya mapato.

Kumbuka: Maagizo ya kujaribu kutoka kwa walioidhinishwa kujaribu programu hayajumuishwi katika ripoti ya usajili.

Weka mipangilio ya dashibodi ya programu yako

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa muhtasari wa Usajili  (Ripoti za fedha > Usajili > Muhtasari).
  2. Katika sehemu ya juu ya skrini yako, chini ya "Weka mipangilio ya ripoti," chagua bidhaa, nchi na kipindi cha muda ambacho ungependa kuangalia data yake.

Mwonekano wa usajili

Vipimo vyote vya utendaji wa usajili vinaweza kuonyeshwa katika aina tatu tofauti za mwonekano, unaolingana na usajili, mpango wa msingi na vipengee vya ofa vilivyopo ndani ya usajili wako:

  1. Mwonekano wa Usajili: Huu ni mwonekano chaguo msingi na huonyesha utendaji kamili wa kipindi chote cha usajili wa mtumiaji, bila kujali mabadiliko yoyote wanayofanya kwenye mipango ya msingi au ofa
  2. Mwonekano wa mpango wa msingi: Mwonekano huu hukuruhusu kuchanganua utendaji wa kila mpango wa msingi uliopo ndani ya usajili, kwa mfano, kulinganisha utendaji wa mpango wa msingi wa mwaka dhidi ya wa kila mwezi. Hupuuza mabadiliko yoyote yanayofanywa na watumiaji kwenye ofa
  3. Mwonekano wa ofa: Mwonekano huu hukuruhusu kuchanganua na kulinganisha utendaji wa kila ofa iliyopo ndani ya mpango wa msingi

Ili ubadilishe mwonekano mmoja kwenda mwingine, katika sehemu ya juu ya ukurasa wa sehemu ya "Weka mipangilio ya ripoti", bofya Badilisha mwonekano, chagua mwonekano unaopendelea kisha bofya Hifadhi

Muhtasari

Ufafanuzi

Katika sehemu ya juu ya skrini, utaona maelezo yafuatayo:

  • Usajili unaotumika: Idadi ya usajili ambao ulikuwa unaendelea kwa angalau siku moja katika kipindi ulichochagua, ikijumuisha watumiaji waliojaribu bila malipo.
  • Usajili mpya: Idadi ya usajili ambao ulianza katika kipindi ulichochagua, ikijumuisha watumiaji waliojaribu bila malipo.
  • Usajili ulioghairiwa: Idadi ya usajili ambao ulighairiwa katika kipindi ulichochagua, ikijumuisha ughairi uliofanywa katika kipindi cha kujaribu kisicholipishwa.
  • Mapato yote: Kadirio la mapato yaliyozalishwa katika kipindi ulichochagua. Hiki ni kiasi cha fedha zinazolipwa na watumiaji, ikijumuisha kodi na ada nyinginezo.
  • ARPAS: Muhtasari wa wastani wa mapato kwa kila usajili unaoendelea. ARPAS huhesabiwa kama jumla ya mapato ya usajili katika kipindi ulichochagua, ukigawanya na jumla ya usajili uliotumika.
  • Urejeshaji wa pesa: Jumla ya matukio ya kurejesha pesa ambazo zilitolewa katika kipindi kilichochaguliwa.

Unapokagua dashibodi ya programu yako, kumbuka maneno yafuatayo:

  • Mteja: Mtumiaji aliye na angalau usajili mmoja unaotumika kwenye programu yako. Hii inajumuisha watumiaji walio na majaribio yasiyolipishwa au wale wa muda wa kutumia bila kutozwa.
  • Usajili unaotumika: SKU ambayo mtumiaji anatumia, ikiwa ni pamoja na majaribio yasiyolipishwa. Usajili unaoendelea humalizika wakati mtumiaji anaghairi usajili wake, hata kama idhini yake ya kufikia itaendelea hadi mwisho wa kipindi cha sasa cha malipo.
  • Waliojisajili kwa mara ya kwanza: Usajili wa mara ya kwanza ambao mtumiaji amenunua katika programu yako.
  • Usajili unaorudiwa: Usajili wa pili au zaidi ambao mtumiaji amenunua katika programu hiyo. Kwa mfano, mtumiaji alighairi usajili wa kwanza mwezi wa Mei na kununua mwingine mwezi wa Septemba.
Jumla ya usajili

Kadi ya jumla ya usajili katika programu yako huonyesha usajili wote unaoendelea, mpya na ulioghairiwa katika kipindi ulichochagua, ikijumuisha watumiaji wanaotumia vipindi vya kujaribu visivyolipishwa.

Mapato yote

Kadi ya mapato ya programu yako huonyesha mapato ya kila siku na ya kila baada ya siku 30, yaliyozalishwa katika kipindi ulichochagua, ikijumuisha kodi na ada nyinginezo.


Udumishaji wa watumiaji

Kadi ya wanaoendelea kutumia usajili huonyesha asilimia ya usajili unaoendelea kutumika katika kipindi mahususi. Unaweza kutumia maelezo haya kuelewa vizuri jinsi SKU mbalimbali zinavyoshawishi wateja.

Ili uone uchanganuzi wa kina wa data ya watumiaji walioshawishika na wanaoendelea kutumia usajili, chagua Kagua ripoti.  

Usajili ulioghairiwa

Kadi za kughairi zinaonyesha muhtasari wa mabadiliko ya usajili katika kundi lako. Unaweza kutumia maelezo haya kubaini njia za kupunguza matukio ya kughairi katika hali mbalimbali. 

Ili uone uchanganuzi wa kina wa data ya kutamatishwa na kurejeshwa kwa usajili wako, chagua Kagua ripoti.

Angalia ripoti za kina

Unaweza kuona ripoti za kina za kutamatishwa na kuendelea kutumia usajili wowote wa programu yako kwa kuchagua kiungo cha ripoti kilichopo chini ya kila kadi.

Ripoti ya kudumisha watumiaji

Kwenye ripoti yako ya Kudumisha watumiaji, unaweza kulinganisha asilimia ya watumiaji walioshawishika na wanaoendelea na usajili kati ya makundi mawili ya usajili ili uelewe vyema njia bora za kushawishi na kudumisha watumiaji. Unaweza kuweka mipangilio ya makundi kulingana na usajili, mpango wa msingi au ofa, nchi ya ununuzi na kipindi ambacho usajili ulianza. Makundi yaliyo kwenye ripoti ya kudumisha wateja yanajumuisha watumiaji wote wapya, ikiwa ni pamoja na watumiaji wanaorejesha usajili na wanaojisajili kwa mara ya kwanza.

Linganisha asilimia za kudumisha wateja

Unaweza kutathmini jinsi kila kikundi kinavyodumisha wateja na wakati au iwapo watabadilika kwa kutumia chati za “Waliodumishwa kulingana na kipindi cha bili” na “Waliodumishwa kulingana na siku”.

Kwenye chati ya “Waliodumishwa kulingana na kipindi cha bili”, unaweza kuona idadi ya vipindi vya kutuma bili ambapo wateja wanaendelea kutumia programu. Hii inaweza kukupa maarifa kuhusu jinsi unavyoendelea kuchuma mapato kutoka kwa wateja katika kila kikundi.

Kumbuka: Iwapo umeweka vipindi vya kutozwa vya bei ya utangulizi kwenye usajili, vitajumuishwa kwenye vipindi vya bili. Iwapo mpango wa msingi wa awamu umechaguliwa, ripoti itaonyesha usajili wa awamu zilizotozwa katika kipindi cha bili.

Kwenye chati ya “Waliodumishwa kulingana na siku”, unaweza kupata maarifa ya kina kuhusu muda ambao wateja hufika kwenye kipindi cha bili kabla ya kukatisha. Chati hii inajumuisha siku ya kwanza ambapo usajili ulianza kutumika hadi siku ulipoghairiwa, ikijumuisha kipindi chochote cha kujaribu kisicholipishwa, kipindi cha kutumia bila kutozwa na kipindi ambapo akaunti ilisimamishwa kwa muda.

Chini ya kila chati, unaweza kuona data katika jedwali kwa kuchagua kishale cha chini karibu na Jedwali la data.

Linganisha asilimia ya walioshawishika

Chini ya chati ya kudumisha wateja, kuna kadi ambazo zinaonyesha jinsi wateja wanavyoshawishika katika hali zifuatazo:

  • Kutoka ofa ya jaribio lisilolipishwa kwenda usajili unaolipishwa
  • Kutoka ofa ya bei ya utangulizi kwenda bei kamili
  • Kutoka kipindi cha malipo kamili ya mara ya kwanza kwenda malipo kamili ya mara ya pili

Kwenye kila kadi, unaweza kuona idadi ya wateja katika kundi waliofikia hali ya usajili na idadi ya wateja waliondoka katika hali ya kujisajili kwa kutamatisha au kwa kuhamia kwenye usajili unaolipishwa, pamoja na uchanganuzi wa kina wa sababu za kutamatisha usajili.

Kwa mfano, chukulia ulikuwa na wateja 2,000 mwanzoni mwa ofa ya jaribio lisilolipishwa na wateja 1,000 kati ya hao sasa wamekamilisha ofa ya jaribio lisilolipishwa, labda kwa kutamatisha usajili au kwa kuhamia kwenye usajili unaolipishwa. Iwapo wateja 200 kati ya hao 1,000 hawatumii tena jaribio lisilolipishwa kwa sababu walitamatisha usajili na wateja 800 walihamia kwenye usajili unaolipishwa, asilimia ya waliotamatisha usajili itakuwa 20 na asilimia ya walioshawishika itakuwa 80.

Ikiwa umechagua mwonekano wa mpango wa msingi, vipimo vyako vya waliotamatisha usajili vitaonyesha pia watumiaji waliohamia kwenye mpango tofauti wa msingi uliopo ndani ya usajili. Ikiwa umechagua mwonekano wa ofa, vipimo vyako vya waliotamatisha usajili vitaonyesha pia watumiaji waliohamia kwenye mpango wa msingi au ofa tofauti.

Ripoti ya kughairi

Kwenye ripoti yako ya Waliorejesha na walioghairi usajili, unaweza kupata maarifa ya kina kuhusu sababu zilizofanya watumiaji waghairi usajili wao na jinsi vipengele vya kurejesha usajili, kama vile muda wa kutumia bila kutozwa na akaunti kusimamishwa kwa muda, vinavyofanya kazi.

Baada ya kuchagua usajili, mpango wa msingi au ofa, nchi na kipindi ambacho ungependa kuangalia data yake, unaweza kuangalia chati zinazotoa muhtasari na kuainisha sababu za watumiaji kughairi usajili wao. Takwimu zinaonyeshwa kama asilimia kwa chaguomsingi ili kurahisisha shughuli ya kulinganisha sababu kuu za kutamatisha usajili. Ili ungalie data ikiwa thamani halisi, chagua Thamani halisi kutoka kwenye menyu kunjuzi ya Skrini.

Ili upate maelezo kuhusu tarehe mahususi, wekelea kiashiria juu ya grafu.

Angalia sababu za kutamatisha usajili

Kadi ya Kutamatisha huonyesha uchanganuzi wa sababu kuu za watumiaji kutamatisha usajili baada ya muda:

  • Kwa Hiari: Usajili ambao umetamatishwa kutokana na hatua dhahiri ya mtumiaji (k.m., kughairi kwenye Duka la Google Play, kufuta akaunti yake, kuwasiliana na huduma ya usaidizi ili kuomba kutamatisha) au kutokana na msanidi programu (k.m., kwa kutumia API ya Msanidi Programu wa Google Play au kueleza wasimamizi watamatishe usajili).
  • Bila hiari: Usajili ulioghairiwa kutokana na tatizo la kukamilisha malipo (k.m., mabadiliko ya bei ambayo hayajathibitishwa au tatizo la kulipa, kama vile ukosefu wa pesa za kutosha, akaunti kufungwa, n.k.).
  • Kupandisha au kushusha kiwango: Usajili ulighairiwa kwa sababu mtumiaji alihamia kwenye kiwango kingine cha usajili.
  • Badiliko la mpango wa msingi: Mtumiaji alihamia kwenye mpango mwingine wa msingi uliopo ndani ya usajili mmoja (huonyeshwa tu katika mpango wa msingi na mwonekano wa ofa).
  • Badiliko la Ofa: Mtumiaji alihamia kwenye ofa nyingine iliyopo ndani ya mpango sawa wa msingi (huonyeshwa tu katika mwonekano wa ofa).
  • Nyingineyo: Usajili ulioghairiwa kwa sababu nyinginezo (k.m., akaunti ambayo haifanyi kazi, kusimamisha programu).

Angalia majibu ya utafiti kuhusu kutamatisha usajili

Watumiaji wanapoghairi usajili wao wakitumia kituo cha usajili, huombwa watoe sababu za kughairi. Majibu ya watumiaji wanaochagua kutoa sababu za kutamatisha usajili yanaonyeshwa kwenye kadi ya Majibu ya utafiti kuhusu kutamatisha usajili.

Watumiaji wanaochagua “Nyingineyo” wanaweza kutoa kwa hiari sababu ya kughairi. Unaweza kupakua faili ya CSV iliyo na majibu haya kutoka kadi ya Majibu mengine ikiwa una ruhusa ya jumla ya "Kuangalia data ya kifedha".

Jinsi ya kutumia dashibodi hii na nyenzo zingine za Dashibodi ya Google Play

  • Dashibodi ya usajili: Inajumuisha data yote inayopatikana na inayohusiana na usajili.
  • Ripoti za fedha: Zinajumuisha mapato yote kutoka kwa mauzo ya programu, bidhaa za ndani ya programu na usajili.

Maudhui yanayohusiana

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

true
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
2435037989381898929
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false