Sambaza programu yako inayofunguka papo hapo

Baada ya kusanidi programu inayoweza kufunguka papo hapo, unaweza kutumia Dashibodi ya Google Play ili kuisambaza kwa watumiaji.

Masharti ya msingi

Ikiwa unaunda hali ya matumizi ya papo hapo kwa mara ya kwanza, unapaswa kutumia Android App Bundle kubuni programu yako. Kutumia App Bundle inayofunguka papo hapo inamaanisha kuwa unahitaji tu kubuni, kuambatisha cheti na kupakia kizalia kimoja cha programu mara moja ili utumie toleo lililosakinishwa la programu na hali ya matumizi ya papo hapo.

Hatua ya kwanza: Ruhusu Programu zinazofunguka papo hapo

Kwanza, unahitaji kuweka Kipengee cha Google Play Kinachofunguka Papo Hapo kuwa aina ya toleo na uhakikishe kuwa kinatumika.

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha nenda kwenye ukurasa wa Mipangilio ya kina (Toleo > Mipangilio > Mipangilio ya kina).
  2. Chagua kichupo cha Umbo.
  3. Bofya + Weka umbo na uchague Kipengee cha Google Play Kinachofunguka Papo Hapo.

Baada ya kukamilisha hatua hizi, "Kipengee cha Google Play Kinachofunguka Papo Hapo" huorodheshwa kama aina ya toleo. Unapaswa pia kuona hali iliyoorodheshwa kuwa "Inatumika" pamoja na alama ya kuteua yenye rangi ya kijani.

Hatua ya Pili: Unda toleo

Toleo ni mchanganyiko wa muundo wa kizalia kimoja au zaidi cha programu utakachotayarisha ili kusambaza programu au sasisho la programu. Unaweza kuunda toleo la papo hapo kwenye vikundi vifuatavyo:

  • Jaribio la ndani: Matoleo ya majaribio ya ndani yanapatikana kwa hadi watumiaji 100 unaochagua ambao wanajaribu ndani ya kampuni.
  • Jaribio la watu wachache: Matoleo ya majaribio ya watu wachache yanapatikana kwa watumiaji wachache unaowachagua, ambao wanaweza kujaribu toleo la programu yako na kutoa maoni.
  • Toleo la umma: Matoleo ya umma yanapatikana kwa watumiaji wote wa Google Play katika nchi ulizochagua.

Muhimu: Lazima uwe na ruhusa ya Kusambaza programu kwenye vikundi vya majaribio ili uunde toleo jipya. Mipangilio ya kulenga nchi ambako utasambaza matoleo ya jaribio la watumiaji wachache hutolewa kwenye mipangilio iliyowekwa katika Toleo la umma na huwezi kuweka mipangilio tofauti.

Ili kuunda toleo la programu inayofunguka papo hapo:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye kikundi ambako ungependa kuanzisha toleo lako:
    • Jaribio la watumiaji mahususi(Toleo >Jaribio > Jaribio la mahususi)
      • Kumbuka: Ili kuweka toleo kwenye kikundi kilichopo cha jaribio la watu mahususi, chagua Dhibiti kikundi. Ili uanzishe kikundi kipya, bofya Anzisha kikundi.
    • Jaribio la ndani(Toleo > Jaribio > Jaribio la ndani)
    • Toleo la umma (Toleo > Toleo la umma)
  2. Karibu na sehemu ya juu kulia kwenye ukurasa, kuna kichujio cha aina ya toleo chenye mipangilio ya Kawaida iliyoteuliwa kwa chaguomsingi. Bofya kishale cha chini ili uangalie aina za toleo na uchague Programu zinazofunguka papo hapo pekee.
  3. Kuunda toleo la papo hapo hutofautiana kidogo kulingana na kikundi ambacho unaundia toleo:
    • Kwa jaribio la ndani na matoleo ya umma: Karibu na sehemu ya juu kulia kwenye ukurasa, bofya Unda toleo jipya.
    • Kwa matoleo ya jaribio la watumiaji mahususi: Bofya Dhibiti kikundi karibu na kikundi cha "Alpha", kisha chagua Unda toleo jipya.
      • Kumbuka: IkiwaSehemu ya Unda toleo jipya imezimwa, huenda ukawa na majukumu kadhaa ya kuweka mipangilio ambayo hujakamilisha. Majukumu haya yanaweza kuorodheshwa katika ukurasa wa Dashibodi.

Kwa maelezo zaidi kuhusu kuweka kila aina ya kikundi, chagua sehemu inayofaa hapa chini. Ili upate maelezo zaidi kuhusu majaribio kwa ujumla, nenda kwenye Weka mipangilio ya majaribio ya watu wengi, wachache au jaribio la ndani.

Maelezo ya Kikundi

Jaribio la ndani au la watu wachache

Weka watumiaji wanaojaribu

Fuata maagizo kwenye makala yetu ya jaribio ili kuunda orodha za watumiaji na uwaalike watumiaji wanaojaribu kutumia programu na kusambaza jaribio la papo hapo katika toleo la jaribio la ndani au jaribio la watumiaji mahususi.

Kabla hujashiriki kiungo cha programu yako na wachunguzaji, kumbuka mambo yafuatayo:

  • Mipangilio ya wachunguzaji hutumika katika makundi husika ya programu zilizosakinishwa na kikundi cha programu inayofunguka papo hapo. Kwa mfano, unapoongeza orodha ya wachunguzaji kwenye toleo la jaribio la watumiaji mahususi la programu yako iliyosakinishwa, orodha hiyo itatumika kwenye toleo la jaribio la watumiaji mahususi la hali ya matumizi ya papo hapo.
  • Wachunguzaji wanaweza tu kujaribu programu moja inayofunguka papo hapo kwa kikundi kimoja lengwa kwa wakati mmoja. Hii inamaanisha kwamba ikiwa mtumiaji anajaribu toleo lako la jaribio la ndani kisha ajijumuishe kwenye toleo la jaribio la wachache, ataondolewa kiotomatiki kwenye toleo la jaribio la ndani.
Toleo la umma

Wakati unaunda toleo la umma, unaweza kubadilisha nchi ambako programu yako inayofunguka papo hapo inapatikana. Kwa chaguomsingi, nchi zilizochaguliwa zitalingana na nchi ambazo unatoa programu yako iliyosakinishwa.

Unaweza kulenga nchi na maeneo ambayo yamechaguliwa kwa ajili ya programu yako ya kawaida katika toleo la umma au la kujisajili mapema. Ili ubadilishe usambazaji wa programu yako, chagua kichupo cha Nchi au maeneo kwenye toleo la programu inayofunguka papo hapo katika ukurasa wa Toleo la umma (Toleo > Toleo la umma).

Hatua ya tatu: Tayarisha toleo la programu yako inayofunguka papo hapo

  1. Fuata maagizo yaliyo kwenye skrini ili uweke App Bundle inayofunguka papo hapo na ulipe jina toleo lako.
    • Jina la toleo litatumika katika Dashibodi ya Google Play pekee na halitaonekana kwa watumiaji.
    • Tutaweka data kiotomatiki kwenye sehemu ya jina la toleo katika faili ya maelezo.
    • Ili kufanya iwe rahisi kutambua toleo lako katika Dashibodi ya Google Play, weka jina la toleo ambalo linakufaa, kama vile toleo la muundo ("3.2.5-RC2") au jina la msimbo wa ndani ("Banana").
  2. Ili kuhifadhi mabadiliko yoyote unayofanya kwenye toleo lako, chagua Hifadhi.
  3. Baada ya kutayarisha toleo lako, chagua Kagua toleo.

Hatua ya 4: Kagua na usambaze toleo lako

Masharti: Kabla ya kusambaza toleo lako, hakikisha kuwa umekamilisha ukurasa wa programu katika Google Play na sehemu za daraja la maudhui na umeweka mipangilio ya bei.

Kama umejaza sehemu hizi katika toleo la programu yako iliyosakinishwa, maelezo hayo yatatumika pia katika hali ya matumizi ya papo hapo. Kumbuka, upatikanaji wa programu zinazofunguka papo hapo hufafanuliwa na faili ya maelezo ya programu yako inayofunguka papo hapo bali si mipangilio ya kutojumuisha kifaa chako.

Wakati uko tayari kusambaza programu yako inayofunguka papo hapo, unaweza kufuata maagizo ili ukague na kusambaza toleo lako.

Hatua ya 5: Kagua maelezo ya toleo

Baada ya kuunda toleo, utaona maelezo ya toleo jipya la programu kwenye ukurasa wako wa Jaribio la watumiaji mahususi, Jaribio la ndani, au Toleo la umma. Tumia kichujio cha aina ya toleo (Kawaida huchaguliwa kwa chaguomsingi) ili uchague Programu zinazofunguka papo hapo pekee, tafuta toleo lako na uangalie maelezo yafuatayo:

  • Muhtasari wa toleo: Maelezo kuhusu toleo ikiwemo muda wa kutolewa, tarehe na upatikanaji wa kifaa.
  • App Bundle: Orodha ya App Bundle zinazofunguka papo hapo zinazotumika, zinazoendelea kutumika na zilizoondolewa ambazo zinahusiana na toleo hili.
  • Historia ya usambazaji: Ratiba ya matukio inayoonyesha muhuri wa wakati ambao toleo la programu yako lilisitishwa au kurejeshwa.

Unaweza pia kupata toleo la papo hapo kwa kulitafuta kwenye ukurasa wa Muhtasari wa matoleo (Toleo > Muhtasari wa matoleo).

Watumiaji wa moja kwa moja kwenye wavuti wa vifaa vya mkononi

Asilimia ya watumiaji

Kama ungependa kujaribu utendaji kati ya wavuti wa vifaa vya mkononi na hali ya matumizi ya papo hapo, unaweza kuelekeza asilimia fulani ya trafiki kwenye wavuti wa vifaa vya mkononi. Hali hii inajulikana kama watakaoelekezwa kwenye wavuti.

Ili kuweka mipangilio ya watakaoelekezwa kwenye wavuti:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uchague programu.
  2. Nenda kwenye ukurasa wa kikundi cha toleo la papo hapo unalotaka kubadilisha (Jaribio la watumiaji mahususi,Jaribio la ndani, au Toleo la umma), au ulitafute kwenye ukurasa wa Muhtasari wa matoleo (Toleo > Muhtasari wa matoleo).
  3. Karibu na sehemu ya juu kulia kwenye ukurasa, bofya kichujio cha aina ya toleo (Kawaida huchaguliwa kwa chaguomsingi) na uteue Programu zinazofunguka papo hapo pekee.
  4. Chagua kichupo cha Wavuti wa Vifaa vya Mkononi.
  5. Karibu na "Watumiaji wa kuelekeza kwenye wavuti wa vifaa vya mkononi" weka asilimia ya idadi ya watumiaji ambao unataka kuelekeza katika wavuti wa vifaa vya mkononi. Kwa mfano, ukiweka 0.95, asilimia 95 ya trafiki inayoruhusiwa ya hali ya matumizi papo hapo itatumwa kwenye wavuti wa vifaa vya mkononi. Asilimia 5 inayosalia itatumwa kwenye hali yako ya matumizi ya papo hapo.
  6. Hifadhi mabadiliko uliyofanya.
Watumiaji wote

Kama una tatizo la programu yako inayofunguka papo hapo na ungependa kuelekeza watumiaji wako wote (kwenye vikundi vyote) katika wavuti wa vifaa vya mkononi:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha nenda kwenye ukurasa wa Mipangilio ya kina (Toleo > Mipangilio > Mipangilio ya kina).
  2. Nenda chini kwenye sehemu ya “Kipengee cha Google Play Kinachofunguka Papo Hapo” na ubofye Dhibiti.
  3. Batilisha uteuzi wa kisanduku cha programu inayofunguka papo hapo inatumika.
  4. Bofya Hifadhi.

Kurekebisha hitilafu

Kama unapokea hitilafu kuhusu APK za kugawa, nenda kwenye tovuti ya wasanidi programu wa Android ili upate maelezo zaidi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
11677732990814508580
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false